Enyi CCM, kinachodaiwa na CHADEMA na ninyi kinawahusu. Wanachofanyiwa akina Mpina na Gwajima ni kwasabb ya ubovu wa katiba

Enyi CCM, kinachodaiwa na CHADEMA na ninyi kinawahusu. Wanachofanyiwa akina Mpina na Gwajima ni kwasabb ya ubovu wa katiba

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
27,640
Reaction score
65,111
1. Kama katiba ingelikuwa bora, Samia asingejipitisha mwenyewe kuwa mgombea urais ndani ya CCM. Lkn katiba imempa mamlaka makubwa sana, kiasi kwamba kila mwanaccm anaogopa kumpinga.

2. Kama katiba ingelikuwa ni bora, Gwajima asingelikuwa mafichoni. Kwani kafanya kosa gani? Kusema ukweli ni kosa?

3. Kama katiba ingelikuwa bora Mpina angelipongezwa sana na rais kwa hotuba yake ya jana. Lkn kwakuwa katiba inampa rais umungu mtu,amlewa ukubwa, amejawa na kiburi na kuuchukia ukweli.

Anaitumia katiba hiyo mbovu kutoa maagizo kana kwamba ashashinda uchaguzi tayari "niachieni Luhaga Mpina kwenye nafasi zangu zile 10".

CCM mnapinga mapambano ya kuitafuta katiba mpya lkn wanaoumia zaidi ni ninyi wenyewe wanaccm. Ilianza kwa Ndugai, ikaja kwa Gwajima na sasa kwa Mpina.

Je, ni mwanaccm yupi atafuata??
 
Yes
Ingelikuwa tume huru wasingejaribu kumtenga mpina kwa sababu wangejua fika Jimbo watalipoteza
Ila wanajua hata wamweke mbwa kuwa mgombea, tume yao itamtangaza
 
Yes
Ingelikuwa tume huru wasingejaribu kumtenga mpina kwa sababu wangejua fika Jimbo watalipoteza
Ila wanajua hata wamweke mbwa kuwa mgombea, tume yao itamtangaza
Na ndiyo maana huyu mama anatamba hadharani kana kwamba amaeshashinda uchaguzi
 
Back
Top Bottom