Barua ya Evarist Chahali kwa viongozi na wafuasi wa upinzani (Hususani CHADEMA)

Zawadi B Lupelo

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
2,549
3,722
*BARUA YANGU KWENU VIONGOZI NA WAFUASI WA UPINZANI (HUSUSANI CHADEMA)*

Na Evarist Chahali

Kwanza poleni sana kwa yote yanayowasibu. Nimeandika mara kadhaa kwamba tangu kuruhusiwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, kamwe vyama vya upinzani havijawahi kupewa haki zao za kikatiba kuendesha shughuli zao bila kuingiliwa.

Kadhalika, nimekuwa nikieleza kwamba chama tawala CCM hakikuridhia kuanzishwa mfumo wa vyama vingi kwa vile kiliona wazo hilo ni zuri au haki ya Watanzania, bali kililazimishwa na mazingira ya wakati huo, kubwa zaidi likiwa upepo wa mageuzi ya kisiasa na uchumi uliokuwa ukivuma sehemu mbalimbali duniani kufuatilia kuanguka kwa ukomunisti katika uliokuwa Muungano wa Jamhuri za Kisoshalisti za Sovieti (USSR).

Kwa upande mwingine, licha ya Tanzania kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi, Katiba ambayo ni sheria mama — licha ya kuwekwa viraka mara kwa mara — imeendelea kulea mfumo wa chama kimoja.

Sheria mbalimbali si rafiki kwa vyama vya upinzani na, japo hili limepuuziwa kitambo, zimekuwa zikitoa mwanya kwa nchi yetu kujikuta inatawaliwa na dikteta, or to make things even worse, ikapata rais mwenye matatizo ya akili.

Pengine fundisho kubwa kabisa kwa vyama vya upinzani ni kupigania kwa nguvu zote upatikanaji wa Katiba mpya, kwa sababu hii ya sasa sio tu inakwaza ustawi wa demokrasia bali pia inatengeneza mazingira mazuri ya kuendelea kuwa chini ya utawala dhalimu wa CCM, sambamba na kurahisisha Tanzania kuongozwa na rais dikteta.

Kama kuna eneo ambalo limeathiriwa mno na sheria mbalimbali kutoendana na mfumo wa vyama vingi basi ni katika taasisi za dola. Kinachoonekana waziwazi ni jinsi jeshi la polisi linavyowaonea viongozi na wafuasi wa upinzani kana kwamba ni wahaini au wasiostahili kuishi Tanzania.

Lakini wadichofahamu wengi ni hujuma kubwa zinazofanyika kwa kutumia “sanaa za kiza” (dark arts) dhidi ya vyama vya upinzani. Maadili yananizuwia kutoa mifano hai (naam, “Kitengo” kimekuwa kikutumiwa na wahuni flani kunibughudhi lakini taaluma niliyowahi kuifanya ni kubwa zaidi ya kenge hao wasumbufu. Mie ni bora kuliko wao, ndo maana kamwe siwezi kusaliti kiapo changu cha utii, “kuropoka” vitu vilivyo kinyume na maadili. Kamwe siwezi kuongelea “sources and methods” si kwa kuogopa sheria hizo za ovyovyo zilizopo bali kwa vile mie ni bora mara kadhaa dhidi ya watesi wangu.

Eneo jingine ambalo limegoma kwenda na mazingira ya siasa za vyama vingi ni utumishi wa umma, ambapo watendaji mbalimbali wanaopaswa kuwatumikia Watanzania bila kujali utikadi zao, wanafanya kazi kikada, kana kwamba ofisi zao ni ofisi za CCM pia.

Mawaziri na manaibu wao, viongozi wakuu wa wizara na watendaji wao, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, RAS na DAS, na kwa ujumla mfumo mzima wa utumishi kwa umma hauna tofauti na utumishi ndani ya CCM. Nchi inaendeshwa kisiasa hata pale inapihitajika utaalam, taaluma au hata busara tu.

Majuzi nimepata taarifa kwamba msaada muhimu uliotolewa na serikali ya Israeli kwa “Kitengo” umeishia mikononi mwa “kitengo kingine” kinachoongozwa na Daudi Albert Bashite kwa ridhaa ya “babake” John Magufuli.

Nawalaumu wana-Kitengo wanaofahamu kuhusu hilo lakini wamekaa kimya. Hivi mtaendelea kunyanyaswa na huyo emlty brain hadi lini? Msaada husika ipaswa kutumiwa na watu wa “Ufundi/Machungwa” lakini umeelekezwa kwa Bashite kwa minajili ya kunasa mawasiliano ya kila asiyempenda.

Pindi Tanzania ikiangamia, ninyi wanafiki mnaokalia kimya maovu haya mtaandamwa na guilty consciousness for the rest if your lives. Huo mnaofanya sio kuzingatia maadili ya kazi bali kuwa part of mfumo corrupt.

Hata hivyo, naendelea kuwashukuru wana-kitengo wachache walio tayari kuhatarisha ajira na maisha yao kutujulisha kinachoendelea. Mna sehemu maalum ya amani inawasubiri huko mbeleni.

Nitumie barua hii kwenu viongozi na wanachama/wafuasi wa vyama vya upinzani kuwakumbusha kuwa licha ya ukweli kwamba tangu kuruhusiwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 vyama vyenu vimeendelea kunyanyaswa mfululizo, hali ni mbaya zaidi chini ya utawala wa kidikteta wa Magufuli.

Wakati huko nyuma hujuma nyingi dhidi ya vyama vyenu zilifanyika kwa siri, sasa zinafanywa waziwazi bila uoga. Magufuli amenuwia kuuwa vyama vyenu, na kama kuna anayedhani huu ni utani, arejee makala hii Oktoba 2020.

Magufuli anafanya kila awezalo ku-unmake miaka 26 ya mfumo wa vyama vingi vya siasa. Anafanya hayo waziwazi bila aibu wala uoga.

Alianza kwa kuzuwia shughuli zenu halali za kisiasa — mikutano na maandamano, akahamia kwenye kuviziba midomo vyombo vya habari, akazuwia matangazo ya bunge, akajenga utiifu wa kikondoo ndani ya chama chake, akaweka watu wake wa Kanda ya Ziwa katika kila sehemu muhimu — Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Jaji Mkuu, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Katibu Mkuu Hazina… orodha ni ndefu

Baada ya kujenga mfumo imara wa kuendesha nchi kidikteta, akahamia kwenye kuvibomoa vyama vya upinzani kwa kununua baadhi ya viongozi wa vyama hivyo. Lakini msichojua ni nini kinachkfanywa na baadhi ya hao walionunuliwa. Mkijihangaisha mtafahamu, lakini kwa kifupi tu, baadhi yao wameingizwa katika mfumo wa serikali, mahali penye kazi moja tu: kuuangamiza upinzani.

Baya zaidi, kabla ya kununuliwa, wanasiasa hao hupewa maelekezo ya kujenga mfumo wa usaliti ndani ya vyama vyenu, na muda huu ninapoandika kuna lundo la maoandikizi wanaohangaika kuviangamiza vyama hivyo kutoka ndani. Nnawajua baadhi ya wasaliti hao lakini ni jukumu lenu kuwabaini.

Nadhani kitu hatari zaidi kwa mustakabali wa vyama vyenu chini ya utawala huu wa kidikteta ni kutarajia miujiza, au kudhani Magufuli atabadilika. Wengi nwenu mnajipa matumaini kuwa “yana mwisho haya.” Naam, yanaweza kuwa na nwisho lakini what if mwisho huo ndo pia utakuwa mwisho wa vyama vyenu?

Kosa kubwa kabisa ni kupuuza umungu mtu alionao rais wa Tanzania, unaohalalishwa na katiba isiyoendana kabisa na mazingira ya mfumo wa vyama vingi. Nchi yetu ikiwa na rais dikteta, ataweza kutimiza matakwa yake kirahisi tu kwa vile kuna upenyo mwingi kwenye katiba unaomruhusu kufanya atakacho.

Kama katiba imeshindwa kumzuwia amwajibishe huyo mwanae mwenye makalio makubwa, kichwa empty Bashite, na kama katiba imeshindwa kumzuwia kumteua mtoto wa dada yake kuwa ndio mwidhinishaji wa pesa za serikali Hazina, na kama katiba imeshindwa kumzuwia aendelee kumtumia mlevi mbwa Kitwanga kwenye madili mbalimbali, mnategemea nini?

Kuna nchi moja jirani inanufaika na uwepo wa Magufuli madarakani. Na itafanya kila iwezalo kuhakikisha anadumisha utawala wake wa mkono wa chuma. Na kama katiba imeshindwa kuzuwia uwezekano wa kibaraka wa nchi nyingine kuwa kiongozi, mnatarajia nini?

Na kama katiba imeshindwa kuwafumbua macho Watanzania kuhusu yaliyojiri na yanayoendelea kujiri huko MKIRU, mnategemea nini?

Jana, CAG amewasilisha ripoti inayoonyesha kuwa licha ya Magufuli kujigamba kuwa anapambana na ufisadi, hali bado ni mbaya. Lakini kitu ambacho ripoti ya CAG haikukizungumzia ni ufisadi wa passport za kielektroniki ambao Magufuli anaufahamu lakini ameukalia kimya.

Ripoti ya CAG pia imekwepa kugusia masuala mengine yanayitatiza kama ununuzi wa bombadia na ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa huko Chato “kwa Bwana Mkubwa.”

Wasichoelewa Watanzania wengi ni kwamba ufisadi umerejea, na pengine zaidi ya ulivyokuwa zama za JK, ila sasa unafanywa kwa siri na wanufaika ni watu wa karibu wa “Bwana Mkubwa.”

Kuna watakaotulaumu tuliompigia kampeni Magufuli mwaka 2015. Ni haki yao kikatiba kutulaumu, lakini kabla ya kukimbilia kutulaumu, tutendeeni haki kwa kujihangaisha kufahamu sababu zilizopelekea kuacha kusapoti upinzani na badala yake kumsaidia mgombea wa CCM amshinde huyo wa upinzani.

Sitaki kutonesha vidonda lakini kosa kubwa kabisa la upinzani lilikuwa sio tu kumpokea Lowassa bali kumteua kuwa mgombea wa urais. In fact pengine kosw kubwa zaidi ni kuendelea kumwacha aangamize upinzani “ndani kwa ndani.” Mtapokuja kushtuka, itakuwa too late, lakini angalau makala hii itakuwa ipo kuwakumbusha kuwa “tuliwaonya.”

Binafsi nasikitishwa na jinsi Magufuli alivyokwenda kinyume kabisa na matarajio ya baadhi yetu tuliomnadi mwaka 2015. Hata hivyo, sijalaumu kuchukua uamuzi huo kwa sababu Upinzani “ulitufukuza” baada ya kumpokea Lowassa.

Na kwa vile nikishiriki kumnadi Magufuli, najiona mwenye kila sababu ya kumkosoa, licha ya ukweli kuwa kumkosoa kiongozi ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania.

Nihitimishe makala hii kwa kufanya mambo mawili: kwanza, kukiri kwamba tukio la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine wa ngazi za juu wa chama hicho jana, kuwekwa rumande na kisha kupelekwa mahakamani na “kugeuziwa kibao”+ “kubambikiziwa” kesi ya mauaji ya mpendwa wetu Akwilina, ambaye wote twafahamu ameuawa na jeshi la polisi kama alivyouawa huyo kijana wa Mbeya, limenisukuma kuwaandikia hii kuwatahadharisha kuwa mkiendelea kudhani huu ni mzaha basi upinzani upo njiani kuelekea kaburini.

Kama kasi ya Magufuli kuwanyanyasa kiasi hiki — amemfunga Sugu, alimfunga mbunge wangu Peter Lijuakali, akamweka jela Mbunge Godbless Lema kwa muda mrefu tu… na hapo sijagusia jaribio la kumuuwa Tundu Lissu, kuuawa kwa Kamanda Mashaka, Diwani Godfrey Luena na Katibu wa Chadema Kata ya Hananasifu Daniel John — hakutoshi kuwaamsha na kutambua “huyu mtu kadhamiria kutumaliza” basi nanyi mtakuwa washiriki katika dhamira yake hiyo ovu.

La pili ni kujibu swali ambalo pengine wengi wenu mnajiuliza hadi muda huu, kwamba “ah Bwana Chahali maneno meeengi bila kushauri tufanyeje.” Kuna short-term plans na long-term plans. Short-term plans ni pamoja na kuhakikisha maandamano ya amani yaliyopangwa kufanyika April 26 mwaka huu yanafanikiwa.

Mafanikio ya maandamano hayo yatapeleka ujumbe muhimu mno kwa Magufuli, Bashite na genge lao kuwa Watanzania wamechoshwa na yanayoendelea. Kama kuna anayehitaji hamasa kuhusu umuhimu wa nguvu ya umma kwa kutumia maandamano basi na arejee kilichojiri Ethiopia, taifa linaloendeshwa kwa mkono wa chuma lakini lililoshindwa kukabili nguvu ya umma hadi waziri mkuu aliyekuwa dikteta akalazimika kujiuzulu, na hatimaye taifa hilo limefanikiwa kupata Waziri Mkuu mpya kutoka kabila kubwa lakini linalonyanyaswa la Oromo.

Long-term plan ni pamoja na kudai mabadiliko ya Katiba kwa kila njia. Sambamba na hilo ni kumweka wazi Magufuli, ambaye hadi sasa bado ana sapoti kubwa tu kwa wanaoendelea kuamini kuwa anapambana na ufisadi. Laiti “waumini wake” watakapobaini kuwa “ah kumbe huyu nae ni walewale” basi huenda kilio cha kudai mabadiliko kikasikika hata kutoka ndani ya CCM.

Naomba nihutimishe barua hii kwa kurudia tena kuwapa pole kwa yote yanayowasibu. Japo natamani sana kusema “yana mwisho haya” lakini nachelea kuwa kusema hivyo ni sawa na kujidanganya iwapo hakuna mkakati dhabiti wa kuleta mwisho wa udikteta unaoendelea huko nyumbani.

Asanteni
 
Duh....
Nanukuu..

1. Majuzi nimepata taarifa kwamba msaada muhimu uliotolewa na serikali ya Israeli kwa “Kitengo” umeishia mikononi mwa “kitengo kingine” kinachoongozwa na Daudi Albert Bashite kwa ridhaa ya “babake” John Magufuli.

2. "Kuna nchi moja jirani inanufaika na uwepo wa Magufuli madarakani. Na itafanya kila iwezalo kuhakikisha anadumisha utawala wake wa mkono wa chuma. Na kama katiba imeshindwa kuzuwia uwezekano wa kibaraka wa nchi nyingine kuwa kiongozi, mnatarajia nini?"

Mwisho wa Kunukuu...
 
Naona mambo ya short term plan hapo.....
Hivi leo ndio tar 29
 
  • Thanks
Reactions: PNC
"Sheria mbalimbali si rafiki kwa vyama vya upinzani na, japo hili limepuuziwa kitambo, zimekuwa zikitoa mwanya kwa nchi yetu kujikuta inatawaliwa na dikteta, or to make things even worse, ikapata rais mwenye matatizo ya akili" Mwisho wa kunukuu. Hapo palipopigiwa mstari pamenikumbusha maneno ya James Lembeli:
image-jpeg.485820
 
Back
Top Bottom