Eneo la Somaliland linabadilika kuwa karata ya wanasiasa, badala ya eneo linalotakiwa kuendelezwa?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,014
1,038
1642994500589.png

Fadhili Mpunji

Katika siku za hivi karibuni imetokea hali ya ajabu katika siasa za eneo la Pembe ya Afrika, ambayo inafuatiliwa na jumuiya ya kimataifa. Hali ya kushangaza mgogoro wa ndani wa Somalia, au tunaweza kusema taabu ya watu wa Somalia sasa inaanza kuonekana kama ni neema ya wanasiasa wanaojitafutia madaraka na maslahi ya kisiasa. Hili limeotokea nchini Somalia, ambapo eneo la Somaliland sasa linaonekana kuendelea kuwa uwanja wa mchezo wa siasa hasi kwa baadhi ya wanasiasa wa ndani na nje ya eneo hilo.

Kimsingi hali ya Somalia kwa sasa bado ni tete, na Somaliland ni eneo la shirikisho la Somalia, bado si eneo lenye mamlaka kama nchi huru. Jumuiya ya kimataifa imekuwa ikifanya juhudi kwa muda mrefu sasa kutatua changamoto za amani, usalama na umoja wa kitaifa wa Somalia. Lakini matokeo ya hivi karibuni yaliyofanywa na baadhi ya wanasiasa wa Somaliland kwa kushirikiana na wanasiasa wa nje ya Somalia, zinaonekana kuhujumu juhudi hizo na hata kuleta utatanishi ambao mwisho wake unaweza kuwa mbaya.

Ikumbukwe kuwa mwezi Februari mwaka 2020 ofisa mmoja wa Somaliland alikwenda Kisiwani Taiwan na kukutana na ofisa wa mambo ya nje wa kisiwa hicho, na kusaini makubaliano ambayo kimsingi yanakwenda kinyume kabisa na sheria za kimataifa na hata msimamo wa Umoja wa Afrika. Hivi karibuni pia ujumbe wa baraza la wawakilishi la Marekani ukiwa na maseneta na wawakilishi ulikwenda Somalia kwa kile walichokiita kuangalia hali halisi ya eneo hilo, ili kujua kama eneo hilo litaifaa Marekani. Ziara hii inafuatia ziara ya kutafuta “kiki” iliyofanywa na wanasiasa wa Somaliland nchini Marekani waliokwenda kutafuta kuongea na wabunge wa Marekani, wakisema wao na Marekani wana adui mmoja ambaye ni China (bila kutaja sababu ya maana ya wao kuwa adui wa China) na kusema wanapambana na China na nguvu ya ushawishi ya China barani Afrika, kwa hiyo wanastahili uungaji mkono wa Marekani.

Umoja wa Afrika umekuwa na msimamo wazi tangu kwenye miaka ya 90, kuwa baadhi ya wanasiasa wa eneo la Somaliland ni wafarakanishaji wenye lengo la kulitenga eneo hilo kutoka Somalia, na umekuwa ukihimiza tofauti kati ya jimbo hilo na serikali kuu ya Somalia zitatuliwe kwa njia ya mazungumzo. Na umekuwa ukipinga uingiliaji unaofanywa na baadhi ya nchi za Afrika au za nje ya Afrika unaoleta utatanishi kwenye utatuzi wa changamoto za Somalia.

Kwa sasa nchi nyingi za Afrika zinatambua kuwa baadhi ya nchi za magharibi zimekuwa na tabia ya kuwatumia wanasiasa fulani wa nchi za Afrika na kuwatelekeza baada ya nchi hizo kufikia malengo yao, au kuzitumia nchi fulani za Afrika na hatimaye kuzitelekeza baada ya kufikia malengo yao. Historia imeonyesha kuwa katika kipindi cha vita baridi kuna baadhi ya wanasiasa walionekana kuwa “wapendwa” wa nchi za magharibi, lakini baada ya vita baridi kwisha walitupwa na wengine kukumbwa na mwisho mbaya. Bahati mbaya ni kuwa baadhi ya wanasiasa wachanga ni kama wamesahau somo hilo, au wameamua kupuuza kwa makusudi kwa maslahi yao ya kisiasa ya muda mfupi.

Ukweli huu umethibitishwa na kauli iliyotolewa na ujumbe uliotolewa baada ya ziara ya wabunge watano waandamizi wa Marekani ambao ni wajumbe wa kamati ya mambo ya nje ya bunge la Marekani. Walichosema baada kurudi kutoka kwenye ziara yao ni kuwa, “wanaamini kuwa eneo la Somaliland lina thamani kwa Marekani kukabiliana na nguvu ya ushawishi ya China barani Afrika”. Hakuna aliyemzungumzia hali ya maisha ya watu wa eneo hilo, au mahitaji kwa ajili ya maendeleo ya eneo hilo. Ni wazi akili na mawazo ya wabunge hao ni kufanya eneo hilo kuwa karata watakayoicheza kwenye mvutano wao na China, na baada ya mchezo kugonga mwamba au kwisha, litatupwa.
 
China anafanya uwekezaji Somali mogadishu... mtafute balozi wa china somalia huko twitter utaelewa, na somalia ni nchi tajiri hivyo ni kama wanaigombania pamoja na fujo zilizopo... sasa marekani yeye anafahamu utamu uliopo somalia hivyo hawa wa somaliland ni kama wana chagiza vita ya mataifa mawili china na mmarekani ili wao malengo yao ya kujitenga na kupata mamlka kamili yatimie kwa mgongo wa mmarekani kama ilivyo tokea kwa south sudan

ni ujanja unao ambatana na uroho bila kutaka kujua hatima ni nini ya tamaa zao
 
China anafanya uwekezaji Somali mogadishu... mtafute balozi wa china somalia huko twitter utaelewa, na somalia ni nchi tajiri hivyo ni kama wanaigombania pamoja na fujo zilizopo... sasa marekani yeye anafahamu utamu uliopo somalia hivyo hawa wa somaliland ni kama wana chagiza vita ya mataifa mawili china na mmarekani ili wao malengo yao ya kujitenga na kupata mamlka kamili yatimie kwa mgongo wa mmarekani kama ilivyo tokea kwa south sudan

ni ujanja unao ambatana na uroho bila kutaka kujua hatima ni nini ya tamaa zao
sure mkuu
 
Back
Top Bottom