SI KWELI Eneo la Kihistoria lililogunduliwa fuvu la binadamu wa kwanza (Olduvai Gorge) lipo Kenya

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Habari,

Kuliwahi kutokea madai yakisema kuwa Olduvai Gorge ipo nchini Kenya. Rosemary Odinga alisema Olduvai Gorge ipo Kenya, Tazama video hapa chini:


Je, mnaweza kutusaidia kuweka kumbukumbu sawa hili?

1707451335400.png
 
Tunachokijua
Olduvai Gorge ni eneo la kihistoria la kijiolojia. Ni mahali ambapo mabaki ya kale ya binadamu na wanyama wengine wanaopatikana, ambayo yanatoa ufahamu mkubwa juu ya mageuzi ya binadamu na historia ya kale ya bara la Afrika. Eneo hilo limejulikana kwa ugunduzi wa mabaki ya kale ya wanadamu, kama vile mifupa ya watu wa kale na vifaa vya mawe ambavyo vinaonyesha mchakato wa mageuzi ya binadamu.

Katika Eneo hili liligunduliwa na Mwanahistoria Dkt. Louis Leakey na Mary Leakey mwaka 1959 waligundua fuvu la kichwa cha Binadamu wa Kale ( Zinjanthropus) ambaye alisadikiwa kuishi miaka zaidi ya Milioni mbili iliyopita.

Mnamo mwaka 2015 Binti Mkubwa wa Raila Odinga (Rosemary Odinga), alipokuwa akizungumza mbele ya vijana zaidi ya 1,000 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa huko Jiji la New York tarehe 18 Agosti 2015, alitoa kauli zilizoibua taharuki kwa raia wengi wa Afrika Mashariki hasa Tanzania baada ya kusema Olduvai Gorge inapatikana nchini Kenya Tazama Video hapo Juu.

Katika mkutano huo Rosemary Odinga alisema:

"Hadi sasa nimefundishwa kuwa tanga ya kwanza ilipatikana Kenya, mahali panaitwa Olduvai Gorge na Kenya ni mahali pa asili ya binadamu. Hivyo japokuwa kila mtu katokea nchi tofauti, kwa upande wangu nawachukulia kama ninyi nyote ni Wakenya."

Je, kuna ukweli wa madai hayo?
JamiiCheck imefuatilia madai haya kwa kupitia vyanzo vya Kijiographia na Kihistoria imebaini kuwa madai hayo ya Rosemary Odinga hayana ukweli.

Katika vyanzo vya kijografia JamiiCheck imepitia Ramani ya Afrika Mashariki ili kujiridhisha Olduvai Gorge ilipo lakini ramani zote zinaonesha Olduvai Gorge ipo Tanzania maeneo ya Ngorongoro na sio Kenya kama Rosemary Odinga alivyodai. (Tazama ramani hapa Chini):

ramani-inayoonesha-ilipo-olduvai-gorge-jpg.2898276

Ramani inayoonesha ilipo Olduvai
Kwa upande wa vyanzo vya kihistoria JamiiCheck imepitia vyanzo mbalimbali vya kihistoria ikiwamo Makala Maalumu iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais wa Tanzania ambapo katika ukurasa wa 11 Olduvai Gorge inapatikana katika Ngorongoro Kreta mkoani Manyara nao Mwananchi mwaka 2017, BBC Swahili 2019 na Millard Ayo wanaelezea Historia ya Olduvai Gorge huku wote wakibainisha kuwa eneo hilo lipo upande wa Tanzania. Mathalani Millard Ayo katika andiko lake anaeleza:

Olduvai Gorge ni eneo la kihistoria linalopatikana katika Eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha nchini Tanzania.
Eneo hili ni bonde lenye utajiri mkubwa sana wa historia ya chimbuko la asili ya mwanadamu.
Katika Eneo hili ambalo linapatikana nchini Tanzania pekee, Mwanahistoria Dr. Lois Leakey na Mary Leakey mwaka 1959 waligundua fuvu la kichwa cha Binadamu wa Kale ( Zinjanthropus) ambaye alisadikiwa kuishi miaka zaidi ya Milioni mbili iliyopita.


Zaidi ya hayo JamiiCheck imefuatilia sakata hili na kubaini kuwa mwaka 2016 makala ya The Standard ilieleza kuwa Rosemary Odinga alijitokeza na kuomba radhi kwa kupotosha umma kuhusu ilipo Olduvai Gorge. Katika andiko hilo The Standard wanaeleza:

Binti mkubwa wa Rosemary Odinga, ameomba radhi kwa Watanzania baada ya kusema kwamba eneo la kihistoria la Olduvai Gorge liko Kenya.
Marianne Mwiki, Mtanzania, alizindua ombi mtandaoni siku ya Jumanne kumlazimisha Rosemary kuomba msamaha hadharani.

Kwanini Rosemary Odinga aliamua kusema hayo kwa makusudi?
JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa ni tabia ya Wakenya wengi kwenye mitandao kujihusisha na watu mashuhuri pamoja na vivutio vya kiutalii ili kuwavutia wageni kutembelea katika nchi yao. JamiiCheck imebaini mambo mengine ambayo ya Tanzania ambayo Wakenya wamejitangazia yapo kwao kama vile Mlima kilimanjaro.

Hivyo, kutokana na vyanzo hivyo vilivyopitiwa hapo juu JamiiCheck imejiridhisha kuwa uvumi humo ulioanzishwa na kiongozi huyo hauna ukweli.
mnagombana tu waafrika lakini mgunduzi ni mzungu, angalau mtanzagiza angegundua hilo fuvu ningeelewa logic yenu …
 
Tanzania 255(BongoLand) ama kweli tumebarikiwa vitu vingi Sana Am really proud of BongoLand
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom