Emmanuel Mbasha, ni nani alikuroga?

Emmanuel Mbasha, ni nani alikuroga?

Joined
Aug 13, 2015
Posts
94
Reaction score
75
Ndoa na mapenzi ni mambo ambayo mara nyingi huwa hayaingiliwi,yametawaliwa na msemo kuwa'mapenzi ni wawili tu akiongezeka wa tatu ni mchawi',lakini pia huwa inapobidi watu wanaingilia hasa pale wahusika au mhusika mmoja anapovuka mstari mwekundu,

Hakuna asiyejua sakata la mbasha na mkewe flora,huyu jamaa alituhumiwa kumbaka shemeji yake,mmoja wa shahidi muhimu upande wa mashtaka alikuwa mkewe flora,ina maana flora alitaka mumewe aozee jela,na kweli wakati kesi ikiendelea flora alienda mahakamani na kutoa ushahidi wa kumkandamiza mumewe ili afungwe,

Mungu mkubwa hukumu ilipotoka mbasha kashinda kesi na sasa yupo huru,kilichoshangaza umma wa watanzania ni kauli ya mbasha kuwa bado anampenda sana mkewe flora na yupo tayari kuendelea kuishi nae,najiuliza kwa vitendo vyote alivyotendewa na huyo mwanamke bado anampendea nini?Huyu jamaa alirogwa?

Amerukwa na akili? Unampendaje mwanamke aliyetaka uozee jela? Watu wa karibu na mbasha msaidieni huyu jamaaa maana anakoelekea ni kutafuta kifo,msimcheke pls msaidieni tu.
 
upendo wa kweli huvumilia, hauhesabu mabaya, hauna sababu, husahau yote, hauishi moyoni milele, hauna unafiki!!! yereeeee uwiiiiiiii Mbasha amependa kikweeee kikweliiiii

Chezea maloveee weyeee acha kabisaaaa
 
kama kuvumilia kunahusisha na kiwango hiki cha mbasha basi msamiati kama TAFAKARI ufutwe kwenye kamusi. huyu mbasha inaonekana si mapenz ila nje ya frola hana maisha. kiwango cha juu kabsa cha utegemezi.
 
The counsellor Kama huna moyo wa kusamehe & kuvumilia ni bora usioe kabisa.
 
Ya Ngoswe mwachie Ngoswe mkuu.

Hakikisha unalinda kadi yako ya kura na siku ikifika ukawapigie wagombea wa UKAWA kwa mustakabali mzuri wa taiga letu.

Mkuu kweli aisee. Ila naona hapo kwenye taiga sijui ka tupo pamoja
 
Hayo waachie wenyewe,nakukumbusha october 25 weka tick kwenye picha ya magufuli.
 
the Counseller

Mhariri pls, hii thread ikapambe kurasa za mmu!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mbona umeandika kwa uchungu sana?, wewe ulitaka amuache mkewe?, unasema kwamba Flora alitaka aozee jela wewe ulitaka Fora afanye nini wakati aliyedaiwa kubakwa ni mdogo wake?, ungekuwa wewe ungefanya nini?. Flora alitimiza matakwa ya kisheria na ndo maana baada ya Mahakama kuona hana hatia Flora alimpongeza na akasema bayana kuwa yupo tayari kurudiana na mumewe. Mimi nilichojifunza hapa ni kwamba kama Fora angemtetea Imma bila suala hili kupelekwa katika vyombo vya sheria angetengeneza mgogoro mkubwa na familia yake. Kwa maoni yangu mimi hawa wanandoa kama wamesameheana ni jambo jema sisi tulio pembeni tusichochee kuni wakati inawezekana ndoa zetu zina matatizo zaidi ya hayo.
 
Asimpende mchezo????
Mpunga wote anaoringia mjini source ni flora...... kitegauchumi chake muacheni

Anyway mapenzi huwa ya wawili wakigombana wengine tubebe majembe tukalime
 
Flora ni mjukuu wa marehemu Askofu Mkuu Moses Kulola aliyekuwa muhubiri maarufu wa kimataifa, nafikiri ni Msukuma
Nilidhani nae ni wa kule inakosifika katerero
 
Ndoa na mapenzi ni mambo ambayo mara nyingi huwa hayaingiliwi,yametawaliwa na msemo kuwa'mapenzi ni wawili tu akiongezeka wa tatu ni mchawi',lakini pia huwa inapobidi watu wanaingilia hasa pale wahusika au mhusika mmoja anapovuka mstari mwekundu,

Hakuna asiyejua sakata la mbasha na mkewe flora,huyu jamaa alituhumiwa kumbaka shemeji yake,mmoja wa shahidi muhimu upande wa mashtaka alikuwa mkewe flora,ina maana flora alitaka mumewe aozee jela,na kweli wakati kesi ikiendelea flora alienda mahakamani na kutoa ushahidi wa kumkandamiza mumewe ili afungwe,

Mungu mkubwa hukumu ilipotoka mbasha kashinda kesi na sasa yupo huru,kilichoshangaza umma wa watanzania ni kauli ya mbasha kuwa bado anampenda sana mkewe flora na yupo tayari kuendelea kuishi nae,najiuliza kwa vitendo vyote alivyotendewa na huyo mwanamke bado anampendea nini?Huyu jamaa alirogwa?

Amerukwa na akili? Unampendaje mwanamke aliyetaka uozee jela? Watu wa karibu na mbasha msaidieni huyu jamaaa maana anakoelekea ni kutafuta kifo,msimcheke pls msaidieni tu.

Anataka kulelewa tuu huyo hana lolote!mario huyo
 
Hakuna mtu mbaya au mzuri..wote ni waathirika wa roho ziishizo ndani yetu.
 
Back
Top Bottom