The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,355
- 17,321
Huduma ya internet ya bei nafuu na yenye kasi kubwa ya Bwana Elon Musk ya Starlink sasa inapatikana Msumbiji.
Sasa karibu nchi zote zinazoizunguka Tanzania zina Starlink. Tanzania tunasubiri Elon Musk aje ajenge ofisi Tanzania kwanza.
Huduma ya Starlink inanunuliwa kwa dollar 500 sawa na milioni 1.2 ila hiyo pesa unarudishiwa kwenye matumizi ya kila mwezi hadi iishe.
Huduma ya Starlink unapewa Terabyte 1 kwa shilingi elfu 80 kwa mwezi. Ukiimaliza kabla mwezi haujaisha utapata huduma ya internet kwa siku zilizobaki ila kwa speed ndogo sio kasi sana. Kwa maana nyingine huduma ya internet ya Starlink ni unlimited.
Kwa sasa Vodacom wanauza GB moja kwa TZS 2,083.33, yani karibu elfu 2 na mia moja
Kwa GB 1,024 ambayo ni Terabyte 1 utapata kwa (2,083x1,024) TZS 2, 133, 333.33(Milioni 2 na laki 1 elfu 33).
Huduma ambayo tungeweza kupata kwa elfu 80 sasa tunaipata kwa milioni 2 na bado speed ni ya kobe. 5G ama 4G iko kwenye makaratasi ila uhalisia tunapata speed ya 3G.
Nape anatukosea sana.
View: https://twitter.com/elonmusk/status/1743364627138814108?s=19