Licha ya tangazo la kufunga shule na El Nino, shule ya Carmelite imepanga kuendelea na masomo

Licha ya tangazo la kufunga shule na El Nino, shule ya Carmelite imepanga kuendelea na masomo

Umsumbalembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
946
Reaction score
873
Narejelea Waraka wa Wizara ya Elimu Na. 3 wa mwaka 2026, uliotolewa Oktoba 2, 2026, unaoelekeza kuwa shule za awali, msingi na sekondari zifungwe Novemba 13, 2026, kwa lengo la kulinda usalama wa wanafunzi, walimu na wafanyakazi.

Hata hivyo, inashangaza kuona Shule ya Carmelite ikipanga kuendelea na masomo licha ya maelekezo hayo ya Wizara.

Kwa kuwa shule binafsi zinasajiliwa na kusimamiwa chini ya mfumo wa elimu wa Serikali, ni kwa msingi gani shule hii inajipa mamlaka ya kupuuza waraka huo? Je, shule binafsi hazipaswi kuzingatia maelekezo rasmi yanayotolewa na Wizara ya Elimu?
 
Wewe ni mwalimu au mzazi mwenye mtoto iyo shule? Kama mwalimu, ikifika Tarehe iyo usiende. Kama mzazi nadhani unajua cha kufanya.
 
Narejea Waraka wa Wizara ya Elimu namba 3 wa mwaka 2026 uliotolewa tarehe 2.10.2026 ukihusu ufungaji wa shule za awali,msingi na Sekondari kuwa ni tarehe 13.11.2026.
Sababu ya msingi ikiwa ni kulinda usalama wa wanafunzi,walimu na wafanyakazi.
Ni jambo la kustaajabisha kwa Shule hii ya Carmelite kutaka kuendelea na masomo bila kujali waraka huu!
Ikiwa shule binafsi zinasajiliwa na kusimamiwa chini ya mfumo wa elimu wa serikali,kwanini shule hii inajipa ruhusa ya kupuuza waraka huu?k
Kuna tatizo lolote mtoto kuendelea kusoma? Uko mkoa gani?
 
Narejea Waraka wa Wizara ya Elimu namba 3 wa mwaka 2026 uliotolewa tarehe 2.10.2026 ukihusu ufungaji wa shule za awali,msingi na Sekondari kuwa ni tarehe 13.11.2026.
Sababu ya msingi ikiwa ni kulinda usalama wa wanafunzi,walimu na wafanyakazi.
Ni jambo la kustaajabisha kwa Shule hii ya Carmelite kutaka kuendelea na masomo bila kujali waraka huu!
Ikiwa shule binafsi zinasajiliwa na kusimamiwa chini ya mfumo wa elimu wa serikali,kwanini shule hii inajipa ruhusa ya kupuuza waraka huu?
huwa wajinga sana hawa ila hakuna shida wakiendelea na masomo wewe toa taarifa kiwakute ujinga wa hivi hatutaki
 
Kwani si walisena ni kuongezeka kwa joto,hiyo mvua inatoka wapi?
 
Kwani si walisena ni kuongezeka kwa joto,hiyo mvua inatoka wapi?
Kitaalamu kuongezeka kwa joto baharini kunasababisha more evaporation so bahari inatoa mvuke mwingi kwenda kuganda kuwa mawingu juu then inashuka kama mvua kubwa inayoleta madhara
 
Kitaalamu kuongezeka kwa joto baharini kunasababisha more evaporation so bahari inatoa mvuke mwingi kwenda kuganda kuwa mawingu juu then inashuka kama mvua kubwa inayoleta madhara
Mhhhhh unaweza kufikiri tofauti na haya ya kuambiwa ?
 
Kitaalamu kuongezeka kwa joto baharini kunasababisha more evaporation so bahari inatoa mvuke mwingi kwenda kuganda kuwa mawingu juu then inashuka kama mvua kubwa inayoleta madhara
Mamlaka ya hali ya hewa nchini haikusema hivi tena iliwakana waliotoa taarifa za uwepo wa mvua
 
Back
Top Bottom