JACKLINE CELESTINE KITALE
Member
- Jul 29, 2021
- 81
- 158
Jamii yetu imechukulia mahusiano ya kimapenzi kuwa ni kitu kibaya Sana na hata tumelelewa kuamini ya kuwa mapenzi au hisia za kimapenzi ni kosa la jinai. Mfano mzuri ni mashuleni, ukiwa na mahusiano na mwanafunzi mwenzio inakuwa kosa kuu ambalo unaweza hata kufukuzwa shule.
Sisemi kwamba wanafunzi waruhusiwe kuwa na mahusiano, hapana, lakini kabla ya kuwa laumu tujiulize wenyewe kama tulishawapa wanafunzi hawa elimu ya mahusiano na mapenzi.
Majumbani mwetu hawaongelei kabisa kuhusu mahusiano, shuleni ndo kabisa, na kwenye nyumba za ibada wanasema tusubiri mpaka ndoa, sawa sikatai Ni vizuri lakini ndo itamaanisha kwamba tusiwafundishe kuhusu Jambo hili.
Inajulikana katika umri fulani watoto huanza kubadilika kimaumbile na kubalee. Na katika muda huo na kuendelea huvutiwa na vijana wa jinsia tofauti. Na mara kwa mara hupata mihemko ya kimapenzi. Sasa bila kuwa na elimu kutoka kwa wazazi, walezi au walimu unategemea huyu kijana tafanyaje?
Unakuta mtoto anabaniwa na kuchungwa Sana, lakini hapewi elimu, sasa ikifika muda anapopata uhuru, mfano mzuri vijana wa vyuoni, ndo unasikia amepewa mimba, na magonjwa mengine ya zinaa. Hii Ni kwasababu ameachiwa sasa, hamna anayemwambia wala kumzuia kufanya kitu, na kwasababu hana elimu ya mahusiano na hawezi kuongea na wazazi wake anakimbilia kwa marafiki na makundi mengine na pia mitandano ya ngono. Sasa hapo unategemea kutakuwa na matokeo chanya kweli?
Kiukweli nimeona rafiki zangu wengi wakipotea, mwingine alikuwa chuo, lakini akaishia njiani baada ya kupata mimba na kuzaa mtoto. Hii yote Ni kwasababu jamii yetu inaogopa kuongelea mambo ya mapenzi na watoto wakiamini ya kuwa watatuharibu, lakini ukweli ni kwamba, “asiyefunzwa na mamaye ufunzwa na ulimwengu” wazazi tukishindwa kuwaelimisha watoto wetu, wataenda kuitafuta hiyo elimu mahala pengine na haitakuwa sahihi. Mwishowe itawaletea matatizo makubwa sana.
Kwahiyo tujifunze kutokana na makosa na tuwaelimishe Watoto wetu au hata ndugu zetu.