Elimu ya Bure kwa Wasafirisha Maiti zinazogoma kwenda Kuzikwa Kwao ili zisikudhuru kwa Ajali mbaya barabarani

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
1. Chukua Jiwe Dogo rusha upande wa mbele lilipo Jeneza Marehemu wako hata kama hakutaka Kusafirishwa Kwao atafika tu na wala hamtadhurika njiani na Gari yenu haitopata Ajali.

2. Chukua Jiwe Kubwa liweke Juu ya Jeneza hapo mnafika nae Kijijini Kwao Salama na wala hamtopata Jambo lolote baya Njiani hasa Ajali.

3. Mkimuingiza Marehemu ndani ya Gari lenu au lile mliloliandaa hakikisheni mnaanza Kuingiza ule upande wa Miguu ( na siyo Kichwa ) na hapo atafika na hakuna ambaye atadhurika au Ajali mbaya kutokea.

Atakayefuatisha hivi nilivyoelekeza hapa na bado Marehemu akakataa kwenda Kwao nakuruhusu Unidai Kiasi chochote kile cha Pesa na nitakupa kama ipo Mfukoni.
 
Au wamtumie mtani akaongee na marehemu ikibidi amtukane kabisa aache ujinga

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Kuna dogo mmoja aligoma mama ake asimzike basi bana kama unavyojua mipango ya mungu dogo akafariki kimbembe kumsafirisha kwao akazikwe safari ilitaka ituuwe gari ikaaribika njiani maiti ikatangulia tukabaki ma mama porini akuna ata gari moka usiku kufika msibani tukakuta washazika kitambo.
 
Kwani jiwe linakuwa na uhusiano gani na marehemu kiroho?

Na nini tafsiri ya kumtupia jiwe au kumkalishia jiwe kubwa kwenye jeneza linalomfanya marehemu aweze kutii hata kama si kwa hiari yake?

Je, unapomgeuza aangalie alipotoka(kwa maana ya uelekeo wa kichwa) na sipo anapokwenda unakuwa umelenga nini?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom