Kama kweli ushirikina ndio sababu kubwa ya ajali nchini Tanzania basi nitasafiri tu kwa miguu!

GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
29,926
Likes
37,207
Points
280
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
29,926 37,207 280
Za Jumapili waheshimiwa Wapendwa na natumai nyote mmekuwa na siku murua kabisa huku mkitafakari ni jinsi gani mtainza wiki mpya ya Kesho huku wengine mkiwa mmeishiwa kabisa Hela na wengine kuchunwa kisawasawa na wengine mkiwaza ni jinsi gani sasa mtakuwa mnawakwepa wale mliowakopa ili tu msheherekee vizuri Siku Kuu iliyokwishamalizika ya Eid. ( Msijali nimechomekea tu muanze kutabasamu kwanza kabla ya baadae kuja kulia kwa ninachowaletea hapa chini )

Wapendwa tokea siku ya Ijumaa tarehe 8 hadi jana Jumamosi tarehe 9 niliamua kuungana na Wenzangu kadhaa ambao kiukweli tumekuwa tukikerwa sana na hizi ajali zinazozidi kutokea hapa nchini kwetu Tanzania kufanya UTAFITI mdogo ambao tulihusisha Vituo vikuu vinne vya Mabasi ya Mikoani cha Dar es Salaam, Arusha, Mbeya na Mwanza na nawashukuru sana wale wote waliotudhamini kwa suala zima la usafiri wa Ndege maalum ya kukodi kuruka katika hiyo mikoa tajwa na pia kwa malazi kwani ninaamini haya majibu tuliyoyapata yanaweza yakaasisi tatizo zima ambalo litatusaidia kujua nini cha kufanya ili kujiokoa au kumaliza tatizo.

Katika UTAFITI wetu huu mdogo tuliweza kuwahoji sana Madereva wa haya Mabasi na swali tulilowauliza lilikuwa ni KWANINI SIKU HIZI KUNA AJALI NYINGI NA AMBAZO NI ZA KIZEMBE SANA HAPA NCHINI TANZANIA TOFAUTI NA MIAKA YA NYUMA?

Wapendwa yafuatayo ni majibu ya 90% ya hao Madereva tuliobahatika kuwahoji baada ya kukutana nao katika hiyo Mikoa ambayo naomba niyawakilishe kwenu bila kuongeza au kupunguza chochote:

  1. Wakubwa ( wakimaanisha sisi Watafiti ) sisi Madereva tunasikitika mno pale ambapo kila inapotokea tu ajali lawama zenu zote mnatuletea sisi wakati ukweli ni kwamba WAMILIKI wetu wanayafanyia mno mambo ya KISHIRIKINA haya Mabasi yao na ukikataa kile kinachofanyika basi unaambiwa ukabidhi funguo hivyo sisi hukubaliana na matakwa yao ilimradi familia zetu zisilale njaa.
  2. Wakubwa inapoelekea huko mbele kuna siku tutasema UKWELI wote kwani sisi Madereva hasa wa hapa Ubungo huwa tunabahatika kabisa usiku wa manane kukutana na WAFANYABIASHARA wakubwa tu na VIONGOZI wakubwa wa KISIASA hapa nchini wakija kufanya mambo ya ajabu ya KISHIRIKINA pale katika geti la kuingilia na hasa hasa pale mataa Ubungo kwani kuna muda hawa Watu huja wenyewe na wakijua kuwa tumewagundua basi hutupa PESA nyingi tu za kutufanya tusiseme lolote.
  3. Wakubwa Mimi binafsi ni Dereva wa Basi la Dar - Mwanza lakini kila nikianza tu safari yangu Bosi wangu hunipa kitu fulani kikiwa katika mfuko na kunielekeza kuwa nikifika tu maeneo ya Morogoro na Singida basi nikirushe na nitamke neno " kula chakula chako " na nimekuwa nikifanya hivi kwa muda kidogo ila Magari ya wenzangu tu ndiyo hupata ajali ila la kwangu hapana na Bosi wangu ananipenda kupita hata Wanafamilia wake.
  4. Wakubwa huyu hapa ni Dereva wa ruti za Dar - Mbeya hebu muulizeni ni kwanini kila akiwa anatoka Mbeya au Dar kuna akina Mama huwa anakabidhiwa asafiri nao kisha akifika Kituo fulani awashushe na kapewa SHARTI la kutowasemesha chochote wakiwa wamepanda humo.
  5. Wakubwa sisi Madereva wenyewe hatupendani kwani wengi wetu kutokana na ugumu wa maisha na kuwa na roho mbaya ya wivu huamua tu KUROGANA ili Magari yetu yapate ajali TUFE kabisa au tupate ULEMAVU wa kudumu kisha wakabidhiwe wao Magari kuendesha. Kama huamini fanyeni UKAGUZI wa ghafla hapa mtagundua kuwa kila Dereva hapa AMEVAA HIRIZI au AMEWEKA HIRIZI yake chini ya kiti chake yote hiyo ikiwa ni moja ya KINGA yake. Huyu Mzee hapa kila akisafiri akifika maeneo ya KITONGA lazima tu ataona Watu wanakatisha na JENEZA na nakumbuka kuna siku aliwahi kuwakwepa na Basi lake likapinduka na kuja kuangalia nje akakuta wale Watu hawapo ila tokea nae aende kwao Kigoma siku hizi akikutana tu na hiyo hali yeye hunyoosha tu na kuwagonga kwani wale huwa si Watu kweli bali ni MAJINI.
  6. Wakubwa kuna Abiria wengine nao hakika ni WASHIRIKINA sana kwani wapo wengine ambao safari zao ni za kutoka au kwenda kwa Waganga Mikoani ambapo wakiwa huko hupewa Dawa na kutakiwa kufanya KAFARA la DAMU hivyo wengi wao huamua kuingia na hizo Dawa " Ndumba " zao katika haya Mabasi ambapo ndani ya muda fulani Basi huanguka na kusababisha ajali mbaya. Kwa mfano kuna ajali moja tuliikuta maeneo ya Mwanga hivyo ikatubidi tusimame na kutoa msaada ambapo kuna baadhi ya Maiti kama tatu hivi wakati tunawabeba tuliwakuta wana yai mfukoni limepakwa rangi nyeusi, mwingine tukamkuta mfuko wake wa Suruali kuna nyoka mdogo na mwingine tukakuta ana hirizi kubwa kabisa.
  7. Wakubwa labda tu leo tuwapeni SIRI kubwa ambayo hamuijui ambapo mkisikia tu ajali yoyote ya Basi imetokea halafu mkasikia Dereva au Madereva wamepona basi hapo jueni 100% kuwa ni NGUVU YA KISHIRIKINA na Dereva huwa ameshajua kwani haya Mabasi yetu mengi usiku kabla ya Safari kuanza kule mbele ( kwenye Kichwa tu ) huoshwa na ama Maji yaliyooshea Maiti au Damu ya Kondoo na endapo mkisikia tu ajali imetokea halafu Dereva au Madereva wote wamekufa hapo hapo basi jueni kuwa MADEREVA wenzao wamewafanyia kitu mbaya kwani katika hii Kazi kuna fitina nyingi sana.
Wapendwa japo kuna sababu zingine hawa Madereva walizitoa kama ubovu wa barabara, uzembe upande wa askari wa barabarani na tatizo la magari yao kutofanyiwa service mara kwa mara ila kama nilivyobainisha hapo juu wengi wao walitoa hizo sababu saba ( 7 ) nilizoziorodhesha hapo juu na kusema kuwa dunia sasa imekwisha na Watu wanaendekeza sana masuala ya USHIRIKINA katika kujipatia riziki tofauti na zamani ambapo Watu walikuwa wanajituma huku wamkimwomba mno Mwenyezi Mungu.

Ni hayo tu Wapendwa na sijui nyie kama Wataalam, Wasomi na Wajuvi wa mambo mbalimbali hizo sababu zao hapo juu mmezipokeaje na labda nini kifanyike.

Karibuni na muwe na Jumapili njema na tulivu ila binafsi nadhani itabidi tu sasa niwe tu nasafiri kwa miguu hadi Vijijini kwetu Kyaka Nkunde na Ikupilipa Nkoba kwani " NIMEOGOPA " sana na najuta hata kwanini nilienda kufanya huu UTAFITI kwani umenifanya sasa nikisikia tu Rafiki yangu au Ndugu yangu yoyote anasafiri basi " nalia " kidogo kisha ndiyo namtakia safari njema!

The Boss

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Messages
37,832
Likes
23,139
Points
280
The Boss

The Boss

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2009
37,832 23,139 280
Ushirikina ndo unaowafanya waendeshe kwa spidi?
ushirikina ndo unaowafanya waendeshe kwa kuhama hama kwa mbwembwe wakikutana?
ushirikina ndo unawafanya wajaze abiria wengi kuliko kiasi
ushirikina ndo unawafanya wabadili siti za magari na kuongeza idadi ya siti?
ushirikina ndo unaowafanya wahonge mizani na trafiki?
 
R

runemo

Member
Joined
Apr 1, 2016
Messages
86
Likes
59
Points
25
R

runemo

Member
Joined Apr 1, 2016
86 59 25
Selikali ingewaamuru hao wamiliki wa mabasi waunde kampuni hayo yote yasingetokea,kuliko kila mtu kufanya biashara kivyake,nazani hilo lingesaidia kupuajali ajali
 
Richard

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Messages
9,737
Likes
6,438
Points
280
Richard

Richard

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2006
9,737 6,438 280
Hizo sababu 1-7 ni kibwagizo tu.

Madereva wengi hawana elimu tosha ya uendeshaji mabasi na hawapimwi kuangalia ufanisi, uzoefu na afya zao kiakili na hata leseni zao inawezekana wanabadilishana.

Wenye mabasi hawayapeleki mabasi yao kwenye kufanyiwa service and maintenance ambapo inatakiwa kila baada ya safari mbili kama sikosei.

Matairi ya mabasi mengi ni yale yaliyotumika kutoka nje ya nchi, hivyo TBS kupitisha yatumiwe bila uchunguzi wa kina.

Kukosekana kwa vitumo maalum vya huduma (service stops) kwa wasafiri wa mabasi na madereva angali kupumzika kila baada ya masaa mawili au matatu wawapo safarini.

Kukiwa na "service stops" abiria watachuma dawa, kupunguza uzito, kupumzika kwenye viti, kula, kutulia kiakili na hiyo ni pamoja na madereva wa mabasi.

Hakuna "control room" na supervisors kuhakikisha usalama na performance ya madereva hivyo mabasi kuendeshwa kiholela.

na matatizo mengine mengi tu ukiondoa hayo ya ushirikina.
 
MO11

MO11

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2014
Messages
16,345
Likes
20,075
Points
280
MO11

MO11

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2014
16,345 20,075 280
kipindi kile mabasi yanapaki mnazi mmoja wamiliki wa mabasi (mfano njia yetu njombe) wanafika saa nane wanasubiri basi la kwanza kutoka njombe dereva wa kwanza anapokelewa kama shujaa kisha anakula dili mpya kesho anaamsha gari ambapo atalipwa hadi mara mbili ya hela matajiri ni moja ya matatizo
 
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
29,926
Likes
37,207
Points
280
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
29,926 37,207 280
Ushirikina ndo unaowafanya waendeshe kwa spidi?
ushirikina ndo unaowafanya waendeshe kwa kuhama hama kwa mbwembwe wakikutana?
ushirikina ndo unawafanya wajaze abiria wengi kuliko kiasi
ushirikina ndo unawafanya wabadili siti za magari na kuongeza idadi ya siti?
ushirikina ndo unaowafanya wahonge mizani na trafiki?
Nikirudi tena nitakuulizia hayo maswali yako ila kwa kuanzia walichotujibu ndiyo hivyo na tulishindwa kuwabishia kwani tuliogopa pengine na sisi wangeturoga tusirudi Dar salama.
 
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
29,926
Likes
37,207
Points
280
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
29,926 37,207 280
Hizo sababu 1-7 ni kibwagizo tu.

Madereva wengi hawana elimu tosha ya uendeshaji mabasi na hawapimwi kuangalia ufanisi, uzoefu na afya zao kiakili na hata leseni zao inawezekana wanabadilishana.

Wenye mabasi hawayapeleki mabasi yao kwenye kufanyiwa service and maintenance ambapo inatakiwa kila baada ya safari mbili kama sikosei.

Matairi ya mabasi mengi ni yale yaliyotumika kutoka nje ya nchi, hivyo TBS kupitisha yatumiwe bila uchunguzi wa kina.

Kukosekana kwa vitumo maalum vya huduma (service stops) kwa wasafiri wa mabasi na madereva angali kupumzika kila baada ya masaa mawili au matatu wawapo safarini.

Kukiwa na "service stops" abiria watachuma dawa, kupunguza uzito, kupumzika kwenye viti, kula, kutulia kiakili na hiyo ni pamoja na madereva wa mabasi.

Hakuna "control room" na supervisors kuhakikisha usalama na performance ya madereva hivyo mabasi kuendeshwa kiholela.

na matatizo mengine mengi tu ukiondoa hayo ya ushirikina.
Jifunze KUHESHIMU tafiti za Watu kwani yawezena ukapingana nazo hizo sababu ila ukifanya uchambuzi wa Kina ukakuta na zenyewe zinahusika. Haya mambo yapo, yanatendeka na kuna wenye ushuhuda nao. Hata hivyo naheshimu mchango wako.
 
josam

josam

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2011
Messages
1,917
Likes
348
Points
180
josam

josam

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2011
1,917 348 180
Ni nani wewe uliyefanya utafiti? Mlikuwa team ya watu wangapi mlio fanya tafiti hiyo? Nashauri watu wa system wawe wanaufuatilia watu kama nyie.
 
Richard

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Messages
9,737
Likes
6,438
Points
280
Richard

Richard

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2006
9,737 6,438 280
Jifunze KUHESHIMU tafiti za Watu kwani yawezena ukapingana nazo hizo sababu ila ukifanya uchambuzi wa Kina ukakuta na zenyewe zinahusika. Haya mambo yapo, yanatendeka na kuna wenye ushuhuda nao. Hata hivyo naheshimu mchango wako.
Nafikiri hujanielewa nimemaanisha nini katika kutumia neno kibwagizo.

Yaani kitaalam na kiteknolojia, hayo mambo ya ushirikina hayawezi kupewa uzito sana ukilinganisha na matokeo ya ajali hasa mwendo kasi, madereva kusinzia, kulewa, kubadilishana leseni na magari (dereva halisi kumpa basi utingo) na matairi yasiyo bora kutumiwa sana kupita kiasi.

Ila kimazingara mambo hayo yanakuwemo pia na yameshamiri sana kutokana na imani iliyopo kwamba bila tunguri hujapata mafanikio kimaisha.

Sasa kiufundi kama tukiweka "control room" na kufuatilia kila basi na dereva kwa "CCTV" na "radio call" ili tuone mwenendo wa uendeshaji wake na ufanisi, si tutashuhudia mengi na ndipo tutakapoamini kweli waafrika hatuwezi kuendelea kama bado tunaendeleza imani za kishirikina

Hapa pia nazungumzia pia biashara hii ya mabasi kufanywa kitaalam na kuwashirikisha wadau wengi wenye maarifa na ujuzi (si wa kutengeneza tunguri) kwa mfano wenye mabasi kuwa na kampuni moja au mbili na kuwa partners.
 
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
17,654
Likes
51,725
Points
280
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
17,654 51,725 280
Sina haja ya kumaliza kusoma hii thread kwa vile haiingii akilini..!

Huko ni kuficha uzembe wa madereva
 
Buyuni Kwetu

Buyuni Kwetu

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2013
Messages
569
Likes
328
Points
80
Buyuni Kwetu

Buyuni Kwetu

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2013
569 328 80
Nikirudi tena nitakuulizia hayo maswali yako ila kwa kuanzia walichotujibu ndiyo hivyo na tulishindwa kuwabishia kwani tuliogopa pengine na sisi wangeturoga tusirudi Dar salama.
Wewe ulitegemea wakujibu kuwa 80% ya ajali inasababishwa na uzembe wao na kutofuata sheria za barabarani?
 
The Businessman

The Businessman

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2014
Messages
7,434
Likes
7,258
Points
280
The Businessman

The Businessman

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2014
7,434 7,258 280
Tukianza kuamini hivi basi kila kitu kin achokwama tutasema ni ushirikina...msije mkasema ushirikina umesababisha hata Sukari kupata...
 
MU-ARSENAL

MU-ARSENAL

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2012
Messages
957
Likes
566
Points
180
Age
33
MU-ARSENAL

MU-ARSENAL

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2012
957 566 180
Hizo sababu 1-7 ni kibwagizo tu.

Madereva wengi hawana elimu tosha ya uendeshaji mabasi na hawapimwi kuangalia ufanisi, uzoefu na afya zao kiakili na hata leseni zao inawezekana wanabadilishana.

Wenye mabasi hawayapeleki mabasi yao kwenye kufanyiwa service and maintenance ambapo inatakiwa kila baada ya safari mbili kama sikosei.

Matairi ya mabasi mengi ni yale yaliyotumika kutoka nje ya nchi, hivyo TBS kupitisha yatumiwe bila uchunguzi wa kina.

Kukosekana kwa vitumo maalum vya huduma (service stops) kwa wasafiri wa mabasi na madereva angali kupumzika kila baada ya masaa mawili au matatu wawapo safarini.

Kukiwa na "service stops" abiria watachuma dawa, kupunguza uzito, kupumzika kwenye viti, kula, kutulia kiakili na hiyo ni pamoja na madereva wa mabasi.

Hakuna "control room" na supervisors kuhakikisha usalama na performance ya madereva hivyo mabasi kuendeshwa kiholela.

na matatizo mengine mengi tu ukiondoa hayo ya ushirikina.
Mkuu hakuna Dereva makin kama wa Bus. Tatizo route ndefu mfano Mbeya - Arusha unafikiri Dereva atatembea huo mwendo unaotaka??
Miundo mbinu yetu ndo inasababisha yote haya Dereva analazmika ku over take magar hata sita ili awah
 
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
29,926
Likes
37,207
Points
280
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
29,926 37,207 280
Ni nani wewe uliyefanya utafiti? Mlikuwa team ya watu wangapi mlio fanya tafiti hiyo? Nashauri watu wa system wawe wanaufuatilia watu kama nyie.
System na UZI wangu vinahusiana vipi? Stupid!
 
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
29,926
Likes
37,207
Points
280
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
29,926 37,207 280
Nafikiri hujanielewa nimemaanisha nini katika kutumia neno kibwagizo.

Yaani kitaalam na kiteknolojia, hayo mambo ya ushirikina hayawezi kupewa uzito sana ukilinganisha na matokeo ya ajali hasa mwendo kasi, madereva kusinzia, kulewa, kubadilishana leseni na magari (dereva halisi kumpa basi utingo) na matairi yasiyo bora kutumiwa sana kupita kiasi.

Ila kimazingara mambo hayo yanakuwemo pia na yameshamiri sana kutokana na imani iliyopo kwamba bila tunguri hujapata mafanikio kimaisha.

Sasa kiufundi kama tukiweka "control room" na kufuatilia kila basi na dereva kwa "CCTV" na "radio call" ili tuone mwenendo wa uendeshaji wake na ufanisi, si tutashuhudia mengi na ndipo tutakapoamini kweli waafrika hatuwezi kuendelea kama bado tunaendeleza imani za kishirikina

Hapa pia nazungumzia pia biashara hii ya mabasi kufanywa kitaalam na kuwashirikisha wadau wengi wenye maarifa na ujuzi (si wa kutengeneza tunguri) kwa mfano wenye mabasi kuwa na kampuni moja au mbili na kuwa partners.
Tengeneza na Wewe research topic yako ukafanye na yako kisha utuletee humu hizo so called intellectual findings zako badala ya " kubwabwaja " tu. Halafu mbona unapinga sana hii kitu au na Wewe ndiyo " wale wale " mnaotutoa " makafara " kila uchao? Narudia tena hili jambo la USHIRIKINA unaweza ukalidharau ila nakuambia unaweza ukakuta hizo sababu walizozitoa hao Madereva zikawa na ukweli ila tunakataa tu kwa dhania ya kwamba siku hizi hakuna Uchawi huku yawezekana hata wengine sasa hivi hizo Elimu au Pesa zenu mmezipata au mnazipata kwa kuwafanyia " ulozi " na " makafara " wenzenu ila humu JF mnajifanya " kupovuka " kwa kupinga. Acheni UNAFIKI UCHAWI UPO NA WATANZANIA NI WAAMINI UCHAWI WAZURI TU NA NDIYO MAANA MWEZI JANUARY KUNA RIPOTI ILITOLEWA NA GAZETI LA MWANANCHI KUWA TANZANIA NI YA PILI AFRIKA KWA WITCHCRAFT BAADA YA GHANA. Msidhani Watu tunapokuja humu na " kutiririka " basi huwa ni mambulula bali tunafahamu tunachokifanya na tuna uhakika nacho.

Hata hivyo akhsante kwa kuzidi kuchangia.
 
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
29,926
Likes
37,207
Points
280
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
29,926 37,207 280
Sina haja ya kumaliza kusoma hii thread kwa vile haiingii akilini..!

Huko ni kuficha uzembe wa madereva
Hata hivyo nakushukuru kwa kuusoma mpaka hapo ulipoishia katikati kwani yawezekana kwa uchawi ulionao pengine ungemalizia kuusoma wote UZI nao ungefutika " kimazingara ". Ubarikiwe kwa kuuokoa UZI wangu AMEN!
 
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
29,926
Likes
37,207
Points
280
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
29,926 37,207 280
Wewe ulitegemea wakujibu kuwa 80% ya ajali inasababishwa na uzembe wao na kutofuata sheria za barabarani?
Hata ukiwahoji Abiria kwa uzembe wao wanajitetea na ukisema uwahoji Trafiki nao hujitetea na ukimalizia kwa SUMATRA na Wamiliki wa Mabasi nao hujitetea je unadhani nani atakubali awe " Mbuzi wa Kafara " katika hili?
 
Forum statistics

Threads 1,235,977
Members 474,928
Posts 29,242,380