SoC02 Elimu ni mwanga ila kwa upande huu ni giza

Stories of Change - 2022 Competition

P Didy Wa Tanzania

JF-Expert Member
May 6, 2022
2,376
3,891
UTANGULIZI

Elimu ni nini ?

Ni ujuzi wa utambuzi wa jambo na uwezo wa kuwa na maarifa juu ya jambo fulani na kuwa na mbinu stahiki ya kuhamisha maarifa hayo katika utendaji yakaleta matokeo chanya kwa jamii.

Sera ya elimu ya mwaka 2014 inaeleza katika Dira yake ni pamoja na kuwa na Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa , stadi , umahiri , uwezo na mitazamo chanya ili kuweza kuchangia katika kuleta maendeleo ya taifa

Na Dhima ya sera hiyo ikiwa ni kiunua ubora wa elimu na mafunzo na kuweka mifumo na taratibu zitakazowezesha kupata idadi kubwa ya watanzania walioelimika na wanaopenda kujielimisha zaidi ili waweze kuchangia katika kufikia malengo ya maendeleo ya taifa letu. " www.moe.go.tz" (Tovuti kuu ya wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia).

lakini sera ya elimu na mafunzo imekuwa ipo tofauti na utelekelezaji wake, miongoni mwa malengo ya elimu ya msingi ni kumpa mwanafunzi ujuzi wa kusoma, kuandika na kuhesabu. Ila kipimo cha ujuzi huo ni kusiliba kwenye jibu sahihi (kubahatisha).

Je, ikiwa msingi haupo imara tunaweza kufikia malengo ya Sera ya elimu ya 2014 ?

Andiko hili tutaangazia changamoto zinazoikikumba sekta ya elimu nchini , suluhisho na ushauri .


CHANGAMOTO

Mitahala ya elimu ambayo imepitwa na wakati;

Kuna watu waliosoma hadi kufikia hadhi ya taaluma za fani mbalimbali na kuwa wabobezi katika taaluma hizo ila wameshindwa kuzitumia taaluma zao kujikomboa na badala yake wamekuwa watumwa wa elimu zao badala ya elimu kuwapa fikra za kuwa huru kwa kujikomboa wao na jamii zao. kwa sababu ya kukosa msingi bora wa elimu ya chini.

Mitaala tuliyonayo haimuandai mwanafunzi kufikiri nje ya alichofundishwa darasani. imeshindwa kumtengenezea mazingira ya kujiajiri.

Kijana anatumia miaka takribani kumi na nane kutafuta elimu toka Chekechea mpaka Chuo Kikuu, Elimu ambayo nje ya cheti kijana hawezi kusimama na kujitetea. pia elimu yake haendanani na ushindani wa soko la ajira la dunia.

Miundombinu mibovu; inachangia uzoroteshaji wa maendeleo ya elimu nchini . kwani shule nyingi hazina mazingira mazuri kwa kusomea wala kufundishia kwa ufanisi.

Ukosefu wa madarasa , wingi wa mwanafunzi katika darasa moja, upungufu wa walimu hasa wa masomo ya sayansi ni changamoto ambayo imesababisha wanafunzi wengi kuacha shule , kushindwa kuendelea na masomo na wengine kufeli kwa kushindwa kufanya mitihani kwa baadhi ya masomo.
kwani baadhi ya masomo hayana walimu kabisa.

Hali inayoleta ugumu kwa mwanafunzi kuweza kupata alama za juu na kupelekea wengine kuacha shule kabisa kwa kukosa ushawishi wa kimiundombinu ya usomaji.

Maslahi Duni kwa Walimu; Mwalimu ndio mtendaji mkuu wa sera ya elimu.

Changamoto kubwa iliyopo ni ni mwalimu kukosa thamani . wakati uwalimu ndio kada Mama inayozalisha kada zingine.

Na tafsiri mbovu kuwa uwalimu ni kazi ya wito .tunaitafsiri vibaya na kuhalalisha walimu wapokee mazingira yeyote kiutendaji hata kama si rafiki kwa ajili ni wito.


Lugha ya kufundishia ; Ufundishaji unategemea nguzo kuu mbili , Moja ni UNACHOKIFUNDISHA na Pili KINAVYOFUNDISHWA.

Nguzo ya kwanza ni tegemezi kwa nguzo ya pili na kwenye nguzo ya pili ndiko tunapopata lugha ya kufundishia

Changamoto kubwa inayoikabili sekta ya elimu ni kukosa misingi mizuri ya ufundishaji wa lugha ya usomeshaji

Ushiriki duni wa wazazi ; changamoto nyingine ni kushiriki wa wazazi kwenye masuala ya elimu.
baadhi ya wazazi hawafati hata ripoti za watoto, Kwenye vikao hawafiki.


SULUHISHO

i. Kutengeneza mitaala inayoendana na wakati na soko la ajira la dunia.

• Tusitengeneze mitaala ambayo ajenda kuu itakuwa ni kujibu mitihani bali kupata ufahamu.

Mitahala ijikite kufundisha mwanafunzi haweze kufanya kitu fulani. Na waweze kutenda mambo pasi na cheti kwa kuzingatia mazingira ya sasa.

ii. Kuwapa motisha na thamani walimu na ushiriki wa wazazi kwenye sekta ya elimu.

• Ili kuanza kuboresha ubora wa elimu ya nchi yetu walimu wanahitaji kupewa nyenzo zaidi na mafunzo bora ya kitaaluma. Kwa kuwapa Walimu motisha itasaidia katika utendaji kazi wao, lakini motisha hizi haziji tu kwa kuwalipa mishahara ila kwanza tuwathamini na kuwaheshimu na kuwapa mazingira bora ya kuishi.

Walimu wanahitaji motisha na sio kuwadharau. na motisha sio lazima iwe pesa ingawa hali ya maisha imebadilika pesa inaitajika zaidi. ila thamani ya walimu na kutambuliwa kunaitajika zaidi.

lakini pia wazazi waongeze ushiriki katika kufuatilia maendeleo ya watoto shuleni. watoto wanastahili kupewa malezi na wazazi wote. ni muhimu kuwapa watoto elimu.

iii. Tunaishauri serikali kutoa vipaumbele kwa Vyuo Vikuu / Kati.

• Ili kurekebisha hali hii, kuna haja ya kuwa na ongezeko la vyuo vikuu vilivyojengwa na serikali inahitaji kusaidia mchakato huu kupitia ruzuku au fedha.

Vyuo vikuu na vyuo vya kati hufungua fursa nyingi kwa wanafunzi na jamii zinazowazunguka kupitia mafunzo ya ufundi . tuige mifano kutoka China . tunaishauri serikali kuanzisha vyuo vikuu na vyuo vya ufundi karibia kila mkoa nchini.

lakini pia pawepo na utoaji wa mikopo ya elimu kwa vyuo vya vikuu / kati hii itachochea wananchi wengi wa hali ya chini kujiendeleza na elimu.

Vyuo vikuu / kati vinahitaji kuanzishwa ili kutoa mafunzo kwa vijana na ujuzi unaohitajika ili kupunguza idadi ya watu waliokosa elimu na kupanua soko la ajira .

iv. Tunaishauri Serikali itengeneze mazingira rafiki ya kujisomea kwa wanafunzi kulingana na mahitaji.

• Moja ni mazingira rafiki ni pamoja na lugha rafiki na nyepesi kwa mwanafunzi itasaidia wanafunzi wengi wapate kuelewa wanachofundishwa. huku lengo kuu ni kutafuta lugha ambayo itasaidia kufikisha maarifa kiurahisi zaidi wa wanafunzi wengi nchini.


•Pili ni mahitaji ya elimu bora ni miundombinu bora ambayo inajumuisha darasa na samani zake. lakini pia upatikanaji wa nyenzo nyingine zitakazo msaidia mwanafunzi kusoma kwa vitendo zaidi. uku tukizingatia upatikanaji wa huduma kwa makundi maalum.


v. Kutengeneza sera imara/ bora na kuzitekeleza kikamilifu.

• ubora ni kuhakikisha kile kinachotolewa shuleni kinakuwa na matokeo mazuri ili kuwapa maarifa wanafunzi ambayo yataweza kupanua ufahamu wao.

pia sera zinaitaji upatikana walimu, wakufunzi na wahadhiri wa kutosha wenye sifa stahiki, miundombinu na vitendea kazi.lakini mipango ya sera ilete matokeo mazuri.


HITIMISHO.

Ili sekta ya elimu iweze kujimudu inabidi iwekewe misingi ya kujitegemea kwa kuwa na vyanzo vya mapato na uwekezaji mkubwa.

Mapato hayo yatasaidia kujenga nyumba za walimu na miundombinu ya shule. hivyo basi tutengeneza mazingira bora ya kujifunza na ufanyiaji kazi . lakini swala la elimu lipewe kipaumbele cha kwanza kwa Serikali , Wananchi na Wadau wa elimu wote nchini.


20220906_093015.jpg


(Ukosefu wa madawati na wingi wa mwanafunzi ndani ya darasa moja) Picha Dhamana.
 

Attachments

  • 20220906_093302.jpg
    20220906_093302.jpg
    689.8 KB · Views: 14
Andiko hili limeandika kwa kuzingatia tafiti binafsi ( Muandishi wa andiko ) .

ambazo zimefanywa katika shule mbili za msingi Kwa mashirikiano ya walimu wa shule ya skuli ya msingi mfenesini iliyopo Mkoa wa kaskazini Unguja Zanzibar na skuli ya msingi Makunduchi iliyopo Mkoa wa kusini Unguja Zanzibar.


Nawakalibisha wote kwa ajiri ya majadiliano juu la andiko langu pia nilikuwa naomba mulipigie kura andiko hili.

ASANTENI SANA.
 
Ahsante kiongozi, kwa kuongezea ; mila na tamaduni za baadhi ya makabila Tanzania zimekuwa kichocheo kikubwa cha kuzoroteaha ustawi wa elimu Tanzania, Mfano katika jinsia ya kike, wengi wamekuwa wakipata changamoto ya kuozeshwa kwa lazima wakiwa wadogo sana huku wakikatishwa masomo yao. Nikiwa kama mdau wa elimu, ni vyema serikali ikaliona hili na kulishughulikia.
 
Ahsante kiongozi, kwa kuongezea ; mila na tamaduni za baadhi ya makabila Tanzania zimekuwa kichocheo kikubwa cha kuzoroteaha ustawi wa elimu Tanzania, Mfano katika jinsia ya kike, wengi wamekuwa wakipata changamoto ya kuozeshwa kwa lazima wakiwa wadogo sana huku wakikatishwa masomo yao. Nikiwa kama mdau wa elimu, ni vyema serikali ikaliona hili na kulishughulikia.
asante sana mkuu kusoma andiko langu .na kuongezea wazo lako mkuu katika sekta ya elimu
 
Back
Top Bottom