Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 37,156
- 55,653
Hapa nilipo nina vyeti vingi kweli, vinakaribia kujaa begi, lakini sina uwezo wa kuvumbua chochote kile kwa kutumia elimu niliyoipata kutokea chekechea mpaka uprofeseri. Nazidiwa ata na mafundi majiko walioishia darasa la saba, wanaweza kutengeneza kitu. Yaani nisipo ajiriwa na huu wingi wa vyeti nilivyonavyo, sitaweza kuishi kabisa. Sasa najiuliza swali, elimu ni kupata ujuzi au ni kupata cheti tu? Kwa sababu, ata huku mashuleni na vyuoni tunajifunza namna ya kujibu maswali tu, na tunafaulu vizuri kwa alama A; ila kiuhalisia hatuvumbui vitu, tunategemea kuajiriwa tu.