Elimu ni cheti au ni ujuzi?

Elimu ni cheti au ni ujuzi?

Umewahi kujiuliza mtu kasoma form one hadi four, let's say akapata div four, hii div huwa haichaguliwi kwenda five. Huyo mtu alisoma pysics, chemistry, biology na masomo mengine mengi tu. Sasa jiulize huo ujuzi alioupata ataenda kuu apply wapi? Kuna sehemu ataajiriwa akachanganye madawa? Kuna shule ataenda kufundisha equation? Huyo mtu hatatambulika kabisa na waajiri! Huo ujuzi atajiajiri mwenyewe labda afungue tuisheni afundishe anayoyajua kwa level yake ya elimu. Ndio hiyo tunasema kuna watu wana ujuzi waliupata shuleni/chuoni ila hawakutunukiwa cheti, ni ama mtu hakufikisha alama za kupewa cheti baada ya kutahiniwa au aliacha shule/chuo hakumaliza ila alipapa maarifa/ujuzi.
 
Ingekuwa watu wanaomba kazi bila cheti ingekuwa safi sana. Waajiri wangepata wajuzi wa kweli. Kama ni shuleni unaomba kufundisha wanafunzi, unasailiwa darasani moja kwa moja kama unazimudu mada za kufundisha. Kama ni kwenye madawa unachanganya makemikali mpaka kinapatikana kinachohitajika. Watu wengi wana ujuzi ila hawana vyeti ili waajiriwe
 
Tukisema, chimbuko la elimu ni mawazo ya watu ambao hawakwenda shule ila walizaliwa na vipaji vyao, tutakuwa tunakosea?
Nami naamini hivyo, Kwanza tujue elimu ni nini, tushasema ni maarifa, haijalishi maarifa haya unayapatia shule ama nyumbani, shule ni mfumo tu uliowekwa, ili pia mbele ya safari tupunguzane katika suala la ajira.
Shule inatoa maarifa lakini sio akili, na maarifa(elimu) mengi tunayasoma kutoka kwa watu wa zamani wenye akili.
Kufundishwa kuvua ni elimu haijalishi umeipatia hapo DMI ama ulifundishwa na babu, ila yule wa kwanza aligundua kuogelea ndio anachukua credit na wengine hawakuanza kurupu, la hasha ni kidogo kidogo maarifa ambayo yalirekebishwq na kuboreshwq mpaka kufikia ubora

Kuna issue nilisoma katika dini ya kiislam kuhusu mambo ya elimu, kuna kisa cha malaika kumkandia nabii adam katika kuumbwa kwake kwamba ataleta uharibifu na elimu hana..
Ila mungu alipomuumba adamu akampa ufahamu mkubwa(ni kama program kichwani alimuwekea adamu, ambayo ina mafaili kedekede ni wewe kujituma tu vitu vitafunguka) akwaweka malaika na adam mbele kisha akawaswalika maswali, adam akapatia na malaika walikuwa hawajui, hapo ndipo kwangu niliona kuna kitu cha asili mwanadamu alipewa, sijui ndio akili tuite..
Sababu kuna aya pia anazungumzia roho, ile inaonesha ishu ya roho hatuijui na hatutakuja kuijua sababu hiyo sio elimu aliyotufungulia, hii ipo katika quraan, hivyo vingine tutavijua sababu tayari tushajzwa sijui niseme, hope umenielewa kidogo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom