kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,332
- 12,646
Upo wajibu wa Rais, wajibu wa Makamu wa Rais, waziri mkuu, Mawaziri, wabunge, spike na wananchi. Hivyohivyo kwenye ngazi ya familia uko wajibu wa baba, wajibu wa mama na wajibu watoto. Kila wajibu (role) una matarajio (expectations) kwa wale unaowahudumia na mara nyingi kama sio mara zote kila wajibu una malipo yake,
Kama vile ambavyo watoto hawampigii makofi ya pongezi baba anapowaletea chakula au kuwanunulia nguo ndivyo hivyohivyo kila mtu aliyepewa jukumu (na malipo ya jukumu hilo) asivyohitaji kusifiwa sana, kupigiwa makofi kila anapotimiza majukumu yake. Zawadi kuu ya mtu anaetimiza majukumu yake sawasawa na matarajio ya watu wake ni kuheshimiwa na zawadi ya asiyetimiza majukumu ni kulaumiwa na kubezwa na kuondolewa kwenye nafasi.
Inawakera sana wapiga kura wenu kumsikia na kumuona mwakilishi wake bungezi akipoteza muda na nafasi ya kuwatetea kwa kumsifia sana mtu aliyetimiza majukumu yake vizuri. Yaani na watoto wapige makofi kila siku mama abapopika chakula, wapige makofi kumshukuru dada aliyefagia sebule, Tunataka mbunge atumie kila nukta/sekunde anayoipata mule bungeni kwaajili Yao na taifa.
Pili, wazungu hawana kitu Cha Bure hata kimoja. Ukiona anakupa, anakulipia na kukutembelea lazima ushituke kwelikweli. Ukienda kule Ulaya na Marekani Kuna watu maskini sana, wagonjwa sana, na wasio na chakula Wala pakulala lakini serikali haiwajali lakini inatoa msaada kwako wewe mmatumbi, shitukeni.
Mfano, Marekani anakopa China ili atupe sisi msaada!! Umeshaona wapi mtu anakopa Ile akatoe sadaka na zaka? Shitukeni humo bungeni mnaposikia misaada na mikopo imemiminwa Tanzania.
Unakaria kuwa upuuzi unapomsikia mtu anashangilia kupewa mapesa mengi na wazungu halafu huyohuyo analaumu sana kuenea kwa ushoga nchini. Kama mazuzu vile.
Dawa pekee ni kujitegemea, kulipishana Kodi, na kuzilinda Kodi zetu kwa nguvu zetu dhidi ya wezi na wabadhilifu baaasi.