SoC01 Elimu bora ni haki ya kila Mtanzania

Stories of Change - 2021 Competition

Dayone

Member
Aug 24, 2017
85
200
WanaJF salaam,

Naitwa Dayone, kitaaluma mimi ni mwalimu na karibu tujadili mfumo wa elimu yetu na jinsi elimu ilivyo na thamani kubwa kwa watoto wetu wa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Nchi yetu kwa sasa ina tatizo kubwa sana la ukosefu wa ajira kwa vijana hasa wahitimu wa vyuo mbalimbali, chanzo cha tatizo hili ni serikali yenyewe.

Kuna mjadala mkubwa sana kuanzia mtaani mpaka bungeni ukija kwenye suala la ukosefu wa ajira, ambapo lawama nyingi zimekuwa zikitupiwa katika “Mfumo Mbovu wa Elimu Tulionao” ndio chanzo cha tatizo. Lakini tunasahau jambo moja la muhimu kwamba, ili uweze kutatua changamoto yoyote hapa duniani unatakiwa uelewe SWALI sahihi la kujiuliza, kwa maoni yangu swali sahihi la kujiuliza ni:- nini maana ya MFUMO WA ELIMU? Wengi wetu tunaamini kwamba tukibadili mfumo wa elimu tulionao sasa, watoto wetu watasoma vitu tofauti na wanavyovisoma leo, guys your WRONG! Sayansi na Hesabu tunayoisoma Tanzania inasomwa Singapore, Marekani, nchi zote duniani zinasoma the same contents.

Utofauti upo kidogo sana hasa kwenye masomo ya sanaa na lugha na hii ni kwa sababu suala la sanaa na lugha linatofautiana kulingana na nchi moja hadi nyingine, mfano somo la historia kila nchi ina hisitoria yake hivyo hatuwezi kufanana katika hilo, lakini haina maana ya kwamba somo la historia halina thamani kama tunavyo lazimishwa kuamini na wapiga stori zisizo na mantiki. Watanzania vitu tunavyovisoma darasani viko SAHIHI, mfumo wa elimu yetu unatakiwa uende mbali zaidi ya masomo yetu. Mtaala wa elimu, Tafiti za kielimu (educational research), sera za kielimu, miundo mbinu, mwaalimu na mwanafunzi vyote kwa pamoja tuvitengenezee muunganiko (coordination) ili viweze kuwasiliana muda wote, hii itatufanya tuwe na mfumo imara wa kielimu na wenye kuleta tija kwa watanzania. Siwezi kumlaumu sana mbunge ambaye hana elimu anaposimama bungeni na kuiponda ELIMU na WASOMI wetu ilihali hajui hata hiyo simu (Feature phone & Smartphone) aliyonayo imetengenezwa kutokana na Mathematical formula ya hesabu na fizikia tunayoisoma darasani. Nikupe kisa kimoja, wakati nasoma chuo kuna siku profesa aliingia darasani kutufundisha somo fulani ilikuwa mwaka 2018 nipo mwaka wa tatu alipo project notes zake pale kwenye projector ni za mwaka 2009!! Can you imagine sayansi ya mwaka 2009 inafanana kwa kila kitu hadi mifano na ya mwaka 2018, it doesn’t make sense yaani hata mwaka mwalimu amesahau kuedit maana yake hajajiandaa wakati anakuja darasani. Kwanini mwalimu utumie notes zilezile wakati mambo kila siku yanabadilika?

Nimekupa hicho kisa ili uelewe hasa kwamba, kama sayansi tunayoisoma sisi ni sawa na sayansi inayosomwa huko duniani Korea kusini, Marekani na kwingineko, kwanini sisi tuko hivi tulivyo leo? Kwa dunia hii ya sasa yenye internet na masimu makubwa mwalimu unaingiaje darasani bila kujiandaa? Hata kama unafundisha historia ya vita vya pili vya dunia tuambie kwa mazingira ya sasa kwanini Marekani na Urusi wanamsuguano kila siku sio kutuaminisha eti kisa ni somo la hisitoria ndo ushindwe hata kuedit notes zako!! Mwalimu ana nafasi kubwa sana ya kuleta mabadiliko katika jamii kwa sababu yeye ndio anayetoa mrengo wa kizazi au jamii fulani. Waalimu tunapofundisha tunatakiwa tuwaamshe watoto waweze kujitambua na kuelewa umuhimu wa masomo wanayojifunza darasani mbali na kufaulu mtihani, mfano kidogo kwenye Photosynthesis waambie wanafunzi mmea usipopata mwanga wa jua wa kutosha na mahitaji mengine mmea huo utakuwa dhaifu na hautasitawi vizuri, ili siku moja mwanafunzi atakapokuwa mtaani anaproject ya kulima bustani ya nyanya atafute shamba sehemu ambayo ni ya wazi ili mmea wake ustawi vizuri na apate mavuno ya kutosha na sio kulima chini ya kivuli. That is a kind of education we need.

Viongozi wetu pia wa kielimu (waziri wa elimu) azingatie na a-support tafiti za kielimu kila mwaka ili wizara ije na sera za kielimu zenye kuleta tija katika taifa. Sera za elimu zinatakiwa kupitiwa mara kwa mara kwa sababu ELIMU ndio uhai wa taifa. Angalia sekta ya kilimo ndio mwajiri namba moja wa watanzania (80% nikiwemo na mimi), je viongozi wetu wanamikakati ipi ya kuiboresha hii sekta, kwanini serikali isiwekeze kwenye kilimo cha umwagiliaji kwa kutenga maeneo maalumu na kuweka miundo mbinu ya umwagiliaji ili watanzania wapige kazi sio kuwahimiza wajiajiri pasipo kujua mitaji wanaitoa wapi. Wizara ya kilimo itoe feedback kwa wizara ya elimu ili serikali iweze kujua ni wapi nguvu kubwa iwekeze ili kulikwamua taifa letu na tatizo la ajira, mfano kwa kuwa tumeamua kussurport kilimo nchini kwetu basi tutoe vipaumbele kwa watoto wetu wanaotaka kusomea masuala ya kilimo kwa kuwapa mikopo ya kielimu, ikiwezekana hata tuwape full funded scholarship watanzania 100 wakasome kilimo kwenye nchi zilizofanikiwa kama Israel. Israel pamoja na kwamba sehemu yake kubwa ni jangwa lakini they are leading in case of Mechanized agriculture, angalia mbegu bora kabisa zina toka nchi gani hapa duniani ni Israel, mfano Hazera mbegu ya nyanya bora kabisa inatokea kwa wayahudi pamoja na kwamba hiyo kampuni iko acquired na kampuni ya Ufaransa (LimaGrain) lakini bado hiyo ni brand ya Waizirael.

Singapore na Korea kusin ni moja ya nchi ambazo zina mfumo bora kabisa wa elimu pamoja na kwamba miaka ya 1960’s walikuwa sawa na sisi (Afrika), walichokifanya mpaka leo hii wanatuzidi kwa kila kitu ni kwa sababu walifanya Industrial Espionage yaani walituma vijana wao kadhaa kwenda kusoma nchi za Ulaya na Marekani, baada ya kuhitimu masomo yao wakarudi nchini kwao kuja kueneza na kutumia ujuzi walioupata katika nchi zilizoendelea, waangalie leo walipo they ten times bigger than we are!! Siasa ndio mchawi namba moja tuache kuingiza siasa kwenye mfumo wetu wa elimu, viongozi wetu pia waache kuingilia elimu ya watoto wetu bila tafiti za kueleweka.
MCHANGO WANGU KATIKA ELIMU​

Mimi ni mdau katika sekta ya elimu (mwalimu wa sayansi i.e Biology & Chemistry). Wakati namaliza chuo mwaka 2018 nilikuwa na hamasa kubwa sana ya kuja kuitumikia jamii yangu kama mwalimu ngazi ya sekondari, baada ya kumaliza na kuingia mtaani hali ikawa tofauti na matarajio baada ya kukuta magoli yamehamishwa (hamna ajira), bila kujua niliendelea kupiga mpira uelekeo uleule (kutafuta ajira) nikitarajia one day nitafunga goli. Baada ya kusota sana na vyeti mtaani (Moshi, Kilimanjaro) niliamua kurudi Dar es salaam ili niuze stock ya mpunga wangu niliokuwa nimelima Malinyi mkoani Morogoro kipindi nasoma chuo.

Nilikoboa mpunga wangu nikauza kisha nikahamishia mapambano Moshi, nilikuwa nafuata mchele Didia na Kahama kisha nausafirisha kwenda Moshi nauza. Nilikuwa nauza mchele mchana kisha usiku saa moja hadi saa nne nilikuwa na watoto watatu nawafundisha tuition ghetto kwangu (Teaching is in my marrow, I like it that’s why I never tire). Siku moja niliitiwa mpunga kijijini kwetu zilikuwa gunia 45, nilizichukua bila malipo sikuwa na cash nikazipeleka Tinde kukoboa kisha nikapaki kwenye mifuko nikahifadhi hapo mashineni. Nilitoa hela pale Tinde kuna ATM mashine ya Crdb kisha nikampelekea hela yake mwenye mpunga kule kijijini kwetu. Siku hiyo nililala nyumbani kijiji cha Bugogo-Shinyanga, kabla sijaondoka asubuhi kuna madogo walikuja nyumbani wananifahamu nimewahi kuwafundisha tuition, wakaniomba sana niwafundishe tena kwani walikuwa wanajiandaa na mtihani wa kidato cha nne (NECTA) na shule yao haikuwa na mwalimu wa sayansi. Niliwaambia nitawapa jibu kwa njia ya simu sikutaka kuwavunja moyo kwa sababu nilitamani kuwasaidia hivyo niliona ni bora nijipe muda wa kufikiri jinsi ya kuwasaidia pasipo kuharibu ratiba yangu.

Nilikuwa nasafiri kila wiki mara moja kutoka Moshi kwenda Shinyanga, baada ya wiki mbili niliamua kuwasaidia wale vijana wa nyumbani (wanafunzi). Nilikuwa na wazo la muda mrefu toka nipo chuo na hapo ndio nikaamua kulitekeleza, nikawa najirekodi nafundisha kwa kutumia Laptop yangu huku nikiwa nimeandaa notes kwenye PowerPoint kisha namtumia dogo fulani aliyekuwa na smartiphone pekee pale kijijini anadownload kisha anawaazima simu wale vijana ili waweze kujifunza ninachokifundisha kwenye video. Nilifanya hivyo hata kwa hawa watoto watatu Moshi, matokeo yake yalinishangaza!!! Wanafunzi kwa pamoja walitoa feedback ambayo ni positive (mwalimu tunaelewa). Niliwafundisha topic zote walizohitaji kwa njia hiyo na kwa msaada wa walimu wao shuleni leo hii kati ya watoto watano niliokuwa nawafundisha watatu wapo form five, unfortunately wawili matokeo yao hayakuwa mazuri.

Ndugu MwanaJF naambatanisha kipande cha video hapa chini uweze kujionea jinsi gani watoto wetu wanaweza kupata elimu bora bila kujali mazingira waliyopo. Video quality (sauti) inaweza kuwa chini kwa sababu ya miundo mbinu huu ni mwanzo tu tuna-improve along the way.





Hiyo ilikuwa ni wake up call kwangu kuweza kutambua nguvu kubwa iliyopo kwenye teknolojia. Pamoja na miundo mbinu hafifu niliyonayo bado sijaacha kuwasaidia watoto wetu napambana ili siku moja atleast tuwe na darasa moja janja (Smart Class) litakalofundisha wanafunzi wote nchi nzima. Kubadili mfumo wetu wa elimu ni pamoja na kubadili jinsi ya kufundisha na jinsi watoto wetu wanavyojifunza, tutumie teknolojia hiihii tuliyonayo kuweza kutoa elimu bora kwa vizazi vya leo na kesho. I don’t care wanasiasa wanatuonaje sisi wahitimu tunaoteseka mtaani cha msingi ni kwamba one day we gonna WISE UP na ili tuweze kutimiza malengo yetu ni lazima tuanze na chochote tulichonacho. Mtanzania mwenzangu karibu kwa mchango wako wa mawazo chanya, marekebisho, msaada wa aina yoyote ili tuweze kusonga mbele kitaaluma katika nchi yetu na huu ni mwanzo tu wa safari yetu ya Elimu Bora ni haki ya kila Mtanzasnia. Usisahau KURA yako moja ni hatua moja wapo itakayofanikisha ndoto ya maelfu ya wanafunzi kuweza kupata ELIMU BORA. Asante!
 
Mimi napata ukakasi kukubaliana naww, kama hesabu, kemia, physics inayofundishwa huko majuu ndo hii hii tunafundishwa sisi, Kwanini wao wanafanya vizuri kimaendeleo kuliko sisi kwa kutumia elimu ileile.​
 
Dayone nimekuelewa vizuri, kikubwa unachofanya na mimi nafanya na nimetengeneza video kadhaa YouTube (Tafuta @EDUSTUDIOtz kwa maada za GENERAL CHEMISTRY (A-level) na MOLE CONCEPTS & RELATED CALCULATIONS (O-level)] ni video bora hujapata kuona na natumia simu kufanya hayo yote. Napenda nachokifanya, kufundisha, na napenda fedha.
Hauwezi kutegemea shughuli hii kama chanzo cha kipato, kwa sababu hiyo natumia advantage ya teknolojia kufundisha huku nikiendelea na shughuli zingine mtaani

Malengo ni makubwa na na yanafurahisha. Na 'mpango kazi' upo. Vilevile nafundisha kwa njia ya WhatsApp na Telegram [ #SomaChemistryKwaWhatsApp , #SomaPhysicsKwaWhatsApp na #SomaBiologyKwaWhatsApp A & O level) na wanafunzi wanaojiunga kwa kutuma ujumbe “tumaSMSniunge0759170823”

Kitu elimu yetu kinahitaji kufanyika ni kuwaongezea wanafunzi uwezo wa kufikiri (critically & creatively). Inawezekanaje sasa ni katika kuwa sisimua watembee katika njia hiyo. Katika madarasa ya a ya kawaida kuna mambo mwl hawezi kufanikisha kwa mf. Kuleta ukaribu wa somo katika uhalisia wake ... Kwa misaada waTEHAMA inawezekana

Unaweza kufundisha kwa staili tofauti tofauti kulingana na wanafunzi wetu wa leo walivyo na wakajua nini cha kufanya katika Taifa hili

@Dayona naomba nicheki 0759 170 823 kuelezana mengi zaidi
 
Mimi napata ukakasi kukubaliana naww, kama hesabu, kemia, physics inayofundishwa huko majuu ndo hii hii tunafundishwa sisi, Kwanini wao wanafanya vizuri kimaendeleo kuliko sisi kwa kutumia elimu ileile.​
Mkuu ni kwamba shida ipo kwenye approach jinsi tunavofundisha watoto wetu ni tofauti kabisa na wao wanavyofundisha watoto wao, wame-base katika practical zaidi kwa sababu wana-facilities kama Maabara kwa ajili ya masomo ya sayansi na Computer labs, vyote hivi vimewezeshwa na serikali zao wakishirikiana na sekta binafsi. Njoo hapa kwetu unakuta mfano maabara ya biology ina microscope moja tena outdated na inaguswa na mwalimu tu wakati anafanya demonstration. So wenzetu wamewekeza zaidi kwenye vitendo(practicals) na sisi tumekomaa na theory ndio maana tupo hapa leo bora liende.
 
Dayone nimekuelewa vizuri, kikubwa unachofanya na mimi nafanya na nimetengeneza video kadhaa YouTube (Tafuta @EDUSTUDIOtz kwa maada za GENERAL CHEMISTRY (A-level) na MOLE CONCEPTS & RELATED CALCULATIONS (O-level)] ni video bora hujapata kuona na natumia simu kufanya hayo yote. Napenda nachokifanya, kufundisha, na napenda fedha.
Hauwezi kutegemea shughuli hii kama chanzo cha kipato, kwa sababu hiyo natumia advantage ya teknolojia kufundisha huku nikiendelea na shughuli zingine mtaani

Malengo ni makubwa na na yanafurahisha. Na 'mpango kazi' upo. Vilevile nafundisha kwa njia ya WhatsApp na Telegram [ #SomaChemistryKwaWhatsApp , #SomaPhysicsKwaWhatsApp na #SomaBiologyKwaWhatsApp A & O level) na wanafunzi wanaojiunga kwa kutuma ujumbe “tumaSMSniunge0759170823”

Kitu elimu yetu kinahitaji kufanyika ni kuwaongezea wanafunzi uwezo wa kufikiri (critically & creatively). Inawezekanaje sasa ni katika kuwa sisimua watembee katika njia hiyo. Katika madarasa ya a ya kawaida kuna mambo mwl hawezi kufanikisha kwa mf. Kuleta ukaribu wa somo katika uhalisia wake ... Kwa misaada waTEHAMA inawezekana

Unaweza kufundisha kwa staili tofauti tofauti kulingana na wanafunzi wetu wa leo walivyo na wakajua nini cha kufanya katika Taifa hili

@Dayona naomba nicheki 0759 170 823 kuelezana mengi zaidi
Safi sana mkuu, sisi ndio tunapaswa kuwa chachu ya mabadiliko katika sekta ya elimu na sio kusubiri mtu atoke nje ya nchi kuja kutufundisha namna bora ya kujifunza na kufundisha. Nakucheki mkuu tuexchange ideas.
 
Back
Top Bottom