Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,811
- 6,506
Mbona hili halina ubishi wowote.Kama tunataka mabadiliko ya kweli katika nchi hii, hakuna njia ya mkato, CCM ni lazima iwekwee benchi. Hayo mengine ni woga tu kwani wapo Watanzania wengi hawajawahi kuonja maisha nje ya utawala wa CCM. Siku CCM inapigwa chini, watu watajawa mwamko mpya na kugundua kuwa yale yote waliyoaminishwa hayawezekani kumbe yanawezekana. Tanzania mpya yawezekana sana tu bila CCM; that's the bottom line.
Ni kweli watu wanataka mabadiliko na hasa ikichukuliwa kuwa binadamu tumeumbwa katika mfumo wa kubadilika.
Mfumo wa mabadiliko katika Afrika unaisaidia sana CCM kuendelea kubakia madarakani kutokana na sababu mbali mbali zilizo katika mfumo huo ambazo wanazijengea hoja ili wabakie madarakani.
1)Wapinzani wanapambana siyo na CCM pekee bali pia na mazingira ya kisiasa Afrika. Ninasema hivi kwa sababu historia ya mageuzi katika nchi za Afrika haijatoa mageuzi chanya ambayo watu walidhani kabla ya kuiweka pembeni serikali iliyoko madarakani badala yake imenufaisha kwa kiwango kikubwa kundi la viongozi waliopata madaraka katika mageuzi. Mageuzi yaliyofanyika katika nchi za kiafrika yamenufaisha kifisadi kundi la viongozi badala ya wananchi wengi.
CCM itaendelea kuwaamisha watu uharali wake kubakia madarakani na ninaamini watu wataendela kuamini kwa sababu historia inaisaidia CCM katika hoja zake.
2) Watanzania pia tumelelewa na tumeishi katika mazingira ya kutopenda sana mabadiliko ya kimaisha. Mazingira hayo yamejenga tabia ya kuridhika sana katika mazingira tuliyonayo bila kujali kama ni duni au siyo duni. kwa maana nyingine, tumekuwa taifa la masikini tajiri. Hatuna wivu wa kimaendeleo ambao chachu yake ni mabadiliko ya kimaisha. Hii dhana na tabia inasaidiwa sana kuendelea kuwepo hasa pale jamii nyingine ya nchi za Kiafrika iliyojaribu hayo mabadiliko na wananchi wakajikuta hawayapati baada ya kubadilisha serikali.
NInaamini kama hoja ingekuwa ni utawala mbovu wa serikali ya CCM, basi CCM kwa sasa ingekuwa tayari iko kwenye bench la kiutawala kwa sababu muda wa CCM kuwepo madarakani na mrejesho wa maendeleo unaihukumu kifungo cha kukaa kwenye benchi. CCM imefanya madudu mengi mno.
Mpaka pale wanasiasa wa upinzani nchini watakapoweza kuishinda hoja ya hali ya kisiasa katika nchi zingine za Kiafrika zilizofanya mageuzi, basi hapo watakuwa wameweza kuishawishi jamii kuwa Tanzania mpya yawezekana bila CCM.