Elezea furaha yako,siku CCM ikitoka madarakani

Ushirombo

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2013
Posts
3,558
Reaction score
2,714
ndugu zangu,i declare interest that mimi ni mwanachama wa cdm
Napenda mtoe ya mioyoni mwenu mtakavyopokea kushindwa kwa ccm
Binafsi siku hiyo kwangu itakua ni ya furaha sana,ntagawa sana ofa, kama siku ambayo aliekua mgombea ubunge wa shinyanga mjini ile 2010 alipotangazwa kushinda, nilifurah sana furaha ambayo sijawah kuipata maishani,lakin bahati mby ccm walimchakachua mbunge wetu shelembi eti kwa kura moja rip shelembi.
Nawasilisha
 
ndugu zangu,i declare interest that mimi ni mwanachama wa cdm
napenda mtoe ya mioyoni mwenu mtakavyopokea kushindwa kwa ccm
binafsi siku hiyo kwangu itakua ni ya furaha sana,ntagawa sana ofa, kama siku ambayo aliekua mgombea ubunge wa shinyanga mjini ile 2010 alipotangazwa kushinda, nilifurah sana furaha ambayo sijawah kuipata maishani,lakin bahati mby ccm walimchakachua mbunge wetu shelembi eti kwa kura moja rip shelembi.
Nawasilisha

kauzi kako kamekaa kiajabuajabu hivi,kanaweza kakakosa wachangiaji mkuu.
 
Wacha nionekane chizi tu walah nita enda kukaa njia panda yoyote na boxer lenye rangi za cdm!
 
Nitaliangusha roli la nyonya mavi posta mpya likiwa full tanki nikiwa nimetoka konyonya kwenye mashimo ya ikulu coz mimi ni dereva wa hao maroli.
 
Mi sina la kusema ila ntavunjavunja vioo vya magari ya chama chakavu
 
Nita andika kitabu cha kuhusu ushetani tulio fanyiwa na maccm kwamiaka mingi iwe kumbukumbu
 
Watanzania matatizo yetu ni makubwa kuliko CCM, ni makubwa kuliko vyama vya siasa, kwa kweli ni makubwa kuliko siasa.

Yamezama katika utamaduni na mila, katika malezi, katika elimu, katika wengi kukosa ushujaa wa kujitoa muhanga katika mapambano, katika ubinafsi, katika uchu wa madaraka, katika umangimeza, katika kupenda dezo, katika kutotaka kufanya kazi, katika kupenda shortcuts za ujanjaujanja uliojaa hatari na mengine mengi kama hayo.

Sasa matatizo haya hayawezi kuisha kwa chama kimoja kutoka madarakani kikipishe chama kingine chenye watu wenye utamaduni ule ule.

Zambia wenzetu walipandwa na mzuka wa mageuzi, wakamtoa Mzee Kaunda. Mzee wa watu hakujua hata kuiba kura, akaondoka Ikulu Lusaka kumpisha Chiluba.

Chiluba akaenda kufanya Ikulu ya Zambia pango la wahalifu, kapiga ma deal mpaka na kina Abdi Msomali.

Wananchi kuja kustuka wameruka majivu na kukanyaga moto.

Mimi siifagilii CCM. CCM imechoka na inabiodi iondoke.

Lakini hizi habari za kusema kwamba mwisho wa CCM kuwa madarakani ndio suluhu ya matatizo yetu, naona ni kukosa kuelewa kwamba matatizo yetu yako katika kina kirefu sana kilichopita kina cha vyama vya siasa na siasa kiujumla.
 
Nimekuelewa vema sana Mkuu Kiranga, sasa unashauri tufanye nini ili kuhakikisha watanzania tunarudi kwenye mstali,na kama njia zipo ni zipi hizo?
 
Kama tunataka mabadiliko ya kweli katika nchi hii, hakuna njia ya mkato, CCM ni lazima iwekwee benchi. Hayo mengine ni woga tu kwani wapo Watanzania wengi hawajawahi kuonja maisha nje ya utawala wa CCM. Siku CCM inapigwa chini, watu watajawa mwamko mpya na kugundua kuwa yale yote waliyoaminishwa hayawezekani kumbe yanawezekana. Tanzania mpya yawezekana sana tu bila CCM; that's the bottom line.
 
Historia ya mageuzi katika nchi za kiafrika inaifanya jamii ambao haijaonja mageuzi ijiulize mara mbili mbili (wazee na wanawake) katika kufanya maamuzi ya kuiweka pembeni serikali iliyopo.

Katika makundi ya kijamii, Vijana mara nyingi huwa ni watu wa kuchukua maamuzi hata yenye risk na ndiyo maana sishangai kuona wengi wao ndiyo wanakuwa kwenye mikutano ya vyama vya upinzani. Wanaenda kusikiliza na kupima hoja za wapinzani ili waweze kuchukua hiyo risk ya kimageuzi.

Kuna watu wanashangaa na kujiuliza kwa nini CCM wanakuwa na wanawake wengi na pia wazee katika mikutano yao lakini pia wanashindwa kutambua kuwa historia ya chaguzi nyingi za 'kidemokrasia' katika Afrika inalifanya hili kundi kusita katika maamuzi ya kimageuzi. Kwa maana nyingine, wao wameishakata shauri katika sanduku la kura.

CCM imechoka lakini kuchoka kwake kunasaidiwa sana na historia za chaguzi za nchi za Afrika ili kuendelea kuwepo active katika ulingo wa kisiasa na hasa pale viongozi wetu wa vyama vya upinzani wanapoanza kuhusishwa na nyendo za kifisadi kabla hata ya kupewa uongozi wa nchi.

Kwa hoja na mitazamo hiyo, Watanzania bado wanasema 'bora zimwi likujualo halikuli likakwisha'.
 
Nimekuelewa vema sana Mkuu Kiranga, sasa unashauri tufanye nini ili kuhakikisha watanzania tunarudi kwenye mstali,na kama njia zipo ni zipi hizo?

Tuimarishe upinzani na kuondoa utani katika kazi ya kuimarisha demokrasia.

CHADEMA kwa mafano, mwaka uliopita huu imejishusha hadhi sana tu kama "chama mbadala" kwa viza, vituko na vitimbwi tulivyoviona, hata kufikia sehemu sisi wengine ambao hatuna chama lakini tumechoka CCM tunaanza kujiuliza tofauti ya kimsingi ya CHADEMA na CCM ni nini?

Tuangalie matatizo systemic katika utamaduni wetu ambayo nimeyataja hapo juu.
 
Watanzania matatizo yetu ni makubwa kuliko CCM, ni makubwa kuliko vyama vya siasa, kwa kweli ni makubwa kuliko siasa.

Yamezama katika utamaduni na mila, katika malezi, katika elimu, katika wengi kukosa ushujaa wa kujitoa muhanga katika mapambano, katika ubinafsi, katika uchu wa madaraka, katika umangimeza, katika kupenda dezo, katika kutotaka kufanya kazi, katika kupenda shortcuts za ujanjaujanja uliojaa hatari na mengine mengi kama hayo.

Sasa matatizo haya hayawezi kuisha kwa chama kimoja kutoka madarakani kikipishe chama kingine chenye watu wenye utamaduni ule ule.

Zambia wenzetu walipandwa na mzuka wa mageuzi, wakamtoa Mzee Kaunda. Mzee wa watu hakujua hata kuiba kura, akaondoka Ikulu Lusaka kumpisha Chiluba.

Chiluba akaenda kufanya Ikulu ya Zambia pango la wahalifu, kapiga ma deal mpaka na kina Abdi Msomali.

Wananchi kuja kustuka wameruka majivu na kukanyaga moto.

Mimi siifagilii CCM. CCM imechoka na inabiodi iondoke.

Lakini hizi habari za kusema kwamba mwisho wa CCM kuwa madarakani ndio suluhu ya matatizo yetu, naona ni kukosa kuelewa kwamba matatizo yetu yako katika kina kirefu sana kilichopita kina cha vyama vya siasa na siasa kiujumla.

imechoka vipi? je CCM ina uradhini wa binadamu mpaka itende na ichoke? je unaweza kuupima uchovu kwa kiwango kipi?
 
Kama gari linaweza kupimwa na kuonekana limechoka kwa kukongoroka, na gari si binadamu, vivo hivyo CCM inaweza kupimwa na kuonekana kukongoroka.

Kati ya vipimo vingi, naweza kuupima uchovu kwa CCM kushindwa kutekeleza ilani yake ya uchaguzi pamoja na ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni, kwa mujibu wa mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete.
 
gari ni object unaweza ukalishika na ukaliona dhahiri so unaweza kusema limechoka...
sasa CCM unaiona vipi kama imechoka? unaweza kuishika?
 
Nitakodi ukumbi maarufu hapa kwetu Disko lakufa mtu hadi asubuhi ambapo kiingilio na vinywaji itakua bule.
 
Back
Top Bottom