Electrical Engineers kujadili tatizo la Umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Electrical Engineers kujadili tatizo la Umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nikupateje, Jul 25, 2011.

 1. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2011
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wataalamu wa umeme nchini (Electical Engineers), na wadau wengine watakutana kujadili ufumbuzi wa kitaalamu wa matatizo ya umeme nchini.

  Barua ya mwaliko huo inasambaa kwenye internet na mimi nimeipata kuiweka humu inaonyesha kwamba kikao hicho kitafanyika kwenye ukumbbi wa Karimjee Hall, siku ya Jumamosi, July 30, 2011 kuanzia saa 04:00 hadi saa 06:00 mchana.

  Barua inaonyesha kikao hicho kinaratibiwa na Taasisi ya Wahandisi hapa nchini yaani Institute of Engineers Tanzania.

  Watoa mada watakuwa ni Dr. Maingu, Dr. Kyaruzi na Eng. Mgaya.

  Dr. Kyaruzi ni yule aliyemaliza hoja ya kitaalamu kwamba umeme unaopita juu ya Kanisa la Kakobe hauna madhara.

  Hivyo wale wenye kutaka kujua wataalamu wa umeme wanasema nini kuhusu hali ya sasa hii ni fursa yao.

  *****
  Barua ya mwaliko inasema hivi hapa chini na vilevile unaweza kui-download kwenye attachment:
  *****
  View attachment ADVERT - MATATIZO YA UMEME.doc
  *****  THE INSTITUTION OF ENGINEERS TANZANIA


  MKUTANO WA KUJADILI TATIZO LA UMEME NCHINI TANZANIA:


  MAHALI: KARIMJEE HALL

  SIKU/TAREHE: JUMAMOSI, 30/07/2011

  MUDA: SAA 4 ASUBUHI – SAA 6 MCHANA


  MADA: UFUMBUZI WA KIHANDISI WA KUTATUA TATIZO LA UMEME NCHINI TANZANIA


  WATOA MADA: (1) ENG. DR. M.I. MAINGU
  (2) ENG. S. M. MGAYA
  (3) ENG. DR. A. L. KYARUZI


  WADAU NA WANANCHI MNAKARIBISHWA


  RAIS
  21/07/2011
  *******
  Maswali zaidi wasiliana na anuani ifuatayo:

  *****
  Eng. S.N.A. Kassera
  Executive Secretary,
  The Institution of Engineers Tanzania,
  Pamba Road, Opp. Former Hotel Agig
  P.O. Box 2938,Dar es Salaam, Tanzania,
  Tel: +255 22 2124265/2122836,
  Mob: +255 717 110411/0784 909060,

  *****
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Jul 25, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mbona mimi Eng. Ngabu sijapata huu mwaliko?
   
 3. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Msisahau kumkaribisha Engineer, Ambassador, M.P, Dr., Rev. Prof. Captain Rwegasira Esq.
  Mlikuwa wapi nyie mainjinia siku zote? Hili tatizo limeanza toka 1990's?
  Hata mkiweka huo mkutano na mkija na hoja zenu za kutatua hili tatizo, can't you see ni yaleyale kama mapendekezo ya tume ya Warioba na majina ya wauza madawa kapelekewa report raisi na kaziweka reports kwenye kabati?
  Ni vema mkafanya huo mkutano wenu but I think it's a waste of time and resources sababu JK ameshasema eti tatizo la umeme ni ukame na yeye hana uweza wa kuleta mvua. Solution ameshanena kuwa ni hadi mvua zinyeshe. Msipoteze muda wenu labda mkutane tu for a get together
   
 4. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Wanaokutana ni Members wa Institute of Engineers Tanzania siyo Electrical engineers kwa mujibu wa vyanzo vyangu vya habari.

  By the way ina maana wizara ya Nishati haina Electricla Engineers? Ahaa usanii huu alafu Karimjee!
   
 5. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  msisahau kutupa feedback..., alafu please tumeongea sana sisitizeni action sababu kama ni kuongea walishaonge, tumeongea na wataendelea kuongea sana...
   
 6. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Academic and technical solutions of electricity are well known but at the moment we need political solution. Makongamano na midahalo ya nini? Kipya gani ambacho watazungumza hawa watu?
   
 7. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2011
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Sorry mkuu,

  Ni kweli mwaliko ni kwa ma-engineer japo kwa tatizo la umeme na haraka ya ku-post nikajikuta nakazia Electrical Engineers japo pia niliongezea neno na wengine wa fani hiyo.

  Lakini kila kitu kingine kinabaki kama barua ilivyo.

  Suala kwamba WIzara haina ma-engineer hilo ni juu yao. Kama na wenyewe watakuwepo mkutanoni basi itajulikana kwa nini kuna matatizo na wao wamo humo wizarani.

  Suala ni kwamba hata usiwe engineer naamini unaweza kutoa na kusikia aoni yako. Vinginevyo hata hapa JF matatizo ya umeme yangekuwa anaongelewa na hao wa wizarani tu amba kila siku wanataja hesabu za Megawati.
   
 8. Yeccotltd

  Yeccotltd JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa taarifa kiongozi!!
   
 9. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Msiwasahau wachumi tu kwani malengo hayatafikiwa. Engineers watatoa utaalamu wao wa kiufundi ila utaalamu wa kimipango ni kazi ya wachumi.
   
 10. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Na wiki 3 za Ngeleja ndo zinakaribia kwisha...!!ngoja tuone, Engg Nsiande nadhani atakuwepo!!
   
 11. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2011
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ikiwa ni hivyo basi hata thread unazojadili hapa JF zifutwe kwa sababu JF hardly imeanza mwaka 2005 na matatizo kibao ya nchi hii yalikuwepo.

  Je, ulipitia ile thread kwamba ilikuwa ni makosa kuweka 80MW pale Mtera? Je, unajua kwa nini ilikuwa ni makosa?
  Ilikuwa ni makosa kwa sababu MasterPlan ya Mtera haikuwa kuzalisha umeme. Mtera iliwekwa kwa ajili ya kuisaidia Kidatu inapozidiwa, kwamba maji yakikauka Kidatu basi yaweze kuletwa yalioko Mtera.

  Sijui ni nini kiliingia vichwani na kufanya pale Mtera waweke 80MW na iwe ni ile inayojitegemea.

  HIvyo Mtera ilikuwa kama standby source. Sasa tume-utilize hadi standby na matatizo yenyewe ndiyo haya.

  Wewe kwa upeo wako hulioni hilo na hutaki lijadiliwe.

  Waache wajadili kama mnavyojadili humu JF.
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mbona sioni mtu kutoka wizarani au tanesco kama watoa mada
  Jamani ni aibu hii,mhando ni engineer si aje tupa master plan yao tuidiscuss
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Jul 25, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hawa wahandisi wa Kiafrika hawana lolote. Watakutana hapo na kunywa maji yao ya Kilimanjaro na tuvitafunio twao (vibajia, sambusa, ufuta, kashata, kachori, n.k.). Halafu watataoka hapo na makabrasha kibao. Hamna lolote la maana watakaloliongelea. Mgao utaendelea kuwepo. Na rhumba litazidi kuwa kali. Ndiyo wahandisi wa Kiafrika hao. Ingenuity sufuri kabisa. Miaka yote hii ya matatizo ya umeme leo ndiyo wanagutuka? Get outta here...
   
 14. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwakuwa si member wa IET ama vinginevyo masuala ya umeme huyafahamu kwahiyo hawakuona umuhimu wako, ama vinginevyo hauko kwenye mtandao wao!!
  Hapana shaka eng.stella manyanya atakuwepo kuwakilisha,...

  Waswahili wana kamsemo kao kwamba "better late than never" kwahiyo waache wahandisi wakutane kisha tusikie watasema nini.  Wapo ma engineer wa kutosha kabisa pale wizarani; kuanzia kwa naibu katibu mkuu eng.mwihava, eng.mushi, eng.kitonga kwa kutaja wachache wakiongozwa na ma profesa wao Dr. eng.ngeleja na Dr.eng.malima

  Inabidin wakutane si unajua tena mambo ya sitting allowance mkuu, bila hivyo hiyo mil 460 iliyochangishwa na jairo itakosa justification!! Matatizo ya umeme ndani ya nchi hii hayawezi kumalizika kama ccm itaendelea kuiongoza nchi hii, iwe wameshinda kwa halali ama kwa haramu. Sasahivi wanatumia pesa nyingi kwa mamilioni kugawana posho kwa kisingizio cha kusherekea uhuru wakati nchi iko gizani, aibu kiasi gani kwa watanzania!!??

  Wachumi wetu hawa hawa wanaotuhubiria kwamba uchumi wa nchi unakuwa kwa kiwango cha juu wakati mifukoni hatuna hata senti ya kununua maandazi?? Labda tupate wachumi wa kichina, hawa watanzania hawafai kabisa, hovyooooo!!!

  Punguza jabza mkuu, kila mmoja ana uhuru wa kutoa mawazo yake na hayo ndio mawazo yake kama na wewe unavyotoa yakwako.
  Mwisho wa siku tutaangalia hoja ya msingi imetoka wapi na ni ipi kwa utekelezaji na manufaa ya wananchi.
   
 15. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  mhando anauza umeme kwa hasara, ananunua umeme kwa bei ghali toka kwa songas na wengineo lakini anatuuzia kwa bei poa, ukichanganya na vishoka mitaani plus umeme unaopotea kutokana na uchakavu wa miundombinu, sidhani kama atathubutu kuwa msemaji siku hiyo, sana sana atakuja kama msikilizaji!!

  wanataka kuuza sura tu kwenye mikamera ili jioni yake tuwaone na tukiamka tukute wamejazana kurasa za mbele za magazeti.
   
 16. Rocket

  Rocket Senior Member

  #16
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  haya mambo yanaendeshwa kisiasa jmani,labda washauri tu na ushauri wenye nchi wataweka kabatini
   
 17. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  hata wakitoa mapendekezo mazuri vp,serikali kiburi ya magamba itayaweka makabatini.nahis kichwa kupasuka nikiwafikiria politicians njaa wa nchi hii
   
 18. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #18
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,277
  Likes Received: 3,008
  Trophy Points: 280
  Wakaongee na kujadiliana na maamuzi yafnywe kwa vitendo....Kenya wametengeneza mradi wa umeme kwa miaka 3....Uganda wanatengeneza bwana lingine la umeme.....hku kwetu watu wamekazania posho za vikao tu....na ufisadi
   
 19. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2011
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kikubwa ni kwamba wameamua kukutana waziwazi na si kwa kujificha kama humu ambamo hata majina hatujuani.

  Jambo lenyewe professionally ni rahisi sana. Peleka swali kwenye University yoyote duniani halafu uliza kifanyike nini kuondoa tatizo la umeme kwenye nchi yenye tatizo kama letu.

  Sidhani kama hiyo thesis yako utataja jamaa anaitwa Kikwete, Pinda au Ngeleja.

  Ukifanya hivyo nadhani huo Supervisor itabidi akupe negative max ili hata zeo usiipate! Umeambiwa kwamba kwa utaalamu tuliokufundisha kama engineer lete soultion halafu unatutajia majina ya wanasiasa!

  Ni utoto kuanza kuwaza kwamba watapuuza kwani anayefikiri hivyo basi huenda ni mtoto wa juzi ambaye hajui kuwa hata mwanzilishi wa CCM yaani Nyerere ilifika mahala wakampuuza akiwa hai!
   
 20. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,124
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Hivi jamani,

  Siyo kwamba siku yenyewe ni mgao wa umeme kwenye eneo la kutano huo!
   
Loading...