Electoral votes na namna rais wa Marekani anavyopatikana

Electoral votes na namna rais wa Marekani anavyopatikana

Electors wasipo mpa Trump kura, ita angalia kama Clinton atapewa kura zika fika 270,atakuwa ndiye rais
Lakini ikitokea electors wengi waka haribu kura basi clinton asifikishe 270 wala Trump asifikishe 270 uchaguzi utapelekwa kwenye baraza la wawakilishi ambao hao wata mchagua rais.
Mkuu bado huwa sielewi bunge la marekani lilivyo,tofauti ya senate na congress ni ipi? katika hao wakina nani wanaweza kupiga kura ya rais kama ilivyotokea huo mwaka 1824?
 
Kumekuwa kuna maswali mengi, kwa nini Trump amepitwa kwa kura lakini kashinda Uraisi? Nataka nitolee maelezo ili tupate kujua kama ifuatavyo, japo maelezo yatakuwa mengi kidogo.

Rais wa Marekani hupatikana kutokana na wingi wa 'electoral votes' ambazo ni kura maalum zinazo wakilisha maamuzi ya jumla ya watu wa majimbo mbali mbali ya marekani. Na hili ni jambo la kikatiba na kundi la wapiga kura za electoral votes huitwa electoral college

Kwanini electoral college?
Marekani ni muunganiko wa majimbo {federal state) na si jamuhuri ya watu wa marekani kama ilivo TZ (republic) hivo, rais lazima ashinde uwakilishi mwingi wa majimbo na si idadi ya watu.
Pia waanzilishi wa taifa la marekani waliona majimbo makubwa yata wanyanyasa majimbo madogo, kwani kama mfumo wa wengi wape ukitumika mwenye jimbo dogo ndio asingesikilizwa kila maamuzi yanapo fanyika yakiwemo ya uchaguzi

Idadi ya electoral votes
Zipo 538 amabzo zina wakilisha idadi ya viti vya majimbo yote kwenye baraza la wawakilishi (435) na seneti (100) pia kwa sababu washington si jimbo ila ni wilaya maalum yenyewe inapata nafasi (3) za upendeleo hapo unapata jumla ya 538. Ili uwe rais wa Marekani lazima ufikishe electoral votes kuanzia 270 ambayo ni zaidi ya nusu ya electoral college yote.
Majimbo mengi mshindi huchukua electoral votes zote, kasoro Maine na Nebraska ambapo mshindi na mshindwa hugawana electoral votes ikiwa mshindwa kashinda kwenye congresional district pia.

Electors ni kina nani?
Kwa kuwa katiba ya marekani hairuhusu wawakilishi au maseneta kupiga kura kama electors, kila jimbo huwa na utaratibu wake wa kupata watu watakao kwenda kupiga kura rasmi katika electoral college, ambao wengi hutokana na chama kilicho shinda kwenye jimbo hilo, pia wengi huwa hawajulikani kwani ni hatari kwa usalama wao na ili kuepuka vishawishi mbali mbali siku ya kuchagua yenyewe. Tukio la kupiga kura rasmi hufanyika siku tofauti na uchaguzi wa wananchi, mfano mwaka huu kura rasmi za electoral college zitapigwa disemba 19, na hapo ndio trump atathibitshwa rasmi kama rais mteule. Electors wanaweza kubadili mawazo kwa kuchagua mgombea ambaye jimbo lake halikumchagua. Kwa hiyo hata Rais mteule Trump bado hajapita rasmi kwani electoral college inaweza kuwageuka wana nchi wao hiyo tarehe 19 ya mwezi ujao. lakini hii huwa ngumu sana kwani majimbo mengi yana viapo vikali ili kuhakikisha hubadilishi kura yao kwa hiyo tuna tegemea apite

Kama wagombea wote hawata fikisha electoral votes270
Uchaguzi hupelekwa kwa baraza la wawikilishi ambao huchagua rais kwa niaba ya majimbo yao, lakini huchagua wanavo taka, hivo hii huwa faida kwa chama kilicho na wabunge wengi.

Faida na hasara za electoral college
Faida zake ni kuwa majimbo makubwa pekee ni ngumu kuamua mshindi, mfano county ya Los Angeles peke ina watu milioni 8.2, hii ni sehemu tu ya jimbo la California, lakini jimbo zima la idaho lina watu milioni 1 hivo inawezekana hata wakat wa kampeni wagombea wakapiga kambi LA na wasikanyage Idaho hivyo jimbo zima la Idaho kupoteza umuhimu katika maamuzi makubwa ya nchi. Pia mara nyingi watu walioko mijini ambao kwa kawaida huwa wengi si rahisi kuwa control watu walioko vijijini kwani huwa wachache, mfano uchaguzi huu watu wa vijijini ndio wame mpitsha Trump kwa wingi kuwa rais, faida nyingine ni kwa kuwa marekani huwa na wagombea wawili tu wenye nguvu hivo kila jimbo huwa na umuhimu kwani kila electoral vote huwa ina changia kushinda mfano clinton kashindwa Wisconsin kwa sababu hakwenda kupiga kampeni akidhani atashinda kwani ni jimbo linalopendelea kuchagua democrat hivo kapoteza electoral votes 10 zilizo enda kwa Rais mteule Trump

Hasara
Mfumo huu hata wamarekani wenyewe wengine hawaujui ndio maana unaona kelele nyingi, askudanganye mtu kwa kuwa yuko USA wengi hawaujui na kwa kuwa hutokea mara chache mambo yakawa kama ya Rais mteule Trump basi wanakasirika halafu wanasahau na kupuuzia.
Pia kwa kuwa kuna majimbo ambayo siku zote yamekuwa yaki jihusianisha na vyama, mengine huwa democrat mengine huwa republican, wagombea hutumia muda wao mwingi kuwepo kwenye majimbo ambayo hubadilika badilika kama vile Ohio na Florida.
Hasara nyingine mtaongeza wenyewe.

Mwisho
Ni mara chache sana hutokea hali kama hii ambapo mshindi wa jumla aka shindwa kuwa raisi na imetokea mwaka 1824, 1876, 1888, 2000, na 2016.
Hivo kura za wamerekani zina umuhimu katika kuamua electoral vote ya jimbo la mpiga kura iende kwa nani, pia ina ondoa uwezekano wa watu wengi wa sehemu moja kuwa amulia watu wa maeneo mbali mbali, mfano rais mteule Ttrump kashinda majimbo karibu 30 kati ya 50 hivo majimbo mengi yana mtaka yeye.

*Karibuni kwa masahihisho au nyongeza
Hongera kwa ufafanuzi wako wa kina kwa lugha rahisi kuhusu Uchaguzi wa Marekani.

Pole kwa maswali tunayokuuliza na hongera kwa kujaribu kumjibu kila mmoja.
 
Alicho pata juzi Trump ni alocation ya electoral colleges, ndio maana mpaka sasa hivi matokeo ya jumla hayaja tangazwa, zile kura zimeonesha kuwa siku ya kura rasmi, mpaka sasa majimbo yame amua Trump apewe Electoral votes 301, Clinton 222 hivo siku ya kura rasmi tuna tegemea wapewe hivo.

Lakini katiba iliwapa uhuru electors ili kama mgombea ambaye watu walimchagua ana dalili zote za kuto faa kuwa rais(mfano amethibitika ni kichaa), wao wabadilishe matokeo kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa.
Ili hili la watu kutegemea eti matokeo kubadiriki wanashauriwa kufuta tu, kwani kama hizo kura hazikuweza kubadili matokeo yaliyokua na utata na tofauti ndogo ya George Bush, wasitaraji kama yatabadili matokeo yenye gap kubwa hivi ya 301 didi ya 222.
Zaidi waliompinga wote wameanza kumpongeza na kumuahidi ushirikiano, huku Hillary akionyesha dalili zote za kuchanganyikiwa huku akiwatupia lawama watu waliomsaidia akiwemo Obama. The way is green for Trump.
Besides, never put your money against Trump.
 
Ahsante sana na kweli nimeona umeelewa
Kilicho mpitisha Trump ni kashinda states nyingi
Kilicho mfanya clinton kupata popular vote ni kashinda states chache zenye watu wengi, na state ndogo ambazo watu wana mlengo mmoja wa kisiasa na kimaisha kwa hiyo kura yake haikugawanywa sana.
Hata hivo ishu siyo kubwa kama watu wanavo sema
Kwa source yangu mimi ina niambia
Trump kashinda states 30-20
Katika wapiga kura milion 125 trump kapitwa kura chini ya laki 4

Lakini Trump kapata electoral votes 306 kwa 232, bado Trump kafanya vizuri sana, hizo kura za jumla hata si kigezo cha kulalamikia uchaguzi.
Shukran sana mkuu Iceman 3D, sasa nimeelewa. Umefanya la maana sana kuanzisha huu uzi, maana wengi tulikua hatujui haya mambo. Tushazoea bongo na figisu figisu za jecha. Asante pia kwa kujibu maswali ya watu kwa moyo bila kuchoka. Ubarikiwe
 
Mkuu bado huwa sielewi bunge la marekani lilivyo,tofauti ya senate na congress ni ipi? katika hao wakina nani wanaweza kupiga kura ya rais kama ilivyotokea huo mwaka 1824?
Bunge la marekani linaitwa Congress, Congress imegawanyika katika makundi mawili
Seneti na jumba la wawakilishi (house of representative)

Kama uchaguzi usipo pata mtu aliye fikisha electoral votes 270, rais huchaguliwa na jumba la wawakilishi
Seneti itamchagua makamu wa rais

*ukitaka kulijua vizuri bunge la US post #34 nime lielezea vizuri
 
Hongera kwa ufafanuzi wako wa kina kwa lugha rahisi kuhusu Uchaguzi wa Marekani.

Pole kwa maswali tunayokuuliza na hongera kwa kujaribu kumjibu kila mmoja.
Ahsante kwa kuchangia uzi huu, nashukuru pia kwa kunipa changamoto ya maswali na kwa kuelewa.
Shukran
 
Ili hili la watu kutegemea eti matokeo kubadiriki wanashauriwa kufuta tu, kwani kama hizo kura hazikuweza kubadili matokeo yaliyokua na utata na tofauti ndogo ya George Bush, wasitaraji kama yatabadili matokeo yenye gap kubwa hivi ya 301 didi ya 222.
Zaidi waliompinga wote wameanza kumpongeza na kumuahidi ushirikiano, huku Hillary akionyesha dalili zote za kuchanganyikiwa huku akiwatupia lawama watu waliomsaidia akiwemo Obama. The way is green for Trump.
Besides, never put your money against Trump.
Ni kweli
Kwa sasa ni 306 kwa 232
Hiyo ni ushindi wa kishindo kwa electoral college.
Trump ndiye rais wa 45 wa US hakuna namna

Kina Clinton saa hii mara wamlaum Obama, mara Comey, mara vyombo vya habari, ukishndwa bila kutegemea ni tabu sana
 
Shukran sana mkuu Iceman 3D, sasa nimeelewa. Umefanya la maana sana kuanzisha huu uzi, maana wengi tulikua hatujui haya mambo. Tushazoea bongo na figisu figisu za jecha. Asante pia kwa kujibu maswali ya watu kwa moyo bila kuchoka. Ubarikiwe
Nshukuru sanabkwa kupitia kwenye uzi huu na kuchangia ndugu yangu
 
huu mfumo mgumu sana kwangu kuuelewa siutofautishi na kitu kinaitwa bit coin kimo humu ndani, nimesoma weeeeeee lkn wapi! ahaa hata hivyo siitaji kujua kila kitu.
 
Tatizo yule jamaa ushabiki ulikuwa mwingi kuna vitu alikuwa ana ongea nikawa naombea visitokee ili nione ata semaje, sijajua ana hali gani huko US mpaka sasa
Mkuu wewe ni mwalimu wa walimu, mkuu pamoja na maswali ya Jf umekuja na kujibu kwa ufasaha na kwa kurudia tena bila kinyongo, salute sana man, una Moyo mkuu

Binafsi ukinipa pepa leo kuhusu uchaguzi wa marekani napata 100 kwa darasa ulilotoa. Kila siku niliona kwa Tv na redio nilisikiliza, wachambuzi sikuambulia kitu ILA leo najua mengi sana.

Sasa ni comment
Kwa maelezo haya sijaona ubaya wa electoral Votes, zinatoa Democrasia chanya kwa watu wote kusikilizwa hasa kuanzia minority to Majority vinginevyo rais wa marekani angeamuliwa na akina Calfonia kila siku.

Naweza litazama hili kama vile Nchi tano za jumuia ya A.mashariki tukiamua kuwa na Rais mmoja, uwezi sema tufanye majority vote iwe final say, nchi kama Burundi, na Rwanda, Sudani kusini watakuwa hawana sauti, bila shaka Rais ataamuliwa na Kenya na Tanzania daima. Ivo electral vote zinawapa sauti hadi wadogo nakufanya walio wengi wasiwe na maamuzi ya mwisho.

Naona huu mfumo uwe injected kwenye Bunge la Tanzania, tuondoe zile Kura za wingi wa CCM

Once again, Tank yo for da clas bros
 
huu mfumo mgumu sana kwangu kuuelewa siutofautishi na kitu kinaitwa bit coin kimo humu ndani, nimesoma weeeeeee lkn wapi! ahaa hata hivyo siitaji kujua kila kitu.
Pole mkuu
Ni mfumo ambao hata walioko marekani wenyewe wengine wanashindwa kuelewa, ila nimetafuta namna ambayo ninge eleza ki urahisi zaidi pengine ungeelewa.
 
Mkuu wewe ni mwalimu wa walimu, mkuu pamoja na maswali ya Jf umekuja na kujibu kwa ufasaha na kwa kurudia tena bila kinyongo, salute sana man, una Moyo mkuu

Binafsi ukinipa pepa leo kuhusu uchaguzi wa marekani napata 100 kwa darasa ulilotoa. Kila siku niliona kwa Tv na redio nilisikiliza, wachambuzi sikuambulia kitu ILA leo najua mengi sana.

Sasa ni comment
Kwa maelezo haya sijaona ubaya wa electoral Votes, zinatoa Democrasia chanya kwa watu wote kusikilizwa hasa kuanzia minority to Majority vinginevyo rais wa marekani angeamuliwa na akina Calfonia kila siku.

Naweza litazama hili kama vile Nchi tano za jumuia ya A.mashariki tukiamua kuwa na Rais mmoja, uwezi sema tufanye majority vote iwe final say, nchi kama Burundi, na Rwanda, Sudani kusini watakuwa hawana sauti, bila shaka Rais ataamuliwa na Kenya na Tanzania daima. Ivo electral vote zinawapa sauti hadi wadogo nakufanya walio wengi wasiwe na maamuzi ya mwisho.

Naona huu mfumo uwe injected kwenye Bunge la Tanzania, tuondoe zile Kura za wingi wa CCM

Once again, Tank yo for da clas bros
[emoji120][emoji122] nashukuru umeelewa na umeiweka kwenye uhalisia wetu zaidi, hahaha! wewe ni mwalimu zaidi yangu kwa ulicho kiandika hapo ni excellent na umeifanya iwe simple kuielewa kwa mtu yeyote

Shukrani kwa kupitia uzi huu ndugu yangu
 
Mkuu wewe ni mwalimu wa walimu, mkuu pamoja na maswali ya Jf umekuja na kujibu kwa ufasaha na kwa kurudia tena bila kinyongo, salute sana man, una Moyo mkuu

Binafsi ukinipa pepa leo kuhusu uchaguzi wa marekani napata 100 kwa darasa ulilotoa. Kila siku niliona kwa Tv na redio nilisikiliza, wachambuzi sikuambulia kitu ILA leo najua mengi sana.

Sasa ni comment
Kwa maelezo haya sijaona ubaya wa electoral Votes, zinatoa Democrasia chanya kwa watu wote kusikilizwa hasa kuanzia minority to Majority vinginevyo rais wa marekani angeamuliwa na akina Calfonia kila siku.

Naweza litazama hili kama vile Nchi tano za jumuia ya A.mashariki tukiamua kuwa na Rais mmoja, uwezi sema tufanye majority vote iwe final say, nchi kama Burundi, na Rwanda, Sudani kusini watakuwa hawana sauti, bila shaka Rais ataamuliwa na Kenya na Tanzania daima. Ivo electral vote zinawapa sauti hadi wadogo nakufanya walio wengi wasiwe na maamuzi ya mwisho.

Naona huu mfumo uwe injected kwenye Bunge la Tanzania, tuondoe zile Kura za wingi wa CCM

Once again, Tank yo for da clas bros

wewe jamaa umeelewa vizur sana,,,, hata mimi mfano uliokuja kichwan ni huu wa EAC....... ....

ukiweka Tz, Ken, Ug, Rwd, Burund, Zanz, South sudan iwe nchi moja na zitoe raisi mmoja utagundua popular vote haifai.......

kwa mazingira hayo Tz, Ken na Ug ndio wataamua utawala na hvo nchi zngne zitakua neglected na watawala.......

ndio maana mimi kila nikiutafakari huu mfumo wa USA ambao uhai wake ni miaka 200 nagundua hawa walioutengeneza walikua na akil sana tena waliona mbali.......... walkua na haki ya kututawala 100%.......

angalia sisi tulivofanya upumbavu kwenye muungano, yaan chama kinaweza kisipige kampeni zenj na wala kisiwe na wabunge kule lkn kikipata support ya Tanganyika kitatawala Tz nzima.......

mpk leo wabunge toka zenj hawana sauti kabisa ktk bunge la JMT, wala kura zao mgombea urais hua hazihitaj kabisa as hazimwongezei chochote!!!...........

huu mfumo mzur sn aisee, uje na hapa kwetu
 
Hongera sana mkuu kwa uchambuzi wako,lakini bado kuna vijimaswali je hizo au hao electral votes ni watu au ni vitu gani?? naomba majibu kwa kutolea mfano ingekuwa Tz
 
Asante sana. Umenisaidia sana kufahamu haya. Ninatamani gr hili lingejielekeza kwenye mambo ya ufahamu kama haya. Maana wataalamu wamo humu humu.
 
Back
Top Bottom