eFootball Special Thread

Kitu ambacho tunapaswa kujua ni kuwa hizi individual instructions kila mtu anaweka kwa mapenzi yake kulingana na mahitaji ya kikosi chake.

Ni vizuri kutumia kwa CF kama maelezo hayo yalivyo lakini lazima uelewe kwamba ukimpa anchoring CF hatokuwa na mikimbio mingi ya kuweza kuwavuta mabeki na inaweza kuwa rahisi kwake kufanyiwa marking.
 
Dah we mkorofi sana🀭 Razorblade πŸ˜€
Hanisumbui huyo πŸ˜‚, binafsi siwezi mpa CF instruction ya anchoring maana hawezi fanya kazi navyotaka ila mtu kama Selikavu hawezi elewa πŸ˜‚

Leo asubuhi kwenye PvP event nimekutana beginner kipindi cha kwanza tumecheza vizuri ila kipindi cha pili akafanya ujinga kumark CF wangu halafu akanifunga kwa smart assist.

Sasa embu fikiria ndo unampa anchoring CF halafu unakutana na mtu anawamark hapo inakuwa kazi juu ya kazi.
 
Hakuna aliyekupangia kaka ni kwenye harakati za kuelekezana plus utani nothing serious mzeeπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ


Kwanza leo twende room kaka nina kikosi kipya cha moto balaa
 
Kiukwel siwezi elewa ndugu watazamaji🀣
 
Yeah Individual instructions zinaendana na mechi husika kuna muda zinaweza kufanya kazi kwa opponent huyu halafu kwa opponent mwingine zikakataa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…