Edward Ngoyai Lowassa alishiriki vita vya Kagera

Edward Ngoyai Lowassa alishiriki vita vya Kagera

Joined
Oct 17, 2015
Posts
46
Reaction score
46
EDWARD NGOYAI LOWASSA ALISHIRIKI VITA VYA KAGERA

Ninamfahamu vizuri Edward Lowassa. Nilibahatika kuwa mmoja wa Walimu wake wa Siasa alipokuwa Afisa Mwanafunzi Kundi la Nane (Intake 08) mwaka 1978 katika kilichokuwa kinaitwa Chuo cha Taifa cha Uongozi (CTU), Wilaya ya Monduli. Alipata Kamisheni ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania mwaka huo huo 1978.

Akiwa Luteni, Edward Lowassa alishiriki kikamilifu Vita vya Kagera akiwa 206 KV (Kundi la Vikosi) chini ya Brigedia Jenerali Silas Mayunga. Baadaye Kundi la Vikosi 206, liliongezewa nguvu maradufu na kupewa jina la Task Force, likiongozwa na Meja Jenerali Silas Mayunga.

Task Force ilifanyika kazi kwa weledi na ujasiri mkubwa na kufanikiwa kukomboa maeneo yote Magharibi ya Uganda hadi kuukamata mji wa Koboko uliopo mpakani mwa Uganda na Sudani Kusini, alikozaliwa Nduli Iddi Amin. Koboko ilikombolewa tarehe 3 Juni 1979, siku inayohesabiwa kama ndiyo mwisho wa Vita vya Kagera.

Mimi nilikuwa Afisa Mnadhimu Makao Makuu ya Task Force na kipindi chote hicho tulikuwa naye Lt Edward Ngoyai Lowassa.

Lt Col Patrick Marwa Nyaborogo (Mstaafu)
Tel: 0789 392013
Email:nyaborogopm@gmail.com
 
Sawa. Ila angetueleza pia kuwa alishiriki kwenye hiyo vita akiwa mtumbuizaji kutokana na sanaa yake ya uigizaji na vichekesho
 
Kumbe Lowasa ni Luteni. Huyu ndio kamanda wa ukweli! Mkuu wa maelezo tafadhali tueleze pia nafasi ya magufuli kwenye vita hivi vya kagera. Ama ni yeye ndie aliyejenga daraja pale Mutukula!
 
Kumbe Lowasa ni Luteni. Huyu ndio kamanda wa ukweli! Mkuu wa maelezo tafadhali tueleze pia nafasi ya magufuli kwenye vita hivi vya kagera. Ama ni yeye ndie aliyejenga daraja pale Mutukula!

daraja la kyaka wala mutukula haina daraja
 
Kikosi cha mayunga ndicho kilikuwa tegemeo kubwa sana kwenye vita hiyo,ndio maana baada ya vita pale mjini bukoba likawekwa sanam kubwa la mayunga kwenye uwanja wa Uhuru platform,which means lowasa naye alikuwa sehem kubwa ya mafanikio hayo
 
Labda alikuwa mtumbuizaji!!

Mleta mada hii kitu iko kwenye CV YAKE?
 
tunaomba majibu magufuli alishiriki vita? sio kupiga pushup uku akishangiliwa tunataka mwanaume aliepiga pushup uku risasi zikirindima
 
Haya sasa fisiemu tuambieni tena jipya. Awamu hii si ajabu mtasema hakuzaliwa Tanzania
 
Sasa hapa kati kilimpata nini mpaka akaja kuwa fisadi wa karne!
 
Mwanaume wa kweli huwa hapandi juu ya bati kujieleeeeezaa.....anatulia na kuacha ukweli udhihiri.
 
]kama watu kama makamba jk na kinana hawana taarifa ya ushiriki wa lowassa vita vya uganda ni jeshi tu ndio lingeweza kutupa taarifa sahihi. vinginevyo ni muendelezo wa uongo na usanii.

atoe japo picha kuthibisha. tumeona picha za wanasiasa wakiwa vijana jeshini kama jk na kinana.

uongo una mwisho wake.
 
kama watu kama makamba jk na kinana hawana taarifa ya ushiriki wa lowassa vita vya uganda ni jeshi tu ndio lingeweza kutupa taarifa sahihi. vinginevyo ni muendelezo wa uongo na usanii. atoe japo picha kuthibisha. tumeona picha za wanasiasa wakiwa vijana jeshini kama jk na kinana. uongo una mwisho wake.

Nani alikwambia JK alishiriki vita vya Kagera ingawa alikuwa mjeshi?unajua JK aliondokaje jeshini Monduli?Unataka jeshi litupe taarifa za ushiriki wa Lowassa ktk vita ilhali limeshindwa kutoa taarifa ni wapi alipokuwepo mkuu wake baada ya kumaliza ziara ya kikazi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom