Edward Lowassa special thread

Mkuu,
Yale unadhani wewe/yeye ni maamuzi magumu kwa watu wengine yanaweza yakawa ni maamuzi rahisi sana.

Nimesema Lowassa anaweza kuondoka CCM kama atakuwa amejihakikishia kama CCM haichaguliki tena katika kiti cha Urais wa Tanzania. Kinyume cha hivyo, hawezi kuhama CCM.
 
Vaeni tisheti zenu tu muondoke hapo dodoma.tayari jina la fisadi limeondolewa .hafai hata kidogo.
 
wanafanya nini wote hao 3600 Dodoma hawana kazi za kufanya huko makwao

Hawana kazi ya kufanya na wamelipiwa kila kitu na mafisadi Kwa nini wasiwe Dodoma?nitawashangaa ccm kuchagua MTU kwa shinikizo la fedha.shame on you mafisadi.
 
Mkuu,
Kwangu mimi sifahamu upinzani watachukua nchi lini lakini ninachofahamu kama ulivyosema, Lowassa hawezi kuhama CCM kama ana amini CCM bado inachagulika katika kiti cha Urais wa Tanzania.

Watu walio nyuma yake hawawezi kumruhusu kuhama CCM na CCM ya sasa haiwezi kumruhusu kuhama CCM kwa amani!
 
3600 duu,hapo inabidi timu eddo wavae tsheti mbilimbili,ili kama ikitokea jina lake likikatwa basi wanatoa ya juu,wanabaki na tisheti nyingine mbadala.
 
Tunachojua ni kwamba ukweli ndiyo huo na sisi vijana wengine yupo Iringa na sehemu nyingine za nchi huu ndiyo uwamuzi wetu vijana. Tupeni chaguo letu la siyo basi tusilaumiane mbele ya safari. Tuonaomba tutendewe haki tukashindwe kwenye kura!
Hata mimi ni kijana na wala simtaki hata kidogo. Aelezee kwanza ilikuwaje huko Richmond. Vinginevyo huna hoja
 
mkuu yote uliyoandika yanaukweli na logic ila hilo la kuwapa redet bil 35.5 bila shaka ume-exaggerate

 
Mungu tuepushe mbali na huyu fisadi lowassa asije akawa Rais JMT,Mungu tunakuomba sana huyu mwizi asie na aibu,mtoa rushwa mkubwa huyu tuepushie mbali
 
Sema kabisa utagawa kabaang... ubet na watu... uone utafanyiwa nn...!!!!

Lowassa anapita iwe mchana au ucku...!!!

Huu ndio wakati wake...mmanina...!!!
 
kwanini unishangae kwa kutoifahamu ccm vizuri? what the hell is ccm?

umeharibu mada yako kwa kipengele hicho tu. byeee
Mkuu,
Kuharibu mada siyo tatizo, tatizo ni kutokuikarabati mada unayodhani imeharibika!

Kama huifahamu vizuri CCM hata uwezo wako katika kutoa maamuzi ya kisiasa katika sanduku la kura utakuwa umekosa mwelekeo unaofahamika.

Watu wenye fikra pana huwa hawapigi kura kwa kutumia msukumo wa ushabiki bali kwa kutumia sera, Ilani za Vyama na ahadi binafsi za wagombea.

Kama ungefahamu CCM ni chama kikongwe barani Africa kuongoza nchi kwa kipindi kirefu mfululizo nadhani usingepata hata nguvu za kuandika what the hell is CCM!
 
YAH.TAMKO LA KUPONGEZA KAULI YA MKUU WA MKOA WA MWANZ NDUGU STANSLAUS MAGESA MULONGO.



Ndugu wanahabari na watanzania wote.

Kwanza nitumie fursa hii kuwashukuru kwa kuitikia wito na kukubari kuja kuungana nasi kwa lengo la kuwajuza watanzania kwa kile kinachoendelea katika mkoa wetu Wa mwanza kwa faida na manufaa ya watanzania wote.






Siku ya 6/7/2015, mkuu wetu wa mkoa Wa mwanza alitoa maelekezo kwa makamanda wa polisi kuzuia watu wasio kua na malengo mazuri kwa nchi yetu na taifa letu. Wanao kwenda Dodoma kwa lengo la uvunjifu wa amani,katika kipindi hiki cha mchakato
wa vikao vinavyoendelea vya kuchuja na kupata kiongozi atakae peperusha bendera ya chama cha mapinduzi,Huo ni wajibu wake akiwa ni mwenyekiti Wa kamati ya ulinzi na usalama
wa mkoa, na ndio muwakirishi Wa rais kwa ngazi ya mkoa anawajibu na kila sababu ya kukemea,kuonya,kushauri na kuelekeza mambo yote yanayohusu raia
na Mali zao hivyo sisi wana mwanza na watanzania kwa ujumla hatukuona ubaya Wa aina yeyote kwa kauli ya mkuu wetu wa mkoa.



Cha kusikitish Jana 7/7/2015. Kuona katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari mtu

anae jiita mtemi Sylvester yared. ambae ndio mratibu Wa genge la vijana wahuni wanaojiita 4U movement. Akidhihaki na kupinga tamko la mkuu wetu Wa mkoa wa mwanza. Binafsi nilishitushwa sana


Katika Katiba yetu ya chama cha mapinduzi na kanuni zake tuna jumuiya tatu
1.Jumuiya ya wanawake(UWT)
2.Jumuiya ya wazazi
3.Jumuiya ya vijana (UVCCM)
Ndani ya cham cha mapinduzi hatuna taasisi wala jumuiya inayoitwa 4Umovement.
Swali la kujiuliza jeuri, kiburi na mamlaka ya kuunda chombo kisicho rasmi chenye lengo la kuvuruga,kuhatarisha mustakabari wa chama chetu na Taifa letu kwa maslahi ya mtu binafsi,anaetumia kundi la vijana wasio jitambua kwa gharama yeyote ili aingie ikulu,na huyu si mwingime bali ni ndugu Edward Lowasa.




Ninayaongea haya kwa ushahidi, ninao hapa viongozi wawili kutoka kundi la mabaunsa na machinga,wa mkoa wa mwanza ambao walifatwa na kupewa kazi ya kuandaa na kukusanya vijana wasiojielewa kwa lengo la kwenda Dodoma. Kushinikiza viongozi Wa chama kumchagua mgombea wao, na kundi jingine la vijana na akina mama Wa CCM kusimama njiani kusimamisha misafara ya wajumbe Wa NEC, na mkutano mkuu wa chama Taifa kuwapa shinikizo na vitisho, kwamba lazima warudi na mgombea wao ndugu Edward Lowasa.Hayo yote yanafanywa kwa malipo, Na kila kijana atalipwa tsh 100,000.kwa kila siku ,kwa siku zote atakazo fanya kazi, mpaka kieleweke.






Ndugu wanahabari Mimi kijana mzalendo wa Tanzania ninapata wakati mgumu na Mashaka makubwa pindi ninapo ona mtu ambae hakubaliki katika jamii ya watanzania mwenye madoa na kashfa chungu nzima tena afya yake ikiwa ya kususua analazimisha kwa kutumia gharama kubwa ili afike Ikulu mtu huyu kwa kauli ya hayati baba Wa Taifa,namnukuu, Tumuogope kama ukoma hafai.mwisho wa kunukuu.





Nimalizie kwa kuwashukuru na kuwapongeza viongozi wetu wakuu wa chama na serikali kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kujenga na kuimarisha chama na serikali kwa kutatua na kusimamia maslah ya watanzania, Mwisho kwa nafasi ya kipekee niwashukuru wanahabari wote mlio hudhuria na watanzania wote mnao nisikiliza na kunitazama.Mungu kibariki chama chetu CCM, Mungu ibariki Tanzania.






Imeandaliwa na
Hussein.A.kimu
Mw/kiti UVCCM(W)nyamagana mwanza.
 
Inamaana kujaa huko kunaonesha wengine sio bora ila lowassa pekee? ?. Vipi kingu anawekwa position gani maana nasikia kwa lowassa mmeshajipa mpaka vyeo
 
Mtaji mkubwa wa El ni anawapata na kuwatumia wajinga na wapumbavu kama hawa wakina .. budget
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…