Edward Lowassa special thread

Edward Lowassa special thread

SAFARI ya matumaini kuelekea ikulu imewadia. Tulianza pamoja kwa umoja na tutamaliza pamoja kwa umoja. Tumaini letu ni kwa mgombea mwenye maamuzi.

Njoooni hapa wana LOWASSA tupeane update kwa yanayojili tangu sasa mpaka magogoni. TAREHE 30 mei 2015 Mr Edward Ngoyai lowasa kwa kishindo kikubwa azindua safari ya matumaini jijini arusha. Maelfu wamiminika. Mzee msukuma, kangi lugola na Mzee Kingungwe wasababisha mtikisiko taifa.

Gwajima naye ahofiwa kuleta Maelfu! Safari ya,lowasa yaonesha matumaini kwel kweli TAREHE 31 mei, Mr WASIRA naye akifuata nyayo za mbunge wa monduli atangaza nia. Kikongwe huyu wa miaka 80 anataka kuliongoza taifa la TANZANIA.

Taifa limeshuhudia watu wachache katika ukumbi wakijitokeza kumsikiliza. Pia Tofauti na lowassa ni watu wachache wamejitokeza kumuunga mkono waakiwemo mbunge Nyangwine aliye poteza sifa na kukataliwa na watu wa tarime.

Kuthibitisha kuwa Lowassa ni Jembe Wassila hakusita kuonesha woga wake. Alimtupia Kijembe Lowassa kwa ile hoja dhaifu akidai kuwa eti ikulu haiongozwi na mafisadi.

TUNAMTAKIA MAPUMZIKO MEMA WASSIRA kwani hawezi kufurukuta katika nafasi ya uraisi, hata jimboni kwake anamshindani wake pia.

====================================
Endelea kufahamu kidogo kidogo kuhusu Lowassa
====================================

Lowassa alizaliwa tarehe 26 August 1953 mkoani Arusha. Ni waziri wa 8 wa JMT akipokea kijiti kutoka kwa Mh Fredrick Sumaye kutoka 30 Desemba 2005 hadi 7 Februari 2008 na kumuachia Mh Mizengo Pinda ambaye hadi tunavyooandika hapa ndie waziri mkuu wa JMT nae ametangaza nia ya kugombea urais kwa tiketi ya ccm mwaka 2015!


Kabla ya kuwa waziri mkuu, Lowassa alikuwa waziri wa Maji na Maendeleo ya mifugo kuanzia mwaka 2000 hadi 2005 akiwa chini ya rais Mkapa. Wizara hii alimuachia Mh Stephen Wassira baada ya yeye kuteuliwa kuwa waziri mkuu mwaka 2005. Aliingia bungeni kama mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM mnamo Novemba, 1995.

Lowassa aliwahi kuwa waziri katika ofisi ya waziri mkuu kipindi cha pili cha urais wa Mh Ali Hassan Mwinyi. Mwaka 1995 alianza harakati zake za kuwania urais wa JMT ndani ya CCM. Hakufanikiwa kupata ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM mwaka huo wa 1995 hivyo aliamua kugombea ubunge wa jimbo la monduli na kushinda kwa zaidi ya 90%.

Mnamo mwaka 1997 aliteuliwa kuwa waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais - mazingira na umaskini. Lowassa alidhihirisha uwezo wake wa kiongozi zaidi akiwa waziri wa Maji na Mifugo kuanzia mwaka 2000 hadi 2005.

Mwaka 2005 Lowassa aliacha harakati zake za kuusaka urais badala yake akaanza harakati za kumuunga mkono Mh Jakaya Kiwete kwenye mbio zake za urais. J Kikwete alikuwa ni rafiki yake wa muda mrefu sana, naye Lowassa alikubali kuwa campain manager kwenye mbio zake urais, ambapo Mh Jakaya Kikwete alishinda urais wa JMT kwa zaidi ya 80% chini ya menejimenti ya Lowassa

===================
Elimu ya Edward Lowassa
===================

Lowassa alipata shahada yake ya sanaa na elimu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na Shahada ya uzamili ya Maendeleo ya jamii kutoka Chuo Kikuu cha Bath kilichopo UK.

Elimu yake ya sekondari alipata kutoka shule ya Ilboru moja ya shule maalum kwa ajili ya wanafunzi wenye vipaji maalum darasani wakati huo; na kumalizia elimu yake ya kidato cha 5 na 6 kutoka shule ya sekondari Milambo mwaka 1977. Lowassa anapozungumzia maendeleo anajua anachozungumzia, habahatishi.

===================================
General summary kuhusu utumishi wa Lowassa
===================================


  • Mkurugenzi Mtendaji, AICC, 1989 - 1990
  • Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais (Sheria na mambo ya bunge), 1990 - 1993
  • Waziri wa ardhi na maendeleo ya makazi, 1993 - 1995
  • Waziri wa nchi, makamu wa rais - mazingira na umaskini, 1997 - 2000
  • Waziri wa maji na mifugo, 2000 - 2005
  • Waziri Mkuu, 30 Desemba, 2005 - 7 Februari 2008

Alianza kuwa mbunge tangu mwaka 1990, na kuteuliwa kuwa waziri kama tulivyoonyesha hapo juu! Hadi sasa bado ni mbunge alietia nia kuwania urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2015

Kauli mbiu yake: Safari ya matumaini

=========
updates
=========

Steven Wassira na Makongoro Nyerere wakutana na kihunzi kikali ndani ya ya fomu ya kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM. Kwa maelezo zaidi soma hapa chini:




Baada ya kumaliza kusoma hio comment hapo juu sasa soma hii thread hapo chini:

Makongoro Nyerere na Steven Wassira wanyong'onyea ghafla kwenye mbio za urais, Lowassa anaendelea kufanya yake

----------------------------------------------------------------------------------------------------------
----------------------------------------------------------------------------------------------------------
(d).Uanachama katika vyama vingine

i. Sijapata/nimepata kuwa mwananchama wa chama kingine cha siasa (Ukiacha TANU na ASP)

ii. Kama umepata taja jina la Chama hicho na muda ulio kitumikia........

KODI YA MAPATO

Je umewahi kupatikana na hatia mahakamani kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali? (ndiyo/hapana)..........

Kama ndiyo eleza ni kodi gani na ulipewa adhabu gani?.....................

6. TABIA

(a). Mashitaka dhidi yangu

i. Je umewahi kushitakiwa kwa makosa ya jinai na kuhukumiwa? (ndiyo/hapana).
(Kama ndiyo, taja kosa na adhabu uliyopewa).....

ii. Nimepata/sijapata kudhibitiwa ndani ya chama au Jumuiya ya chama kwa kosa lolote. (kama umepatata eleza)......

-------------------------------------------------------------------------------------------------------
-------------------------------------------------------------------------------------------------------

Members wanaendelea kudadavua hizo vipengele tajawa hapo juu:















==============================================
Tumeikotoa humu humu JF, endelea kujisomea taratibu!
==============================================



==========================================
Tunaendelea kuokota humu humu JF, endelea kujisomea
==========================================

Maneno mengiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii hayavunji mfupa. Tusubiri July.
 
Bila shaka Raisi Kikwete na watu wake wanahofia vibaya mno kufunikwa na Bw.Lowasa pindi achaguliwapo kuwa Raisi wa JMT na ndio moja ya sababu ya kusuasua na fitina nyingi zisizo maana!

Wanajua wazi ya kwamba kwa maozo waliyoyafanya kwa Miaka 10 waliokaa madarakani Bw.Lowasa atayarekebisha yote ndani ya miezi 6 kwanza kama alivyoahidi ataanza na alipoishia alipokuwa Waziri Mkuu la kuondoa foleni pale alipoanzisha njia tatu wazo zuri lkn alipotoka kama kawaida ya Kikwete &Co wakashindwa usimamizi na mpango kuharibika!

Sasa hii ni hofu yao kubwa wanajua baada tu ya Mwaka wa Utawala wa Bw.Lowasa wananchi wataanza hata kujuta kwa nini hawakuingia brn. kumtoa Bw.Kikwete miaka 8 iliyopita!


Nina uhakika watu kama akina Bw.Nape Nnauye sijui Makonda, Membe, Makorongo & Co. watakuwa hawana nafasi kwenye serikali ya Bw.Lowasa!

Hivi Lowasa atakuwa na ilani yake au ilani ya CCM!?
 
Hivi Lowasa atakuwa na ilani yake au ilani ya CCM!?

Ilani ya CCM ni bora siajabu klk zote Duniani tatizo liko kwenye Utekelezaji na usimamizi na hapo ndipo Bw.Lowasa anapoziba pengo lililopo CCM!
 
Hivi ni kweli kua bado hajatimiza idadi au ndo kaanza kampeni kimtindo CCM tuambieni!!!!!!!
 
Labda hajatimiza idadi yake yeye hatujui ni wadhamini wangapi. Ila wa CCM ni 450 Tanzania nzima ambao karibia waliochukua fomu wote wametimiza. Labda aulizwe kwake yeye idadi ya wadhamini ni wangapi pengine tutamuelewa.
 
Nikweli ndani ya ccm hakuna wa kumkemea mwenzake kwani mfumo unawalinda lakini kwa mamvi imezidi kiburi jeuri fisadi HAFAI KUWA RAISI.
 
Nafikiri ungekuja na ufafanuzi zaidi pengine wengi tusingekuwa na maswali, lkn kusema tu eti jeuri imemzidi hafai kuwa rais, hapo lazima uzue maswali na pengine tuseme umetumwa au ni chuki binafsi.
 
hivi kuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuthubutu kumsimamisha FISADI MKUU kuwania nafasi ya urais??
 
vipi kuna kikao cha dharura kiliitishwa jana na mwenyekit taifa ccm.je kuna mwenye habari
 
I am sure pamoja na matusi yote hapa Lowasa he won't make it . Hakuna wa kumkemea lakini he will be told in the open kwamba hafai na hata amini . Matusi si bisara na haiwezi msaidia Lowasa .
Lowasa ana hasira na amejawa na umimi, hana vision hawezi kujieleza .Kashindwa hata kusema why he stepped down as a PM , kama hahusiki na kashfa then why did he step down ?

Wana CCM wana mheshimu late Mwalimu , so kwa kuwa alisha kataliwa mapema kwa matendo yake nina hakika they are ready to be a cursed political party .Lowasa hana la kutueleza sisi watanzania la kunifanya nimwelewe hana hata mfano kuanza Monduli hadi alikpokuwa Waziri Mkuu . Hana na nasema hana . Tujenge hoja tuone ukweli upi matusi si faida wala msaada kwa a soon ditched Lowasa .
 
Ee Mungu, Wewe Ndo utuchagulie Rais..maana Wewe watizama mioyo na nia Ila Sisi tunatizama kwa macho..Mungu atuchagulie Rais..Wote tuseme Amiin
 
Eti anasema tusiomtaka tuhame, anashindwa kujiuliza
1. Tukishahama yeye atabaki Ikulu kumtawala nani?
2. Ni nchi gani na lini aliona rais anaomba watu awaongoze ila anawatahadharisha wahame kwanza?
3.Tukisema kwa kusema hivyo tayari mgombea kavunja katiba kwa kutangaza mapema vita ya ndani ( civil war ) hats kabla hajawa rais tutakuwa tunakosea?
 
Kama tuliweza kumshitaki Pinda kwa kuvunja katiba akisema wapigwe kwanini isifungiliwe kesi ya kikatiba kwa Lowassa kutishia amani ya nchi hata kabla hajawa rais, huyu akiwa rais si atataka kuichezea katiba yetu ambayo Mwl Nyerere alituhasa asiichezee mtu?
 
Wakuu,

Msafara wa lowassa umepita sasa hivi hapa magomeni mataa wanatokea kariakoo wanaelekea ilala.

Mwanzoni nilizani kuna bodaboda kagongwa na gari maanaa group kubwa la madereva bodaboda wamepita kwa mbwembwe (walikuwa wakipiga honivna kuinua matairi ya mbele ya bodaboda zao).ilinilazimu nisogee nione vizuri ndipo nilipoona msafara wa magari nyumba ya hizo bodaboda.

Huyu mheshimiwa anatisha sana. Yuko vizuri.
 
Back
Top Bottom