Edward Lowassa special thread

Edward Lowassa special thread

Nimekua nikiwasikia baadhi ya watu wakisema, iti lowassa hafai kuwa rais kwa sababu ni fisadi. Sasa kama ni fisadi, kusanyeni ushaidi mpelekeni mahakamani,ni nini kinachowazuia mpaka sasa? Mnabaki kulalamika tu? Mmezaliwa kulala mika nyinyi watuh roho inamuuma Lowassa akiwa rais basi ahame nchi. Kila watu wakijitokeza kumpokea lowassa watu wanasema iti, ananunua wa hivi watu wale wote nani katika hii nchi, anaweza kunnua watu kama wale hata hiyo bajeti ya serikali ya 2015/2016 ya trilion 22.5 isingeweza kuninua wale watu wote. Watanzania tuache kuwa domo kaya, na tuache wivu wa kiume. Mimi naona kabisa lowassa ndio chaguo la watanzania na ccm ikitaka kupoza dira wahuondoe jina la Lowasa.
 
Dira Ya Ufisadi Imezeeka Na Ni Mfu Ndani Ya Chama.

Wenye Misingi Ya Uasisi Wa Chama .. WanaNguvu Zote Toka Kwa Wakulima Na Wafanyakazi.

Afya inaweza kuhamisha Mtu Nchi. lakini Pia Passport.

Ajipime mwenyewe njia atakatumia.
 
Yeye akiwa kama mtumishi wa Umma, huo mtaji wa HISA wa kuweza kumpa mabilioni ya pesa katoa wapi?

wenzako walikua na asset tangu wewe hujawa hapa duniani.ardhi,majumba etc.kama ulikua hujui asset inakuwezesha kupata mkopo hata wa bilioni kadhaa,ukitumia asset kama colateral,then unainvest bilioni ulizopata,waweza jenga kiwanda kitakachokuletea more bilions,ama waweza invest katka makampuni kama ya sigara,pombe,simu etc na ukakaa kwako umekunja nne huku bilions zikimiminika kama maji.
inatakiwa tu kuwa na akili ya uwekezaji.


kwani mkuu hapo kwenu hamna hata nyumba,kama ipo hata iwe hoi ifanyie renovation then kaombe mkopo ukiitumia kama dhamana,utatoka tu,badala ya kukaa kijiweni ukihoji hela za majamaa jinsi wanavyozitumia......
 
Samuel Sita Ndio kipoko basi Lake Lina kila kitu ndani kuanzi office inayojitosheleza kama GROUND FORCE ONE ya Rais wa Marekani aliagiza special order kutoka S Korea, wabongo mlie tu CCM hakuna msafi
 
1. Mlikusudia kumvua gamba, ikashindikana!
2. Mlimfungia (kwa mwaka moja) kwa kosa la kutia nia kabla ya wakati, ikashindikana!
3. Sasa anapiga kampeni ya kuwania urais kila wilaya na kila kata nchini kote wakati NEC haijatangaza kuanza kwa shughuli hiyo. Kisingizio anakusanya wadhamini 450 kutoka mikoa 15 kwa mjibu wa watia nia wa CCM! NEC (Tume huru ya Uchaguzi), CCM na vyama vya upinzani (UKAWA) wanaliona hilo lakini imeshindikana!

Sasa basi kwa mstakabali wa Taifa letu, mkubali tu yaishe kwani katuzidi kete.

Tumuachie tu nchi yetu aiongoze ki- Hitler hitler maana naona wananchi wengi (wafuasi wake) ndiko wanakotaka tuende. Hitler aliongoza ujerumani kwa mtindo wa mchakamchaka, mazuri na mabaya yake yanafahamika. Mhhh... na mseto huu sijui utatufikisha wapi - yaani kule Seif na huku EL, hadi raha kwa kweli!!

Mungu ibariki Tanzania.
 
UVUMILIVU WA LOWASSA WAMZIDISHIA HESHIMA KWA WANANCHI :

Lowassa ana fanya siasa mpya nchini

Siasa ambazo watanzania hawakuzizoea kabisa

Lowassa anafanya siasa za kistaarabu zisizo kifani.

Pamoja na kejeli na kebehi nyingi anazopata kutoka kwa wapinzani wake lakini mzee huyu amekuwa na subira

Mungu anawapenda wenye kusubiri na hawapendi wenye kukata tamaa na kama hivyo ndivyo basi sina budi kusema mh. LOWASSA dini anaijua na Mungu ana mwongoza kwa mengi

Vijana wa nchi hii tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa nguli huyu wa siasa nchini

Lowassa hekima na busara zake ndizo zilizo sababisha wananchi wasisikilize maneno ya wazandiki

Wananchi wanasema sasa basi, matusi yenu kwa LOWASSA tumeyasikia sasa tuleteeni boksi la kura tuwajibu kama tumewaelewa au la

Wananchi wanasubiri oktoba waonesha kwa vitendo namna wanavyo mhusudu Komredi Lowassa.

Watanzania wa sasa hawana mapenzi na siasa za maji taka maana zimeturudisha nyuma kwa miaka hamsini na ushee

Watanzania wa leo wanapenda siasa kama anazo fanya Lowassa, siasa zilizojikita katika kuelezea changamoto za wananchi na sio matusi na maslahi binafsi

Vijana kuna haja ya kujifunza kuwa na hekima na busara kama za Lowassa kwa ajili ya kujenga Taifa letu

Mungu ibariki Tanzania
. Mungu ibariki Afrika
 
Hivi mtu anasema NI LAZIMA AWE RAIS NA KUSEMA WASIOMPENDA WAONDOKE CCM bado mnasema anafanya siasa za kistaarabu? Kweli mmelewa pesa za Lowassa.
 
Ukiona mtuhumiwa wa ufisadi anagombea uongozi na wewe ukamshangilia kama zuzu, basi mwombe akufadhili nauli ya Mirembe maana hakika we sio mzima

SAY NO TO FISADI
 
Lowassa si swala la CCM Bali ni swala la wazalendo wote kuungana na kumkataa kunzia sasa
 
Lowassa is not man of the people at all, is a man of tycoons
 
Bila shaka Raisi Kikwete na watu wake wanahofia vibaya mno kufunikwa na Bw.Lowasa pindi achaguliwapo kuwa Raisi wa JMT na ndio moja ya sababu ya kusuasua na fitina nyingi zisizo maana!

Wanajua wazi ya kwamba kwa maozo waliyoyafanya kwa Miaka 10 waliokaa madarakani Bw.Lowasa atayarekebisha yote ndani ya miezi 6 kwanza kama alivyoahidi ataanza na alipoishia alipokuwa Waziri Mkuu la kuondoa foleni pale alipoanzisha njia tatu wazo zuri lkn alipotoka kama kawaida ya Kikwete &Co wakashindwa usimamizi na mpango kuharibika!

Sasa hii ni hofu yao kubwa wanajua baada tu ya Mwaka wa Utawala wa Bw.Lowasa wananchi wataanza hata kujuta kwa nini hawakuingia brn. kumtoa Bw.Kikwete miaka 8 iliyopita!


Nina uhakika watu kama akina Bw.Nape Nnauye sijui Makonda, Membe, Makorongo & Co. watakuwa hawana nafasi kwenye serikali ya Bw.Lowasa!
 
Mmh!! Akili yako fupi sana. Nadhani Lowassa mwaka huenda akapata wake wengi sana, maana wachumba zake wamejaa kila mahali.
 
Habari wanajamvi! Kuna kauli ambazo zinaibuka ama kutoka kwa viongozi wa dini au viongozi wa siasa lengo likiwa ni kuwaaminisha watanzania kuwa huyu anaegombea ni mtu safi. Kuna kauli iliyotolewa na mwenyekiti wa ccm mkoa wa Arusha Onesmo Nangole alisema kupitia gazeti la Nipashe namnukuu "Lowassa ni mtu mkarimu na mpole na chakula chake huliwa na maskini na mtu mwenye nywele nyeupe anautukufu" ,mwisho wa kumnukuu kauli hii inanikumbusha kauli ilyosema Kikwete ni chaguo la Mungu! watanzania waliamini nakumchagua lakini matokeo yake wameyapata!

Sasa kwa kauli kama hizi ninawaasa watanzania kuamakini nazo watakuja jutia huko mbeleni!
 
Back
Top Bottom