Yeye hakusali? Si alipewa hadi jina la Abdallah?
Siamini kama hawa bodaboda wanapewa hizo pesa..mi nadhani ni uzushi...mwenye evidence alete hapA..mi nadhani huyu Lowassa wanampenda tu sio pesa zake...
Kuna kambi moja inaweweseka sana.
Ilitumia mbinu ya kumfitinisha Lowasa na Kikwete kwa hoja kuwa anataka kupindua nchi na kuifanya nchi isitawalike ,wakasema kuwa alitaka kumtoa JK kwenye uenyekiti wa chama ,wakamchonganisha na Mwakyembe bila kujua kuwa Mwakyembe alikua mwenyekiti tu wa kamati na hakua adui wa Lowasa.
Wakataka kutumia mbinu ya udini kwamba Lowasa sio mkatoliki hivyo asiungwe mkono lakini maaskofu karibu wote wa kanisa katoliki na waumini wengi wanamuunga mkono.
Wakaja na uchochezi wa kidini kuwa Lowasa ndiye aliyekuja na MoU lakini waislam wengi ni waelewa wa historia ya nchi hii na wanajua ni nani aliyefuta historia yao na wengi wanamkubali Lowasa kwani ameonyesha moyo wa kushirikiana nao katika kuwaletea maendeleo . Yote hayo yalishindikana na hawakuweza kuondoa imani ya wananchi kwa Lowasa.
Sasa wamekuja na mbinu nyingine ya kupandikiza watu wanaojitokeza kwenye vyombo vya habari kujifanya kuwa wanalalamika kuwa waliahidiwa kupewa pesa ili wahudhurie mikutano ya Lowasa. Mwanzoni walidanganya watu kuwa kila anayehudhuria mkutano wa Lowasa anapewa pesa lakini baadae walipoona kuwa ni vigumu kueleza kuwa hayo makontena ya pesa yanasafirishwa kwa kutumia ulinzi gani wakasema kuwa wanarushiwa kwenye mitandao.Walipoulizwa hivi pesa inayotushwa kwenye mtandao nayo ni siri tena mana msg zake zipo. Na mfano tu ni nyomi ya watu kila mkoa wanawezaje kurushiwa mamilioni ya pesa za rushwa kupitia mitandao toka kwenye akaunti ya Lowasa halafu bado iwe siri isiyoweza kubainika na kuchunguzwa na TAKUKURU? Kwa sasa wamejitengenezea wafanyabiashara wao wenyewe ambao ni wabia wao kwenda kujifanya kuwa wanawashawishi kwa fedha ili wawaunge mkono na kujirikodi kuwa wamekataa kipokea pesa hizo.
Mbinu yao ya mwisho waliyopanga kuitumia ni kutumia watu wao wenyewe kujipa rushwa ,kujirikodi na kujikamatisha wenyewe na kisha waseme kuwa wametumwa na Lowasa. Na hii mbinu wanaitumia kwenda kuwadanganya wajumbe wa vikao mbalimbali vya CCM ili kuwapandisha hasira wakijua fika kuwa wajumbe hao tayari wanampinga Mh.Lowasa.Wanajifanya kuwa wametumwa na Lowasa ili wawape fedha jambo linalowafanya wajumbe hao wapandwe na hasira na wakati ukifika wakate jina lake kwa maana kuwa anatumia fedha kuungwa mkono.
Mbinu zote hizi zimekua zikitumiwa na kambi moja iliyofilisika kisera na kimaono zaidi ya kutumia majina ya watu wengine na kutaka urahisi wa kupenya kwa kuhakikisha jina la Lowasa linakatwa.
Kambi hii haina historia yoyote katika kukijenga chama tangu awali zaidi ya kukitumia chama kunufaika kwa vyeo tu na madaraka ya kiserikali. Ni kambi ambayo mtu wao hajakulia maisha ya kukipigania chama kwa hali na mali mpaka kuendelea kuwepo madarakani.
Hii ni kambi inayowaza kuendelea kunufaika na vyeo serikalini bila kujua kuwa kukata jina la Lowasa ambaye amebeba theluthi mbili ya wanachama ni kukiua chama.Hawajui kuwa Huwezi kuvunja makundi ndani ya chama kwa kuzuia kundi lililobeba zaidi ya nusu ya wanachama wote eti uimarishe chama kwa kutumia kundi lenye thumuni ya wanachama. Hayo maajabu yatakuwa yanatokea Tanzania tu na ndani ya CCM.
Hii kambi inayotumia muda,mali na nguvu zao zote kumchafua Lowasa na kukibomoa chama hawaoni hasara yoyote maana wengine walishakuwa wanachama wa vyama vya upinzani na wengine waliunda CCJ, hawaoni hasara ya kuua chama cha mapinduzi na ndio maana hata agenda wanazobeba ni za wapinzani na wengine wametishia kuwa Lowasa akipita watahamia upinzani. Hawa ni CCM madaraka.
Watu wengi wanamkubali Lowasa kutokana na umahiri wake wa kuweka mikakati bila kutukana mtu. Anatambua kuwa uhusiano mzuri na wananchi ndio utakaompeleka Ikulu na sio chuki na matusi kwa wengine.
Hizi mbinu za hawa wengine za kutukana ,kuchafua watu,kutumia udini na ukabila kujinadi,na kila aina ya ujasusi wa kuchonganisha kambi moja dhidi ya nyingine hauna tija kwa nchi yetu.