Lowassa alianza na Mungu kwa njia ya kupanda mbegu kwenye nyumba za ibada. Pale walipomtuhumu kwa uongo hakuwajibu alienda madhabahuni, alikaa kimya na kusikiliza sauti ya Mungu "usijibizane na hawa nitakupigania na utashinda"
Baada ya miaka Saba ya vita kali Mungu akamuinua Lowassa baada ya sala zake na sadaka yake kupokelewa na Mungu.
Waliodhani hatasimama tena Mungu amemsimamisha Mara nyingine tena. Na hii ndiyo nguvu ya Lowassa ni ucha Mungu wake. Hili litamfikisha mbali, na viunzi vyote kwa msaada Wa Mungu ataviruka na taji atavikwa.
Tusichokijua hakuna kiongozi hata Mmoja Wa CCM au Wa upinzani anayemchukia Lowassa. Wote wanamkubali kuwa uwezo na busara anazo. Wanajua siyo mnafiki bali mungwana sana.
Ni mtu ambaye ni msikivu sana mpole asiyevumilia mamba ambao hayana tija. Ni MTU straight forward siyo mbabaishi. Ukifanya jambo atakutazama machoni na kusema hapana Y hili siyo sahihi. Na ndiyo siri ya mafanikio ya watu wengi wenye kusema kweli kwa kusimamia wanachokiamini ni cha kweli.