Edward Lowassa: Nasali sana ili nipate Urais

Edward Lowassa: Nasali sana ili nipate Urais

Lowassa alianza na Mungu kwa njia ya kupanda mbegu kwenye nyumba za ibada. Pale walipomtuhumu kwa uongo hakuwajibu alienda madhabahuni, alikaa kimya na kusikiliza sauti ya Mungu "usijibizane na hawa nitakupigania na utashinda"

Baada ya miaka Saba ya vita kali Mungu akamuinua Lowassa baada ya sala zake na sadaka yake kupokelewa na Mungu.

Waliodhani hatasimama tena Mungu amemsimamisha Mara nyingine tena. Na hii ndiyo nguvu ya Lowassa ni ucha Mungu wake. Hili litamfikisha mbali, na viunzi vyote kwa msaada Wa Mungu ataviruka na taji atavikwa.

Tusichokijua hakuna kiongozi hata Mmoja Wa CCM au Wa upinzani anayemchukia Lowassa. Wote wanamkubali kuwa uwezo na busara anazo. Wanajua siyo mnafiki bali mungwana sana.

Ni mtu ambaye ni msikivu sana mpole asiyevumilia mamba ambao hayana tija. Ni MTU straight forward siyo mbabaishi. Ukifanya jambo atakutazama machoni na kusema hapana Y hili siyo sahihi. Na ndiyo siri ya mafanikio ya watu wengi wenye kusema kweli kwa kusimamia wanachokiamini ni cha kweli.


Waungwana wanasubiri wakti tu. Huyo ni fisadi, anaelazimisha aende ikulu. Hapendwi isipokuwa na wanaondekeza njaa
 
Kwani nani hasali jamaa asijifanye mcha mungu anayesali asingetuletea RICHMOND Na asingewahonga wanaccm ili wamuunge mkono
 
Jamani jamani. Hivi mbona mnaendelea kuongelea hawa watu? Kila kukicha ni Membe, Lowasa. Hawa wote hawafai kabisa kwenye nafasi ya urais. Tunataka Rais wa kutuunganisha Watanzania na si kutugawa
Wewe unamtaka nani?
 
Wadau, ukweli ni kwamba watia nia wote wanasali sana ili Mungu (bila kujali dhehebu) anawassidia kuingia Magogoni. Swali langu ni kwamba; kwa baadhi tayari wameshamwaga pesa nyingi sana ili kuhakikisha wanaingia magogoni, sasa kwa nini mtu asali sana ilhali alishaweka matumaini yake kwa pesa (rushwa)?

Kuna nini Ikulu hadi mtu asali ili kuingia. Wananchi wanajua nani anafaa ikulu sasa sala ni za nini?

Binafsi nafikiri uchu umepitiliza na watu wa jinsi hii wanaweza kuwa watu hatari sana!


Anauchungu na umasikini wa watanzania,wewe unadhani anasali ili iweje? kama hela anazo,njoo lowasa utuondolee hii aibu.
 
Lowassa ndiye mwana ccm pekee mwenye dhamira ya dhati ya kuwa rais wa Tanzania..

Huyu ni mgombea mchamungu ndomana kila alifanyalo humtanguliza mungu mbele
Lowassa hamtangulizi Mungu mbele, ila anatanguliza nguvu ya fedha. Watu waliozoea kuhonga wanafikiri kwakuwa wanawahonga wanadamu fedha, basi hata Mungu wanaweza kumuhonga kwa ibada ya mdomo tu na wala si ya moyo.
 
Waziri Mkuu aliyejiuzulu na mtia nia ya Urais kupitia CCM amesema kuwa anasali sana ili aupate Urais wa JMT, ameyasema hayo akiwa mkoani Kigoma akitafuta wadhamini.

Source: RFA-Magazetini leo

ili akawaingize wakina chenge,rostam,tibaijuka na karamagi madarakani,hakuna mungu wa namna hii,
 
Anauchungu na umasikini wa watanzania,wewe unadhani anasali ili iweje? kama hela anazo,njoo lowasa utuondolee hii aibu.

utajili wake utusaidie nini kama wewe haufanyi kazi unasubili ngao utakuwa masikini adi mwissho.
 
Lowasa acha ufara wako ivi unadhan watanzania nimang'ombe sana,,hapa urais upati labda ukawe rais wa ukoo wenu...
 
Waziri Mkuu aliyejiuzulu na mtia nia ya Urais kupitia CCM amesema kuwa anasali sana ili aupate Urais wa JMT, ameyasema hayo akiwa mkoani Kigoma akitafuta wadhamini.

Source: RFA-Magazetini leo

na sisi tunasali hili genge la majambazi liingie nyumba takatifu,tukaona mungu ni wa nani zimebaki siku 12 tu mungu atatujibu.
 
Hats shetani huomba sana ili kuweza kutawala giza
 
Anasali aupate urais ili aufanyie nini? Hii shauku ya urais iliyovuka mpaka ndiyo inatia wasiwasi watu wenye uwezo wa kufikiri, huyu Lowassa aende zake huko

Mkuu, mtazamo wako unashabiana na wangu!

Huyu jamaa ana nini na huo urais wa JMT?
Mara atume watu kumuomba atangaze nia/gombee urais, mara alipe wanaomdhamini ili aonekana anakubalika sana...., nini kiini au dhamira kuu katika yote hayo?!

Simchukii Lowassa bali yale anayoyafanya ili kuhakikisha anateuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama chake ndio yanayonipa mashaka!
 
Ccm haiwez kutupatia rais bora hao wote. EL & membe wote ni vibaka
 
Back
Top Bottom