Edward Lowassa hukukidhi kiu ya wanawake!

Edward Lowassa hukukidhi kiu ya wanawake!

Heshima kwenu wana JF.

Nimefatilia kwa karibu sana sana hotuba ya Mhe. Mgombea u Rais kupitia UKAWA aliyoitoa hapa LAPF kwenye kongamano la wanawake BAWACHA na kubaini jambo moja kubwa sana.

Kauli mbiu ya kongamano ni "LOWASA NA HATMA ZA CHANGAMOTO ZA WANAWAKE TANZANIA"

Nimesikitika kuwa nilitegemea kwenye hotuba Yake ataweza kuelezea mikakati ya ukombozi huo wa mwanamke. Nasikitika kuwa sikuona mahali popote akiongelea changamoto hizo na jinsi ya kuzitatua.

Ameishia kuimba Wimbo wa Mhe. Magufuli "Alinselema Hadija, mchaka mchaka chinja" na kuzungumza mambo ya MAHABA!!!!!!!!

Nasikitika kusema mimi kama mwanamke nimeondoka na kiu yanguuuu!!!!!!!!!! Ngoja nimsubiri mzee original wa Alinselema. I hope atatuondolea kiu hii!!!!!! Tunataka kuona SERA za ukweli za kumkomboa mwanamke, sio MAIGIZO.

Naomba kuwasilisha.

Queen Esther
Queen Esther, kwanza pole sana. Pili vuta subira, kiu yako ya matumaini karibu itatulizwa. Tatu nianze kwa kukupongeza kwamba pamoja na umeme kukatwa bado uliweza kufuatilia mkutano ulioitishwa na Baraza la Wanawake Chadema. Tukubali tusikubali UKAWA, Chadema na Lowassa ndio habari ya mjini na anayejaribu kuzima sauti ya mabadiliko asije akashangaa kusikia hata mawe yakinguruma.

Lowassa hakualikwa kutoa hotuba, hapana, hiyo shughuli bado...huo ulikuwa ni muendelezo tu katika ratiba ya kukutana na kuwasikiliza wananchi. UKAWA, kama huna habari, hawajazindua hata hiyo kampeni yao, kazi hiyo itafanyika Uwanja wa Jangwani Dar es Salaam siku ya Jumamosi tarehe 29 mwezi huu na kwa sasa bado tu saa 30. Hakikisha unawahi uwanjani na eneo maalum kwako limetengwa tayari.

Kwa sasa Lowassa hakutani na vikundi mbalimbali katika jamii kuwatatulia matatizo yao, hapana, hilo wakati wake bado; anakutana nao kusikiliza wanavyonyanyasika kila siku chini ya utawala uliochoka na kupoteza dira. Anawakumbusha kwamba hatua ya kwanza ya kuondokana na kero za miaka 50, ni kufanya mabadiliko...mabadiliko ambayo hayawezi kuletwa na chama kile kile kilicho chanzo cha kero hizo.

Akiendelea anawaomba wampe fursa ya kuwatumikia kwa kuyaongoza, kuyasimamia na kufanikisha hayo mabadiliko na kazi hiyo hawezi kuifanya mpaka hapo tarehe 25 Oktoba 2015 atakapopewa idhini kwa njia ya kura. Kama sehemu ya jamii, wanawake wanayo turufu kubwa katika mustakabali wa taifa hili na asante sana kwa kuacha shughuli zako na kukaa karibu na redio uweze kuwa sehemu ya matumaini.
 
Tatizo watu wengi wanashindwa kutofautisha sifa ambazo anakuwa nazo kiongozi na mwanasiasa kiongozi haitakiwi awe anaongea sana ila mwanasiasa. Kuongea sana ndio kazi yake mwanasiasa anaweza kuongea chochote
Kwa upande wangu na kutokana na uelewa wangu naona lowassa yupo sahihi sana na anafaa kuwa rais wetu.
 
Changamoto tunazijua sanaa hata kipindi yeye akiwa waziri na PM zilikuwepo pia. Maswali ni kua Je anahistoria gani na changamoto za wanawake? Na pia hajaeleza ni kwa kivipi atazitatua, na hatumpigii kura mke wake. #HapaKaziTu #Magufuli for president.

Jinsi ya kuzitatua kasema msikilizeni kwa umakini siku ya Jumamosi tarehe 29 leo kawatuma kazi moja tu nayo ni kumtafutia kura. Naona technic yake hii imewatoa jasho
 
Mimi sijaelewa alichoongea zaidi ya kuomba kura yani akina dada mmepoteza muda kwa ajili ya huo ujinga. Eti mgombea wa urais yeye hana cha kusema zaidi ya kumuonesha mahaba tu. Wakati hapo kulikuwa na madada poa, walemavu wa ngozi, mama ntilie, baamedi, nk.

Lakini sijasikia jambo la msingi ambalo ameongea kuhusu hayo makundizaidi ya kuomba mmtafutie kura. Akina mama wa Dar es Salaam jitambueni na si kufuata mkumbo.
 
Duuuuu!!!! Sasa Yale matangazo yoooteee ya BAWACHA kupitia kwa Mhe. Halima Mdee yalikuwa ni ya nini????? Tena mkarusha live??????

Nimependa sana Mhe. Mbowe alipoongea, at least alitoa direction ya kongamano otherwise tulikuwa tumechanganyikiwa. Hiki ni nini tena Mungu wangu??????? Kweli tume toka majumbani kuona vituko na usanii????

Mtuonee huruma jamani wanawake. Kweli tumeacha familia kuja kusikiliza alinselema??? mara MAHABA??? Mara kudeka???

Queen Esther

Mbona jamani Mzee alisema mwanzoni kabisa mwa salamu zake?alisema kuwa leo hajakusudia kutoa hotuba...bali anawatuma kina mama wakamuombee kura!!Sisi wengine hatutaki maneno zingiiiiiii za kina Magufuli...hayo hayo ya Eddo yanatosha,maana kama kuongea tu,CCM wametuambia sana sana na hakuna walichafanya
 
Asante Great Thinker.

Queen Esther

Jinsi ya kuzitatua kasema msikilizeni kwa umakini siku ya Jumamosi tarehe 29 leo kawatuma kazi moja tu nayo ni kumtafutia kura. Naona technic yake hii imewatoa jasho
 
Hakuenda kufanya hotuba alienda kutoa maagizo kuwa wanawake wamsaidie kutafuta kura baasi . Siku ya hotuba ni jumamosi . Andaa kinywa chako tukunyweshe dawa
 
Kumbe watu wanapend maneno mengi

Na yawe na 'uongo' na 'ahadi' hewa nyingi.... With my due respect to Queen Esther,but not for her thread kwakweli. EL aliweka wazi awali kuwa hakusudii kutoa hotuba, yeye ni mwalikwa as the rest..na ndiyo maana kwa maudhui ya mkutano (just wanawake), Mama Regina ndiyo 'key-character' alikuwa.
 
Mgeni rasmi alikuwa ni mama Regina Lowasa na sio Lowasa. Lowasa alikuwa mgeni tu pale. Lakini pia ameongea vitu muhimu pamoja na kuwaomba akina mama wamtafutie kura. Pia aliwataka akina mama waazishe mijadala ya kuzungumza matatizo na maendeleo yao pamoja na kujifunza maana ya mabadiliko.
 
Asante Great Thinker.

Queen Esther

Jinsi ya kuzitatua kasema msikilizeni kwa umakini siku ya Jumamosi tarehe 29 leo kawatuma kazi moja tu nayo ni kumtafutia kura. Naona technic yake hii imewatoa jasho
 
Utakuwa hata matangazo ya mkutano hukuyaona au kuyasoma??? Kachungulie tena nani alikuwa Mgeni rasmi????

Queen Esther

Mgeni rasmi alikuwa ni mama Regina Lowasa na sio Lowasa. Lowasa alikuwa mgeni tu pale. Lakini pia ameongea vitu muhimu pamoja na kuwaomba akina mama wamtafutie kura.
 
nadhani kasoro IPO kwenye. tangazo la mkutano,tangazo lilimtaja lowasa kama mwenye mkutano lakini Yale aliyotakiwa kuwaambia kayasema mke wake ambaye kimsingi hawezi kulaumiwa kwa namna alivyoyaelezea kwa kuwa yeye sio mwanasiasa,Mimi huwa nawakubali UKAWA na ni muumini wa mabadiliko,lakini ukweli ni muhimu zaidi,CHADEMA/UKAWA waelewe huu sio wakati wakufanya makosa yasio ya lazima kabisa
 
Hotuba ya katibu mkuu wa BAWACHA ilikuwa inataja ndugu mgeni rasmi. Mgeni rasmi alikuwa ni nani? Kwanza wakati wa hotuba ya katibu mkuu Lowasa alikuwa hajaingia ukumbini.Ameingia baada ya hotuba ya katibu mkuu. Hii ina maana kuwa Regina ndiye alikuwa mgeni rasmi na sio Lowasa.
 
Kwa nini unadhani wanawake wanahitaji kukombolewa sasa mkuu...?

Miaka yote ya tawala zilizopita kipi kilichoshindikana kama kweli kuna ukombozi wa mwanamke?

Mambo Kama haya ya kumkomboa mwanamke ni ya ki Taifa, hayana chama.

Queen Esther
 
Kila mtu na maumbile yake.Kuna waongeaji wazuri na kuna wengine si waongeaji.Ni hulka ya.watu kuwa.tofauti.Lowassa aonekanavyo si muongeaji sana.Sijawahi msikia akiongea kama mwanasiasa hata alivhokuwa CCM so siwezi kumuhukumu kwa maumbile yake.

Sasa anatafta nn kwenye uchaguzi? Kayataka mwenyewe sisi tutamtia d
Tobo tuuu
 
Back
Top Bottom