Economic Freedom Fighters Tanzania

Jul 21, 2023
23
17
Salaam,

Huu utakuwa ukurasa rasmi wa Vuguvugu la Kimapinduzi la Ukombozi wa Kiuchumi Tanzania, amboa utakuhabarisha kuhusu Itikadi, falsafa, sera, utangamano, dira ya Economic Freedom Fighters Tanzania, maoni, mtazamo na mambo mengi ya kisiasa, Kiuchumi, kijamii, Sayansi na teknolojia na Uhuru kamili wa kiuchumi wa Afrika.

Vuguvugu (movement) alichangamani na upande wowote wa kisiasa, bali linalenga kuhamasisha nguvu ya mtu mweusi na wote wasiyo na sauti Duniani kote kujikomboa kiuchumi.

Vuguvugu hili linapinga ubaguzi wa aina yoyote ile ikiwa ni pamoja na makundi maalumu ya kijamii ndani na nje ya Nchi.

Karibu sana Watanzania wote.

Economic Freedom Fighters Tanzania,

Ujamaa ni Imani.
Screenshot_20230610-124211_PDF%20Reader.jpg
 
Ujamaa ni Imani.View attachment 2695905
Tatizo letu nchiinafuata siasa ya Ujamaa kimaandishi , lakini kivitendo tuna fanya siasa ya Kibepari.
Waekezaji wakija wakisoma Katiba zetu wanaona Ujamaa ambao unaruhusu Kutaifisha mali za Mabepari. Wanakimbia mbali sana. kwa kukwepa hasara.Wanasepa.

Na ikitokea
Wakija Huhitaji Mikataba Yenye Masharti Maalumu na Sheria za Nchi ya tatu kama UK au South Afrika ili kulinda Maslahi yao.
 
Mimi nasimama na nchi yangu ya Tanganyika.
Mimi nasimama na nchi yangu Zanzibar. Sasa Tanzania itasimama na Nai? Hili nalo ni tatizo jingine la Jamhuri yetu ya Kufikirika.

Shida nyingine ni kuwa bado tuna mawazo ya kiujima ujima. Yaani tunataka tubaki na mali zetu wakati hatuwezi kuzivuna na kuzifaidi matunda yake.

Kwa mfano, madini. Serikali ingalihamasisha uchimbaji wa wazalendo wenyewe na kukusanya dhahabu, almasi na madini mengine na kuuza wenyewe nje. Lakini tatizo sisi hatuna soko (network) ya kibiashara, tunaweza kujikuta tunabaki na mzigo ghalani kwa kisingizio kuwa uko chini ya viwango vya kimataifa. Kwa hiyo, inatulazimu tuwaite makampuni maarufu ya uchimbaji duniani ambao wenyewe wanazo network za kuuza na wanaaminika kwa uzoefu wao na wana kibali na assurance ya ubora wa thamani.

Kwa hiyo, bado Waafrika ni lazima tuendelee kuliwa tuu.
 
Kujikomboa kiuchumi ni lazima kuepuka kutumika kwa Afrika kama eneo maalumu la Mabepari. Mapinduzi ya kweli ni Ukombozi wa kiuchumi.
 
Economic Freedom Fighters, tunayo furaha kutambulisha vuguvugu hili kama sehemu ya mapambano ya uhuru wa kiuchumi Tanzania. Vuguvugu hili linauwaunganisha maskini, wanyonge, wakulima na wafanyakazi, makundi maalumu, wanaharakati, wanamapinduzi, wanamageuzi na wanasayansi, wasomi na wote wasiyo Elimu kushirikiana katika kuleta Mapinduzi ya kiuchumi.

Vuguvugu hili limeundwa chini ya misingi madhubuti ya Nidhamu ( Discipline) na Uongozi madhubuti katika kutekeleza majukumu ya vuguvugu hili hapa Tanzania. Ipo nia, sababu na uwezo wa kuakikisha tunashinda ushawishi wa wale wote wanaofikiri Tanzania inaweza kuendelea kuwa Nchi maskini ikiwa Pamoja na watu wake kuendelea kuogelea kwenye dimbwi la ufakara.

Vuguvugu la Economic Freedom Fighters, tunayo Itikadi na falsafa ambayo inalenga Mazingira, utamaduni na sifa za Tanzania katika kuakikisha tunamasisha matumizi ya Rasilimali zetu Tanzania (Afrika) zitumike kwa watu wake.

Itikadi na falsafa yetu inalenga Ukombozi wa kiuchumi Tanzania.

Inaendelea.......
 
Mimi nasimama na nchi yangu ya Tanganyika.
Mimi nasimama na nchi yangu Zanzibar. Sasa Tanzania itasimama na Nai? Hili nalo ni tatizo jingine la Jamhuri yetu ya Kufikirika.
Shida kubwa ndo ipo hapo..
Serikali ya Zanzibar inaboronga na kuvurugana na wawekezaji (a.k.a mabeberu), JMT ndo inashtakiwa huko nje, gharama zoote za kesi na kulipa fidia kwa mujibu wa hukumu ni juu ya Tanganyika pekee..

Early in 2022, the Revolutionary Government of Zanzibar (SMZ) through the ministry of lands terminated a land lease held by British property developer Pennyroyal Limited in Matemwe, after it was claimed that an area of 20 hectares out of the 411 hectares inside the project was owned by another third party

The Blue Amber Resort project was under construction with first phase delivery of units initially set for December 2022.
The termination was followed by a letter on July 25, 2022, from the Zanzibar Investment Promotion Authority (ZIPA) informing Pennyroyal Limited that it will not renew its construction permit following the termination of leasehold by the Ministry of Lands.

In an earlier press release, Mr Brian Thomson, owner of Pennyroyal, exclusively confirmed that the company intent to file for arbitration under the Convention on the Settlement of Investment Disputes between States and Nationals of Other States (the ICSID Convention).

He said that they were left with no choice but to seek international arbitration.

“We have followed the requisite process, We wrote to the government of the United Republic of Tanzania regarding our intent to file a case following the termination of our land lease, but to date we have not gotten any response,” Mr Thomson said then.

It was further confirmed by Tanzania’s Attorney General Dr Eliezer Feleshi that he was aware of the claims and they were preparing to meet with the developer, however, it was never confirmed whether the meeting ever took place....

Hili vuguvugu liwe huru, liwe kwa ajili ya kuwamsha watu kuhusu kujua haki zao, wajibu wao, kutetea na kulinda rasilimali za taifa. Na pia hili vuguvugu liweze kupiga kelele utekelezaji wa kesi ya Mtikila kuhusu mgombea binafsi. Ambaye hatofungwa na miiko ya chama cha siasa pindipo atakapo tetea rasilimali za nchi, kama ilivyo sasa kwa mbunge mmoja mmoja kushindwa kusimama kutetea maliasili zetu kwa kuogopa kuvuliwa uwanachama na kusahau kama alipigiwa kura na wananchi wasio na chama sema walimwamini yeye sio chama.
 
The Economic Freedom Fighters Tanzania. (EFF)

Tunaendelea kuhusu vuguvugu la kiasiasa la Mapinduzi ya kiuchumi.

Vuguvugu hili limeanzishwa rasmi tarehe 24 May 2023, ni vuguvugu la kisiasa lenye mtazamo wa kimataifa ( International Outlook). Vuguvugu hili ni sauti ya watu maskini na fukara, wanyonge ambao wako tayari kusimamia rasilimali zao kwa maslahi yao wenyewe na vizazi vyao.

Vuguvugu hili la kisiasa linafuata siasa kali ya Mlengo wa shoto, falsafa na itikadi yake ni nyenzo ya jamii yenyewe kujikomboa kiuchumi na hasa jamii ambayo imekuwa chini ya matabaka ya kinyonyaji.

ITIKADI

Vuguvugu hili la kisiasa linaamini katika Ujamaa na kwa Umoja wetu tunasema "Ujamaa ni Imani" Jamii nyingi ya Watanzania (Afrika) imeendelea kuishi misingi ya Ujamaa licha ya msukumo mkubwa sana wa kiuchumi kutoka nje ya Tanzania ( Afrika) katika mazingira ya kuamuliwa namna ya kuishi na kuzalisha mali kwa Jamii yetu. Kwa mtazamo wetu Ujamaa bado ni nyenzo na itikadi imara ya kupambana na umaskini, matabaka au kiwango kikubwa cha umaskini kwa watu wetu. Hatuna budi kuunganisha jamii yetu ili kwa pamoja ishiriki katika maendeleo yake yenyewe bila kupangiwa na mifumo ya kinyonyaji ya wageni. Ujamaa ni Alama ya Ukombozi wa kiuchumi kuwatoa watu kwenye ufakara kwa kutumia rasilimali zao wenyewe, kusimamia mambo yao ya kiuchumi, kisiasa na Kitamaduni ikiwa Pamoja na sayansi na teknolojia iliyobuniwa na jamii yenye Uhuru kamili wa kiuchumi .

FALSAFA

Nguvu na Kazi. Falsafa hii ni muhimu ili kuumba kizazi chenye kutumia nguvu ya ziada ili kujikomboa kiuchumi kutoka mikononi mwa wanyonyaji na wote wasiyotaka tujikomboe kiuchumi. Kizazi kinachofanya kazi kwa bidii, kuzalisha mali kwa bidii kwa ushiriki wenyewe katika kukuza uchumi wao na kusimamia rasilimali zao wenyewe ili ziwanufaishe. Jamii isiyo fanya kazi kwa bidii utawaliwa na wageni na ambao uleta mitaji na faida ya mitaji hiyo upelekwa kwa wageni wakati huo Jamii inayomiliki rasilimali ubakia maskini na fukara kwa kwakukabidhi urithi wao kwa vizazi vya wageni.

Imani yetu ni madhubuti katika kukoleza moto na hamu ya Ukombozi wa kiuchumi, kubuni njia mbadala za kupambana na wanyonyaji na mifumo Kandamizi dhidi ya jamii yetu yenye kutumwa na kuamuliwa namna ya kutumia rasilimali zake. Uwezo wetu ni kusimamia rasilimali zetu kutumika kwa ajili ya jamii yetu inayoishi chini ya mstari wa umaskini.

Je tupo tayari kwa ajili ya Vuguvugu hili la Ukombozi wa Kiuchumi?

Ujamaa ni Imani.
Screenshot_20230610-124211_PDF%20Reader.jpg
 
Salaam,

Huu utakuwa ukurasa rasmi wa Vuguvugu la Kimapinduzi la Ukombozi wa Kiuchumi Tanzania, amboa utakuhabarisha kuhusu Itikadi, falsafa, sera, utangamano, dira ya Economic Freedom Fighters Tanzania, maoni, mtazamo na mambo mengi ya kisiasa, Kiuchumi, kijamii, Sayansi na teknolojia na Uhuru kamili wa kiuchumi wa Afrika.

Vuguvugu (movement) alichangamani na upande wowote wa kisiasa, bali linalenga kuhamasisha nguvu ya mtu mweusi na wote wasiyo na sauti Duniani kote kujikomboa kiuchumi.

Vuguvugu hili linapinga ubaguzi wa aina yoyote ile ikiwa ni pamoja na makundi maalumu ya kijamii ndani na nje ya Nchi.

Karibu sana Watanzania wote.

Economic Freedom Fighters Tanzania,

Ujamaa ni Imani.View attachment 2695905
Kile chama cha MALEMA kimeanzisha tawi lake Bongo.
 
Economic Freedom Fighters Tanzania (EFF)

MALENGO MAKUU YA VUGUVUGU LA (EFF)

1. Kuuanganisha Watu weusi Duniani kote katika harakati za kujikomboa kiuchumi. (International Outlook)
Kujikomboa kiuchumi ni nyenzo muhimu ya kulinda UTU wa watu weusi ambao tumefanywa daraja la tatu tangu kuumbwa kwa Dunia, pamoja na nguvu ya watu weusi (Black Supremacy) lakini tumeshindwa kutumia nguvu hii kushinda ubepari na Ubeberu mamboleo.

Afrika ni bara changa na Tanzania ni Nchi changa kiuchumi, lakini tajiri kwa rasilimali zake na utamaduni, namna pekee ya kuitumia nguvu hii ni kujikomboa kiuchumi na The Economic Freedom Fighters Tanzania (EFF), tuko tayari kuungana na yeyote anayeifikiria Tanzania miaka 100 mpaka 200 ijayo. Uthubutu wetu ni kuandaa kizazi cha mapinduzi ya Kiuchumi hapa Tanzania na kutumia rasilimali zetu kwa maslahi ya Watanzania wenyewe.

2. Kuunda na kuweka misingi ya Umoja wa Mataifa ya Afrika (THE UNITED REPUBLICS OF AFRICA).
Ili tuwe na nguvu ya kiuchumi na kujikomboa kiuchumi lazima tuungane kama Afrika na kuwa Taifa moja lenye Jeshi moja, Rais mmoja, Bank kuu Moja, Sarafu moja na dhamira thabiti ya kuunda THE UNITED REPUBLICS OF AFRICA.

Wazo la Muungano wa Mataifa ya Afrika (THE UNITED REPUBLICS OF AFRICA) limekuwepo tangu kuasisiwa kwa Ukombozi wa kisiasa na viongozi wetu kama Mwalimu Julias Nyerere na Kwame Nkrumah.

Haya ni malengo makuu ya The Economic Freedom Fighters Tanzania (EFF) kwa maana ya mtazamo wa kimataifa na mtazamo wa Kitaifa ni dhabiti ya taasisi hii kukuwajulisha Wananchi kadri ya uwezo wetu wa kuwafikia

Vuguvugu hili ni sehemu ya sauti ya wananchi wanyonge na maskini wa Tanzania na Afrika, sauti hii haipo kwa ajili ya Mabepari na Mabeberu, kama tulivyosema vuguvugu hili linafuata Itikadi ya Ujamaa inayooegemea Mlengo mkali wa kushoto.

Tupo tayari kwa gharama kwa ajili ya Mapinduzi ya Ukombozi wa Kiuchumi Tanzania.

"Ujamaa ni Imani"
Screenshot_20230610-124211_PDF%20Reader.jpg
 
Back
Top Bottom