Economic Freedom Fighters Tanzania

Economic Freedom Fighters Tanzania

Shida ni nchi zetu za Afrika kutunga Sheria za kutugawa, tulitakiwa tuwe na sheria inayomuhusu vijana wa Africa kujumuika pamoja kiitikadi. EFF fit to serve as a machinery that could put African Youth together with common interests and Common Agenda
Hii ndo maana ya uwepo wa The Economic Freedom Fighters Tanzania, tunataka kuunganisha Vijana, makundi maalumu, Wanasiasa, wanaharakati, wanamapinduzi na wanamageuzi. Wanataaluma, wanasayansi, wanahistoria na kila mtu na hasa wafanyakazi, wakulima na wajasiliamali kama injini muhimu katika Ukombozi wa kiuchumi.

Vijana kuungana kwa maslahi ya wao wenyewe ili kuungana kupigania Ukombozi kamili wa Tanzania.

Bila Falsafa madhubuti ya Mapinduzi hakuna Mapinduzi kamili ya kiuchumi Tanzania na Afrika.
 
Maoni yangu yanafungwa na mipaka ya kisheria ya kila nchi Ila mtafiti sheria gani za Kimataifa zinaweza kutumika kufanya tujumuike pamoja kwa Uhuru, for me I wish Eff iwe Tz Kama ilivyo SA.
Ndiyo maana tunasema The Economic Freedom Fighters Tanzania (EFF) ni vuguvugu tu ambalo linawaunganisha Vijana wote na wote tuliyo wataja hapo juu kuakikisha uchumi wetu unamilikiwa na Watanzania wenyewe. Bila kuingiliwa kwa utamaduni na mila zetu kama Taifa.

Wazo kuu la Vuguvugu hili la Ukombozi wa Kiuchumi ni kuwaamasisha Watanzania na Waafrika kujikomboa kiuchumi kutoka kwenye makucha ya Waliberali mamboleo.
 
Mie ninalowaza hasa ktk tecnological world nikiwa kama mwanamajumui wa kiafrika.
Nina wazo kuwa tuandike blue print ya How African science education iendeshwe.
Lakini nina mtazamo tofauti ktk technological company building and "catch up" . Sisi tupo ktk primitive industrial revolution
Natamani tuanzishe cutting edge tech company lakini ktk mrengo tofauti na wakimagharabi. Ikumbukwe hatuna jabisa cutting edge tech building bali tuna matumizi tu

Wenzetu wamarekani weusi wameanzisha kitu kinaitwa "phychological recovering from slavery trauma" re education, councelling nk. Kiujumla ni tiba dhidi ya maumivu ya utumwa na ukoloni.
Kama hutofanya mind recovery basi economic recovery aitafanikiwa kamwe.
PAN AFRICA ni msamiati tu usiokuwa na nguvu, ukianzisha jambo lenye mrengo huo halitakuwa na nguvu kwa hio ni vizuri kusajili taasisi kuliko kuwa harakati tu.
Tukumbuke vile vile jambo lolote linalo empower wanyonge hupingwa na mababiloni ambao wapo kwenye mfumo kwa sababu huofia kuwa powerless.
Serikali za kiafrika nyingi zinaishi ktk mfumo wa kupiga nyundo nguvu mbadala hata kama ni nzuri.
Tegemea uchunguzwaji wa hali ya juu na mamluki wa kutosha ktk kujitafuta na hatimae jitihada nyingi hufubazwa.
Sina imani sana na mifumo yetu kuwa watu wanaweza kuwa empowered wakabadili hali bila kupitia vyama vya siasa au NGO.
Walioishika Afrika wanataja jambo lolote lipitie mikononi mwao kwa manufaa ya kisiasa.
Muanzilishi wa jambo unatakiwa uwe na andiko la mwanzo kama proposal ili watu wakukuunga mkono wawe na pa kuanzia na kuongezea kurekebisha nk.
Kwenye start up tech company muanzilish huja na prototype au kitu ambacho ni tangible ili kuwavutia wadau wengine sio maneno tu.
 
Tunashukuru sana kwa maoni yako na tunayachukua yote na ushauri wako. Lakini vuguvugu hili ni sehemu yetu kama Watanzania, mchango na mawazo yako yasiishie hapa tafadhali tufahamiane zaidi kama mwanamajumuhi mwenzetu karibu sana.
 
The Economic Freedom Fighters Tanzania. (EFF)

Tunaendelea kuhusu vuguvugu la kiasiasa la Mapinduzi ya kiuchumi.

Vuguvugu hili limeanzishwa rasmi tarehe 24 May 2023, ni vuguvugu la kisiasa lenye mtazamo wa kimataifa ( International Outlook). Vuguvugu hili ni sauti ya watu maskini na fukara, wanyonge ambao wako tayari kusimamia rasilimali zao kwa maslahi yao wenyewe na vizazi vyao.

Vuguvugu hili la kisiasa linafuata siasa kali ya Mlengo wa shoto, falsafa na itikadi yake ni nyenzo ya jamii yenyewe kujikomboa kiuchumi na hasa jamii ambayo imekuwa chini ya matabaka ya kinyonyaji.

ITIKADI

Vuguvugu hili la kisiasa linaamini katika Ujamaa na kwa Umoja wetu tunasema "Ujamaa ni Imani" Jamii nyingi ya Watanzania (Afrika) imeendelea kuishi misingi ya Ujamaa licha ya msukumo mkubwa sana wa kiuchumi kutoka nje ya Tanzania ( Afrika) katika mazingira ya kuamuliwa namna ya kuishi na kuzalisha mali kwa Jamii yetu. Kwa mtazamo wetu Ujamaa bado ni nyenzo na itikadi imara ya kupambana na umaskini, matabaka au kiwango kikubwa cha umaskini kwa watu wetu. Hatuna budi kuunganisha jamii yetu ili kwa pamoja ishiriki katika maendeleo yake yenyewe bila kupangiwa na mifumo ya kinyonyaji ya wageni. Ujamaa ni Alama ya Ukombozi wa kiuchumi kuwatoa watu kwenye ufakara kwa kutumia rasilimali zao wenyewe, kusimamia mambo yao ya kiuchumi, kisiasa na Kitamaduni ikiwa Pamoja na sayansi na teknolojia iliyobuniwa na jamii yenye Uhuru kamili wa kiuchumi .

FALSAFA

Nguvu na Kazi. Falsafa hii ni muhimu ili kuumba kizazi chenye kutumia nguvu ya ziada ili kujikomboa kiuchumi kutoka mikononi mwa wanyonyaji na wote wasiyotaka tujikomboe kiuchumi. Kizazi kinachofanya kazi kwa bidii, kuzalisha mali kwa bidii kwa ushiriki wenyewe katika kukuza uchumi wao na kusimamia rasilimali zao wenyewe ili ziwanufaishe. Jamii isiyo fanya kazi kwa bidii utawaliwa na wageni na ambao uleta mitaji na faida ya mitaji hiyo upelekwa kwa wageni wakati huo Jamii inayomiliki rasilimali ubakia maskini na fukara kwa kwakukabidhi urithi wao kwa vizazi vya wageni.

Imani yetu ni madhubuti katika kukoleza moto na hamu ya Ukombozi wa kiuchumi, kubuni njia mbadala za kupambana na wanyonyaji na mifumo Kandamizi dhidi ya jamii yetu yenye kutumwa na kuamuliwa namna ya kutumia rasilimali zake. Uwezo wetu ni kusimamia rasilimali zetu kutumika kwa ajili ya jamii yetu inayoishi chini ya mstari wa umaskini.

Je tupo tayari kwa ajili ya Vuguvugu hili la Ukombozi wa Kiuchumi?

Ujamaa ni Imani. View attachment 2716069
Hamna kitu hum, maneno mengi tu ,
 
Salaam,

Huu utakuwa ukurasa rasmi wa Vuguvugu la Kimapinduzi la Ukombozi wa Kiuchumi Tanzania, amboa utakuhabarisha kuhusu Itikadi, falsafa, sera, utangamano, dira ya Economic Freedom Fighters Tanzania, maoni, mtazamo na mambo mengi ya kisiasa, Kiuchumi, kijamii, Sayansi na teknolojia na Uhuru kamili wa kiuchumi wa Afrika.

Vuguvugu (movement) alichangamani na upande wowote wa kisiasa, bali linalenga kuhamasisha nguvu ya mtu mweusi na wote wasiyo na sauti Duniani kote kujikomboa kiuchumi.

Vuguvugu hili linapinga ubaguzi wa aina yoyote ile ikiwa ni pamoja na makundi maalumu ya kijamii ndani na nje ya Nchi.

Karibu sana Watanzania wote.

Economic Freedom Fighters Tanzania,

Ujamaa ni Imani.View attachment 2695905
Mimi nina ubunifu wangui kwanini biashara zinakufa na nini kifanyike
 
Tunashukuru sana kwa maoni yako na tunayachukua yote na ushauri wako. Lakini vuguvugu hili ni sehemu yetu kama Watanzania, mchango na mawazo yako yasiishie hapa tafadhali tufahamiane zaidi kama mwanamajumuhi mwenzetu karibu sana.
Sawa ila ni safari ngumu sana. Maana wanyonge wenyewe hawapendi kukombolewa. Muda mwingi utaishia kuwapigania wakati wao hawana mda na ukombozi.
 
NYERERE DAY

Julius Nyerere was among the first African leaders to recognise the Palestine Liberation Organisation (PLO) under Yasser Arafat

In 1973, Dar es Salaam became home to the first PLO embassy in Africa after cutting all diplomatic ties with Israel

“Our generation was a generation of the nationalist struggle for the independence of our own countries, but the plight of the Palestinians is very different and much worse… They have been deprived of their own country; they are a nation without a land of their own. They, therefore, deserve the support of Tanzania and the entire world,” Nyerere said in an interview in 1984

Economic Freedom Fighters Tanzania (EFF).

Hili la kuunga mkono PLO libaki kuwa mtazamo binafsi wa JKN wala sio mtazamo au suala la kitaifa.
 
Economic Freedom Fighters Tanzania (EFF)

Tuandikie maoni, ushauri na kwa namna nyingine yoyote ungependa tuwasiliane kupitia

economicfreedomfightestanzaia@gmail.com

Kumbuka soma kwa makini Email address na tutumie ushauri wako, maoni yako au kwa namna nyingine ambayo ungependa kuwasiliana na sisi.

Ujamaa ni Imani.

Ujamaa ni umasikini sera ya ujamaa haina nguvu kwa ulimwengu wa sasa.
 
Endelea kujifunza Comrade na hii siyo ya kuiga kabisa, ila hii ni Black movement ambayo inakusaidia kupigania Uhuru kamili wa kiuchumi. (Economic Emancipation)
Kubali tu mkuu,umeiga mpaka logo yao, hadi ideology yao,na ndiyo inayopelekea Julias Malema apoteze uungwaji mkono huko SA,kwa sera zake za uhamiaji.
 
Walioanzisha sera ya ujamaa wamekurupuka, kabla ya kuuanzisha ujamaa walitakiwa kuwaelimisha watanzania maana, malengo na dhana ya uzalendo.
Sera ya ujamaa na kujitegemea ilipaswa iwafuate watanzania na sio watanzania waifuate. Hii ni kwasababu sheria na kanuni za umoja wa mataifa zinapinga sera hii ya ujamaa hivyo, watanzania wangeelimishwa kizalendo basi watu wangewajibika kijamaa bila kupata upinzani kutoka umoja wa mataifa kwa haki za binadamu na uhuru wa mtu mmojammoja kujitegemea.

Lakini pia kutokana na mifumo ya kiuchumi ya dunia ya leo sera ya ujamaa haiwezi kuendelea kuwepo. Hii ni kutokana na mifumo ya kifedha, kiuwekezaji, kibishara. Automatic ujamaa umeshakufa.

Ni kitu cha ajabu kutwa kucha unafungua nchi, kwa wawekezaji wa nje, miladi ya uzalishaji mikubwa, sekta za afya, elimu, mawasiliano, kilimo nk . yoote inawawekezaji halafu unajipa imani kua wewe unaujamaa na kujitegemea!!
Inashangaza sana.
Bajeti ya nchi % kubwa kutoka kwa nchi wahisani.

Mimi kwa mtazamo wangu, sera ya UJAMAA NA kUJITEGEMEA iondolewe ili kuendana na dunia, lakini kama kuna kitu wanahofia watafute mfumo wa udhibiti wa hiko wanachohofia.
 
Kwahiyo hii Movement yako ya kuiga na pia inaiga Siasa za Kikomunisti?
Uliberali na Ubepari umefeli pakubwa Sana, nadhani tu mashahidi communist states walivyofanyia makubwa nchi zao, ni Afrika tu ndio ulifeli au tumefeli
 
Back
Top Bottom