Economic Freedom Fighters Tanzania

Economic Freedom Fighters Tanzania

Salaam,
Huu utakuwa ukurasa rasmi wa Vuguvugu la Kimapinduzi la Ukombozi wa Kiuchumi Tanzania, amboa utakuhabarisha kuhusu Itikadi, falsafa, sera, utangamano, dira ya Economic Freedom Fighters Tanzania, maoni, mtazamo na mambo mengi ya kisiasa, Kiuchumi, kijamii, Sayansi na teknolojia na Uhuru kamili wa kiuchumi wa Afrika.
Vuguvugu (movement) alichangamani na upande wowote wa kisiasa, bali linalenga kuhamasisha nguvu ya mtu mweusi na wote wasiyo na sauti Duniani kote kujikomboa kiuchumi.
Vuguvugu hili linapinga ubaguzi wa aina yoyote ile ikiwa ni pamoja na makundi maalumu ya kijamii ndani na nje ya Nchi.
Karibu sana Watanzania wote.
Economic Freedom Fighters Tanzania,
Ujamaa ni Imani.View attachment 2695905
 
Salaam,

Huu utakuwa ukurasa rasmi wa Vuguvugu la Kimapinduzi la Ukombozi wa Kiuchumi Tanzania, amboa utakuhabarisha kuhusu Itikadi, falsafa, sera, utangamano, dira ya Economic Freedom Fighters Tanzania, maoni, mtazamo na mambo mengi ya kisiasa, Kiuchumi, kijamii, Sayansi na teknolojia na Uhuru kamili wa kiuchumi wa Afrika.

Vuguvugu (movement) alichangamani na upande wowote wa kisiasa, bali linalenga kuhamasisha nguvu ya mtu mweusi na wote wasiyo na sauti Duniani kote kujikomboa kiuchumi.

Vuguvugu hili linapinga ubaguzi wa aina yoyote ile ikiwa ni pamoja na makundi maalumu ya kijamii ndani na nje ya Nchi.

Karibu sana Watanzania wote.

Economic Freedom Fighters Tanzania,

Ujamaa ni Imani.View attachment 2695905
Upuuzi.

Mkipata pesa mtakuwanatugawia au mnataka tuwe ngazi yenu kupata pesa?
 
Mnahadaa wananchi kisha mkipata vipesa mnawageuka kama alivyofanya Dr. Mihogo kibarua kilipoota majani amerudi tena siasani
 
Economic Freedom Fighters Tanzania.

Economic Freedom Fighters ni vuguvugu la Ukombozi wa Kiuchumi Tanzania, kwa sasa vuguvugu hili siyo chama cha siasa, na tutaendelea kuleta Malengo, Misingi, kanuni, Muundo, Uongozi, Itikadi, falsafa, mfumo, utaratibu, utamaduni, Tunu na nguzo kuu 7 za vuguvugu hili kwa Mazingira na utamaduni wa Tanzania.

Shabaha yetu ni kuunganisha makundi yote hapa Tanzania na Afrika kwenye mapambano mapya ya Ukombozi wa kiuchumi. Economic Freedom Fighters kuonekana katika mataifa mengine hapa Afrika ni sahihi kwa sababu Misingi ya kuundwa kwa vuguvugu hili hapa Tanzania ni Pamoja na mtazamo wa kimataifa katika Ukombozi wa kiuchumi ( International Outlook).

Tuandikie kwa maoni na ushauri. economicfreedomfightertanzani@gmail.com
 
Economic Freedom Fighters, tunayo furaha kutambulisha vuguvugu hili kama sehemu ya mapambano ya uhuru wa kiuchumi Tanzania. Vuguvugu hili linauwaunganisha maskini, wanyonge, wakulima na wafanyakazi, makundi maalumu, wanaharakati, wanamapinduzi, wanamageuzi na wanasayansi, wasomi na wote wasiyo Elimu kushirikiana katika kuleta Mapinduzi ya kiuchumi.

Vuguvugu hili limeundwa chini ya misingi madhubuti ya Nidhamu ( Discipline) na Uongozi madhubuti katika kutekeleza majukumu ya vuguvugu hili hapa Tanzania. Ipo nia, sababu na uwezo wa kuakikisha tunashinda ushawishi wa wale wote wanaofikiri Tanzania inaweza kuendelea kuwa Nchi maskini ikiwa Pamoja na watu wake kuendelea kuogelea kwenye dimbwi la ufakara.


Vuguvugu la Economic Freedom Fighters, tunayo Itikadi na falsafa ambayo inalenga Mazingira, utamaduni na sifa za Tanzania katika kuakikisha tunamasisha matumizi ya Rasilimali zetu Tanzania (Afrika) zitumike kwa watu wake.

Itikadi na falsafa yetu inalenga Ukombozi wa kiuchumi Tanzania.

Inaendelea.......
Wa Kwanza kujiunga. Vuguvugu hili ni muhimu Sana hasa kipindi hiki ambacho hili CCM limejigeuza beberu jeusi. Gap linazidi kuwa kubwa.
1. Rasilimali si za wananchi tena bali za wageni.
2. Wanyonge hawana haki kuchagua mahala la kuishi.
3. Miradi ambayo ingepunguza umasikini Una pull factor kuegemea kwa mabwanyenye wa CCM mfano lile daraja la kwa mheshiniwa jerry slaa .hela badara iingie kupunguza ufukara pull factor inaenda kwa wenye nacho so miradi haina impact kwa jamii anymore
 
The official Platform for Economic Freedom Fighters to champion radical Economic policies in Tanzania. It's for fearless Fighters.

Usikose kutufuatilia, kwa miongozo, Itikadi, falsafa, Muundo, mfumo, Uongozi, sera, nguzo kuu saba (7) za Economic Freedom Fighters Tanzania, misingi na utamaduni, tabia na amali zetu, Elimu, Uchumi siasa na masuala mahususi ya Kitaifa na Afrika.
Wewe ni sehemu ya Economic Freedom Fighters Tanzania vuguvugu la kisiasa lenye malengo mahususi ya kupigania Mapinduzi/ Ukombozi wa kiuchumi katika maisha yetu.

Vuguvugu la Economic Freedom Fighters Tanzania ni kwa ajili ya wote wasiyo ogopa kupigania maslahi ya umma kwa ajili ya maisha ya vizazi na vizazi.
Kumbuka Economic Freedom Fighters Tanzania siyo chama cha siasa hili ni vuguvugu la Ukombozi kamili wa kiuchumi mara baada ya Ukombozi wa kisiasa uliyoongozwa na Mwalimu Julias Nyerere.

Tuandikie; economicfreedomfightertanzani@gmail.com

Kwa maoni, mtazamo, pongezi, maswali na mengine mengi.

"Ujamaa ni Imani"
 
Back
Top Bottom