Ebu umiza kichwa kidogo?

Ebu umiza kichwa kidogo?

Maisha hayana formula inakubidi kukaa kimktakati tu!
Uko sahihi mkuu, unaweza ukawa na Elimu na usitoboe maisha, kuliona Jicho la tatu kwenye biashara duu, kama muda mwingi ulikuwa shule na biashara umeiaza ukubwani ukiwa na majukumu, una familia, una madeni, stress za wana uliokuwa unawaona vilaza saizi wana push lc300 lanzima kichwa kiwake moto.
 
Mi sijasoma kwa mkopo so elimu yangu mali yangu na sko apa kuwasaidia wengne ila nko apa kuwatumikisha wengne ili kujiongezea mafanikio

Unapo muajiri mtu humsaidii ila unamtumikisha kwa manufaa yako na maendeleo yako

Ajira au kuajiri wengne sio msaada iyo ni uduma mnapeana kwa makubaliano ya malipo bas so usiajiri mtu ukasema umemsaidia. Huo sio msaada, misaada ni ile tunapeleka kwa yatima au sku za ijumaa kwa omba omba
 
Ipo hivi tajiri; binafsi ni ngumu kueleza huo uhusiano wa elimu na kujiajiri/kufanya biashara.

Biashara/kujiajiri au vyovyote unavyoita, binafsi naona ni kiu ya mtu, na itoke ndani kabisa ya moyo wake. Kama unavyoona madogo wanakiu ya muziki, soka, siasa au carrier flani, basi na kujiajiri hivyo hivyo. Usifanye kujiajiri kama kuganga njaa wakati unasubiria kupata kazi. 😁

Mtu aone kujiajiri ni maisha yake, aone anapaswa kujiajiri ili aishi hivyo. Huyo atafanikiwa, atapata mtaji na ataajiri wengine.
Sio ujiajiri huku huku moyo wako unataka uajiriwe. 😁 Hutamwajiri yeyote na hukofika popote hata kama una elimu.

Biashara ni tabia, unapaswa kujenga tabia ya biashara, na yenyewe itakujenga.

Ushauri: Jenga tabia ya kufanya biashara, ishi biashara, fikiria biashara kila muda kila wakati, jifunze kuhusu biashara, kosea na jisahihishe katika biashara, kua na ishi biashara, biashara ikulaze macho, biashara ikuamshe alfajiri 5Am, biashara ikustue mapigo ya moyo. Ikiwa hivyo na biashara hiyo isipokupa utajiri na maisha bora, njoo unipige mawe. 😁
 
Back
Top Bottom