idawa
JF-Expert Member
- Jan 20, 2012
- 25,284
- 38,312
Wiki iliyopita Rais Uhuru Kenyatta alifanya ziara binafsi kumtembelea Raisi Magufuli kijijini kwake Kilimani Wilaya ya Chato, waliongea mengi zaidi walisisitiza umoja na ushirikiano kwa wananchi wote bila kubaguana.
Leo Rais Museveni akitokea Angola amefanya Ziara binafsi Kama Uhuru Kenyatta kumtembelea Raisi Magufuli kijijini kwake Kilimani Chato.
Nimefuatilia hotuba zao leo mara nyingi walipokuwa wanaitaja Jumuiya ya Afrika Mashariki walikuwa wanataja nchi tatu tu Tanzania,Kenya na Uganda na hiyo imetajwa mara nyingi sana kwa viongozi wote wawili.
Ajabu haijatajwa Burundi, Rwanda ama Sudan Kusini.
Zaidi wamehitisha kwa kusema inabidi wajane wa Marais wa Zamani, Mwalimu Nyerere, Obotte na Moi inabidi wakutanishwe ili waweze kutoa ushauri jinsi mabwana zao walivyodumisha umoja wa EAC kwa wakati huo.
Wataalamu wa siasa za Afrika Mashariki hili mnalionaje, hasa ukizingatia Uganda na Rwanda mpaka wao haujatulia, Rwanda na Burundi kila siku migogoro kila mmoja akimshutumu mwenzake kutaka kumpindua.... Sudan Kusini nae ndio vile.
Maana imefika wakati vikao vya viongozi wa EAC havifanyikia sababu ya migogoro hiyo.
Je EAC ya Zamani ndio imerudi rasmi na kuwaacha wanachama wapya wahangaike na migogoro yao.?