EAC Chief warns Tanzania on regional Integration


Mkuu@Machambuzi, wakati naendelea kulipitia kwa ufasaha bandiko lako nimeona hayo masuala niliyoweka red, ambayo nilikuwa na mawazo kama yako ya kuona ni uwoga wa Tanzania. Hata hivyo, nimefanyia utafiti zaidi na kubaini ukweli kadhaa.
1.Mutual Difense Pact: Katika suala hili, Tanzania ilipingana na kifungu kilichokuwa kikisema kwamba iwapo nchi moja ya Afrika Mashariki itaingia kwenye vita na nchi nyingine iliyo nje ya Afrika Mashariki, Nchi zote za Afrika Mashariki zishirikiane na kuchangia nguvu ili kumpiga adui wa mshirika wetu. (Kama mfano wa NATO Pact vile. Utafiti wangu umebaini mambo yafuatayo ambayo nahisi Tanzania ilikuwa right kufanya hivyo (not sure kama ndizo hoja walizotumia hizi ni hoja zangu za kitafiti)

a) Nchi nyingi za Afrika Mashariki yaani Rwanda, Uganda na Kenya haziko kwenye mahusiano mazuri na majirani zao na pia ni 'nchi chokozi kiasili" hivyo kitendo cha kuwa na "alliance" ya namna hii, ni kuongeza kujiamini kwa nchi hizo kuingia kwenye vita wakiamini kwamba nchi nyingine wanachama zita-bear cost ya vita hivyo. Hivyo uwezekano wa Tanzania kuingizwa kwenye vita isiyowahusu ulikuwa ni mkubwa sana iwapo wataridhia/wangeridhia kwa muktadha huu.

b) Tanzani ina mipaka na nchi nyingi ikiwa pamoja na DRC ambayo iko kwenye majaribu ya muda mrefu na Rwanda. Kusani kwa makubaliano haya maana yake ingetokea/ikitokea Rwanda kuingia kwenye vita na Congo DR, automatically, Tanzania ingebidi ishiriki kwenye vita ikipigana upande wa Rwanda na kumpiga Congo DRC, pamoja na kuharibu mahusiano ya kibiashara na Zaire, hii kitu ingetutia matatani kule SADC ambapo nchi kama Congo ni mwana SADC

3. Alliances za kijeshi chini ya muundo wa kikanda zina kawaida ya kusababisha kuenea kwa vita kwa eneo kubwa kama historia inavyotueleza kwenye WWI na WWII. EAC ikiwa na Alliance ya kupigana vita, na ile Jumuiya ya Afrika ya Kati (ikitokea) kuwa na alliance ya kivita, maana yake vita (let say) baina ya Rwanda na Congo ingesababisha vita ya nchi zaidi ya nchi kumi. Ukichukua model hii katika multiplier effect yake, utaona kwamba Bara lote la Afrika linaweza kuingia kwenye vita, just iliyosababishwa na migogoro ya nchi mbili tu. Kwa mfano, kwasasa huenda Tanzania ilipaswa kuwa na vikosi vyake Somalia-sipati picha kungetokea nini.

2. Kuhusu Shirikisho la Kisiasa, ni uroho wa hizo nchi tatu kwa sababu wao wanaamni kwamba, njia rahisi ya kuunda shirikisho ni kuanza na shirikisho lenyewe kisha shirikisho litumike ku-enforce Customs Union, Common Market na Monetary Union; kitu ambacho ni kinyume na Mkataba na pia ni kinyume cha Kanuni zinazotawala Jumuiya za Kiuchumi za Kikanda ambazo sababu zao kubwa ni Biashara wala si utawala na ndio maana zinasajiliwa WTO si Baraza la Usalama la UN.

Nina hakika, hata nawe ukifuatilia haya uta-withdrawa na hizi propaganda kwamba Tanzania ni "sleeping elephant" au "stumbling bloc" katika Jumuiya.
cc Nguruvi3, joka Kuu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi,
Huu ni mwendelezo wa bandiko na. 161....Je Wewe binafsi pamoja na Nguruvi3, mnadhani hii model ya kuanza na Shirikisho na kisha shirikisho litumike kuimarisha Soko la Pamoja(niliyoielezea katika bandiko na 161 itaweza ku-function vizuri katika mazingira haya ya kinafiki ya ki-EAC? Ni kweli movement ya kibiashara itastawi vema kupitia model hii kuliko CU-PF?

Na ikumbukwe kwamba hili wazo la kuanza na Shirikisho limekuja baada ya kushindwa kwa wazo la kutaka kubadili Mkataba ili maamuzi yawe yanafanywa kwa kura badala ya consensus, vilevile ni wazo lililokuja baada ya kushindwa wazo la kubadili Mkataba ili eac iwe "community based organization badala ya Intergovernmental organization; kwamba nchi wanachama zitoe full authority (zipoteze authority) kwa Sekretarierti kufanya kila kitu na nchi wanachama ziridhie tu kama ilivyo EU ya sasa (ingawa "variable geometry wangetaka iendelee kuwepo)
.
 
 
Tanzania ni muhimu kuliko EAC
1. No to land purchase
2. No to common tourist visa
3. No to free work permit
ukiangalia wanachokitaka ni ivyo vitatu ambavyo kwa TZ sie tutakua tuna loose hatuna cha kugain ktk ivyo vitatu kutoka kwa hawa wenzetu so tuachane nao kabisa tujiunge na tuimaishe sadc kwani hakuna m south africa atayekuja apa aanze kulia lia akiomba auziwe ardhi au atake kuja kufanya kazi bure!!! wanataka lile jeshi la wasio na ajira kule kenya lije hapa!! big Nooooooooooooooooooooo!!!!!
 

nilifikiri huyu ps wa eac ni daktari wa fani kama uchumi anayeweza kuipeleka eac na wanainchi wake kwenye ukuransa mpya kumbe cv yake ni rebel doctor au war lord, yaani ea nzima kulikuwa hakuna mtu mwenye cv nzuri zaidi!!!!
 

Kama wewe ni incompetent kwenye labor market shauri yako, hatuwezi kusubiri hadi wewe ujitambue ndio tuungane wakati umekumbatia ujinga. Kama woga ndio kuheshimu nchi yako ni bora nionekane siheshimu. Serikali ya awamu ya tatu chini ya Mkapa ilikuwa na ujasiri wa kujadiliana na kutekeleza makubaliano, nyie akina Mwanaasha hamueleweki mnataka nini kwenye jumuia, ni bora kujitoa ijulikane moja kuliko kuwa mguu nje mguu ndani. Ni bora kuwa moto au kuwa baridi kuliko kuwaVUGUVUGU
 
kiingereza ndiyo degree ya kuelewa au?
Akisha kijua atakuwa muelewa au?

ndo maana nikaweka " / " ukizingatia thread ipo kwa kiingereza nilitaka kuestablish kati ya lugha na uelewa jamaa anaweza nini vzuri maana alichojibu ni tofauti kabis na kilichoandikwa
 
nilifikiri huyu ps wa eac ni daktari wa fani kama uchumi anayeweza kuipeleka eac na wanainchi wake kwenye ukuransa mpya kumbe cv yake ni rebel doctor au war lord, yaani ea nzima kulikuwa hakuna mtu mwenye cv nzuri zaidi!!!!
Unaijua Georgetown? au unafikiri ni vyuo vyako vya kata ulivyosoma na wapumbavu wenzako.
 
if your wife is a fool, then you know how to deal with fools then you are a MEGA SUPER FOOL

it doesnt matter who i may be...it is only a "MEGA SUPER fool" who believes that a doctor needs to be extremely ill to treat a patient...
 
UK inatekeleza makubaliano yote ya EU isipokuwa la common currency. Usiwe mwepesi wa kupindisha ukweli.

Sidhani kwamba ukweli umepindishwa hapa. kwanza, sio kweli kwamba UK inatekeleza yote isipokuwa common currency. Baadhi ya mambo ambayo UK ime-opt out (mkataba wa EU unaruhusu nchi ku-opt out) ni pamoja na schengen agreement (immigration entry visa); police and justice (along with Denmark); charter of fundamental rights (pamoja na Poland) nd Commom Security and defence (pampja na Ireland).
 
Kuna mambo ambayo yanapaswa kuangaliwa kwa kina katika hili. Ukweli unabakia kwamba:
1. Integration hailazimishwi. Aidha umo au haumo (kwa faida yako). kama unaona huwezi kasi basi achia ngazi.
2. Hawa majirani walikuwapo, wapo na wataendelea kuwepo. Lililopo ni kuamua kushughulika na swala hili sasa au kusuburi.... japo halitaondoka hili? LIPO na LITAENDELEA KUWEPO!
3. Faida za economic integration hazikaniki. Jinsi gani utatetea maslahi yako ndani ya jumuiya ni swala la ufahamu na kujiandaa for what is an eventuality.
 
Waganda wana msemo mmoja unaitwa SERWAJJA KWOTA,hiki ni kisa cha mtu mmoja aliyekuwa amekoka moto wake nyumbani kwake,pamoja nakupika chakula chake nje kulikuwa na mvua kali inanyesha ikiambata na baridi kali,kwa hiyo moto ulikuwa ukimsaidia kuondoa baridi aliyokuwa nayo.
Ghafra akatokea mtu nje aliyekuwa amelowa chapachapa nakuomba asogee akapashe mwili moto cha ajabu baada yakukubaliwa akajitanua na kumkinga mwenyeji wake, kwa EAC Tanzaia ma SERWAJJA KWOTA itawaona wengi.
Ikumbukwe Tanzania ina uzoefu wa muungano kuliko hizi nchi zote wanachama wa EAC na naona tahadhari zao zina mantiki na kama tuna maana ya kuwa na muungano wa kudumu hatuna budi kwenda taratibu tunakimbilia nini ni lazima ufanyike upembuzi yakinifu na kila mwanachama ajirizishe kwa maslahi ya wananchi wake hakuna sababu ya kukurupuka.
Kama kuna hali yakuburuzana hata kabla safari haijakolea ni bora tukabaki bila ushirika huo maanake huko mbele ya safari mambo hayaelekei mazuri.
 

argument yako ni kama ya mtu yeyote failure,unachoongea ni kwa kutanguliza feelings zako mbele tu...Dr. hajasema chochote kuhusu ardhi ila kila kinachoongelewa hapa ni ardhi ili kupumbaza watu na ku-inculcate chuki kati ya watu...mfano u can't be fair ku-blame rwanda kwa tuhuma zilizofanywa na katibu mkuu wa eac eti kwa kuwa yeye ni mnyarwanda...mambo kama haya nayaona kila mara tu hata hum jamii..pale unapokuwa na mtizamo tofauti katika baadhi ya mambo unaishia kuitwa kibaraka wa kagame...ninachotaka kujua in the first place ni watz tunashindania nini na wanyarwanda/wakenya?mbona kama tunachuki za wake wenza?Rwanda/kenya are member like any other members,isitoshe nchi zote members ni nchi huru kila nchi inamaamuzi on its own for its own intrests....tz haijakubaliana juu ya ardhi na hakuna anyebisha juu yahilo...ndo maana nasema watz hatupo tayari kwa muungano na ndo maana kila kinachofanyika tunaona kama tunataka kuibiwa,flani atafaidika zaidi n.k.....na ni kwasababu ya uoga wetu hadi suala la vitambulisho tunaita ni mlango wa nyuma....usumbufu tunaoupata upande wa migration watz ni mkubwa tukiwa tunavuka kuelekea nchi zingine za jumuiya, imagine utaulizwa maswali weee....wakati upande mwingine ni kutereza tu hii inamaanisha nini?hata kama nje kunafursa viongozi wetu hawatutengenezei mazingira ya kunufaika nazo...wengi mnazungumza kwa hisia tu bila ya kujiuliza pamoja na raslimali zetu kwanini tusifanye kenya,uganda,rwanda na burundi soko la bidhaa zetu?badala yake tunakaa kulalama land land wakati sisi tumegeuzwa soko la east africa....kenya is the 2nd big investor in tz....badala ya kutumia muda mwingi kujiuliza raslimali tunazojivunia zinatusaidiaje kubenefit muungano..tunakaa kusema muungano umelenga kukwapua raslimali zetu...yes inawezekana....tumefanya nini zaidi ya kulalamika hovyo?sijaona juhudi za maksudi mfano tz imeruhusu from 2010-2015 kuwa hawa watu wataingia na kufanya kazi i.e Professionals and Technicians and Associate Professionals....nchi yetu inakabiliwa na uhaba wa waalimu,na ni kwa exchange programs na kuruhusu walimu kutoka nchi wanachama(hasa wale wenye mifumo mizuri ya elimu zaidi yetu kama Kenya,Uganda) ili tuweze kupata ushindani katika soko la ajira matokeo yake working permit kwa mwalim wa english medium kutoka ndani ya eac ni kama "USD 3200" kwa mwaka,tunadhamilia kuondoa ujinga na kupata ushindani katika jumuiya?na zaidi ya hayo walimu kibao wamepeperushwa na kimbunga....for real are we serious?
u have some weak argument eg. umeongelea migingo.... kama issue ya nyasa itasettle itafanya malawi na tz zisiwe SADC?migogoro huwa ipo na humalizwa,na in fact that is one of the benefits of any integration be it EAC,SADC,EU,NAFTA, mention it!
 

tutakaa hivi hadi lini?jeshi la wasiyo na ajira tz ni kubwa pia sana tu...makaburu walojazana migodini hadi kwa kazi za kawaida sana ni wa wapi?hatutaweza kushindana kama tutajifungia ndani doing nothing...WTO is on our neck ina adjust mambo kila kukicha, WB vile vile na IMF vile vile,ipo siku utakumbuka muda ambao tungeutumia kujifunza na kushidana na wenzetu,tuliutumia kujifungia ndani ya bongo na kupiga domo ardhi ardhi..nk ruhusu watu waje turuhusu twende nje japo si kiholela tujifunze wanafanyaje ndo akili itafunguka...nimechoka na nyimbo zile zile za raslimali,ardhi n.k huku sina hata mia mfukoni
 
nimechoka na nyimbo zile zile za raslimali,ardhi n.k huku sina hata mia mfukoni
,Na hiyo mia utaipataje kwa uakika under EAC?

Kwanza hao wenzetu wanaonyesha ubabaifu wao wazi vile ambavyo wanaweza fanya wenyewe na vyenye maslahi kwa Mkenya wanaenda na go ahead ya Waganda na Wanyarandwa hila yakija kwenye mambo ambayo hili maslahi yawe mazuri kwao ndio Tanzania inagwaya.

Mbona kwenye maslahi kama ya kwenye ka reli kao uchwara hawajasubiri na wala kulalamika hila kwenye maslahi yetu ndio sisi tunawachelewesha, kama wangekua na nia ya wote wangelazimisha makubaliano kabla kuwahi kilicho kwenye maslahi yao, nyie ngojeeni wewe, Koba na ma traitors wenzako hiko siku tutawatia ababu kwa unafiki wenu.
 
Ima hujielewi au huelewi au vyote
 
Unaijua Georgetown? au unafikiri ni vyuo vyako vya kata ulivyosoma na wapumbavu wenzako.

Huu ndio unaitwa upofu wa fikra, kwani mtu akisoma Georgetown University ndiye anakuwa perfect kila kitu? Umesahau kuwa Chenge amesoma Harvard? AU Membe aliyesoma John Hopkins, je Georgetown na Harvard kipi kiko juu? na je huyo Graduate wa Harvard anaifanyia nini Tanzania kwa sasa? Comment ya emike still valid, kwamba yeye alikuwa akidhanni udaktari wa Sezibera ni wa PhD tena labda ya Uchumi au related discipline, kumbe si hivyo, hizi habari za Georgetown hazina maana yoyote kwani kusoma kwake Georgetown hakumuondolei uhalisia wake kwamba yeye ni "rebel doctor"
 
Last edited by a moderator:

Kwanza nina masikitiko makubwa sana kwa Idara ya Uhamiaji, RITA ikiwa wewe uitwaye Ruzibiza una-hold tittle ya uraia wa Tanzania. Pia masikitiko yangu yawafikie Kikosi cha Operesheni Kimbunga kama hawajaweza kukufikia na kukurudisha kwenu.

Pili, usitumie Jukwaa hili la JF kuandika chuki, uzandiki na uongo ili kuchafua mamlaka zetu. Ni wapi Mtanzania anapokwenda nchi nyingine za eac anaulizwa "mswali wee" na immigration wa Tanzania na haulizwi maswali hayo kutoka kwa immigration wa Kenya? Kama wewe ni mnyarwanda lazima tukuulize maswali unapotaka kuingia kama fomu yako haina maelezo yanayotosheleza yanayoendana na Mkataba wa Soko la Pamoja.

Tatu, unasema kwa kujua au kuhisia kwamba mfumo wa elimu wa Kenya na Uganda ni mzuri kuliko wa Tanzania? Huoni kama umejichanganya hapa? Mfumo wa Uganda kiasi unafana na wa Tanzania kwamba wana kidato cha sita ule wa Kenya unaishia kidato cha nne kabla ya kuingia chuoni, nini kusudia lako hapa. By the way, Tanzania iko katika "traffic light system" kwa masuala yote na sasa hivi taa inayowaka ni yellow, kwa hiyo wewe na mabwana zako kaeni tayari kuipokea red light itakayowafanya muwe kimya (sidhani kama utakuwa umeelewa hapa). Ungelikuwepo miaka ya tisini, ungejua idadi kubwa ya watanzania waliokuwa wakivuka kwenda Kenya na Ugnada kufuata the so called "international english medium schools", lakini leo hii watanzania wana "International English Medium Schools za kufa mtu; watanzania wanaovuka kwenda Uganda ni wale walifeli Tanzania na wanaenda kufanya-repeatition huko na kuafulu ili wajiunge na vyuo vya huko. Je unajua record ya wahitimu wa vyuo vikuu 10 years back kwa Tanzania ilikuwaje ukilinganisha na nchi za Kenya na Uganda, na sasa hivi hali ikoje? Huu ni mfano mchache wa "yellow light" inayowashwa na Tanzania. Kwa kifupi Tanzania hatuna tatizo kubwa na "mfumo mbaya wa elimu" labda ungelisema usimamizi mbaya wa elimu kidogo ungelieleweka.
 
Last edited by a moderator:
eu mbona hawakuibagua united kingdom?
tanzania knows its identity and position in east africa and it cant bow at elusive demands from its neighbours . This orientation is looked upon very cautiously . Sezibera is a rwandese personnell in east africa trying to propagate the long standing ideology of the bahima empire in east africa. We are not ready. Tumemsikia waziri wa africa mashariki mh. Samuel sita kwahiyo hatuwezi kumpuuza hata kidogo. Huo uhuni unaofanywa na secreatariet inayoongozwa na sezibera hauwezi kuachwa hivihivi na watanzania kamwe hatuko tayari kuingia east africa KICHWAKICHWA bila kujielewa, kamwe haitatokea potezea muendeleee ninyi wenyewe wahuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…