E Fm mbona mnakomalia suala la Bashite hivyo?

E Fm mbona mnakomalia suala la Bashite hivyo?

kuna nesi kafungwa miaka 28 kwa kosa la kufoji vyeti ili apate ugali wa wanawe, je na huyo unamzungumziaje????? hebu jaribu kuvaa uhusika wa watoto wa huyu Mama.

kulia sio sababu ya kutuaminisha yeye hakununua na wala hatumii vyeti vya mtu mwingine, hatutaweza kukaa kimya hadi akiri kuwa anatumia vyeti visivyo vyake ambayo kisheria inajulikana ni makosa, na mtuhumiwa huwa anafungwa jela miaka saba.
 
Hatuwezi kumuacha kwa sababu ya kulia tunataka vyeti, hatukubali kuongozwa na kilaza . watu tupo na PhD Leo kilaza wa division zero ndo atuongoze aende akawe mtendaji wa kijiji cha koromije huko
 
Naunga mkono hoja,jamani itoshe sasa hii ni too much! Tukilala Makonda tukiamka Bashite wengine mpaka tunaota tupo koromije! Loh! Emu kuweni na huruma hata kiduchu.

hapana inaumiza sana kwa wale wazee walio achishwa kazi wakiwa wamebakiza miaka 3 wastaafu kazi kwa kosa la kununua vyeti vya mtu mwingine.
 
Akiweka vyeti mezani tutanyamaza au angekua hana nyodo
 
Hatuwezi kumuacha kwa sababu wa kulia tunataka vyeti, hatukubali kuongozwa na kilaza .
tatizo sio ukilaza tatizo ni kosa kisheria kutumia vyeti visivyo vyako, na unaposhindwa kuikubali sifuri yako hadi kuazima vyeti kama sio kununua kabisa
 
kuna uwezekano wa chozi la jana Mungu "og" kamwambia waonyeshe vyeti watakusamehe.......
 
Naunga mkono hoja! Kwani hata hizo threads sizisomi tena maana ni yale yale tu! Stop!
 
Hata tukiongea 24 hrs kuhusu Makonda hatutaletewa vyakula majumbani mwetu. Mleta mada uko sawa kabisa. Life has to go on, tufanye kazi na tuyaache ya Makonda.

Kwani we ulitegemea uletewe chakula?? Wewe acha kumwongelea wengine waache waaendelee , na wao wakichoka wataacha.. shida ikowapi.... Call Me J..
 
Anashinda makanisani anasumbua watu wanamuombea Paul Makonda kumbe yeye ni Daud Bashite. Dar hatuwezi kuongozwa na KIHIYO aoneshe vyeti yaishe sio analeta sarakasi
Hahahaha! Yaani aibu hii mpaka kwa mzee wa kipara
 
Wakuu tumejadiri mengi kuhusu mheshimiwa huyo, binafsi naona itoshe sasa.

Tuseme imetosha kwa sababu yale machozi ya jana ni kauli ya kuomba msamaha kwa namna moja au nyingine.

Ukiona mwanaume aliyekuwa jasiri na mwenyewe nyodo na majibu ya fedheha na kudharirisha analia , tena analia mbele za watu ujue amejutia makosa yake.

Naomba tuachane na habari za Makonda kama Makonda. Tuendelee na mengine, jamani ameshajifunza somo kubwa sana ninaamini atabadirika sana.

Nawe Bwana Paulo Makonda Maumivu uliyoyapata kwa tukio hili ndiyo waliopata wale ulikuwa unawatukana na kuwadharirisha mbele ya kamera, Mungu amekuonjesha sehemu ndogo sana, acha kutukana na kudharirisha watu.

Nilikwambia siku moja kama unakumbuka kuwa cheo ni dhamana.

Familia ya marehem Kabwe inakutazama kama wewe ndiyo sababisho la yote yaliyomtokea baba yule.

Acha uongozi wa mihemko, tubu kwa wote uliowadharirisha, akiwemo ,manji, mbowe, Gwajima , wema na wengine.

Narudia kuwasihi tena wanajf wenzangu itoshe kuhusu huyu mtu jamani.

Wanaoniunga mkono kwa hili Mungu awabariki sana.

Msiyoniunga mkono niwaombe mjaribu kuvaa uhusika japo kwa dakika moja. Najua mkisha uvaa uhusika kwa dakika moja mtanielewa na kuniunga mkono.
Asanteni.
Usitukane wakunga (umenikumbusha )
 
Back
Top Bottom