Wakuu tumejadiri mengi kuhusu mheshimiwa huyo, binafsi naona itoshe sasa.
Tuseme imetosha kwa sababu yale machozi ya jana ni kauli ya kuomba msamaha kwa namna moja au nyingine.
Ukiona mwanaume aliyekuwa jasiri na mwenyewe nyodo na majibu ya fedheha na kudharirisha analia , tena analia mbele za watu ujue amejutia makosa yake.
Naomba tuachane na habari za Makonda kama Makonda. Tuendelee na mengine, jamani ameshajifunza somo kubwa sana ninaamini atabadirika sana.
Nawe Bwana Paulo Makonda Maumivu uliyoyapata kwa tukio hili ndiyo waliopata wale ulikuwa unawatukana na kuwadharirisha mbele ya kamera, Mungu amekuonjesha sehemu ndogo sana, acha kutukana na kudharirisha watu.
Nilikwambia siku moja kama unakumbuka kuwa cheo ni dhamana.
Familia ya marehem Kabwe inakutazama kama wewe ndiyo sababisho la yote yaliyomtokea baba yule.
Acha uongozi wa mihemko, tubu kwa wote uliowadharirisha, akiwemo ,manji, mbowe, Gwajima , wema na wengine.
Narudia kuwasihi tena wanajf wenzangu itoshe kuhusu huyu mtu jamani.
Wanaoniunga mkono kwa hili Mungu awabariki sana.
Msiyoniunga mkono niwaombe mjaribu kuvaa uhusika japo kwa dakika moja. Najua mkisha uvaa uhusika kwa dakika moja mtanielewa na kuniunga mkono.
Asanteni.