Duuuh, kweli wanawake wengine!

Duuuh, kweli wanawake wengine!

Aisee hawa watu wakati mwingine wanatugombanisha na rafiki zetu wa karibu,tena tuliotoka nao mbali,najiuliza jamaa yangu atanielewa nikimwambia hali halisi ya msichana wake?au ndo utakuwa mwisho wa urafiki wetu?
Piga simu kwa jamaa mbele yake mwambie bint kaja moro kaomba aje akusalimie kang'ang'ania kwako sema yote tena mweleze hutaki tatizo nae ndio sababu ya kumpigia ukidanganya bint anabadilisha maneno hutoongea tena na rafiki yako, hana nia njema huyo atakugombanisha na mchumba wako
 
Mfukuze haraka sana tena mapema
Acha mazoea mabaya na shemeji yako
 
Ndugu yangu kusema ukweli,nashindwa kumwambia jamaa coz anaweza asiamini ntakachomwambia,jamaa anamwamini sana msichana wake,awezafikiri kuwa nawagombanisha tu,nathamini urafiki wetu,sipendi kugombana naye kabisa!!!
Usituvutie mada we huwez kuamua hadi umwambie rfk ako
 
Mkuu we nawe hujielewi...We unaona huyu jamaa ana nia ya dhati ya kukimbia uzinzi???...
Alitakiwa asimkaribishe kabisa huyo mwanamke coz alishaonyesha nn anataka...Nwei tuseme jamaa ni slow mooo,hakuelewa nia ya huyo mwanamke ndo mana akamkaribisha..Mwanamke amefika na kumueleza wazi kabisa anataka nini..Kwa mtu ambaye hataki kufanya uzinzi Angeshafanya maamuzi tayari..Haihitaji kuomba ushauri...
kwa hiyo we mtu ukiona anaelekea kwenye kuzini ndo unamsukuma kabisa aende akazini?usimuangalie yeye jiangalie wewe pia na nafsi yako je hili jambo linamtokea dada yako utazidi kumtia ndimu huyo mwambunnyara aende akazini?
 
Huyo shemu si mwaminifu tena......hata ukimushit hawezi acha tabia chafu....cha kufanya stay away from her na umpeleke Guest ya karibu...then kesho mpe nauli arudi Dom.....akiendelea mjulishe mdau......ni vzr kuvunja uhusiano na huyo shemu kuliko rafiki yako..u will remain mshindi na mfalme km utafanya hivo.
Nashukuru kwa ushauri wako,hapa namalizia kuandaa dinner then niende nikalale hotel tu
 
Sppamoja ya kwamba namheshim sana mke wangu sinaga tabia ya kuvumilia wanawake kiasi hiki aisee. We piga mambo mataokeo utajua mbele kwa mbele mi hata angekuwa mke wa kaka yangu wa dam kwa mazingira hayo nikimuacha mizimu ya Kipare lazima iniadhibu.

Duc in Altum
watu ambao walikuwa wanamsumbua ndalichako kwenye mitihani ya necta badala ya kujibu maswali wanachora katuni utawajua tu
 
kwa hiyo we mtu ukiona anaelekea kwenye kuzini ndo unamsukuma kabisa aende akazini?usimuangalie yeye jiangalie wewe pia na nafsi yako je hili jambo linamtokea dada yako utazidi kumtia ndimu huyo mwambunnyara aende akazini?
We umemkaribisha simba ndani zen unaanza kusumbua majirani waje kukusaidia kumuondoa..Acha akutafune tu..Btw niliandika ile comment kiutani...Ila Niliamua kukupa maelezo baada ya kuona umechukulia serious
 
Nashukuru kwa ushauri wako,hapa namalizia kuandaa dinner then niende nikalale hotel tu
Mkuu samahani kwa swali kama hutajali kwani we na mchumba wako mnaishi mikoa tofauti??kama yuko karibu muite aje ye mpelekeni hotelini kama yuko mbali ndo majanga kalale tu hotelini maana hamna namna
 
Maandiko matakatifu ya biblia yanasema Ikimbie zinaa, kwani aziniye na mwanamke hana akili kwani afanya jambo litakalomwangamiza nafasi yake

Mwambie ukweli kwamba hauko tayari kuzini naye,

Na pia hautaharibu uhusiano wao na mwenzi wake ikiwezekana mshauri aache tabia yake mbaya.
 
Kama una ndugu wa kike wa karibu mpeleke akalale huko.
 
Duuu. Hawa watoto hawatocheki. Hizo k zinapanuka tu. Looooh.
 
Mstue jamaa aje kesho!
Mwanamke kaolewa hana staha kama alitaka mambo hayo asingeolewa!
 
Najaribu kutafakari kwenye situation hio ningefanya nini?!
 
Nina rafiki yangu amekuwa akiishi Dodoma na msichana wake,the same room as Mr and Mrs japo hawajafunga ndoa.
Jamaa wangu amekuwa akimwamini sana msichana wake,kwa sababu kiukweli ukimtazama shemeji yangu huyu ni mpole sana.
Kilichonifanya niandike uzi huu,ni kilichonitokea kwa shemeji yangu huyu,hakika mpaka dakika hii siamini hata chembe.
Tumekuwa na mawasiliano ya kawaida sana kama mtu na shemejiye,kwa kipindi kirefu tu,na sikuwahi kuwa na shaka naye,wala jamaa hakuwahi kuonyesha mashaka kwa shemeji yangu huyu.
Jamaa wangu alikuwa akisaka ajira kwa udi na uvumba,Mungu kamjalia amepata kazi mkoa mwingine tofauti na Dodoma,hivyo ilimlazimu kwenda kazini j.tatu ya wiki hii.
Cha ajabu siku ya j.nne shemeji yangu alinipigia simu majira ya saa nne usiku,tulizungumza mengi,lakini sauti yake ilibadilika sana,ilikuwa yenye ishara ya mahaba mno,sikutilia maanani sana nkajua ni kwa sababu ni usiku,yawezekana ana usingizi mno.
Jana akanipigia tena usiku na kunambia Shem kesho natamani nije nkutembelee,(Mimi naishi Morogoro), ila usimwambie jamaa,nilishtushwa na hiyo statement, kwanini nisimwambie jamaa,akadai jamaa akijua itakuwa noma.
Niliishiwa pozi kwa ghafla,nikamwambia hapana,amsubiri jamaa akija ndo waje wote,lakini hakutilia maanani kile nlichomwambia,baada ya muda mfupi akanitumia ujumbe mfupi wa simu "Shem naomba usijali,sina nia mbaya najua unampenda sana .......(anamtaja jina mchumba wangu,)siwezi kukuharibia,lakini naomba unipokee tu,kesho nakuja").
Leo asubuhi kanitumia SMS, " Shem naenda stand kupanda gari ya kuja Moro,plz usimwambie.......(anamtaja jamaa wangu).
Nlijua huyu ananitania tu,lakini ajabu majira ya saa nane amenambia yupo msamvu stand,anaomba nimuelekeze namna ya kufika home,basi baada ya kumpa maelezo,amefika na nimemkaribisha home.
Baada ya kumwandalia chakula amekula,amekaa kwenye sofa anachart,nkamuuliza vipi una ndugu mwingine hapa Moro kajibu hapana.
Baadaye ananambia "ila Shem sio siri Leo nkwambie tu,namuonea wivu sana mpnz wako,kwa muda mrefu nafikiriaga why didn't I meet you early". Nimeishia kumuangalia tu usoni,coz nlikuwa simuelewi kabisa.
Nimemuuliza shem unarudi SAA ngapi Dodoma ananambia ataondoka kwangu by j.mosi,(na yupo comfortable kabisa kwenye sofa haonyeshi hata chembe ya woga.
Najiuliza,nifanyeje hapa,
1.Nimwambie jamaa yangu?
2.Ninyamaze na nikatafute sehemu nyingine ya kulala nimwache alale peke yake?
Naombeni ushauri wenu wadau,maana siku ya leo naiona kuwa ngumu sana kwangu,daaaah baadhi ya wanawake wetu ni shida kwa kweli,I don't know why is it in this way????
Duuh kweli wanawake wengineee........... Ni shida
 
Back
Top Bottom