Duuu...! Enzi hizo...bora turudi zamani...!

Enzi hizo wanafunzi wanasafiri kwa gari moshi kwa warrant hakuna malipo mkoa hadi mkoa
 
Enzi hizo majeneza yalikuwa mpaka mtu afe ndo linachongwa lakini siku hizi dah majeneza kila kona na viwango kama magari.
 

kwenye migomo hapo umechemka muulize Sita mb alifanyweje na nyerere
 
hahahaaaaaa sana mkuu umenikumbusha sabuni ya imperial ukitoka hapo unapaka mafuta ya kutoka zanzibari yalikuwa kwenye vimikebe hivi yananukia balaaaa mkuu Synthesizer nikumbushe jina la haya mafuta kama unalikumbuka yalikuwa na pisha ya ngalawa
 
Last edited by a moderator:
Enzi zako za zamani ni mwaka gani?

Hata mimi ndo nimejiuliza ni miaka ipi anaongelea maana shule ninazozijua zilizokuwa zikichukua wanafunzi walifanya vizuri toka mkoloni huwezi kuacha kutaja Tabora boys na girls,hata Kibaha ndo magwiji wa siku nyingi.
 
Enzi hizo ukienda kuanza darasa la kwanza ukubwa unapimwa kwa kupitisha mkono juu ya kichwa ili kushika sikio la kushoto,shule nyingi zilikuwa mbali na unawahi namba maana kutoka nyumbani hadi shuleni ni kukimbia,shuleni kulikuwa na vikundi mbalimbali vya fani mfano kuchora,mwandiko,hisabati , kukimbia nk,kipindi hicho mipira tunacheza peku lakini mtu akikukanyaga/akikuchezea rafu unaweza chechemea mwezi mzima...lol! FRANKLY, THOSE WERE GOOD OLD DAYS
 

Duuu! mwana kweli wewe wa zamani kinoma noma!
 
nakumbuka nesi mmoja alikuwa akikuchoma sindano unavimba kalio la upande mmoja.....Ukifika zahanati ukimwona unaliaaaaaaa....hadi unakaukiwa machozi... kuna mwenzie ulikuwa ukimwona unafurahiii akikuchoma sindano hata husikiiiiiiiiiiiii akifikicha hapo na pamba yenye spirit ndo rahaaa inaongezeka then anakwambia poleeee poleeeee we zamani rahaaaa
 
enzi hizo ngono ilikua nyama nyama tofauti na sasa nyama mpira nyama

enzi hizo hatukuwa na maneno ya kuchekesha kama kapuyanga alivyonichekesha mpaka nimepaliwa......ha ha ha hawa watoto wa siku hizi wanchekesha kidigital zaidi.
 
Haya wazee wa zamani tumewaelewa...
Population inakua, changes are inevitable, na uchumi unazidi kuporomoka, hela wanakopa IMF ili wajenge nyumba zao Dubai na California... Kazi burebure si sababu wazungu waliondoka wakawaachia kampuni kibao huku watu wenye elimu ndio walikua wameanza anza kuonekana, kila mtu na degree siku hizi mnategemea nini kama sio kunyang'anyana, mjanja lazima apewe...
Usijeshangaa serikali inasema inatumia zaidi ya bilioni kumi kununulia walimu chai asubuhi..
 
bora sikuwepo enzi hizo nisingefaidi mambo ya smartphone,tv bwelele,computer kibwena,kila mtu anafika sekondari miaka yenu mnamaliza la 7 watoto 150 alafu anafaulu 1...dunia hii ndio tamu acheni kusifia uongo nyie mababu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…