Enzi za kuvaa viatu vya utanikoma saa nane jua likiwaka ama DH(dingi ana huwezo)
hehehe na kupokea simu ilikuwa dilii....simu ikiita tu watoto mnatoka ndukii kuwahi kupokea...
Duuu,
leo nimekaa nimefikiria sana enzi za zamani kwa kweli nimetamani turudi enzi hizo, enzi za zamani, kila kitu kilikuwa poa, upendo amani yaan raha sana zamani kuliko sasa!!
nimekumbuka enzi hizo tunajiendea HOSPITALINI bureee yaani ukifika manesi wanakupokea kwa furaha wanakuhudumia, na unapewa dawa bureeee.....duuu enzi hizo jamani ilikuwa raha saaaana
nimekumbuka enzi hizo kweli ukisikia mwanafunzi kafaulu darasa la saba au form four ujue kweli ni kichwa tena balaaa, yaani wale vichwa wa juu walikuwa wanapatikana MZUMBE, ILBORU, KILAKALA, MSALATO..ifunda, iyunga ....teh teh jamani jamani enzi zetu.safi sana.
nakumbuka enzi izo ukitaja UDSM basi unataja hapo MUHIMBILI, ARDHI, DUCE, IJMC na ilikuwa mtu ili aende chuo kikuuu kweli inaitaji usomeee, kwanza kulikuwa hakuna migomo kabisa. lakini sasa
nakumbuka enzi za makamba dar es salaam, teh teh kina matonya, bongo ilikuwa burudani sana, wanafunzi wa sekondari dar wanavaa vikaptula...teh teh jamani enzi hizo ilikuwa bomba eeeh
.......!!!!
Enzi za kuvaa viatu vya utanikoma saa nane jua likiwaka ama DH(dingi ana huwezo)
tehe tehe teheeeeeeeeee,na gesti ni kizani au vichakani chezea enzi weweeeeeenzi hizo ngono ilikua nyama nyama tofauti na sasa nyama mpira nyama
tehe tehe teheeeeeeeeee,na gesti ni gizani au vichakani chezea enzi weweeeeeenzi hizo ngono ilikua nyama nyama tofauti na sasa nyama mpira nyama
hahahaaaaaa sana mkuu umenikumbusha sabuni ya imperial ukitoka hapo unapaka mafuta ya kutoka zanzibari yalikuwa kwenye vimikebe hivi yananukia balaaaa mkuu Synthesizer nikumbushe jina la haya mafuta kama unalikumbuka yalikuwa na pisha ya ngalawaEnzi hizo tulikuwa tunafanya kazi bila komputer masaa nae, tunatumiana barua kwa posta, tunapanda UDA bila foleni barabarani, tunakula mikate ya siha, tunaangalia sinema za bure Drive In, kuna treni kila siku kwenda Mwanza na Kigoma na mara kadhaa kwa wiki kwenda Arusha, tunalala chuma kimoja watu wawili na tunajifungulia chai na maziwa kweye vibomba UDSM, tukipikiwa wali maharage lazima litoke tangazo kutuomba radhi pale UDSM, tunaheshimu wanasiasa, tunaandamana siku kuu za sabasaba na kushona (sio kununua) nguo mpya, tunapangiwa kazi hadi Uganda na Kenya tkiwa shirika la East African au customs, raisi na mawaziri wakitembelea mikoani tunaenda kuwapokea na matawi ya miti mikononi!
Yaani, basi tu!
Mwisho wa mambo mazuri bwana ilikuwa Idd Amin alipochukua nchi Uganda na Arap Moi alipochukua nchi Kenya.
Tukapigana vita Uganda
Tukaanza kupanga foleni ya unga na sukari, tukajua kuna mwendo wa kuruka, tukaujua ugali wa yanga, tukawa na maduka ya kaya, zikaingia dala dala, tukaanza kununua bia na soda kwa vibali, ice cream zikapotea, Blue Band za Kenya zikapotea, tukaanza kununua Colgate na kanga toka Kenya kwa magendo, tuaka tunatakiwa kuwa na kibali kuleta debe moja ya mchele toka Mbeya kuja Dar, tukawa tukienda ulaya tunafanya shopping ya colgate, sabuni Imperial na viatu vya kukimbilia (raba mtoni), suruali za Jeans na kodurai zikawa mali adimu sana, tukawa tunakosa usafiri wa kwenda mikoani kwa sababu mabasi ya Relwe na Kamata na Kwacha yamejaa mwezi mzima.
Mmh, kweli mambo hubadilika.
Enzi zako za zamani ni mwaka gani?
Enzi hizo wanafunzi wanasafiri kwa gari moshi kwa warrant hakuna malipo mkoa hadi mkoa
Enzi hizo tulikuwa tunafanya kazi bila komputer masaa nae, tunatumiana barua kwa posta, tunapanda UDA bila foleni barabarani, tunakula mikate ya siha, tunaangalia sinema za bure Drive In, kuna treni kila siku kwenda Mwanza na Kigoma na mara kadhaa kwa wiki kwenda Arusha, tunalala chuma kimoja watu wawili na tunajifungulia chai na maziwa kweye vibomba UDSM, tukipikiwa wali maharage lazima litoke tangazo kutuomba radhi pale UDSM, tunaheshimu wanasiasa, tunaandamana siku kuu za sabasaba na kushona (sio kununua) nguo mpya, tunapangiwa kazi hadi Uganda na Kenya tkiwa shirika la East African au customs, raisi na mawaziri wakitembelea mikoani tunaenda kuwapokea na matawi ya miti mikononi!
Yaani, basi tu!
Mwisho wa mambo mazuri bwana ilikuwa Idd Amin alipochukua nchi Uganda na Arap Moi alipochukua nchi Kenya.
Tukapigana vita Uganda
Tukaanza kupanga foleni ya unga na sukari, tukajua kuna mwendo wa kuruka, tukaujua ugali wa yanga, tukawa na maduka ya kaya, zikaingia dala dala, tukaanza kununua bia na soda kwa vibali, ice cream zikapotea, Blue Band za Kenya zikapotea, tukaanza kununua Colgate na kanga toka Kenya kwa magendo, tuaka tunatakiwa kuwa na kibali kuleta debe moja ya mchele toka Mbeya kuja Dar, tukawa tukienda ulaya tunafanya shopping ya colgate, sabuni Imperial na viatu vya kukimbilia (raba mtoni), suruali za Jeans na kodurai zikawa mali adimu sana, tukawa tunakosa usafiri wa kwenda mikoani kwa sababu mabasi ya Relwe na Kamata na Kwacha yamejaa mwezi mzima.
Mmh, kweli mambo hubadilika.
enzi hizo ngono ilikua nyama nyama tofauti na sasa nyama mpira nyama