Iselamagazi
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 5,917
- 6,002
Duuu,
leo
nimekaa nimefikiria sana enzi za zamani kwa kweli nimetamani turudi
enzi hizo, enzi za zamani, kila kitu kilikuwa poa, upendo amani yaan
raha sana zamani kuliko sasa!!
nimekumbuka enzi hizo tunajiendea HOSPITALINI bureee yaani ukifika
manesi wanakupokea kwa furaha wanakuhudumia, na unapewa dawa
bureeee.....duuu enzi hizo jamani ilikuwa raha saaaana
nimekumbuka enzi hizo kweli ukisikia mwanafunzi kafaulu darasa la saba
au form four ujue kweli ni kichwa tena balaaa, yaani wale vichwa wa juu
walikuwa wanapatikana MZUMBE, ILBORU, KILAKALA, MSALATO..ifunda, iyunga
....teh teh jamani jamani enzi zetu.safi sana.
nakumbuka enzi izo ukitaja UDSM basi unataja hapo MUHIMBILI, ARDHI,
DUCE, IJMC na ilikuwa mtu ili aende chuo kikuuu kweli inaitaji usomeee,
kwanza kulikuwa hakuna migomo kabisa. lakini sasa
nakumbuka enzi za makamba dar es salaam, teh teh kina matonya, bongo
ilikuwa burudani sana, wanafunzi wa sekondari dar wanavaa
vikaptula...teh teh jamani enzi hizo ilikuwa bomba eeeh
.......!!!!
Enzi zile, kama dingi ana kauwezo fulani. sehemu maarufu za kuangalia film ni kwenye majumba ya Wadosi: Empress, NewChox, Avalon, Nulite, Cameo, Diamond Talkies, Liberty ....