Duuhh!! Kupima UKIMWI sio kitu ya mchezo!!

The Magnificent

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
2,694
1,247
Unaweza ukafia palepale!!

Inaogopesha zaidi baada ya kuona zile movement za waathirika wanaochukua ARV's

Kwa wale waliopima naomba kushea nao experience hapa,mwenzenu nimepata hard time ambayo sijawahi kupata tangu nimezaliwa!!

Anyway...thanks God nipo fresh,ila cha moto nimekiona......na nimeamua kubadilisha mfumo wangu mzima wa maisha!!
 
ndio ujue sasa........na nina uhakika nikikwambia nenda kapime tena kesho.....wenge linaanza upya.....UKIMWI usikiage tu.........
 
Nimewahi kupima mara kadhaa pale AMREF barabara ya Ali Hassan Mwinyi, inahitaji ujasiri kwa kweli. Kwanza unapoingia unapishana na watu mbalimbali wenye hali tofauti, wengine wanaingia kama wewe, wengine wanasubiri majibu, wengine wameghairi kupima etc. Siku ya kwanza niliuza, "majibu yanatoka baada ya muda gani?".

Nikaambiwa kama nusu saa. Ila yule dada pale mapokezi alijua nina wasiwasi, akasema "kama unahitajika haraka kazini, ni bora ukatafuta siku yenye una nafasi". Nadhani alijua nataka kusepa kabla hata sijapima, ila nilisubiri nikapima. Kule waiting room ndio usiseme, mkanda wa video ya waathirika inaongeza hofu (kama unamjua Phil Lutaaya wa Uganda, alikuwa anawekwa sana ktk video kutoa shuhuda).

Anakuja nesi, anakuita jina bandia (tunaandikisha kwa ID kule kama za JF!!), unaenda kupima, unarudi waiting room kusubiri majibu. Seat hazikaliki. Watu wanapiga stori kupotezea mawazo, lakini wapi! Anakuja nesi tena, hujui anakuita wewe ukachukue majibu au mwingine akapime! Ni hofu tupu! Mara jina lako linaitwa tena, unapewa ushauri tena. Ushauri unahusu mambo mbalimbali, mengine yanatoa reflection kama vile umeathirika. Unaona ushauri wake ni kama vile unakucheleweshea majibu, unatamani kumnyang'anya kadi ili usome majibu.

Mara anakupa majibu, anakuambia ni negative! Unaondoka na amani, ila unasema ngoja nikawaage 'washikaji' niliowaacha waiting room, kwani sasa walau una ujasiri! Ukiingia na tabasamu tu wenyewe wanajua majibu ni safi! Unachukua box mbili tatu za kondomu pale na vipeperushi kibao! Unapita pale mapokezi na kumuaga yule dada!

Tabasamu lako linampa picha halisi ya majibu yako! Anakutania kidogo kwamba sasa wahi kazini, ulikuwa na haraka sana! Mnacheka, unaondoka. Usisahau kumuaga mlinzi pale getini, kwani yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kukupokea! Endeleeni .....
 
Duu mzee mimi nilipita pale usalama tandika kwenye kanisa la waadventist pale wapo angaza nikaingia kwa mhudumu akawa ananipa ushauri kwa njia ya kuniuliza maswali alipo gundua ninauwelewa mkubwa akaniambia pima mpaka nimalize kukupa ushauri majibu yatakuwa yametoka nikamwambia ngoja nikamlete mwenzangu tupime wote nimemuacha hapo nje alivyo niachia upenyo nilchoropoka pale nasikurudi tena hadi leo
 
Nimewahi kupima mara kadhaa pale AMREF barabara ya Ali Hassan Mwinyi, inahitaji ujasiri kwa kweli. Kwanza unapoingia unapishana na watu mbalimbali wenye hali tofauti, wengine wanaingia kama wewe, wengine wanasubiri majibu, wengine wameghairi kupima etc. Siku ya kwanza niliuza, "majibu yanatoka baada ya muda gani?". Nikaambiwa kama nusu saa. Ila yule dada pale mapokezi alijua nina wasiwasi, akasema "kama unahitajika haraka kazini, ni bora ukatafuta siku yenye una nafasi". Nadhani alijua nataka kusepa kabla hata sijapima, ila nilisubiri nikapima. Kule waiting room ndio usiseme, mkanda wa video ya waathirika inaongeza hofu (kama unamjua Phil Lutaaya wa Uganda, alikuwa anawekwa sana ktk video kutoa shuhuda). Anakuja nesi, anakuita jina bandia (tunaandikisha kwa ID kule kama za JF!!), unaenda kupima, unarudi waiting room kusubiri majibu. Seat hazikaliki. Watu wanapiga stori kupotezea mawazo, lakini wapi! Anakuja nesi tena, hujui anakuita wewe ukachukue majibu au mwingine akapime! Ni hofu tupu! Mara jina lako linaitwa tena, unapewa ushauri tena. Ushauri unahusu mambo mbalimbali, mengine yanatoa reflection kama vile umeathirika. Unaona ushauri wake ni kama vile unakucheleweshea majibu, unatamani kumnyang'anya kadi ili usome majibu. Mara anakupa majibu, anakuambia ni negative! Unaondoka na amani, ila unasema ngoja nikawaage 'washikaji' niliowaacha waiting room, kwani sasa walau una ujasiri! Ukiingia na tabasamu tu wenyewe wanajua majibu ni safi! Unachukua box mbili tatu za kondomu pale na vipeperushi kibao! Unapita pale mapokezi na kumuaga yule dada! Tabasamu lako linampa picha halisi ya majibu yako! Anakutania kidogo kwamba sasa wahi kazini, ulikuwa na haraka sana! Mnacheka, unaondoka. Usisahau kumuaga mlinzi pale getini, kwani yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kukupokea! Endeleeni .....
mtaani unakutana na ka teenager kameiva haswa,unaona kutumia kondom hujakatendea haki umesahau unakula kavu kavu
 
ndio ujue sasa........na nina uhakika nikikwambia nenda kapime tena kesho.....wenge linaanza upya.....UKIMWI usikiage tu.........
Em acheni kutisha watu nyie.... Hii si miaka ya 1980 wala 90. Ukimwi una tatizo gani; kula vizuri, lala vizuri lubricate kale kasehemu basi. tatizo linaanzia wapi...
 
Inatisha sana kujifahamu kuwa afya yako sasa iko hatarini lakini nadhani inaweza kutisha zaidi ukifahamu kuwa umeathilika. Tubadili tabia ndg zangu
 
he he he si wengine tumezoea na tunajipima wenyewe ingawa its not ethical.......all that is needed ni kukubali hali yako na kujua kwamba life goes on even if you are positive.all you need is strength to move on
 
Duh, kupima ni kazi kubwa. Mimi nilihangaika vibaya mno. Hadi majibu yanatoka nilisali sala zote. Hata ushauri nliona ni kupotezeana tu muda. Ila wakuu Mungu atusaidie maana watu hawajali tena.
 
Em acheni kutisha watu nyie.... Hii si miaka ya 1980 wala 90. Ukimwi una tatizo gani; kula vizuri, lala vizuri lubricate kale kasehemu basi. tatizo linaanzia wapi...

mkuu....ukimwi hauzoeleki.....tuna ndugu .......jamaa na marafiki wanaugua huo ugonjwa....tena wengine wa karibu sana.....siwaoni wakiwa wamerelax.....sawa matumaini wanayo....ila kuna viusumbufu fulani wanavyo vidogodogo vya hapa na pale.....ki ukweli UKIMWI ni soo.....japo tunaishi kwa matumaini......
 
Nimewahi kupima mara kadhaa pale AMREF barabara ya Ali Hassan Mwinyi, inahitaji ujasiri kwa kweli. Kwanza unapoingia unapishana na watu mbalimbali wenye hali tofauti, wengine wanaingia kama wewe, wengine wanasubiri majibu, wengine wameghairi kupima etc. Siku ya kwanza niliuza, "majibu yanatoka baada ya muda gani?". Nikaambiwa kama nusu saa. Ila yule dada pale mapokezi alijua nina wasiwasi, akasema "kama unahitajika haraka kazini, ni bora ukatafuta siku yenye una nafasi". Nadhani alijua nataka kusepa kabla hata sijapima, ila nilisubiri nikapima. Kule waiting room ndio usiseme, mkanda wa video ya waathirika inaongeza hofu (kama unamjua Phil Lutaaya wa Uganda, alikuwa anawekwa sana ktk video kutoa shuhuda). Anakuja nesi, anakuita jina bandia (tunaandikisha kwa ID kule kama za JF!!), unaenda kupima, unarudi waiting room kusubiri majibu. Seat hazikaliki. Watu wanapiga stori kupotezea mawazo, lakini wapi! Anakuja nesi tena, hujui anakuita wewe ukachukue majibu au mwingine akapime! Ni hofu tupu! Mara jina lako linaitwa tena, unapewa ushauri tena. Ushauri unahusu mambo mbalimbali, mengine yanatoa reflection kama vile umeathirika. Unaona ushauri wake ni kama vile unakucheleweshea majibu, unatamani kumnyang'anya kadi ili usome majibu. Mara anakupa majibu, anakuambia ni negative! Unaondoka na amani, ila unasema ngoja nikawaage 'washikaji' niliowaacha waiting room, kwani sasa walau una ujasiri! Ukiingia na tabasamu tu wenyewe wanajua majibu ni safi! Unachukua box mbili tatu za kondomu pale na vipeperushi kibao! Unapita pale mapokezi na kumuaga yule dada! Tabasamu lako linampa picha halisi ya majibu yako! Anakutania kidogo kwamba sasa wahi kazini, ulikuwa na haraka sana! Mnacheka, unaondoka. Usisahau kumuaga mlinzi pale getini, kwani yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kukupokea! Endeleeni .....

Ha ha ha ha ha!! sasa ngoja na mimi nitoe ushuhuda,make nilikuwa nimeweka kwa kifupi sana....,

Siku za hivi karibuni kipenzi cha moyo wangu amekuwa anasisiza sana suala la kupima....nikawa namshangaa tu make kma ni kugegedana tushagegedana sana...kwa wiki nzima sasa nikawa sipati usingizi hasa nikikumbuka sarakasi zangu miaka miwili ya karibuni.....nikioongea na bibie,sentensi ya kwanza,ya pili anasisitiza suala la kupima(japokuwa nilishapima miaka 6 iliyopita,ila kuna mazingira hatarishi nimepitia sana....mpaka nilipoamua kutulia na mpenz mmoja,,mwaka mmoja sasa,

Basi baada ya kuweweseka sana,leo nikaamka zangu asubuhi,nikaikamata bima yangu......straight to the hospital!! nikafika nikaingia kumuona Dr ,Dr akaniuliza unaumwa nini....nikamwambia nataka kupima magonjwa mbalimbali,akaniambia haiwezekani,niseme naumwa nini...Dah...nikaogopa kusema nataka kupima HIV,ikabidi niseme tumbo na kichwa....!! akanishauri nikapime TYPHOID na MALARIA...nilivofika maabara....nikamvuta yule dada pembeni,"Naomba unipime na HIV kabisa" akakataa kata kata.....akaniambia kama unataka kupima HIV nenda kule CTC ...duh.....nikaondoka zangu,nilipofika njiani nikaamua kurudi tena hosp. staright to CTC....huko hali niliyokuwa nayo,ngoja ibaki kuwa siri yangu.........Hatimae Dr kanipa majibu yangu yapo NEGATIVE nakumbuka pale paliandikwa HIV non Reactve na muhuri wa negative.....kwa kuwa nilimdanganya sina mpenzi....akaniambia siku ukipata mpenzi,,mlete hapa kwanza ndo mengine yafuatie...usimwamini mtu harakaharaka......nikaondoka zangu na tabasamu paaaana!!

Sasa hivi nishamwambia mupenz......"Honey,wknd hii lazima tukachek afya zetu....na nimesisitiza sana hadi anashangaa...(sijamwambia kama nimepima) nataka nae akapitie kale ka-situation nilikokuwa nako siku tutakayokwenda kupima...

Noana mungu kanisaidia sana....nimemuahidi kuwa makini katiaka maisha yangu yote yaliyobaki hapa chini ya jua.....
 
Ndg, nilienda kupima Amana hospital, ilikuwa september 9 2009! Ni ishu kubwa sana, kuna jamaa alikuwa anachonga sana tulipokuwa tunasubiria namba tuingie ndani. Ikafika zamu yake alikaa kama dakika 15 wakati wastani ni dak 5 tu nikajua kaumia tu. Alitoka kimyakimya kichwa chini. Hali ni mbaya maana karibu nusu kama sio 40% ya waliokuwa wametangulia kupima walikuwa wameukwaa, nligundua kwa kuangalia column ya status (P or N)! Ila toka siku nikamilishe kupima 3 times aisee naogopa vibaya haya mambo!
 
Ndg, nilienda kupima Amana hospital, ilikuwa september 2009! Ni ishu kubwa sana, kuna jamaa alikuwa anachonga sana tulipokuwa tunasubiria namba tuingie ndani. Ikafika zamu yake alikaa kama dakika 15 wakati wastani ni dak 5 tu nikajua kaumia tu. Alitoka kimyakimya kichwa chini. Hali ni mbaya maana karibu nusu kama sio 40% ya waliokuwa wametangulia kupima walikuwa wameukwaa, nligundua kwa kuangalia column ya status (P or N)! Ila toka siku nikamilishe kupima 3 times aisee naogopa vibaya haya mambo!
 
Ukimwi siku hizi ni kama common cold tu.

Hivyo sioni sababu za kukosa raha kama unao.
 
Nimewahi kupima mara kadhaa pale AMREF barabara ya Ali Hassan Mwinyi, inahitaji ujasiri kwa kweli. Kwanza unapoingia unapishana na watu mbalimbali wenye hali tofauti, wengine wanaingia kama wewe, wengine wanasubiri majibu, wengine wameghairi kupima etc. Siku ya kwanza niliuza, "majibu yanatoka baada ya muda gani?". Nikaambiwa kama nusu saa. Ila yule dada pale mapokezi alijua nina wasiwasi, akasema "kama unahitajika haraka kazini, ni bora ukatafuta siku yenye una nafasi". Nadhani alijua nataka kusepa kabla hata sijapima, ila nilisubiri nikapima. Kule waiting room ndio usiseme, mkanda wa video ya waathirika inaongeza hofu (kama unamjua Phil Lutaaya wa Uganda, alikuwa anawekwa sana ktk video kutoa shuhuda). Anakuja nesi, anakuita jina bandia (tunaandikisha kwa ID kule kama za JF!!), unaenda kupima, unarudi waiting room kusubiri majibu. Seat hazikaliki. Watu wanapiga stori kupotezea mawazo, lakini wapi! Anakuja nesi tena, hujui anakuita wewe ukachukue majibu au mwingine akapime! Ni hofu tupu! Mara jina lako linaitwa tena, unapewa ushauri tena. Ushauri unahusu mambo mbalimbali, mengine yanatoa reflection kama vile umeathirika. Unaona ushauri wake ni kama vile unakucheleweshea majibu, unatamani kumnyang'anya kadi ili usome majibu. Mara anakupa majibu, anakuambia ni negative! Unaondoka na amani, ila unasema ngoja nikawaage 'washikaji' niliowaacha waiting room, kwani sasa walau una ujasiri! Ukiingia na tabasamu tu wenyewe wanajua majibu ni safi! Unachukua box mbili tatu za kondomu pale na vipeperushi kibao! Unapita pale mapokezi na kumuaga yule dada! Tabasamu lako linampa picha halisi ya majibu yako! Anakutania kidogo kwamba sasa wahi kazini, ulikuwa na haraka sana! Mnacheka, unaondoka. Usisahau kumuaga mlinzi pale getini, kwani yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kukupokea! Endeleeni .....

aisee..what a good narration....hii makitu balaa aise
 
Back
Top Bottom