Duuhh!! Kupima UKIMWI sio kitu ya mchezo!!

Duuhh!! Kupima UKIMWI sio kitu ya mchezo!!

Mi nilinote wenye majibu safi hawakai sana ndani kuchukua majibu, ukiona mtu kazama amechukua muda mreefu anapo toka mwangalie usoni elewa huyo tayari kanasa.
 
Nimewahi kupima mara kadhaa pale AMREF barabara ya Ali Hassan Mwinyi, inahitaji ujasiri kwa kweli. Kwanza unapoingia unapishana na watu mbalimbali wenye hali tofauti, wengine wanaingia kama wewe, wengine wanasubiri majibu, wengine wameghairi kupima etc. Siku ya kwanza niliuza, "majibu yanatoka baada ya muda gani?". Nikaambiwa kama nusu saa. Ila yule dada pale mapokezi alijua nina wasiwasi, akasema "kama unahitajika haraka kazini, ni bora ukatafuta siku yenye una nafasi". Nadhani alijua nataka kusepa kabla hata sijapima, ila nilisubiri nikapima. Kule waiting room ndio usiseme, mkanda wa video ya waathirika inaongeza hofu (kama unamjua Phil Lutaaya wa Uganda, alikuwa anawekwa sana ktk video kutoa shuhuda). Anakuja nesi, anakuita jina bandia (tunaandikisha kwa ID kule kama za JF!!), unaenda kupima, unarudi waiting room kusubiri majibu. Seat hazikaliki. Watu wanapiga stori kupotezea mawazo, lakini wapi! Anakuja nesi tena, hujui anakuita wewe ukachukue majibu au mwingine akapime! Ni hofu tupu! Mara jina lako linaitwa tena, unapewa ushauri tena. Ushauri unahusu mambo mbalimbali, mengine yanatoa reflection kama vile umeathirika. Unaona ushauri wake ni kama vile unakucheleweshea majibu, unatamani kumnyang'anya kadi ili usome majibu. Mara anakupa majibu, anakuambia ni negative! Unaondoka na amani, ila unasema ngoja nikawaage 'washikaji' niliowaacha waiting room, kwani sasa walau una ujasiri! Ukiingia na tabasamu tu wenyewe wanajua majibu ni safi! Unachukua box mbili tatu za kondomu pale na vipeperushi kibao! Unapita pale mapokezi na kumuaga yule dada! Tabasamu lako linampa picha halisi ya majibu yako! Anakutania kidogo kwamba sasa wahi kazini, ulikuwa na haraka sana! Mnacheka, unaondoka. Usisahau kumuaga mlinzi pale getini, kwani yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kukupokea! Endeleeni .....

kupima si mchezo.....siku ya kwanza jamaa wa mbele yangu aliingia mitini.... Mie nilivyoitwa kuchukua majibu wacha nitetemeke...jasho likanitoka mwili mzima...... Ushauri wa mwanzo kabla ya kupewa majibu wala sikuusikia.....chezeya kupima wewe
 
Wakuu kama bado uko salama tulieni kabisa.. HIV isikie na kuisoma vitabuni na kwenye runinga,usiombe,utajiharishia ww.
 
Wakuu kama bado uko salama tulieni kabisa.. HIV isikie na kuisoma vitabuni na kwenye runinga,usiombe,utajiharishia ww.

Baada ya kutoka kupima nilijilaumu......vipi kama ningeambiwa nimeathirika.......khaa!!
 
Kupima noumer, ukisubiri majibu utasali sala zote, utaweka na nadhiri, utaweka mikakati ya kutokufanya tena lakini ukishaambiwa tu negative basi baada ya dakika 30 ushasahau.
Sidhani kwamba baada ya vipimo kuwa negative kusema nitakuwa makini ni sahihi, wakati mwingine sio kwa nguvu zetu, nikuomba tu uwezo wa roho mtakatifu atuwezee na tukingwe na janga hili. Wpo waliocheza sana maeneo hatari lakini ni salama, wapo waliokuwa makini lakini wakaja kuuopata kwa namna wasiyoitaraji.

HIV si swala la kufanya utani, ni neema tu ya Mungu kwani tunapita njia nyingi ambazo sio salama. hata ARVs kuzitumia ni moyo wa ziada wajameni, ukiona wanaozitumia mara wamenyonyoka nywele, mara tumbo limekuwa kubwa, mara kicheefu chefu, mara kuharisha kama bomba......kwa kifupi si hali ya kuridhisha.
 
Unaweza ukafia palepale!!

Inaogopesha zaidi baada ya kuona zile movement za waathirika wanaochukua ARV's

Kwa wale waliopima naomba kushea nao experience hapa,mwenzenu nimepata hard time ambayo sijawahi kupata tangu nimezaliwa!!

Anyway...thanks God nipo fresh,ila cha moto nimekiona......na nimeamua kubadilisha mfumo wangu mzima wa maisha!!

Hii mada imekaa nzuri. Wengine tutapata elimu muhimu sana.
 
Kweli ugonjwa huu unatisha usiombe we acha tu. Lkn kwanini hatutaki kubadili tabia je ni tamaa au?! Manake unakuta hata wana ndoa hali ni tete walipooana wote walikua negative na wana watoto kuthibitisha kua walikua negative . Inakuaje sasa baada ya miaka kadhaaa wanaukwaaa na hawajawahi pata ajali wala uguza mgonjwa, uaminifu ktk ndoa muhimu sana. Tubadilike zinaa mbaya sio ajali kazini mpendwa. Ukikuta negative shukuru na ukikutwa positive pia shukuru kwani umewahi bado waweza kuishi lkn tubadili tabia.
 
Mrembo by Nature
Ni kweli arv sometimes zinaleta madhara . Tuna ndugu zetu wengi wamepotez maisha na wengine ni wazazi wetu. cha msingi tubadili tabia, hasa kwa wanandoa inakuaje mnaoana mkiwa salama mara baada ya miaka 10 mnakua waathirika , ndio maana sina huruma na wanaocheat hata kidogo ukigundua mwenzako si mwaminifu na ni beyond reasonable doubt fanya maamuzi magumu.
 
Last edited by a moderator:
Kweli ugonjwa huu unatisha usiombe we acha tu. Lkn kwanini hatutaki kubadili tabia je ni tamaa au?! Manake unakuta hata wana ndoa hali ni tete walipooana wote walikua negative na wana watoto kuthibitisha kua walikua negative . Inakuaje sasa baada ya miaka kadhaaa wanaukwaaa na hawajawahi pata ajali wala uguza mgonjwa, uaminifu ktk ndoa muhimu sana. Tubadilike zinaa mbaya sio ajali kazini mpendwa. Ukikuta negative shukuru na ukikutwa positive pia shukuru kwani umewahi bado waweza kuishi lkn tubadili tabia.
 
Hivi Magic Johnson ni HIV positive kweli au alijitangaza kuonesha dunia ukimwi upo? Mbona mnyamwezi hatetereki and he is more than happy...
 
Lkn nashindwa kuelewa, kuna wengine wanachakarika sana kwenye mchezo wa hatari lkn wanatoka mzimaaaaaa kwenye vipimo, why this?

Vipimo vya Tanzania ni fake hata hao walio ambiwa they are nefative bado nina mashaka nao kuwa hawaja athirika ila basi tu nchi yetu usanii ni mwingi mno, yaani hata katika uokoaji maisha ya mtu tunaweka usanii. Kwa kweli hapa Bongo tunaishi kimungu mungu tu. Usishangae hata na hzo condomu wanazochukua pale hospitali zikawa zimewekwa magonjwa ya hajabu ili watu wazidi kuugua kwa magonjwa ya hajabu.
 
hata mie nasema vipimo ni fake.ukiambia negative usidhani negative kweli na ukiambiwa positive usiamini sana.pima mara kadhaa sehemu tofautitofauti.

Kuna watu ni mastar wa ngono lakini anapima anaambiwa negative wakati alikua anagongwa daily bila kinga.
 
Well said, mtu kama unakutana na demu hapa Bongo, kabla ya ku do naye pima hata mara tatu sehemu tofauti kama ulivyosema ila useme uingie kichwa kichwa haki ya Mungu utakohowa bila kutaka na mabega kupanda juu ghafla. Sijuwi kwa nini tunapenda kuweka maisha ya watu rehani kihivi. Is it because tume give up on life au ni roho mbaya tu ya kutaka kuuana ili tukose wote? Wabongo nijibuni, tatizo ni nini?
 
Baada tu ya kuachwa na demu wangu nikachanganyikiwa kbs. Nikishtuka tu ucku naanza kukumbuka yale tuliyokuwa tukifanya kisha video mbalimbali na picha za waathirika zinanijia. Hapo hkn usingizi tena mpk asubuhi.

Ktk kuweweseka weweseka nikajikuta nipo angaza Mnazi Mmoja. "KARIBU" ni sauti ya dada moja mrembo aliyevaa sare za manesi ilinikaribisha. Nikamueleza kilichonipeleka, nikapewa namba, nikatulia. Kwny foleni nikawa mtu wa 7. Nje kuna bonge la mvua...mvua inaendelea kunyesha, foleni inazidi kusogea, moyo nao unazidi kwenda mbio...hamadi, bado mtu moja na mvua imepungua kidogo, manyunyu kwa mbaliii, nikajiuliza napima ili iwe nini wkt UKIMWI hauna tiba. Daah ckujiuliza mara ya pili...nikatoka spidi. Ckurudi tena
 
Ha ha ha ha ha ha ha ha haah hii post imenichekesha sana mchana huu!!
 
Back
Top Bottom