I'm HIV + naanza safari yangu ya matumaini

Miracle12

Member
Oct 10, 2017
10
59
Hello guys,

First of all,ningependa kumshukuru Mungu kwa yote anayozidi kunitendea in my whole life since i was born. Na nimeamua kuja hapa sababu najiona kamae I'm alone in this word and maybe you guys wakubwa kwa wadogo wazee kwa vijana mtakuwa na lolote la kunishauri.

Natanguliza shukran kwa wote mtaopitia this thread and may God use all of you kunishauri cas nmekua na ndoto nyingi but now is like I'm nothing in this word.
I have a long story to tell but naona itaniumiza cas maisha nlopitia after my father died God knows. Ila now I'm trying to accept who i am now. (some says is true HIV Exists and others says is a hoax) but to me i see it like true maybe nathani wale ambao ni +ve like me wataelewa what am i talking about. Is very hard for me to believe but is like this:-(

Mimi ni kijana now I'm 22 yrs old na mpaka ninapoandika hivi my mother hajui if i have HIV and she still have so many hope on me cas hakubahatika kusoma but alinisomesha tena shule za ghalama tu kwa biashara zake ndogo ndogo na niafanikiwa kumaliza form 6 though nikapata temporally job here in Dar kwenye kampuni moja hivi nikaona let me work first and after getting money nijiendeleze cas my mom ni kama hali imekuwa ngumu kidogo kwake and alifurahi sana na kuniombea Mungu maana nilianza kumsaidia nae hata viela kidogo vya matumizi akiwa na shida I'm the only person anaweza mpigia akiamini tamsaidia and i always do that hata leo nimetoka kuongea nae na yeye anafurahi sana ila hajajua mimi nina huzuni kuu na nilikuwa natoa machozi wakati naongea nae japo sikutaka ajue if nalia ye yuko mkoani so nkifikiria siku atayojua sijui itakuaje. Though I'm planning not to tell her ever.

Niliumwa nikiwa at work ghafla tu kichwa and nikawa sijielewi but nikajua it will be Maralia so i took medicine (panadol) kutuliza mauvivu then badala ya kupata nafuu hali ilikuwa mbaya and it was just in few moment that happened so cas it was late nikaondoka nikaenda kwangu ninapoishi but all i was thinking was just maralia cas i don't use mosquito net.

Then next day nikaenda hospital kubwa tu down town nikapima and the result comes that ni maralia so i went back home nikiwa na dawa nilizopewa hospital but hali ilizidi kuwa mbaya nikawa siwezi hata kusimama jioni and naishi alone so nikamcontact my friend (she is just like my sister to me cas she is all i ahave in Dar) so nikaenda kwake that night but hali ikawa mbaya sana sana.

Kila nikinywa dawa hali inakuwa mbaya mpaka tukahisi maybe dawa walizonipa zina side effects mbaya sana. So next day jion hivi nikarudi hospital na nilipofika nikawaeleza and nikapata vipimo tena then this time doctor akasema mbona huna maralia ila una UTI na typhord.

Nikapewa dozi nikarudi but that night nilipokunywa dawa nilihisi I'm gonna die cas nilizidiwa mara mbili ya mwanzo so next day early in the morning nikarudi hospital and nilikua nakohoa sana sana mwili hauna nguvu so nikalazwa kabisa.

Nikatundikiw dripu nikapew na dawa but next day nikapata nafuu and i was like what happened i asked nesi wa pale hospital hakunijbu ila aliuliza kama nina ndugu Dar and i said no i have friends only na akaniuliza how i live nikamwambia.

She was so sad but nikajua ni nesi so ananionea huruma nnavo umwa. Next day nikawa ok and nikapew bili yangu ambayo ilikuwa kubwa kidogo kama mnavojua private hospitals. But sikujua naumwa nini and ile nataka kuondoka doctor akaniita ofisini kwake. And he asked me so many questions.

But i will never forget that in a simple way he told me now wewe ni muathirika wa VVU. Guys it was a bad moment ever in my life. And mimi nipo naugulia namuona as he is clrzy telling me such thing yeye akaanza kuniambia so inabidi uanze kutumia dawa. Siwezi kuelezea how i was that time but situation hio sitaisahau nililia kama mtoto mdogo but doctor didnt care na akanipeleka kwenye system yao ya watu wa HIV.

Niliona dunia yote imeniangukia nimetoka hapo kila niliemuona barabarani niliona sifanani nae. The question was where did i get this thing? Nkiangalia zile ARV nlizopew nilikuw nalia. Nilipewa pia dozi ya typhoid so nimefka home nikamwambia sister is just typhoid. Hakuweza kuja kunichukua hospital cas ya nature ya kazi yake na mda.

Guys until now sijamueleza mtu this issue but nikaemda 3 different hospitals kupma cas sikuamini but the answer was im HIV +. Nililia na kutaka kuacha hat kwenda kazini but nikajifikiria nikasema ok i will go. Nimeenda job kila niliemuona nilihisi anajua that nimeathirika.

Nilikuwa na hasira za ajabu na nilizima simu wiki nzima na sikuwa nalala usiku vizuri. But nikaanza kutumia dawa zile ARV. Naomba nisiendelee zaidi but sitasahau those days ever in my life. And trust me we have poor doctors in Tz (some not all) cas isingekuwa Mungu ningejiua trust me cas no doctor aliekuwa ananipa ushauri zaidi ya bla bla bla.

Ok back to the topic. Ndugu zangu nilikuwa nimeplan a lot of things but nimekata tamaa kabisa kabisa na najiona sio mtu tena.

Naomba ushauri wenu katika yafuatayo;
(1) nilikuwa nimeplan kwenda USA au Canada kutafta maisha kwa njia ya kusoma kwanza. But some people kwenye mtandao wanasema MTU mwenye HIV hawakubari katika nnchi hizo. Guys is it true? Because if is true I'm going to die soon kwa presha cas ni ndoto nilizokuwa nazo since niko mdogo sana.
Naomba niishie hapa cas i cant write anymore inaniuma sana guys.

Why world is not fare like this? Everyday I'm trying to figure out nimepata wapi huu ugonjwa but i don't get the answer. But all in all if naweza kupona please advise me how hata kama kuna madaktari wanaitaj mtu wamfanyie experiment here i am. Nchi yeyote.

Guys usiombe yakukute please stay safe always na usimcheke alienao cas you never know like i dont know nlikoupata. Nimekua wa kulia everyday I'm like God mbona umeniacha. But i hope tapona guys i hope one day takuwa ushuhuda kwa dunia in Jesus name Amen.

If una ushauri au maoni please unaweza kuja inbox. Sorry for long story but mengine nitaeleza ndani ya thread.

Thank you for reading this.
 
Andiko lako umelichanganya sana limekosa mvuto kabisa kwangu

Hamna kukata tamaa hapo uzuri sasa umeshajua hali uliyo nayo kinachotakiwa ni kuanza kuishi kuzingatia jinsi ulivyoshauriwa na Daktari

Wapo wengi wenye VVU na wanaishi miak mingi sana na wanakuwa na familia(Kuoa/kuolewa), relax mkuu
 
Pole sana ndugu.Unapojiuliza ulipata wapi kwani hujawahi kufanya ngono zembe kabisa?au maybe ulishare vitu vya ncha kali na mtu?Ungezaliwa nao sidhan kama ungefika 22 bila complication zozote.
Pole.Yani kitu kibaya unachoweza kufanya na kufa haraka sana ni KUKATA tamaa.
Chukulia kama umepata ugonjwa mwingine wowote wowote,ni ngumu ila jitahidi uoke nafsi yako mbali na kifo cha sononi.

Ukiwa sawa waeleze watu wako wa karibu unaowaamini.Kula vizuri,furahia maisha.Sali.
Ukilialia miezi sita mingi uta RIP
 
Pole sana na huko peke yako, wanaotumia ARV's hawana mihuri usoni. Mfano tu ukiwasha tv asubuhi wale unaowaona wengine ni miongoni mwao, unapopopanda basi wamo au ofisini mwenu watakuwepo.

Umefanya vizuri kumficha mama yako maana akiyajua anaweza kuathirika kisaikologia kuliko wewe mgonjwa. Ila unywe dawa kila siku kama ulivyoshauriwa.

Hatari iliyopo ni wewe kutaka HIV iondoke mwilini mwako ikiwezekana mara moja kutokana na maandishi yako. Unaweza kukutana na matapeli watakaokupa dawa au maombi na kukuambia kuwa haviendani na ARV's. Hapo ni kukaribisha mauti.

HIV is real wakuu.
 
Hello guys first of all ningependa kumshukuru Mungu kwa yote anayozidi kunitendea in my whole life since i was born. Na nimeamua kuja hapa cas najiona like I'm alone in this word and maybe you guys wakubwa kwa wadogo wazee kwa vijana mtakuwa na lolote la kunishauri. Natanguliza shukran kwa wote mtaopitia this thread and may God use all of you kunishauri cas nmekua na ndoto nyingi but now is like I'm nothing in this word.
I have a long story to tell but naona itaniumiza cas maisha nlopitia after my father died God knows. Ila now I'm trying to accept who i am now. (some says is true HIV Exists and others says is a hoax) but to me i see it like true maybe nathani wale ambao ni +ve like me wataelewa what am i talking about. Is very hard for me to believe but is like this:-(
Mimi ni kijana now I'm 22 yrs old na mpaka nnapoandika hivi my mother hajui if i have HIV And she still have so many hope on me cas hakubahatika kusoma but alinisomesha tena shule za ghalama tu kwa biashara zake ndgo ndogo na niafanikiw kumaliza form 6 though nkapata temporally job here in dar kwenye kampun moja hivi nkaona let me work first and after getting money nijiendeleze cas my mom ni kama hali imekuw ngum kidgo kwake and alifurahi sana na kuniombea Mungu maana nlianza kumsaidia nae hata viela kidogo vya matumizi akiwa na shida I'm the only person anaweza mpigia akiamini tamsaidia and i always do that hata leo nmetoka kuongea nae na yeye anafurahi sana ila hajajua mimi nina huzuni kuu na nilikuwa natoa machozi wakat naongea nae japo sikutaka ajue if nalia ye yuko mkoani so nkifikiria siku atayojua sijui itakuaje. Though I'm planning not to tell her ever.
Niliumwa nkiwa at work ghafla tu kichwa and nkawa sijielew but nkajua it will be Maralia so i took medicine (panadol) kutuliza mauvivu then badala ya kupata nafuu hali ilikuw mbay and it was just in few moment that happened so cas it was late nkaondoka nkaenda kwangu nnapoishi but all i was thinking was just maralia cas i don't use mosquito net. Then next day nkaenda hospital kubwa tu down town nkapima and the result comes that ni maralia so i went back home nkiw na dawa nlizopew hospital but hali ilizid kuw mbaya nkawa siwez hata kusimama jioni and naishi alone so nkamcontact my friend (she is just like my sister to me cas she is all i ahave in Dar) so nkaenda kwake that night but hali ikawa mbaya sana sana. Kila nikinywa dawa hali inakuw mbYa mpaka tukahisi maybe dawa walizonipa zina side effects mbaya sana. So next day jion hivi nikarudi hospital na nilipofika nkawaeleza and nikapata vipimo tena then this time doctor akasema mbona huna maralia ila una UTI na typhord. Nkapewa dozi nkarudi but that night nlipokunywa dawa nlihisi I'm gonna die cas nilizidiwa mala mbili ya mwanzo so next day early in the morning nkarud hospital and nlikua nakohoa sana sana mwili hauna nguvu so nkalazwa kabisa. Nkatundikiw dlip nkapew na dawa but next day nkapat nafuu and i was like what happened i asked nesi wa pale hospital hakunijbu ila aliuliza kam nna ndugu dar and i said no i have friends only na akaniuliza how i live nkamwambia. She was so sad but nkajua ni nesi so ananionea huruma nnavo umwa. Next day nkawa ok and nkapew billi yangu ambay ilikuw kubw kidgo kama mnavojua private hospitals. But sikujua naumwa nn and ile nataka kuondoka doctor akaniita ofisin kwake.... And he asked me so many questions. But i will never forget that in a simple way he told me now wewe ni muathilika wa vvu. Guys it was a bad moment ever in my life. And mimi npo naugulia namuona as he is clazy telling me such thing ye akaanza kunambia so inabidi uanze kutumia dawa. Siwez kuelezea how i was that time but situation hio sitaisahau nililia kama mtoto mdogo.but doctor didnt care na akanipeleka kwenye system yao ya watu wa HIV.
Niliona dunia yote imeniangukia nimetoka hapo kila nliemuona barabarani niliona sifanani nae. The question was where did i get this thing? Nkiangalia zile ARV nlizopew nlikuw nalia. Nilipew pia dozi ya typhoid so nmefka home nkamwambia sister is just typhoid. Hakuwez kuja kunchukua hospital cas ya nature y kazi yake na mda.
Guys until now sijamuelez mtu this issue but nkaemda 3 different hospitals kupma cas sikuamini but the answer was im HIV +. Nililia na kutaka kuacha hat kwenda kazn but nkajifkilia nkasema ok i will go. Nmeenda job kila nliemuona nilihisi anajua that nmeathirika. Nilikuwa na hasira za ajabu na nilizima cm wiki nzima na sikuwa nalaalla ucku vizuri. But nkaanza kutumia dawa zile ARV. Naomba nisiendelee zaidi but sitasahau those days ever in my life. And trust me we have poor doctors in tz (some not all) cas isingekuw Mungu nngejiua trust me cas no doctor aliekuw ananipa ushauri zaidi ya bla bla bla.
Ok back to the topic. Ndugu zangu nilikuwa nimeplani a lot of things but nimekata tamaa kabisa kabisa na najiona sio mtu tena. Naomba ushauri wenu katika yafuatayo.
(1) nilikuwa nimeplan kwenda USA au Canada kutafta maisha kwa njia ya kusoma kwanza. But some people kwenye mtandao wanasema MTU mwenye HIV hawakubari katika nnchi hizo. Guys is it true? Because if is true I'm going to die soon kwa presha cas ni ndoto nilizokuwa nazo since niko mdogo sana.
Naomba niishie hapa cas i cant write anymore inaniuma sana guys. Why world is not fare like this? Everyday I'm trying to figure out nmepata wapi huu ugonjwa but i don't get the answer. But all in all if nawez kupona please advise me how hata kama kuna madaktar wanaitaj mtu wamfanyie experiment here i am. Nnchi yyte.
Guys usiombe yakukute please stay safe always na usimcheke alienao cas you never know like i dont know nlikoupata. Nmekua wa kulia everyday I'm like God mbona umeniacha. But i hope tapona guys i hope one day takuwa ushuhuda kwa dunia in Jesus name Amen.
If una ushauri au maoni please unawez kuja inbox. Sorry for long story but mengne taeleza ndani ya thread.
Thank you for reading this.
Daaa speechless... I can imagine....nakumbuka Siku nilipewa taarifa ndugu yangu wa karibu Sana yupo kwenye hiyo hali nilihisi dunia mzima unazungukia Kichwani kwangu... Nakumbuka nililia Sana... Namshukuru yy mwenyewe alikuwa aameshaikubali hiyo hali.... Walikuwa wanasubiri nimalize shule ndio niambiwe... Thank God we are very happy... Na familia nzima tumechukulia ni hali ya kawaida... huiwezi hata kujua... hanapambana na maisha kama wengine na pia ana ndoto zake kubwa tuu.... In fact tunamshukuru mungu kwa kweli.... kinachowaumiza wengi ni kunyanyapaliwa... Sisi kwetu haipo hiyo...
...so what I can advice u tafuta unayemwamini mweleze hali yako ambaye atakutia moyo katika safari yako....pekeyako u will be crazy coz i can tell u sio rahisi...maisha lazima yaendelee....u need to take good care of urself...badilisha mfumo wa maisha...HIV sio cancer coz huu mwingine unatisha zaidi...u can live many years kama watu wengine...u can have ur dreams ,family anything ....u can be anyone ....but u need to accept ur situation and learn how to live with it....may God gives u the strength u need in Jesus name..
 
Pole sana ila usikate tamaa na maisha kabisa wala kuhuzunika kupita kiasi. Huu ugonjwa unatisha sana lakini siku hizi wengi wa waathirika wanaishi kwa miaka mingi tu ili mradi wanafuata masharti ya madaktari ikiwemo kunywa dawa, kula vizuri, kuendelea na shughuli zako za kila siku na pia kujaribu kuacha kuwaza sana hali uliyonayo. Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu na pia uache kusononeka na kulia kila wakati.
 
Hiyo kawaida sana kwa sasa Nina MTU Wa karibu ana miaka 18 toka Mume wake aondoke na hiyo ikiwa imechangia huna haja ya kuogopa kitu .

Kubali hiyo hali tumia dawa ulizopewa na Maelezo ya Dr.
Hiyo ni rahisi kutuliza akili yako acha kuiwazia kama wewe ndio pekee unayeugua wako wengi usifikirie sana mambo yataenda vizuri tu
 
Pole sana, hofu yako ni kifo, but unajua ever since umejijua umeathirika ni wangapi wasioathirika wamekufa? Siajabu hata muda huu unasoma hii kuna watu wanavuja damu barabarani humo! Kikubwa ni Dawa, Msosi, Focus ya maisha! Hata humu JF wapo wengi tu.. Then Tulia usitafute maambukizi mapya utaumia..
 
Pole braza. Pamoja watu wanakubeza ulichoandika hapa kwamba hakieleweki lakni,mimi naona upo kwenye wakati mgumu sana.Pia niseme,nimejifunza kitu kutoka kwako mkuu.
Kwanza nashukuru kwa kuja mbelena kusema kuwa unaugua.Maana yake umekubali hali kimtindo lakni bado hujakubalia nalo kutokana na mengi uliyonayo ambayo unataka kufanikisha.
Pia,swala la kumwambia mama nakushauri usimwambie kwanza mpaka utakapopata confindence na uwezo wa kumwambia.
Mwishon usiangalie umepata wapi.Ikiwezekana achana na ngono chafu kabisa maana ukisema uendelee ndio utazidi kuumwa na kuharibu maisha yako na wengine.
Tafuta taasisi wanazotoa ushauri nasaha upate moyo.
Sikushauri umwambie mth yoyote kwanza. Wewe ni mwanaume utafanikiwa tu.
Pole sana brother
 
endelea na maisha kama kawaida kuwa busy km ulivyokuwa mwanzo usifikirie sana kuhusu watu wengine usiache kutumia dawa nadhani baada ya muda utakuwa km watu wengine tu.
 
Pole sana. Fuata masharti na endelea kufanya kazi ndoto zako. Watu wanapata vvu na kuishi muda mrefu sana tu. Ambacho sijui ni kuhusu hizo nchi ulizotaka kwenda kuhassle kama wanapokea watu kwenye vvu. Hata hivyo you can always adjust your ambitions
 
Uwepo wako hai adi muda umeandika huu ujumbe apa, Uwezo wa kumbukumbu ulionao juu ya hali ilipoanza adi apa, Uwezo wako wa kuandika kwa ufasaha tena kwa lugha mchanganyiko ni ishara kwamba bado upo vizur kama mtu yeyote timamu
Hii manaake bado unaweza fanya vitu vyako zaidi na kwa ufasaha mkubwa, Hali unayopitia sasa amini ni changamoto na ni si ndogo inahitaji msaada wa karibu sana toka kwa Mungu
Jipe moyo mkuu amini wakat wa kua na mateso ya nafsi utapita nawe utakua saw .
Ila jumla ya yote nikupe pole mkuu Mungu wako alikuleta duniani akupe nguvu thabiti ili ushinde
Pia nikupe hongera kupata nafasi ya kupima na kujua hali yako kwani wengi hatupimi kisa hofu ila umethubutu na umejua khali yako hio ni sehemu ya ushindi
Songa mbele tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom