Kizigenza_
Senior Member
- Apr 20, 2026
- 144
- 0
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewaomba viongozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kuongeza msaada wa kifedha na kijeshi kwa Ukraine katika miaka ijayo, akisema nchi yake inahitaji angalau euro bilioni 70 zaidi kwa ajili ya ulinzi, silaha na kuimarisha ustahimilivu wake huku vita dhidi ya Urusi vikiendelea.
Akizungumza Ijumaa katika mkutano wa kilele wa viongozi wa EU mjini Brussels, Zelensky amesema gharama za vita kwa mwaka ujao zinakadiriwa kufikia euro bilioni 155.
"Vita vitagharimu euro bilioni 155 mwaka ujao, na tunahitaji angalau euro bilioni 70 zaidi kutoka kwenu kwa ajili ya ulinzi, silaha na ustahimilivu wetu, Hiki ni kiwango halisi. Ninawasihi mpate msaada huo." amesema Zelenskyy.
Ombi hilo limewasilishwa huku viongozi wa EU wakijadili namna ya kuendelea kuisaidia Ukraine kijeshi na kifedha pamoja na kuimarisha usalama wa bara la Ulaya