Duru Za Siasa: U.S Chini ya Donald J. Trump


Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
Wanajamvi

Uchaguzi wa US umekamilika jana baada ya D.J Trump kuwa Rais wa 45
Leo ilikuwa siku ya kwanza kamili ya Trump kama Rais wa US

Uzi utakuwa utaangalia serikali mpya na mwelekeo wa siasa na uchumi
Siasa za Marekani , taifa lenye nguvu katika uso wa dunia zinaathari kubwa duniani

Ni kwa kuzingatia hilo, uzi utaleta kwa kadri, yanayojiri katika Taifa hilo

Tutaendelea kumalizia hotuba ya Trump baada ya kutawazwa katika uzi huu
Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Rais Trump, mfanyabiashara aliyefanikiwa katika biashara ameondoka katika utawala wa makampuni na sasa ni mtawala wa umma na Taifa la Marekani

Kuchaguliwa kwake kama mtawala wa juu wa Taifa lenye ushawishi umekuja na mshtuko kutokana na nafasi aliyopewa katika uchaguzi wa ndani ya chama cha Republican na ule mkuu

Kuna mitazamo tofauti kuhusu kuchaguliwa kwa Trump. Kwasababu zozote ambazo wachunguzi wanaendelea kuzifuatilia kisiasa , uchumi, jamii n.k. Trump ndiye Rais wa Marekani

Siku ya kwanza, Trump amekumbana na changamoto za utawala wa nchi na si kampuni binafsi

Katika historia ya miongo michache ya Marais wa US, siku ya kwanza haikuwa nzuri kwake

1. Maandamano ya wanawake duniani
2. Ziara iliyozua utata katika Intelligence community (IC)

Tutajadili mambo hayo mawili na picha ya haraka ya nini kitarajiwe kwa siku za usoni

Tusemezane
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
KUTHIBITISHWA KWA KAVANAUGH

Kura zinahesabiwa na hakuna mabadiliko licha ya maandamano na kupingwa kuthibitishwa kwake
Wakati wote wapingaji walikuwa wakipiga kelele uingilia hotuba na kutolewa nje

Jaji Kavanaugh anathibitishwa kuwa Associate justice of SC-US kama ilivyotarajiwa

VP Pence amemthibitisha Kavanaugh kwa kura 50 kwa 48
Mwendelezo

Jaji Kavanaugh kaapishwa na Jaji mkuu katika seherehe ndogo iliyofanyika SC huku waandamaji wakipiga kelele katika kuonyesha hisia zao za kutokubaliana na kutibitishwa kwake
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
KAVANA JAJI WA SC ALIYEBEBA 'MIZIGO' NYUMA YAKE

Baada ya kuthibitishwa/ kuapishwa Jaji Kavanaugh anaingia SC-US akiwa ni conservative wa 5
Maamuzi mengi yatabeba itikadi yake pamoja na wenzake 4 waliopo sasa

Hii ina maana moja 'tipping the scale in favor of conservatives and Republicans''.

Majaji Liberal ni wanne hivyo maamuzi yatakayohusu masuala kama ;
RoeV Wade, same sex marriage, Immigration, abortion n.k. yatapata mtazamo wa conservative

Kikiwa ni chombo cha juu cha sheria,mengi kwa miongo mingi ijayo yataegemea katika kura 5-4 yakiegemea bawa la kulia la wahafidhina. Kwa Waliberali hili ni pigo kubwa kwa miaka mingi

RAIS TRUMP ATOA KAULI

Akihojiwa ndani ya ndege safarini kuelekea Kansas katika mkutano jioni hii, Rais Trump amesema ana uhakika asilimia 100 kwamba aliyemtenda Dr Ford si Jaji Kavanaugh

Kauli hii ni tofauti na siku za mwanzo aliposisitiza utangamano wa suala zima kisheria
Ni kauli itakyorudi kumwandama siku zijazo kwa uzuri au kwa ubaya. Itarudi kwa nguvu

JAJI KAVANAUGH AENDA SC NA MIZIGO

Tulisema kauli ya Kavanaugh wakati wa mahojiano haikuwa ina matatizo mbeleni.

Wanasheria na maprofesa 1200 wameeleza kutoridhishwa na jinsi alivyoyakabili mahojiano
Kilichowasumbua ni temper akimjibu senata Klobuchar(D) na kauli kuhusu Dems na Clinton

Jaji mstaafu wa SC John Paul Stevens naye alijitokeza akisema msimamo wake umebadilika kufuatia namna Kavanaugh alivyojieleza akisema ni chini ya kiwango cha Jaji wa SC

Tayari media na makundi ya jamii yanahoji uwezo wake katika maamuzi ya kesi
Kauli yake ya kushambulia Democrats, Clintons na Leftists ilionyesha upendeleo wa kisiasa

Inajulikana kuna hisia za siasa kwa kila mtu na mitazamo tofauti, hata hivyo akiwa anaelekea SC kuweka misimamo yake wazi kuliwakwaza wengi waliomtaka aombe radhi, alifanya hivyo

Hilo halikubadili kura ingawa lilielezwa na seneta Murkowisk, hata hivyo linamfuata huko aliko
Endapo Susan Collins angepiga kura ya hapana, Kavanaugh angejihukumu kwa kauli hiyo

Swali linaloulizwa, kwa hasira zake dhidi ya 'wapinzani wake' kisiasa democrats , Jaji ataweza kutoa maamuzi yasiyotiliwa shaka? Jaji atawezaje kufuta kauli zake ili kurejesha imani ya SC?

Kwa tuhuma zinazomkabili, Jaji atawezaje kutoa maamuzi yanayohusu wanawake?

Kwa kawaida majaji hujitoa katika kesi wanazoona zina mwingiliano wa masilahi 'conflict of interest' au ambazo wana masilahi nazo.

Katika SC hakuna mwongozo unaomtaka Jaji ajitoe 'recuse' katika kesi zenye masilahi

Ikifika hapo, nini itakuwa imani ya SC katika jicho la Jaji Kavanaugh mbele ya Umma?

Maamuzi ya kisheria yatalazimisha SC iyaangalie kwa Jicho la Jaji Kavanaugh.

Miongoni mwa watu walio katika wakati mgumu kifikira ni Chief justice John Roberts

Jaji Kavanaugh ameweka mzigo mzito kwa kuzingatia uhuru wa mahakama na heshima yake

J.Roberts atabeba mzigo aliokuja nao Kavanugh ili kulinda heshima ya mahakama, na huyu ndiye wengi wanamuona kama 'swing vote' katika kulinda heshima ya SC

Tusemezane
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
SENATOR FLAKE, MURKOWISK, MANCHIN NA COLLINS
KURA ZA TURUFU NA KARATA

Baada ya sakata la Kavanaugh kumalizika ipo namna maseneta waliokuwa na kura ya turufu walivyozicheza karata zao. Halikuwa suala la FBI bali kuchanga karata kwa chaguzi

1. Seneta Flake (R-Ar)
Ni mmoja wa maseneta wasiopendwa na Rais Trump. Jeff hajasita kumkemea Rais Trump
Mrengo wa kulia alt-right wametengeneza mkakati kuhakikisha harudi katika seneti
Jeff Flake kaamua kustaafu kutokana na hali ya uchaguzi ambayo kwake haikuwa sawa
Katika wiki hii seneta Flake ameibuka shujaa wa GOP na Rais Trump kuhusu Kavanaugh

Rais Trump na senate judiciary GOP walikataa kata kata kushirikisha FBI wakilazimisha kura
Ni pale Jeff Flake aliposimamishwa na akina mama wakimtaka aeleze kwanini ampigie kura Kav
Ili kujinasua Flake aliyekuwa tayari kupiga kura ya ndiyo katika kamati alilazimisha kuitwa FBI

GOP na Trump hawakuwa na ujanja kwani kura yake ya hapana ingehitimisha safari ya Jaji Kav

Hili lilitoa mwanya kwa senate GOP kutumia FBI kwa ushirikiano na WH katika njia za mkato
Mwisho, Flake alipiga kura ya ndiyo kama alivyodhamiria kabla ya kukutana na akina mama.

Flake alikuwa na nafasi nzuri ya 'kumwadhibu' Trump akijua harudi katika seneti.
Hakufanya hivyo. Sababu kubwa ni moja, Flake anatarajiwa kuwa mgombea wa Republicans tena akisemwa ku challenge Trump 2020.

Iwe mwaka huo au mwingine, Flake hakutaka kuchukua 'risk' ya kuudhi conservatives na Republicans, ndiyo sababu ya kura ya ndiyo katika kamati na seneti

2. Seneta Lisa Murkowisk(R-AK)
Lisa anatoka Alaska kwenye indigenous. Matendo ya ubakaji yameathiri jamii hiyo
Lisa alipata pressure kutoka nyumbani anakoungwa mkono na wanawake

Kura ya Lisa ililenga kutoudhi akina mama wanaokereka na wabakaji.
Katika kamati alipiga kura ya hapana kumkataa Jaji Kavanaugh na hatma ya Kav ukingoni

Murkowisk alitumaini yeye na sens Collins wangeweza kuzuia kuthibitishwa kwa Kav
Kwa njia hiyo angekuwa na kinga ya mama mwenzake na wangeungwa mkono na wanawake

Hoja yake ilijikita katiba tabia mbaya ya Kavanaugh akisema mihemuko yake haifai SCOTUS
Lisa alikwepa kusema uchunguzi wa FBI haukuridhisha ili kutoudhi GOP na wahafidhina

3. Susan Collins (R- Maine)
Alikuwa na turufu iliyomuokoa Kavanaugh, ni shujaa wa GOP na Trump
Kama Lisa, Susan hayupo katika midterm, wote wawili wakiwa senior senators na watetezi wakubwa wa RoeV Wade. Alitegemewa kupiga kura ya hapana akabeba turufu ya ndiyo

Kwa siku mbili, Susan ameudhi watu jimboni na kwingine. Inasemwa, hatagombea useneta tena.

Kitendo cha kupiga kura ya ndiyo ni kutaka kuungwa mkono na conservatives na kupunguza ushindani wa ndani siku za mbeleni, hesabu zinaoonekana kumrudi endapo atagombea tena.

Susan kabeba timbwili la Kavanaugh na kumwacha Mitch McConnell huru

4. Joe Manchi (D-WV)
Ni Dems ndani a ngome ya GOP. Yupo katika midterm akikabiliwa na ushindani mkali.
Manchin si mara ya kwanza kwenda kinyume na Dems, siku za Obama aliwahi kutokubaliana

Manchin amefungwa mikono na watu wa jimbo lake wanaomtaka lakini wakiwa GOP. Analazimika kwenda na wapiga kura wake

Kura ya Kavanaugh ilikuwa ngumu sana kwake. Alijificha katika mgongo wa Flake, Murkowisk na Collins. Ilipobainika Flake na Collins watapiga ndiyo, ilikuwa wazi angekataa kura zingefungana na VP Pence angekuwa na kura ya turufu(break the tie).

Hivyo, Manchin aliona hakuna ulazima wa kusema hapana kwani isingebadili matokeo, lakini kusema ndiyo kungemfunika(cover)

Kura ya Flake ina hesabu za siku za mbele, na kura hiyo ndiyo imemuokoa Manchin kwani Collins alipopiga ndiyo hakukuwa na kikwazo tena.

Hiyo ndiyo sababu kubwa kura ya Susan Collins kuwa ya turufu. Iliwafungua Manchin na Flake na kuziba mianya ya lawama

Miongoni mwa wote, seneta aliyekuwa na kura iliyofungua milango mingi kwa wenzake, GOP, WH na Kavanaugh ni Seneta Jeff Flake. Kitendo cha kusimamishwa na akina mama na jinsi alivyojibu na alivyokataa kupigwa kura hadi FBI kilitoa mweleko mpya kabisa.

Tusemezane
 
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Messages
81,995
Likes
49,147
Points
280
Age
28
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined May 15, 2006
81,995 49,147 280
Democrats clearly overplayed their hand during the Kavanaugh confirmation process.

Even more worse, they enlisted the help of that creepy porn lawyer, Michael Avenatti, who actually lived up to his billing with that Swetnick allegation.

And supposedly he is mulling a presidential run of his own in 2020, as a Democrat.

I say run Michael run....hahahahaaa.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
CHAGUZI KATIKATI YA MUHULA
JITIHADA ZA KMBAKIZIA KESI MUELLER

Tarehe 6 kutakuwa na uchaguzi wa magavana, wawakilishi na maseneta (midterm elections)

Utaratibu wanaotumia US ni mzuri unaohakikisha wawakilishi wanakuwa upande wa wananchi. Kila muhula unakuwa na chaguzi mbili za mabunge , senate na house

Kuna mitazamo tofauti kuhusu uchaguzi wa mwaka huu. Wapo wanaosema GOP watapoteza house na senate. Upo mtazamo wa GOP kubaki na senate na kupoteza house

Chochote kati ya hivyo hakitakuwa kizuri kwa utawala wa Trump. Itakuwa kama Obama alipopoteza midterm ambapo Republicans walikuwa kikwazo cha utekelezaji wa sera zake

Kwa Rais Trump hali ni tofati zaidi. Kwa muda ametumia kamati za senate na house kwa suala la Russia. Inakumbukwa taarifa ya house 'iliyomsafisha' kiaina

Ni kwa mantiki hiyo, Rais Trump ameingia katika kampeni si kunusuru GOP bali klinda masilahi yake mapana hasa uchunguzi unaoendelea ambao haijulikani kwanini anaonekana kuuhofia

Democrats wanasema kutakuwa na 'blue wave' kwa maana ushindi wa kishindo.
Well, pengine hawajasoma ya 2016. Kwa wale waliokuwa jamvini, tulieleza mikakati ya Trump

Trump ana ''Political base'' tiifu sana, hata kama angefanya jambo baya haiwezi kumwacha

Ni base yenye nguvu kwasababu hujitokeza kupiga kura na hupatikana vijijini.
Ni base ya watu wasio na elimu kwa maelezo ya Kimarekani ambayo Trump ni ''masiah''

Trump anajua nini aeleze kwa 'base' yake ili kuipa hamasa. Hicho ndicho anachokifanya sasa

Kwanza, anaaminisha kuwa vyombo vya habari vinamwandama hata pale anaposema mwenyewe. Lengo ni kuhakikisha base yake inamsikiliza yeye na si vyombo vya habari

Pili, kuhakikisha anaipa habari inayotaka kusikia. Trump ni mzuri sana wa kutisha au kupamba

Mathalani, tax cut aliyoifanya haikuwa na matokeo mzuri kwa wapiga kura, sasa ameahidi nyingine kwa middle class akisema itatokea November wakati ambapo congress haifanyi kazi
Base yake haijali kama ni kweli au la, muhimu ni kuwa kaeleza Trump ni kweli

Tatu, anaaminisha msafara wa watu kutoka Latin America (caravan) unakuja kuchukua kazi na ajira za Wamarekani hata pale ambapo takwimu zinaonyesha kuna ajira milioni 7 zisizo na watu, na kwamba kazi wanazofanya Walatino Wamarekani hawazitaki

Trump mwenyewe akiwa mfanyabiashara aliajiri wageni ambao leo anasema ni hatari
Base ya Trump inaamini hivyo, tena akiwatisha Caravan ina magaidi wa middle east bila shahidi

Swali ni je, maarifa anayofanya Trump yanalipa na yana matokeo mazuri?

Inaendelea.....
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
Sehemu ya II

Rais Trump anaelewa mijini kwenye wasomi ni ngumu sana kushawishi. Hivyo, anaonekana 'kuwatosa' wawakilishi wa maeneo ya mijini kutokana na kutokuwa na kura za uhakika

Matatizo yake na akina mama hasa wa mijini na kupoteza ushawishi kwa 'independents' vinamfanya abaki na chaguo moja, la kupigania magavana na maseneta

Kwa ramani ilivyo, maseneta wa GOP wana nafasi nzuri sana kuliko wawakilishi.
Kuna uwezekano wa kuongeza maseneta 3, huko ndiko amelekeza nguvu kuliko House

Trump anaelewa 'kuishika' senate kutazuia hatua zozote zenye lengo la kumuanguasha
Kauli za impeachment zinamtia hofu hivyo kuliko kupoteza meli na mzigo heri kpoteza kimoja
Kwamba, seneti itakuwa kinga dhidi ya House

Maarifa anayotumia ya kuzua kauli za uongo, kutisha na hata kupoteza mwelekeo wa mazungumzo zinamsaidia sana kuamsha hisia za wapiga kura wake na kubadili mzungumzo

Wengi wanaona maarifa hayo kama kuishiwa, ukweli ni kuwa ameyatumia kuwamaliza Republicans 16 ambao leo wengi wao wamegeuka kuwa maswahiba kama Ted na Lindsey

Hivyo kwa kuangalia uchaguzi wa Jumanne, Trump anacheza na base yake ambayo ni tiifu sana
Wakati huo huo anacheza na magavana katika kufanya ''voters suppression''
Anacheza na kupoteza watu kutoka katika real issues na kumfuata kule anakotaka waelekee

Tutaendelea kujadili kwa siku kadhaa hadi Jumanne

MUELLER
Kuna taarifa za kundi la 'nationalist' ambalo hujificha kwa jina la conservative kutaka kutumia wanawake kumbambikizia kesi mchunguzi Mueller. Lengo ni kumtia Mueller katika kashfa ili shinikizo la kujitoa liwekwe na uchunguzi uzimwe

Mueller amelitambua hilo na kutoa taarifa kwa FBI.

Hayo yakiendelea, Steve Banon, mshauri wa Trump aliyeondolewa ameitwa mara kadhaa katika kamati ya Mueller. Inaelezwa kuna mahusiano ya mahojiano ya Mueller, Steve na Roger Stone

Roger Stone anatuhumiwa kuwa 'kiungo' kati ya Wikileaks , kutolewa kwa emails za Dem na kampeni ya Trump. Haieleweki nini kinaendelea ndani ya uchunguzi wa Mueller

Tusemezane
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
MATOKEO YA MIDTERM US

SENETI NI YA REPUBLICANS
HOUSE NI YA DEMOCRATS
MAGAVANA BADO KURA ZINAENDELEA KUHESABIWA

Republicans watatawala seneti ya Marekani hadi uchaguzi mkuu ujao. Kuelekea uchaguzi ilikuwa wazi GOP watashinda seneti kwasababu baadhi ya maseneta wa Democrats walikuwa katika 'Trump land' kwa maana maeneo ambayo Rais Trump alishinda na ni red state (Republican)

GOP walikuwa na advantage nyingine , kwamba, Rais wa seneti ni Vice president ambaye kama kura zinafungana ana uwezo wa kupiga kura ya kuamua

Hivyo, kwa matokeo yaliyopo si kwamba democrats watabaki na namba waliyokuwa nayo (49) bali wanataraji kupoteza maseneta 2 au 3 zaidi.
Kwa mantiki hiyo Republicans watakuwa na zaidi ya 51

Hii ina maana kubwa sana kwasababu katika hali iliyopo margin ilikuwa maseneta 1 au 2.
Ndiyo maana suala la jaji Kavanaugh liliamuliwa na Susan Collins.

Kwa Republicans Susan Collins na Lisa Markowirsik walikuwa na kura ya kuyumba (swing vote) na kufanya kazi ya seneti GOP kuwa ngumu.

Kwa namba inayotarajiwa ya kati ya maseneta 52 au 53(matokeo ya mwisho bado)
itakuwa rahisi kwa seneti kupitisha masuala ndani ya seneti

Umuhimu wa seneti ukiachilia ule wa jukumu la jumla la miswada kwa kushirikiana na house, ni kuthibitisha wateuliwa wa Rais kwa nafasi mbali mbali.

Hivyo Rais Trump atakuwa na urais sana wa kuteua iwe majaji au cabinet member kwasababu ya uhakika wa kura 51 ndani ya seneti

Vile vile kwa miswaada kutoka House of rep lazima ipate baraka za seneti.
Hadi sasa ni wazi house itatawaliwa na Democrats.

Kazi ya utawala itakuwa ni nzito, mabunge mawili kuwa ya vyama viwili dems na GOP

Kwa Rais Trump, hili lilikuwa wazi kwamba atapoteza House hivyo nguvu kubwa akaelekeza kwenye seneti na inalipa. Hata hivyo, kuna magavana na House of reps
House itakuwa mwiba kwa Trump

Inaendelea......
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
DEMOCRATS

Imetangazwa House of representative itaongozwa na majority Dems
Tofauti na seneti , house inatokana na wabunge wa maeneo ndani ya state

Kura za maseneti zinatoka kuanzia vijijini hadi mijini.
Tofauti hiyo imewezesha Republicans kushinda seneti wafuasi wa Trump wapo vijijini.

Kwa upande wa House, mijini Trump amepoteza ushawishi si kwa Republicans tu bali independents. Uchaguzi mkuu wa 2016 '' independents '' walimsaidia Trump kushinda

Uchaguzi wa midterm kapoteza kutokana na wanawake, vijana , wasomi na watu wa rangi

Hili linaonekana katika house kwasababu GOP imepoteza wabunge wengi sana hata maeneo walioshinda ugavana au seneti. Impacts ya kauli za Trump imeumiza house reps wengi sana

Kupoteza House si habari njema kwa Rais Trump. House kupitia kamati zake zilizokuwa zinaongozwa na GOP sasa zitakuwa chini ya Democrats.
Kamati zitakuwa na nguvu ya kuitisha 'subpoena' chochote kutoka katika serikali

Si kwamba Rais Trump hakupenda kukampeni kwa House members, ni kutokana na ukweli kuwa alielewa kuna maeneo 'hostile' kwake kutokana na mazonge zonge ndani ya miaka 2 ya utawala

Trump anafahamu base yake ipo vijijini na huko alielekeza nguvu na amesaidia kushinda seneti. Kwavyovyote iwavyo hali haitakuwa kama ilivyokuwa wakati Spika akiwa Paul Ryan

MAGAVANA
Uchaguzi huu umehusisha magavana takribani 36. Kuna watakaojiuliza kwanini magavana?
Magavana wa state wana Mabunge yao na sheria za state zao. Kisiasa wana impact kubwa sana

''Gerrymandering'' (kugawa) maeneo ya chaguzi kwa mtazamo fulani hufanywa na magavana
Lakini si kila gavana ni muhimu, magavana wa state kubwa ni muhimu sana hasa zenye''electoral college' kubwa kama Florida, Ohio na ''Iowa' .

Iowa haina wajumbe wengi wa college lakini uchaguzi awali ndani ya vyama (primary) huanzia. Ni utamaduni tu, wengi wanasema ukishinda Iowa, uwezekano wa kuwa Rais ni 75%

Kwasasa Florida inakwenda kwa gavana wa Republicans.
Florida ina wajumbe 28 wa electoral college, hivyo gavana atasaidia sana.

Ndivyo ilivyo kwa Ohio yenye wajumbe 29 iliyokwenda kwa Dems na Iowa yenye wajumbe 9 imekwenda Dems

Inaendelea...
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
ATTORNEY GENERAL JEFF SESSIONS ATIMULIWA KAZI
NI BAADA YA MIDTERM ELECTIONS

MPANGO WA KUMTUNGUA MUELLER UPO MBIONI

Jana tuiongelea matokeo ya uchaguzi wa katikati ya term ambapo matokeo ya mwisho ya baadhi ya maeneo hayakamilika. Inatosha kusema Dems watamiliki House, GOP watamiliki senate

Uchaguzi haukuwa na matokeo mazuri kwa Rais Trump kwa kupoteza House na hivyo Dems kuwa na nguvu katika kamati zinazosimamia mambo ya serikali na nchi

Rais Trump alifahamu ramani,kauli na matendo yasingewezesha Republicans kumiliki House

Spika Paul Ryan alitangaza kutogembea huku wabunge zaidi ya 30 wakitangaza kustaafu
Haya hayakutokea kwa bahati, ni kwa ukweli kuwa wasingeweza kurudi katika House, wakajitoa

Rais Trump alifahamu maseneta wa Democrats walio katika state ambazo ni Republicans ni 'vulnerable' kwamba, angeweza kusaidia kwa kutumia base yake kuongeza au kuzuia kupoteza

Nguvu nyingi akazielekeza huko. Ingawa haijulikani ni maseneta wangapi kutokana na kuchelewa matokeo, ni wazi ndani ya Seneti , GOP itamiliki

Hilo linafanya kazi yake ya uteuzi na kupitishwa wateule kuwa rahisi, GOP ni majority bila msaada wa maseneta wa Dems au wa GOP wasiokubaliana naye bado atakuwa na majority

Habari za kupoteza house hazikuwa nzuri kwani lawama zimeanza kutoka Republicans kuelekea kwake. Katika kubadili mwelekeo wa mazungumzo 'news circle' leo amemfukuza AG Sessions

Hili lilikuwa wazi ingawa limetokea mapema kuliko ilivyotarajiwa ili kuzima mazungumzo yanayohusiana na chaguzi. Jeff Sessions, AG, amelazimishwa kujiuzulu

Rais Trump kamteua Mathew Whitaker aliyekuwa chief of staff kuwa Acting AG.

Deputy Roseinstein ambaye kiprotokali angekaimu amewekwa kando.
Rosenstein ndiye anasimamia uchunguzi wa Russia kama Boss wa Robert Mueller

Whitaker ni loyalist kwa Trump kutokana na kauli zake za kumtuhumu Mueller.
Uteuzi kama tulivyosema ulilenga kumweka mtu 'loyal' ili sasa aangalie uchunguzi wa Mueller

Hii ina maana uchunguzi wa Mueller kuhusu Russia utahamishiwa kwa usimamizi wa Whitaker

Mandate ya Whitaker inaweza kuzuia uchunguzi, kuua uchunguzi au kuzuia taarifa isitolewa kwa umma. Katika hali iliyopo, itachukua mwezi January kupata AG, senate itakuwa na majority GOP

Nini kinafuata?

Itaendelea....
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
9,976
Likes
8,299
Points
280
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
9,976 8,299 280
RAIS DONALD TRUMP ALIAMSHA DUDE, AMELIKOROGA NA SASA AKAE TAYARI KULINYWA!

Katika miaka miwili aliyokaa madarakani baada ya kushinda uchaguzi uliogubikwa na vituko ambavyo havikuwahi kutokea wala kushuhudiwa nchini Marekani, Rais Donald Trump wa Marekani;
  • Kasema uongo na kuzua mambo yasiyo na ukweli wowote
  • Katukana sana wenzake na wapinzani aliopambana nao .
  • Kashambulia vyombo vya habari na kuvituhumu kwa uongo
  • Kafanya jitihada za kuiteka mihimili yote ya dola...Bunge na Mahakama
  • Kawagawa Wamarekani katika misingi ya kirangi, kijinsia, kidini na kihali
  • Kawashambulia marafiki wa Marekani na kuwaacha wakikuna vichwa
  • Kashirikiana na maadui wa Marekani kuimarisha utawala wake...ni orodha ndefu
Lakini Rais Donald Trump akasahau kuzingatia mambo ya msingi ambayo yameifanya Mamarekani kuwa taifa tofauti na mataifa mengine duniani. Ni misingi iliyoifanya Marekani kuwa kimbilio la wote walioelemewa na matatizo; yawe ya kiusalama, kisiasa, kiuchumi, kielimu, kisayansi, kiafya, kiutamaduni na kibaguzi.

Kwa miaka miwili Wamarekani wamemtazama, wamemsoma, wamemshangaa, wamelalamikia chini chini, wamemvumilia...na sasa wanasema imetosha. Alianza kwa kuwatukana wahamiaji wanaoingia nchini humo wakitafuta maisha bora...wengi wakiwa ni watu wanaotafuta fursa bora kwa maendeleo yao na familia zao.

Lakini walianza kuwa na wasiwasi naye toka alipotamka kwenye kampeni kwamba angeweza kumpiga mtu risasi hadharini katikati ya jiji na wafuasi wake hawangemuacha. Hata hivyo pamoja na kwamba hawakumpa nafasi yoyote ya kuchaguliwa kuwa Rais waliamini anatania na kwamba ukitokea akashinda atabadilika.

Na kweli, kama walivyo kawaida ya bianadamu, madikteta na watawala wanaotumia ubabe kuliko demokrasia, wanakuwa na wapenzi wanaowaganda kama shati lililoloa hata pale wanapotukanwa hubaki wakishangilia tu kama wehu. Amewasifia viongozi wababe ambao wananchi wao wanateseka na kuishi kwa hofu kwa kunyimwa uhuru wa kusema.

Subirini muone watu waliopigania uhuru na haki wanavyojibu mapigo kwa kiongozi anayejitokeza na kutaka kuwarudisha nyuma huko walikotoka. Donald Trump kaliamsha dude, Donald Trump kalikoroga, Donald Trump kakuta simba wamelala akadhani ni kondoo na kuwavuta sharubu! Shuhudieni Wamarekani wanavyopigania misingi ya demokrasia walizojenga babu zao kwa damu zao.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
RAIS TRUMP NI KAMA 'ANA WEWESEKA'
SATURDAY MASSACRE YA NIXON HAIKUMWACHA SALAMA

Baada ya kumtimua mfuasi wake mtiifu na seneta wa kwanza kumuunga mkono AG Sessions, Rais Trump amemteua Bw Mathew Whitaker kuwa Acting AG

Haikuchukua muda vyombo vya habari vikaanika kauli zake ikiwemo ya kutafuta 'kick'

Whitaker aliuwa chief of staff wa DOJ kwa shinikizo la WH
Gazeti la NYT limeeleza kwa kina, bwana huyo alikuwa 'go between' kati ya DOJ na WH

Whitaker ana mazonge zonge mengi ikiwemo kumshambulia Mueller anayechunguza Russia, kushiriki katika kampuni inayochunguzwa na FBI n.k.

Rais Trump anakana kutomjua licha ya ushahidi wa kutosha kionyesha mawasiliano na uswahiba

Kuna maswali yanajitokeza; Kwanza, ilikuwaje amteua mtu katika nafasi hiyo nyeti bila kumjua
Pili, ni kwanini hakuzingatia taratibu za kumteua deputy au solicitor kwa mlolongo wa madaraka

Kumtimua Sessions hakujamsaidia kama ilivyotokea kwa FBI Dir Comey .
Ikumbukwe, kutimuliwa kwa Comey kulikaribisha uchunguzi wa Mueller

Sessions ingawa hakuhusika na uchunguzi, alijua nini kinaendelea.
Ni kama mtifuano wa Trump na mwanasheria wake Cohen unavyozidi ''kumtafuna''

Katikati ya timbwili la Acting AG Whitaker, Bw Trump ameendelea kumshambulia Mueller kwa uchunguzi 'hoax'. Kwa mtazamo wa haraka, ima hajui taratibu za Washington au ni makusudi.

Uwepo wa Mueller ni wa kisheria, na tayari uwepo wa Whitaker una tatizo

Kamati za House zitakazoongozwa na Democrats zimeandika barua kwa wahusika wa idara ya sheria (DOJ) kuwataka kutotupa nyaraka au ushahidi wowote uliopo na utakaokuja

Kuna taarifa, nyaraka za uchunguzi za Mueller zinahifadhiwa kisheria na FBI kulinda uchunguzi

Kwa mantiki hiyo, kutimuliwa kwa Mueller hakutaondoa tatizo, kutaliahirisha kwa muda na pindi litakaporejea tunaweza kuiona historia ikijirudia kwa jicho la Rais Nixon

Acting AG Whitaker anatumiwa kutafuta sababu za kumuondoa Mueller.
Kwa wakati huu hilo limechelewa kwani Mueller anakamilisha taarifa yake

Wachunguzi wa mambo katika viunga vya DC wanatanabahisha kuwa haya ni 'mauaji ya polepole' slow massacre katika mtindo aliotumia Nixon, siku ya Jumamosi yaliyohitimisha safari yake ya Urais wa Marekani. Kiwewe alicho nacho Trump kinatia shaka kuliko mashaka yaliyopo

Ikiwa uchunguzi wa Russia ni hoax na hakuna collusion, kwanini anaweweseka kiasi hicho?

Tusemezane
 
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
13,369
Likes
5,151
Points
280
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
13,369 5,151 280
Jaji Kavanaugh kaapishwa na Jaji mkuu katika seherehe ndogo iliyofanyika SC
Naambiwa maseneta wote waliompinga ama kupiga kura ya Hapana dhidi ya Kavanaugh wameshindwa kwenye uchaguzi wa muhula wa hivi majuzi huko Marekani. Je. Habari hizi ni za kweli?
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
9,976
Likes
8,299
Points
280
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
9,976 8,299 280
Naambiwa maseneta wote waliompinga ama kupiga kura ya Hapana dhidi ya Kavanaugh wameshindwa kwenye uchaguzi wa muhula wa hivi majuzi huko Marekani. Je. Habari hizi ni za kweli?
TUJITEGEMEE, hivi huamini kabisa blue wave ilivyoufunika huu uchaguzi uliopita? Kama si hujuma ya gerrymandering iliyofanywa na Republicans kuhakikisha wanashinda chaguzi mbalimbali hali ingekuwa mbaya sana kwao safari hii. Democrats walitabiriwa kushinda majimbo 23 ya House lakini hadi sasa wamevuka idadi hiyo na wanachungulia majimbo 35!

Nafasi zilizokuwa zikigombewa kwenye Senate ni 35 tu kati ya 100 huku 65 wakiendelea na nafasi zao kusubiri uchaguzi mkuu wa Rais mwaka 2020 watetee nafasi zao. Hali hiyo ndiyo imewanusuru Republicans kutokupoteza Senate! Kwa House ndiko nafasi zote zilikuwa zinagombewa na Republicans wamepoteza uongozi katika baraza hilo.

Kama si gerrymandering wangepoteza zaidi ya hizo. Congress iliyokuwa likizo toka Trump achaguliwe na kumuacha Trump afanye anavyotaka sasa itarudi kazini, likizo imekwisha. Huyo Kavanaugh imekula kwake na ajitayarishe tu kujibu tuhuma zitakazoelekezwa kwake kwani hakuna tena kukingiwa kifua na Congress.

Na kwa kuonesha kwamba Republicans hawana chao wamarekani wengi wanapojitokeza kupiga kura ni kwamba idadi ya Democrats waliojitokeza hii midterm wamewazidi Republicans kwa asilimia zaidi ya nne. Hii yote ni pamoja na Rais mwenyewe kuacha kazi zake za ofisini na kujikita kwenye kampeni kuliko Marais wote waliomtangulia.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
TUJITEGEMEE, hivi huamini kabisa blue wave ilivyoufunika huu uchaguzi uliopita?

Kama si hujuma ya gerrymandering iliyofanywa na Republicans hali ingekuwa mbaya sana kwao safari hii. Democrats walitabiriwa kushinda majimbo 23 ya House wamevuka hadi 35!

Nafasi zilizokuwa zikigombewa kwenye Senate ni 35 tu kati ya 100 huku 65 wakiendelea na nafasi zao kusubiri uchaguzi mkuu wa Rais mwaka 2020 watetee nafasi zao.

Hali hiyo ndiyo imewanusuru Republicans kutokupoteza Senate! Kwa House ndiko nafasi zote zilikuwa zinagombewa na Republicans wamepoteza uongozi katika baraza hilo..
Mkuu Mag3 unakumbuka asubuhi ya matokeo ndiyo siku Sessions alitumuliwa.

Haikuwa bahati mbaya, ilipangwa ili kufunika mijadala ya GOP na Trump walivyopoteza midterm

Haya mambo yanahitaji kufuatilia kwa analysis. Kusikia tu au kuambiwa inakuwa 'mtihani'

Hoja ya kwanza ilikuwa, Obama ameshindwa maeneo aliyo kampeni kutoka kwa Trump.
Alijua wapo wanaozoa tu bila tafakuri.

Well, Obama alishiriki ku set agenda ya House na Senate akiwaambia wajikite katika ACA au Obamacare. Alitembelea maeneo akifanya mikutano ya House na Senate

Republicans wakadakia hoja ya kuhifadhi '' pre-existing conditions' .
Wapiga kura waliwahoji, walipotaka kubomoa Obamacare walilenga nini?

Trump akaiingiza ajenda ya 'caravans'. Hoja hiyo ikabaki yake na si Republicans
Kukawa na disarray ya nini hasa ni agenda ya Republicans katika midterm

Rais Trump akatumia gerrymandering ku-target maseneta wa Dems ndani ya GOP States

Imemchukua zaidi ya wiki tatu akizunguka Virginia kwa Joe Munchin(D), Nevada kwa Dean Heller(D) , North Dakota kwa Heidi Heitkamp(D), Montana kwa John Tester (D), Arizona kwa Martha McSally (R), Florida kwa Bill Nelson (D) na Missisipi kwa Roger(R)

Katika wiki tatu hiki ndicho kilichotokea . Missisipi watarudia uchaguzi kwa sheria za state
Florida kura zinahesabiwa na ni likely Republicans watashinda

Katika ''vulnerable Dems'' tuliorodhesha, Dems wametetea Nevada, Virginia na Montana
Wameshinda Arizona ambako ni red state. Hadi leo hii tarehe 13 November ni kuwa Senate itakuwa na 51 kwa 47 kukiwa na baki ya Florida na Missisipi

Jitihada za wiki tatu za ku-flip Dems senate seat zimezaa matunda ya maseneta 2 au 3
Ni jitihada nzuri, Republicans wamebaki na uongozi wa Senate! Lakini zina tija?
Hilo limefanyika kwa ghara kubwa sana ya kupoteza House

Dems wanaelekea kuwa na majority ya 230+ ndani ya House.
Hili limekuja baada ya ku-flip Republicans districts zaidi ya 20.
GOP wamepoteza maeneo mengi yakiwemo ya Ugavana wa states na mabunge ya States

Katika ugavana, Dems wamepata mgavana 7 zaidi na sasa kuwa na 23 dhidi ya 25 ya GOP huku majimbo mawili yakiwa yanahesabu kura , Florida na Georgia.

Katika hilo la ugavana, Democrats wamekomboa viti zaidi ya 300 walivyopoteza (takribani 1000)
Hivyo mabunge ya state yaliyotawaliwa na GOP yana Dems wengi kwasasa

Magavana na wabunge wa state wana maana kubwa kwa ''gerrymandering ''kama ilivyojadiliwa
Ni vema kukumbuka, Wisconsin, Kansas, Michigan, New Mexico na Maine zimekwenda Dems

Tukirudi kwa wapiga kura,Republicans wamepoteza 'independents' kwa point 10+.
Wamepoteza kwa wanawake na wasomi wakibaki na wanaume na maeneo ya vijijini

Midterm imeonyesha jambo jingine, kwamba, maeneo kama Texas, Arizona ambayo ni red state yanaingiliwa na Dems. Swing states alizoshinda Rais Trump zinapoteza rangi yake
Ted Cruz aliomba msaada kwa state ya Texas ambayo ni Red state

Kwa mtazamo huo mfupi , kuangalia impact ya kitu kimoja kisicho na maana kama Kavanaugh,ni kujidanganya,kusoma tweets bila tafakuri na kutoelewa siasa za viwango vya viunga vya DC

Tusemezane
 
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Messages
81,995
Likes
49,147
Points
280
Age
28
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined May 15, 2006
81,995 49,147 280
Nguruvi3 umesikia tuhuma dhidi ya Michael Avenatti?

 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
9,976
Likes
8,299
Points
280
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
9,976 8,299 280
Breaking News: Rais Donald Trump wa Marekani apagawa...

Ni baada ya kudokezewa kidogo tu tuhuma zinazoweza kumkabili katika uchunguzi unaoendeshwa na Robert Mueller. Anavyofoka na kutukana hata walio karibu naye wamepigwa na butwaa.

Kwa sasa yapo maswali amepewa kimaandishi kuyajibu akisaidiwa na wanasheria wake lakini hata wao akiwemo Rudy Giuliani, bado wanatafakari namna ya kuyajibu bila wenyewe kujitia kitanzi.

Pamoja na hayo lililompagawisha Trump ni za tuhuma ambazo hata hazikutajwa katika maswali hayo lakini kadokezwa na watu ambao inaonekana wamepata fununu za kinachoendelea, Mueller ni kiboko.

Kaeni mkao wa kula, habari zaidi zitafuata...
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
WIKI KATIKA SIASA ZA US
NI WIKI ILIYOMVURUGA SANA TRUMP KWA MATUKIO

Baada ya uchaguzi wa muhula wa kati 'midterm elections' rais Trump ameonekana kuweweseka
Huko WH aliyekuja mbele yake alichukua 'makavu' kama ilivyokuwa katika tweeter

Uchaguzi haukuwa mzuri, jitihada za wiki tatu, GOP wamepoteza House kwa gharama kubwa. Hali ya ramani ya uchaguzi imebadilika maeneo mengi ikionyesha GOP kupoteza ushawishi

Hali hiyo imemvuruga Rais Trump licha ya makando kando kama suala la Khasoggi

Trump alimwendea kombo mchunguzi Mueller akiuita uchunguzi kama hoax

Gharama ya shambulio hilo ni kubwa, Mueller atahitaji ushahidi mzito kuiondoa dhana ya hoax na kuthibitisha ubora wa kazi yake. Kuthibitisha huko kunaweza kuja na gharama kwa Trump

Trump alitaraji uteuzi wa Acting AG Whitaker ni mwanzo wa kuua uchunguzi wa Mueller
Whitaker sasa ni sehemu ya maongezi huku Trump akimkana kutomjua ingawa ushahidi wa kumjua umejitokeza wiki hii.

Kumevuja taarifa za kikao ambacho Whitaker alihudhuria na Rais Trump akimtaka mshauri wa sheria aiagize wizara ya sheria (DOJ) kumshataki Comey na Hillary Clinton kinyume na utaratibu

Wakati huo huo Whitaker anaandwamwa na masuala binafsi yanayohusiana na kukaimu nafasi Taarifa zake za pesa, na ushiriki katika biashara hazionyeshi mwisho mzuri

Kuteuliwa kwa Whitaker kulikuwa na maana ima kuua uchunguzi Mueller au kuzuia taarifa zitokanazo na kamati hiyo kuwekwa hadharani kwani AG ndiye mwenye mamlaka ya kuamua

Tatizo linajitokeza, Democrats wameandika barua za kuhifadhi nyaraka zote kabla ya kukabidhiwa House na kamati zake na taarifa za Mueller zimehifadhiwa maeneo nyeti

Kiwewe cha Trump ni nguvu ya House na kamati zake hasa katika subpoena nyaraka muhimu
Mpango mzima wa kumweka Whitaker unaonekana kuwa na 'mkwamo' at least kwa wakati huu

Ni katika kiwewe, mzee Trump amewatosa CIA kuhusu Khashoggi.

Trump amemwendea Kombo Jaji mkuu katika mitandao akihoji kuhusu '9th circuit' na jinsi kesi zake zinavyogonga mwamba bila kujua nguvu ya kesi

Ni nadra sana Jaji mkuu kujibu tuhuma, kwa lililotokea alilazimika kuonyeshwa kukerwa

Trump kamwendea Kombo Gen McRaven aliyeongozaseal six kumuua Osama na Saddam

Sehemu kubwa ya matatizo anayatafuta. Kuwafukuza akina Comey au Sessions na wengine kutoka WH waliojiuzulu kunazidi kuvujisha siri za mambo mengi yaliyokuwa hayajulikani

Kwa wiki moja, si Mueller, CIA, Media, McRaven, Jaji mkuu n.k. waliosalimika mbele ya Trump
Hata hivyo hali hiyo inaelezwa kuwa 'unforced error' na inazidi kuweka ugumu kwake

Tusemezane
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,924
Likes
8,925
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,924 8,925 280
MIDTERM IMEKAMILIKA
GOP WATAKUWA NA SENATE, DEMS WATAKUWA NA HOUSE

Uchaguzi wa maseneta na wawakilishi umekamilika.
Ni baada ya kukamilika kwa chaguzi za ushindani kwa maseneta, Florida na Mississipi

Republicans wameshinda maeneo na kuwa na idadi ya maseneta 52.
Kwa kuongeza kura ya VP ni 53. Dems watabaki kuwa na maseneta 47 wakiwa wamepoteza 2

Kwa upande wa House, Dems watakuwa na wajumbe 40 zaidi

Haya yana maana katika siasa za US. Ndani ya senate, GOP na WH watakuwa na kazi ndogo ya kuthibitisha teuzi za Rais Trump kama majaji na viongozi waandamizi

Hata kama kutakuwa na wajumbe 2 watakaoleta 'taabu' kura ya VP itasaidia sana
Kamati za senate zitakuwa chini ya Republicans

Katika House, Spika atatoka Democrats na kamati za House zitaongozwa na Dems
Miswada inayotakiwa kupitishwa itakuwa na ushindani kwani lazima ipate ridhaa ya pande zote

Ndoto ya Rais Trump kufuta Obamacare(ACA) itakuwa nzito na ngumu, hana House

Kwa upande wa senate, kutakuwa na kazi ngumu kidogo kwa Republicans
Uchaguzi mkuu una maseneta takribani 65 , wengine wakiwa katika himaya za Democrats

Maamuzi ya maseneta wa GOP itabidi yalenge maeneo ya wapiga kura kwa kuangalia 2020

Midterm imeonyesha mambo mengi. Kwanza, midterm haielezi uchaguzi mkuu lazima ufuate matokeo ya sasa. Rais Obama alipoteza senate na House, alichaguliwa mara ya pili

Pili, matokeo yametoa fursa kwa state kurudi kwa Dems,hilo litabadili gerrymandering
State kama Pennyslavania, Michigan na Wisconsin zimerudi chini ya Dems

Tatu, matokeo ya House yameonyesha Republicans kupungua nguvu kiasi kwamba Rais Trump amekwenda kukampeni maeneo kama Mississipi na Texas ambayo ni red state

Republicans wamepoteza house reps kwenye maeneo yao jambo linaloashiria hali nyingine
a)Kwamba, Rais Trump na nguvu ya wiki tatu ameongeza maseneta 2 na kupoteza House
b)GOP wamepoteza umiliki wa magavana na viti katika state senate nyingi

Hata hivyo Rais Trump ni maarufu kwa Republicans kwa asilimia 90+
Kwa mtazamo wa haraka anafanya vizuri sana ndani ya Republicans

Kimahesabu kuna tatizo
i) 90% ni kutoka Republicans. Hata kama Republicans watapungua bado haiathiri asilimia hiyo
Ku-''shrink' kwa GOP hakuwezikupunguza umaarufu kwa wale waliobaki hata kama ni 1000, na 900 wanamkubali bado ni 90%

ii) Kwamba, 90% haijalishi wangapi wameondoka. Kwa kuangalia matokeo ya House tunapata hoja ifuatayo. Kwamba, ima Democrats waliompigia 2016 au Independents wameondoka GOP

Tunasema hivyo kwasababu idadi ya wapiga wa midterm imeongezeka, lakini Dems wameongeza kwa zaidi ya milioni 9 dhidi ya Republicans

Pili, ushindi wa Dems ndani ya maeneo ya GOP kama Kansas, Utah, Arizona.
Kwamba, close call maeneo kama Mississipi na Texas kunashadidia hoja ya kupungua GOP

Pamoja na Rais Trump kujinasibu na 'ushindi' ni wazi GOP wana kihoro, wanaliona tatizo
Adui anapingia kupigana nawe 'uani' kwako si dalili njema, na hapo ndipo hofu ilipo

Maswali wanaojiuliza GOP, kwanza,umaarufu wa Trump ndani ya Republicans inayo shrink utaweza kuwasaidia maseneta? Kwanini wamepoteza house, Magavana na state senate?
Wapiga kura waliowachagua wamekwenda wapi? Watarudishwa kwa njia gani?

Hali hiyo itawatia kiwewe maseneta wa GOP katika kupitisha miswada hasa wanaokwenda 2020

Kwa upande wa Dems nako kuna changamoto baada ya kupata House. Tutajadili sehemu ijayo

Tusemezane
 
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
13,369
Likes
5,151
Points
280
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
13,369 5,151 280
Kuna hizi habari za Chini chini...! Nadhani mnazinyima uzito Bure.
======
A UK spy agency did not eavesdrop on Donald Trump during and after last year's US presidential election, a British security official has said, denying an allegation by a US television analyst.

The official, who is familiar with British government policy and security operations, told Reuters that the charge made on Tuesday by Fox News analyst Andrew Napolitano, was “totally untrue and quite frankly absurd.”

>independent.co.uk
-------
Helga Zepp-LaRouche, the founder of the Schiller Institute, headquartered in Washington, DC, told Sputnik that British intelligence agencies сould have been behind the alleged meddling in the 2016 US presidential elections. According to her, the team of then President Barack Obama and the UK's MI6 could have worked together. She believes that Donald Trump's election promises to improve relations with Moscow prompted the actions by the British side, as they could have seen the promises as a threat to their position. Zepp-LaRouche added that as with the alleged US election meddling, the Skripal poisoning case and Syrian chemical dossier emerged to further discredit Russia.
She noted that if meddling on the part of the UK were to be uncovered, it could become the biggest political scandal in the US, even bigger than Watergate.

>sputniknews.com
---

>RT.com
====
UK kupitia 'tools' zake alikuwa na sababu kuingilia uchanguzi wa US kutokana na msimamo wa Trump kwenye kampeni zake. Na inasemekana, Trump alikwamishwa ku 'declassify' baadhi ya nyaraka kati ya mwezi July na Septemba mwaka huu ambazo zingefunua ukweli huu.
 
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
13,369
Likes
5,151
Points
280
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
13,369 5,151 280
As such, the investigation’s focus has shifted this year from looking for collusion to finding obstruction. Mueller’s team have combed through Trump’s tweets and looked at his firing of former FBI Director James Comey with a view to finding this obstruction, so far unsuccessfully.

Cohen's plea comes two weeks before the lawyer is due to be sentenced for the earlier tax and campaign finance violations. He is facing a possible term of 46 to 63 months in prison and a potential fine of up to $1 million. His voluntary cooperation with Mueller, however, could see this punishment lessened significantly.
===
Cohen anachokifanya, ni kumchomoa Trump kwenye 'makandokando' ingawa anadhani ndiye anampaka hayo makandokando. Kwa hili Trump atapeta tu.
 

Forum statistics

Threads 1,250,884
Members 481,523
Posts 29,749,538