Enzi hizo wamarekani walikuwa na adui mmoja tu: USSR; kwa hiyo internal politics hazikuwa tribal kama leo. Siasa za Marekani zilianza kubadilikwa mwaka 1992. Baada ya Soviet Union kubomoka, halafu Clinton (mtoto wa maskini) akaja kumshinda George H.W Bush, wamarekani walianza kugawanyika. Ile health care plan ya Clinton ilipigwa vita vibaya sana wakati huo ambayo ndiyo hii Obamacare ya leo ambayo wamarekani wanaikimbilia. Vita hiyo ndiyo iliyosababisha Republican kuwa majority kwenye Congress baada ya miaka 40. Sasa Gingritch ndiye aliyeharibu kabisa siasa za Marekani, kwani tangu alivyoanza siasa a chuki binafsi dhidi ya Clinton mwaka 1994 hali ndiyo inayoendelea tena hadi leo; wanasiasa wanatazamana kwa chama tu, hawatazamani kwa msingi wa utaifa tena.Kwa ufahamisho tu, House ilipoanza impeachment proceedings dhidi ya Richard Nixon, wengi wa Republicans hawakuunga mkono lakini hizo proceedings ndizo ziliibua ushahidi uliowawezesha hata hao Republicans kubadilisha msimamo. Kabla ya hapo alikuwepo Republican mmoja tu aliyejitokeza na kuunga mkono impeachment ya Nixon lakini baada ya ushahidi wa tapes kuibuliwa kwenye proceedings ndipo na wenzake walipounga mkono.
Hali kama hiyo ndiyo ipo mpaka sasa lakini tofauti inayojitokeza wakati huu ni Spika Pelosi kutaka kabla ya hizo proceedings kuanza ushahidi zaidi upatikane na anajua utapatikana. Hivyo anawataka Democrats kwenda taratibu bila pupa ili wananchi wapate muda wa kutosha wa kujua kwa nini Donald Trump awe impeached. Viongozi wengi wastaafu wa GOP tayari wanaanza kujitokeza kuunga mkono wazo la kumtaka Rais Trump awe impeached.
Katika wiki ya kesho mengi zaidi yataibuliwa kulingana na kesi zinazoendelea mjini New York chini ya grand juries zilizoundwa na Robert Mueller ambapo baadhi ya redactions alizofanya AG Barr zimeamriwa zianikwe kwa wananchi. Na hapa ndipo Trump anapopata wazimu kwa nini impeachment haianzi mara moja kama alivyotegemea yeye. Alitaka impeachment ianze huku wananchi walio wengi ikiwa bado hawajui kinachoendelea lakini Pelosi katia breki.
Hasira yote ya Trump inaanzia hapo; mipango yake na wanasheria wake imevurugika kwani hawajui ni lini House itaanza proceedings na hajui ushahidi utakaokuwa umepatikana wakati huo. Ndugu zangu Marekani mambo kama haya huenda taratibu na si kwa pupa kama wengi wananvyofikiria. Sheria ya Marekani inawalinda sana wenye tuhuma mbali mbali na ni pale tu ushahidi unatosheleza ndipo hatua huchukuliwa na hili Pelosi analijua fika.
Halafu ipo hii dhana inayoenezwa zaidi na GOP kwamba impeachment inaweza ikawaathiri sana Democrats kwenye uchaguzi ujao. Hii ni kweli inaweza ikatokea kama Democrats hawakujipanga vizuri lakini kwa style ya Pelosi ya kukataa kukurupuka bila ushahidi wa wazi na unaojitosheleza. Pia wanafuatilia matamshi yote ya Trump na kila kauli anayotoa inachunguzwa kwa umakini mkubwa kwa sababu wanajua woga wake ndio unamfanya aropoke hovyo.
Hili lipo wazi kabisa, kwamba, kumtuhumu mtu bila kumfikisha mahakamani kujitetea si haki. Tena hoja hiyo ameitumia AG Barr anaposema '' taarifa ya Mueller itakuwa ''redacted' katika makundi manne"Kichuguu, post: 31664771, member: 348"
Ina maana hufuatilii habari hizo kwa karibu na wala hujui hili hapa
Unaonyesha kutokujua namna ya kuunganisha habari za kisheria.
Mueller anasema kuwa yeye hakuwa amepewa mamlaka ya kumshitaki Trump, na pia amesema utaratibu wa fairness unamzuia kumtuhumu mtu bila kumpeleka mahakani akajitetetee.
Kwa hiyo akasema hawakumtuhumu kwa hatia, na pia hawakuona kuwa hana hatia. Hiyo ni neutral conclusion ambayo Barr asingeitumia kusema kuwa hana Trump hatia. Hana mamlaka ya kusema nani ana hatia au hana hatia; kazi yao ni kutuhumu na kuziachia mahakama kuamua kama kuna hati au vipi.
Mkuu Mag3 na Kigarama #816 wamesisitiza sana kuwa siasa za US zikiangaliwa kwa jicho la Tanzania mtu atatatizika sana. Kuna Wanasheria Marekani wanasubiri fursa, lugha tu inaweza kuwapa fursa wanayotaka.Prosecutor anakutuhumu tu anapodhani una hatia. Iwapo wangemwona hana hatia, wangesema kuwa hatumkuta na hatia yoyote ya kumtuhumu. Kuna lugha nyingi za kutumia, kwa mfano hakuna ushahidi wowote, au ushahdi tuliopata hautoshi kumtuhumu, kama ambavyo walivyosema kwenye volume 1. Hata hiyo conclusion ya volume 1, ilisema tu ushahidi upo wa conspiracy, lakini hautoshi kuprove beyond reasonable doubts- standard ya criminal prosecution.
Kuntu, kama haelewi hataelewa tenaKama unakumbuka mwaka 2016 kabla ya uchaguzi, Combey alilaumiwa sana kwa kumtuhumu mams Clinton halafu na kuishia kusemahakuna ushahidi wa kutosha kumshitaki. Hiyo inaitwa character assassination ambayo wanasheria hawafanyi hivyo mahakamani.
Mkuu hii hoja inatumiwa sana na Trump bila kuangalia ukweli au kwa nia ya kupotosha tu. Trump anajua miongoni mwa wafuasi wapo watakaomeza tuTrump anajivuna kuwa uchumi umekuwa imara chini yake huku ikiwa wazi kuwa hakubadilisha trajectory ya Obama, aaliingia kweye msafara wakati uko kwenye lango halafu anajivuna kuwa ni yeye aliyeingiza msafara ndani.
Kwa hiyo akasema hawakumtuhumu kwa hatia, na pia hawakuona kuwa hana hatia. Hiyo ni neutral conclusion ambayo Barr asingeitumia kusema kuwa hana Trump hatia.
Hana mamlaka ya kusema nani ana hatia au hana hatia; kazi yao ni kutuhumu na kuziachia mahakama kuamua kama kuna hati au vipi.
Prosecutor anakutuhumu tu anapodhani una hatia. Iwapo wangemwona hana hatia, wangesema kuwa hatumkuta na hatia yoyote ya kumtuhumu. Kuna lugha nyingi za kutumia, kwa mfano hakuna ushahidi wowote, au ushahdi tuliopata hautoshi kumtuhumu, kama ambavyo walivyosema kwenye volume 1. Hata hiyo conclusion ya volume 1, ilisema tu ushahidi upo wa conspiracy, lakini hautoshi kuprove beyond reasonable doubts- standard ya criminal prosecution.
Maelezo mazuri, wala hamna aliyesema Mueller anaweza kumshtaki Rais aliye madarakani, wala aliyepinga fairness principle kwa jinsi alivyoitumia Mueller.Nafikiri hiki kipande hiki chini ndicho hukuelewa kabisa, inagwa nimeshakigusia hapo juu. Huwezi kumtuhumu mtu ambaye huwezi kumshitaki akajitetea. Mueller alifanya kazi chini ya huo msingi kuwa huwezi kumshitaki Rais; kwa hiyo asingeweza kusema kuwa kuwa ana hatia, kwa vile hakuwa na uwezo wa kumshitaki (Department policy) na kumpa nafasi ya kujitetea (principles of fairness). Kama unakumbuka mwaka 2016 kabla ya uchaguzi, Combey alilaumiwa sana kwa kumtuhumu mams Clinton halafu na kuishia kusemahakuna ushahidi wa kutosha kumshitaki. Hiyo inaitwa character assassination ambayo wanasheria hawafanyi hivyo mahakamani.
Sentensi hiyo ndiyo nyepesi kuliko zote. Anakuambia kuwa criminal justice system aliyokuwa akiendesha haina mamlaka ya kumtuhumu rais kwa makosa; katiba ina utaratibu mwingine wa kufanya hivyo. Maana yake nikuwa utaratibuhuo mwingine ndio utumike.
Again; bado ninaheshimu first ammendment rights zako.
Tena hoja hiyo ameitumia AG Barr anaposema '' taarifa ya Mueller itakuwa ''redacted' katika makundi manne: Intelligence info , security info, grand jury materials na watu waliotajwa ambao hawakushtakiwa, Sababu ya watu hao kuwa redacted ni kwa ukweli kuwa hawakupewa nafasi ya kujitetea''
..anajivuna kuwa uchumi umekuwa imara chini yake huku ikiwa wazi kuwa hakubadilisha trajectory ya Obama, aaliingia kweye msafara wakati uko kwenye lango halafu anajivuna kuwa ni yeye aliyeingiza msafara ndani.
Huyu jamaa naona la,a mo takataka sana. Ana miaka sabini lakini amekuwa kila siku mlalamishi wa kutaka attention tu.
Haya mambo ya kuwa anaandika twitts kila wakati kulalamika lalamika, au kudaia kusifiwa ni dalaili ya utoto sana, na nadhani marais wengine wote wamshamjua; Rais wa China hana taimu naye tena. Trump hanywi pombee ila naona amezeeka na akili ya kitoto.
Tatizo lako wewe unasoma msitali mmoja mmoja badala ya kusoma context yote. Kwa upande conspirancy, ilionekana kuwa ushahidi uliopo hautoshi; yaani kuna ushahidi lakini hautoshi kupeleka mahakamani (kwenye crimal law); hiyo siyo kusema there was NO COLLUSION. Kwanza katika sheria hakuna kitu kinaitwa Collusion, lakini AG Barr ambaye ndiye mwanasheria mkuu wa nchi aliimba mara hivyo kadhaa kabla hajatoa ripotu yenyewe.Katika misingi ya haki, tunasema mtu hana hatia hadi ithibitishwe vinginevyo (presumption of innocence). Katika misingi hiyo muendesha mashtaka hawezi kumtuhumu (indict) mtu hadi awe na ushahidi wa kutosha. Akiwa nayo, mashtaka (prosecution) yanafuata mahakamani, halafu hatia (conviction) au hamna hatia (innocence).
Mueller hakumu-indict Trump katika ripoti yake. Kwa maana kwamba hakuhitimisha kuwa ushahidi aliokusanya unamtosha kumtuhumu kwa kosa la "obstruction." Badala yake hakutoa hitimisho kuhusiana na kesi hiyo.
"..we did not draw ultimate conclusions about the President's conduct."
Ukisoma vizuri conclusion nzima ya Mueller, hakutoa hitimisho la kusema kosa limetendwa kutokana na masuala magumu (difficult issues) ya matendo na dhamira ya Rais aliyokutana nayo, ambayo amesema yanahitaji kuwa resolved kwanza.
"The evidence we obtained about the President's actions and intent presents difficult issues that would need to be resolved if we were making a traditional prosecutorial judgement"
Hakuwa na haja ya kusema hili kwenye hitimisho lake kama lengo lake toka mwanzo lilikuwa ni kutaka utaratibu mwingine utumike kufanya maamuzi. Conclusion ndipo mahali ujumbe husika unapopatikana. Hakuna neno lolote kwenye conclusion ya Mueller lenye muelekeo wa kuitaka Congress ikaamue kuhusu obstruction.
Ukisoma Code of Federal Regulations ya mwaka 1999 na sababu za kushindwa ku-renew Ethics in Government Act ya mwaka 1977, utagundua kuwa AG amepewa mamlaka makubwa katika uteuzi na kumsimamia Special Counsel. Kwa kifupi AG ndiye Bosi wa Special Counsel.
Special Counsel aliandika ripoti akampa bosi wake, akisema amekutana na masuala magumu yanayohitaji kutatuliwa ili kutoa uamuzi fulani. AG kama Chief Prosecutor kwa kushirikiana na Deputy wake na OLC wakatatua masuala hayo na kuhitimisha kuwa ushahidi uliokusanywa hautoshelezi kumtuhumu Trump kwa obstruction.
Hakuna sehemu AG Barr amesema Trump hana hatia, hiyo ni tafsiri yako kama ilivyo kwa watu wengine. Bali Barr alichosema ni kwamba ushahidi uliokusanywa kwenye uchunguzi wa Special Counsel hautoshelezi kudai kuwa Rais amefanya kosa la obstruction.
"After reviewing the Special Counsel's final report on these issues.....Deputy Attorney General Rod Rosenstein and I have concluded that the evidence developed during the Special Counsel's investigation is not sufficient to establish that the President committed an obstruction-of-justice offense."
Mueller ndiye hakuwa na mamlaka ya kusema Trump hana hatia maana hiyo sio kazi yake.
"while this report does not conclude that the president committed a crime, it also does not exonerate him.”
Prosecutor anafanya kazi zaidi ya indictment (kutuhumu mtu kuwa ana hatia), kwa maana kwamba anamshtaki (prosecution) mtuhumiwa kwa kosa fulani ili mahakama iamue kama kuna hatia au lah!
Basis ya hoja yako na kuweka screenshot ni kwamba hukubali kwamba prosector anam-prove mtu "guilty" na sio "innocent"!
Kama unaamini kwamba kwenye mfumo wa haki tuna-assume mtu hana hatia hadi ithibitishwe vinginevyo, prosecutor anawezaje kufanya kazi ya kuthibisha kuwa mtu hana hatia (kwa maana ya "exoneration")? Ina maana ali-assume ana hatia kabla?
Maelezo mazuri, wala hamna aliyesema Mueller anaweza kumshtaki Rais aliye madarakani, wala aliyepinga fairness principle kwa jinsi alivyoitumia Mueller.
Amesema hivyo kwenye ripoti yake? Amezungumzia hilo kwenye hitimisho lake? Alishindwaje hata kuandika hilo pendekezo?
Jambo la muhimu ni kwamba Mueller hajahitimisha kuhusu obatruction, sio kwa sababu ya utaratibu wa kikatiba unaohusu indictment na prosecution ya Rais aliye madarakani, hapana! Conclusion ya ripoti yake ipo wazi na inaelezea sababu wazi.
Mueller sio Special Counsel wa kwanza kumchunguza Rais aliye madarakani, Ken Starr alihitimisha uchunguzi wake kwa kupata ushahidi wa kutosha dhidi ya Bill Clinton.
Unadhani, Mueller angepata ushahidi wa kutosha (sufficient evidence) kwenye "conspiracy", conclusion yake ya Volume I angeiandikaje?
Endelea tu kuheshimu hizo 'rights' mkuu!
Pepripheral third parties sio watu ambao hawakupewa nafasi ya kujitetea, bali ni watu ambao hawakuwa charged na hivyo hawawezi kupata nafasi ya kujitetea.
Mkuu Nguruvi3 mbona hujaonyesha sehemu niliposema underlying evidence zimepigwa mstari?
Kusema kuwa taarifa nzuri za kiuchumi ni "trajectory ya Obama" ni kupindisha ukweli. Tukiuliza Obama alifanya nini hadi mwezi June mwaka 2016, cha kusababisha uwekezaji kuongezeka US leo hii na kuongekeza kwa ajira, hamna jibu!
Hebu tuwalinganishe kidogo Obama na Trump kwenye vipengele hivi viwili : uchumi na ajira;
(Nitatumia namba za miaka miwili ya mwisho ya awamu ya pili ya Obama ili kuondoa visingizio, nikilinganisha na miaka miwili ya mwanzo ya Trump; tutatumia ulinganisho ulio fair na unao-make sense).
(i) Ukuaji wa GDP: Uchumi ulikuwa ukikua kwenye 1.5% katika kipindi cha miezi 18 ya mwisho ya Obama, wakati ulikua mara mbili hadi asilimia 3% katika miezi 18 ya mwanzo ya Trump.
(ii) Ongezeko la nafasi za ajira (job openings): Ongezeko la nafasi za ajira ilikuwa wastani wa nafasi 900 kwa mwezi - kwa miezi 21 ya mwisho ya Obama, wakati ongezeko hilo likiwa ni wastani wa nafasi 75,000 kwa mwezi - kwa miezi 21 ya mwanzo ya Trump.
(iii) Walioajiriwa: Kwa kipindi cha miezi 21 ya mwisho ya Obama, idadi ya wamarekani walioajiriwa iliongezeka kwa wastani wa watu 157,000 kwa mwezi, huku idadi hiyo ikikua kwa wastani wa watu 214,000 kwa mwezi kwa miezi 21 ya mwanzo ya Trump (ongezeko la 36%).
Ukosefu wa ajira haujawahi kuwa chini kama ulivyo sasa kwa wamarekani weusi, latino na wenye asili ya Asia. Ukosefu wa ajira kwa sasa ni 3.6% (wa chini kuliko toka mwaka 1969).
Utafiti wa Harvard na Princeton unaonesha kuwa 95% ya ajira alizotengeneza Obama kwa miaka yote minane ni kazi za muda mfupi (temporary, part time + mishahara midogo).
(iv) Ajira za viwandani (manufacturing): Katika kipindi cha miezi 21 ya mwanzo ya Trump, ajira 396,000+ za manufacuring zimeongezeka, hiyo idadi ni zaidi ya mara 10 ya idadi ya ajira hizo katika kipindi cha miezi 21 ya mwisho ya Obama. Obama alishusha ajira hizi kwa 122,000 katika miaka yake minane. Hizi ndizo ajira ambazo Obama alisema Trump anahitaji muujiza kuzirudisha maana haziwezi kurudi.
(v) Mapato ya wiki (weekly earnings): Katika kipindi cha miezi 21 ya mwisho ya Obama, WE ilipanda kwa wastani wa $1.3 kwa mwezi, huku ikipanda kwa wastani wa $2.31 (ongezeko la 76%) katika miezi 21 ya mwanzo ya Trump.
Obama huwa anadai kuhusika na taarifa nzuri za Uchumi katika kipindi cha Trump na Biden anadai hivyo pia. Kitu ambacho sio kweli kwa sababu namba hazidanganyi. FACT ni kwamba uchumi wa US upo vizuri katika kipindi cha Trump kuliko cha Obama. Dems wanaoelewa hawataki hata kuzungumzia uchumi wanaona bora wakomae na uchunguzi dhidi ya Trump.
Trump ni mfanyabiashara anayejua biashara na uwekezaji unahitaji nini. Ndio maana alivyoingia tu akashusha kodi kadhaa ikiwemo ya makampuni kutoka 35% hadi 21% kwenye tax reform yake, na kuondoa kanuni rundo zilizokwamisha uwekezaji. Matokeo yake uchumi ukapanda.
Obama kwa upande mwingine ni mwanasiasa asiye na uzoefu kwenye uwekezaji, biashara na uchumi. Hata Romney aliongelea hili kwenye Debate yake na Obama mwaka 2012.
Kwamba Obama ameacha legacy ya Uchumi bora Marekani? Labda sio kwa FACTS.
Sidhani kama kuna tatizo Trump kutumia twitter kufikisha ujumbe wake kwa wananchi, ikizingatiwa kuwa media zimekuwa too biased na mifano ni mingi mno mpaka imekuwa wazi sana.
Lakini, watu wenye chuki za wazi kama zako dhidi ya Trump ndio unakuta Mueller aliwateua kumsaidia kumchunguza Trump!
Kiini cha mzozo wa Mueller na AG Barr ni kuhusu executive summary. Ukisoma barua ya Mueller aliyoandika, ni wazi kasema kila jambo la usalama lilizingatiwa na kuondolewa katika exec summaryNaona na wewe unataka kulisha wana JF matango pori.
Kwa ambao wameweza kusoma ripoti yote na underlying evidence wameona wazi kabisa kwamba ugomvi wa Mueller na Barr ni hatua ya Barr kutoa maelezo ya uongo.
Ripoti ambayo Mueller alitaka iwasilishwe Congress kama ilivyo ilikuwa ni ripoti waliyokwishaifanyia reductions zinazotakiwa kiutaratibu.
Hii ndiyo sababu hakupendezwa kabisa na alichokuwa akifanya Barr kwani barua yake ya kwanza ilipotosha kila kitu kilichotakiwa kitolewe kwa umma.
Tatizo lako wewe unasoma msitali mmoja mmoja badala ya kusoma context yote. Kwa upande conspirancy, ilionekana kuwa ushahidi uliopo hautoshi; yaani kuna ushahidi lakini hautoshi kupeleka mahakamani (kwenye crimal law); hiyo siyo kusema there was NO COLLUSION. Kwanza katika sheria hakuna kitu kinaitwa Collusion, lakini AG Barr ambaye ndiye mwanasheria mkuu wa nchi aliimba mara hivyo kadhaa kabla hajatoa ripotu yenyewe.
Umeambatanisha memorandum ya AG Barr kwenda kwa Rosenstein yenye kuonyesha kutofautiana na theories za "obstruction"za Mueller.AG kuhitimisha kuwa there was no obstruction of justice na kufunga mjadala ni kwa sababu alikuwa na hoja ya siku nyingi hata kabla hajawa AG; kwa hiyo alitoa hitimisho hilo bila hata ya kusoma. Alikuwa akisoma kutafuta mistali inayosaidia kuhitimisha maoni yake, siyo kuelewa ripoti ina maana gani. Hiyo inaitwa confimation bias.
Angalia data hizi za unemployment rate: Kuna change gani ya trajectory? Je kweli unaona kuwa graph imebadilika ghafla wakati wa Trump kulinganisha na wakati wa Obama?
Graph uliyoweka sio sahihi maana GDP growth rate haikuwahi kuvuka 3% kwa miaka uliyoonyesha.Halafu angalia data za GDP growth rate: Je kweli unaona kuwa wakati wa Trump uchumi umekuwa kwa kasi kubwa kweli?
Hoja yako ni kwamba kwa sababu 'graph haijabadilika ghafla' maana yake Trump hajamzidi Obama kwenye kushusha tatizo la ajira!.
Kwanza, Obama kwa miaka yote rate ya chini aliyowahi kufikisha ni 4.8%. Hii rate ni ya kawaida ukiangalia hiyo "trajectory" yako (retrospectively) hadi miaka ya 1990s au nyuma zaidi, ndio maana sio habari kuifikisha. Hii ni race to the lowest rate.
Pili, ukiangalia hiyo graph kwa miezi (monthly basis) utaona hayo 'mabadiliko ya ghafla' vizuri kuliko kwa miaka.
Tatu, inabidi utafsiri hizo rate kwenda kwenye namba au idadi ya waajiriwa ili upate picha kamili kuwa uchumi umekuwa ukiongeza waajiriwa kiasi gani kwa wastani kwa mwezi, kwa miaka kadhaa. Ndicho nilichokifanya kwenye post #905.
Hii hoja kwamba 'kama wote tunaelekea juu basi wote tupo sawa,' haiwezi kufaa katika kupata ulinganisho sahihi.
Graph uliyoweka sio sahihi maana GDP growth rate haikuwahi kuvuka 3% kwa miaka uliyoonyesha.
Ukuaji wa GDP US umekuwa chini ya 3.0% kwa mda mrefu, hadi watu wakaanza kuita hali hiyo "new normal".
Ila Trump amevunja dari hilo hadi 3.2% kwa robo ya mwaka huu, asilimia ambazo Obama hakuwahi kufikisha. Unaweza kudhani kutoka 3.0% hadi 3.2% haina maana kwenye uchumi mkubwa duniani. Lakini ina maana sana, kwa mfano ukiangalia wastani wa ongezeko la job openings kwa mwezi kwa miezi 21 ya mwisho ya Obama na ya mwanzo ya Trump utaona tofauti kubwa kama nilivyoeleza kwenye post #905.
Ukiangalia pia indicators kama stock markets indexes, business and consumer confidence, investments, exports v imports etc utaona tofauti kubwa sana kati ya hao Marais wawili.
Huyo El Jefe siku nyingi nimeachana naye, sijui Trump alimpa nini. Kuna wakati alikuwa anasifia sana stock market akisahau ni Obama aliyeitoa shimoni na Trump kaja kudakia tu na wakati anaidakia Dow Jones ilikuwa tayari inaisogelea 20,000 kutoka 5,000 alikoitoa Obama. Siku hizi haongelei tena stock market wala deni la taifa wala bei ya bidhaa chini ya Trump kwa sababu indiketa zote zinaonesha uchumi unakoelekea.(1) Ile ripoti ya Mueller haikuwa na picha.
(2) Hizo graph za uchumi zimetoka US Bureau of Economic Analysis.
Wakati wa Obama GDP ilivuka 3.0% mara nyingi sana labda kama huwezi kusoma graph, ila kwa vile alikuwa anavuta uchumi kutoka shimoni, wengine wenu hawamkuona movement hiyo kwa sababu mlitaka uchumi uwe getini siku hiyo hiyo mlipouporomosaha, kama ambavyo Trump aliukuta umeshafika. Uchumi wa trump haujavuta Kujenga ghorofa huchukua miaka mingi sana ila kulibomoa inachukua sdakika cheche tu. Kama unazijua cycles za Marekani na kodi, basi subiri uone. Imebaki miezi kumi tu, Marekani irudi shimoni tena.
Hizo indicators nyinge unazotumia ni BS kabisa kwani hazina uhusiano wowote na ukuaji wa uchumi. Ukitaka data kamili ziko hapa
hao ndio voters wa Trump!Huyo El Jefe siku nyingi nimeachana naye, sijui Trump alimpa nini. Kuna wakati alikuwa anasifia sana stock market akisahau ni Obama aliyeitoa shimoni na Trump kaja kudakia tu na wakati anaidakia Dow Jones ilikuwa tayari inaisogelea 20,000 kutoka 5,000 alikoitoa Obama. Siku hizi haongelei tena stock market wala deni la taifa wala bei ya bidhaa chini ya Trump kwa sababu indiketa zote zinaonesha uchumi unakoelekea.
Mkuu Nguruvi3, naomba nikukumbushe kidogo matango pori aliyotaka kutulisha El Jefe kuhusu ACA au kwa lugha ya Republicans Obama Care, nanukuu;
Halafu niseme tu kwa wale watu wanaoshikilia bango Obamacare, kuwa haitafutwa na kwamba ikifutwa itafuta wengi Congress waelewe tu kwamba wataofutwa Congress mwaka 2018 ni Democrats na sio Republicans maana ni ya kwao.
Kuna watu wengi tu walimpigia Rais Trump kura kwa ahadi ya ku-repeal na ku-replace Obamacare maana ilikuwa na bado inawaumiza. Rais Trump yupo smart sana, anawaacha wanapiga kelele, wakati hiyo Plan itakapofika Congress kabla ya Mid-term elections watakuwa na wakati mgumu either kulinda 'legacy ya Obama' au kupinga kila kitu kama wengi wao walivyoamua kufanya.
Tofauti na alivyotabiri El Jefe, Obama Care bado ipo na Trump ni kweli hakuwa na mbadala lakini Democrats kwa kutetea Obama Care waliweza kuchukua House kwa ushindi mkubwa. Huyu jamaa ni wa kuachana naye, yaonekana anawapenda sana viongozi waongo, matapeli na wenye roho kuntu.Na hiyo itaishia kuwa-cost wao zaidi kwenye Mid-term elections na Republicans wanaweza kupata Senators 60+, ukizingatia kuna Senators 10 (Democrats) wanaenda kwenye re-elections kwenye States alizoshinda Rais Trump. Kwa mtu asiyejua atasema Rais Trump hana mbadala wa ObamaCare ndio maana anasema Repeal na Replace inaweza kufanyika mwaka 2018. The good thing ni kwamba with President Trump, it will be done.
Mtu yeyote anayemani kuwa Trump ni smart lazima ana matatizo makubwa sana ya kiakili.Mkuu Nguruvi3, naomba nikukumbushe kidogo matango pori aliyotaka kutulisha El Jefe kuhusu ACA au kwa lugha ya Republicans Obama Care, nanukuu;
Tofauti na alivyotabiri El Jefe, Obama Care bado ipo na Trump ni kweli hakuwa na mbadala lakini Democrats kwa kutetea Obama Care waliweza kuchukua House kwa ushindi mkubwa. Huyu jamaa ni wa kuachana naye, yaonekana anawapenda sana viongozi waongo, matapeli na wenye roho kuntu.
Inaeleweka kwamba ulitaka kuonyesha kuwa taarifa zako zimetoka moja kwa moja kwenye "horse's mouth."(2) Hizo graph za uchumi zimetoka US Bureau of Economic Analysis.
Wakati wa Obama GDP ilivuka 3.0% mara nyingi sana labda kama huwezi kusoma graph, ila kwa vile alikuwa anavuta uchumi kutoka shimoni, wengine wenu hawamkuona movement hiyo kwa sababu mlitaka uchumi uwe getini siku hiyo hiyo mlipouporomosaha, kama ambavyo Trump aliukuta umeshafika. Uchumi wa Trump haujavunja record ya Obama. Kujenga ghorofa huchukua miaka mingi sana ila kulibomoa inachukua dakika cheche tu.
Hapa naona unaanza kuzumgumza kama nabii.Kama unazijua cycles za Marekani na kodi, basi subiri uone. Imebaki miezi kumi tu, Marekani irudi shimoni tena mpaka Obama mwingine atokeee.
Kwa mfano indicators zipi ni "BS kabisa na hazina uhusiano wowote na ukuaji wa uchumi"?Hizo indicators nyinge unazotumia ni BS kabisa kwani hazina uhusiano wowote na ukuaji wa uchumi.
Umejuaje sina data kamili?Ukitaka data kamili, ziko hapa
Huyo El Jefe siku nyingi nimeachana naye, sijui Trump alimpa nini. Kuna wakati alikuwa anasifia sana stock market akisahau ni Obama aliyeitoa shimoni na Trump kaja kudakia tu na wakati anaidakia Dow Jones ilikuwa tayari inaisogelea 20,000 kutoka 5,000 alikoitoa Obama. Siku hizi haongelei tena stock market wala deni la taifa wala bei ya bidhaa chini ya Trump kwa sababu indiketa zote zinaonesha uchumi unakoelekea.
Tofauti na alivyotabiri El Jefe, Obama Care bado ipo na Trump ni kweli hakuwa na mbadala lakini Democrats kwa kutetea Obama Care waliweza kuchukua House kwa ushindi mkubwa. Huyu jamaa ni wa kuachana naye, yaonekana anawapenda sana viongozi waongo, matapeli na wenye roho kuntu.
(a) Kwa uwongo kuna ripoti kila sehemu: Pitia website ya Politifact au Washingtonpost uone.John McCain 'aliharibu sherehe' siku ile, Obamacare ingeshaondoka! Ndio maana Dems wanamsifia sana McCain.
Trump ni "tapeli, muongo na mwenye roho ngumu,"!! aisee! mnawezaje kumchukia mtu kiasi hicho? Ukisoma comments za Kichuguu kwenye post #898 , za Nguruvi3 ndio kabisa yupo biased na anapanick sana! Mpo serious sana wakuu!
Obama kuna sera zake na maamuzi yake sikukubaliana nayo, lakini nimejifunza vitu vingi sana kutoka kwake, na yeye binafsi amekuwa honest kusema anadhani aliingia kwenye ile nafasi mapema sana!