Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,526
- 19,381
Enzi hizo wamarekani walikuwa na adui mmoja tu: USSR; kwa hiyo internal politics hazikuwa tribal kama leo. Siasa za Marekani zilianza kubadilikwa mwaka 1992. Baada ya Soviet Union kubomoka, halafu Clinton (mtoto wa maskini) akaja kumshinda George H.W Bush, wamarekani walianza kugawanyika. Ile health care plan ya Clinton ilipigwa vita vibaya sana wakati huo ambayo ndiyo hii Obamacare ya leo ambayo wamarekani wanaikimbilia. Vita hiyo ndiyo iliyosababisha Republican kuwa majority kwenye Congress baada ya miaka 40. Sasa Gingritch ndiye aliyeharibu kabisa siasa za Marekani, kwani tangu alivyoanza siasa a chuki binafsi dhidi ya Clinton mwaka 1994 hali ndiyo inayoendelea tena hadi leo; wanasiasa wanatazamana kwa chama tu, hawatazamani kwa msingi wa utaifa tena.Kwa ufahamisho tu, House ilipoanza impeachment proceedings dhidi ya Richard Nixon, wengi wa Republicans hawakuunga mkono lakini hizo proceedings ndizo ziliibua ushahidi uliowawezesha hata hao Republicans kubadilisha msimamo. Kabla ya hapo alikuwepo Republican mmoja tu aliyejitokeza na kuunga mkono impeachment ya Nixon lakini baada ya ushahidi wa tapes kuibuliwa kwenye proceedings ndipo na wenzake walipounga mkono.
Hali kama hiyo ndiyo ipo mpaka sasa lakini tofauti inayojitokeza wakati huu ni Spika Pelosi kutaka kabla ya hizo proceedings kuanza ushahidi zaidi upatikane na anajua utapatikana. Hivyo anawataka Democrats kwenda taratibu bila pupa ili wananchi wapate muda wa kutosha wa kujua kwa nini Donald Trump awe impeached. Viongozi wengi wastaafu wa GOP tayari wanaanza kujitokeza kuunga mkono wazo la kumtaka Rais Trump awe impeached.
Katika wiki ya kesho mengi zaidi yataibuliwa kulingana na kesi zinazoendelea mjini New York chini ya grand juries zilizoundwa na Robert Mueller ambapo baadhi ya redactions alizofanya AG Barr zimeamriwa zianikwe kwa wananchi. Na hapa ndipo Trump anapopata wazimu kwa nini impeachment haianzi mara moja kama alivyotegemea yeye. Alitaka impeachment ianze huku wananchi walio wengi ikiwa bado hawajui kinachoendelea lakini Pelosi katia breki.
Hasira yote ya Trump inaanzia hapo; mipango yake na wanasheria wake imevurugika kwani hawajui ni lini House itaanza proceedings na hajui ushahidi utakaokuwa umepatikana wakati huo. Ndugu zangu Marekani mambo kama haya huenda taratibu na si kwa pupa kama wengi wananvyofikiria. Sheria ya Marekani inawalinda sana wenye tuhuma mbali mbali na ni pale tu ushahidi unatosheleza ndipo hatua huchukuliwa na hili Pelosi analijua fika.
Halafu ipo hii dhana inayoenezwa zaidi na GOP kwamba impeachment inaweza ikawaathiri sana Democrats kwenye uchaguzi ujao. Hii ni kweli inaweza ikatokea kama Democrats hawakujipanga vizuri lakini kwa style ya Pelosi ya kukataa kukurupuka bila ushahidi wa wazi na unaojitosheleza. Pia wanafuatilia matamshi yote ya Trump na kila kauli anayotoa inachunguzwa kwa umakini mkubwa kwa sababu wanajua woga wake ndio unamfanya aropoke hovyo.