Ukiona mtu analinganisha embe na nanasi kwa kuangalia kuwa yote ni matunda, yana majani, yanaota ardhini, yana utamu bila kuelewa tofauti zake ujue kuna tatizo
Ken Starr alikuwa independent counsel aliyeteuliwa na majaji watatu wa DC Circuit
Ndiyo maana taarifa yake ilikwenda kwa majaji na congress na kwamba hakukuwepo nafasi ya Rais Clinton kutumia ''executive privilege'' kwa namna yoyote. Taarifa ya Ken Starr ipo wazi
Mueller ni special counsel chini ya DOJ. Kwa sheria yupo chini ya AG wa US
Ndiyo maana taarifa yake aliifikisha kwa AG ambaye ni mkuu wa DOJ
Kwa mantiki hiyo shinikizo lililpozidi AG akamshauri Rais Trump aifiche taarifa kwa exec privilege
Kwahiyo impeachment ya Trump inatakiwa iende pamoja na underlying evidence ambazo DOJ kwa kumtumia Trump na exec privilege wamezificha.
Nancy Pelosi na Nadler wanatumia mahakama ili kuweza kupata underlying evidence
Ukiisoma taarifa ya Mueller ni tofauti na ya AG Barr aliyefanya watu wakabugia matango pori
Barr anasema Mueller amesema hakuna collusion kati ya Russia na Trump
Mueller anasema hakuna sufficient evidence za conspiracy kati ya Trump na Russia
Hapa kuna neno, anaposema sufficient tayari anatueleza kuna evidence ambazo haziku rise katika level ya kuendesha mashtaka. Hii haina maana kuwa hakuna evidence kwa wanaosoma between the lines bali haikufikia kiwango cha mashtaka
Kwa upande wa obstruction of justice, AG Barr alisema hakukuwepo na conclusion ya Mueller
Again, ukisoma vizuri Mueller ameainisha hoja 10 za obstruction of justice
Kwa maana nyingine kinachotakiwa ni underlying evidence ili kuanza mshtaka katika congress
Hiyo ndiyo sababu Barr na Trump wametumia exec privilege kwani kuficha underlying evidence kunabakiza hoja ambazo hazisimami wima zenyewe
Wote wawili, independent counsel na Special counsel wana majukumu sawa, tofauti yao ni eneo au mamlaka zinazowasimamia
Ulingano kuwa wote wanachunguza Marais bila kujua mamlaka zao unaeleza jambo, hasa ubishi tu kwavile kuna keyboard mbele
Mamlaka ya Special Counsel au Independent Counsel haiathiri hitimisho la ripoti yake:
Nixon ndiye Rais wa kwanza kumteua Special Prosecutor (Archibald Cox) mwaka 1973 ili kuchunguza Watergate. Hakukuwa na sheria ya kusimamia uteuzi wa Special Counsel wala mamlaka na mipaka yake. Ndio maana Nixon aliweza kumtimua Cox alipohitaji WH tapes na akasumbua katika kumteua Jaworski akidai hawakuwa na mamlaka hayo.
Mwaka 1977, Congress wakapitisha sheria ya Ethics in Government Act (EGA) ili kuunda utaratibu wa kumteua wachunguzi maalum (special investigators).
Katika utaratibu huu AG anaanzisha uchunguzi, akiona kuna haja kuwepo uchunguzi maalum anapeleka hilo ombi mbele ya majaji watatu ili wateue mchunguzi maalum (independent counsel). Pia Congress inaweza kumuomba AG aanzishe uchunguzi. Huyu mchunguzi anafanya uchunguzi kwa Approval ya AG. AG au Congress walikuwa na mamlaka ya kumuondoa huyu mchunguzi maalum.
Huu ndio utaratibu uliotumiwa kumteua Ken Starr mwaka 1998, ambaye alikuwa approved na AG Janet Reno. Mwaka huohuo (1998) Supreme Court wakaamua kuwa sheria ya EGA ya mwaka 1977 ni constitutional (8-1). Huku Justice Scalia pekee akiipinga, akisema sio constitutional kwa sababu inapoka mamlaka ya mhimili wa Executive na kuunda mhimili wa nne wa serikali. Kwa maoni yake, Independent Counsel alikuwa na mamlaka makubwa ya DOJ ya uchunguzi na uendeshaji wa mashkata. EGA ili-expire mwaka 1999 na haikuwa 'renewed'.
Toka mwaka 1999, kanuni mpya ya Code of Federal Regulations ndio inatumika kumteua mchunguzi maalum (Special Counsel). Kanuni hii imempa mamlaka makubwa AG kwenye uteuzi wa mchunguzi maalum na kusimamia uchunguzi wake. Congress inaweza kumuomba AG ateue mchunguzi maalum. Huyu mchunguzi anaweza kuondolewa na AG. Special Counsel ana mamlaka kama US Attorney.
Huu ndio utataribu unaotumika hadi leo na ndio aliotumia AG Rod Rosenstein kumteua Bob Mueller mwaka 2017.
Ukiangalia utaratibu wa uchunguzi wa Ken Starr na Bob Mueller, Congress sio mteuzi wala msimamizi wa mchunguzi maalum bali ni mtumiaji wa ripoti za mchunguzi maalum kwa ajili ya shughuli zake za kikatiba za "oversight".
Independent Counsel Starr na Special Counsel Mueller wote walikuwa na mamlaka sawa ya kushtaki makosa.
Katika taratibu zote mbili bila AG kuamua, kusingekuwa na teuzi za wachunguzi maalum. Tofauti ndogo ya utaratibu wa teuzi za Mueller na Starr hakuwezi kuathiri hitimisho za ripoti zao, na kumfanya Mueller ashindwe kuhitimisha na kutoa mapendekezo baada ya uchunguzi. Na kusingekuwa na watu wanaotaka kumuuliza Mueller sababu za kufanya hivyo.
Kingine, Mueller anaposema "insufficient evidence to warrant a charge of criminal conspiracy" baada ya miaka miwili ya uchunguzi, maana yake hamna "indictment" kwenye criminal justice system. Utakuwa ni ujuha kwa mtu kuhitaji underlying evidence ili kumcharge Trump kwa kosa hilohilo la conspiracy kwa sababu definition ya "conspiracy" inayotumika ni ileile.
Kitendo cha Dems kusubiri underlying evidence kwa ajili ya kesi ya "obstruction", maana yake kwa ripoti jinsi ilivyo hawaoni hoja nzito? Kwamba episodes 10 za Mueller hazisimami wima zenyewe?
Mueller amesisitiza kuwa ripoti yake ndio ushahidi wake, kwamba haoni cha kuongeza! maana yake ripoti yake inasimama yenyewe.
Dems hawahitaji underlying evidence ili kuanzisha impeachment! Wanaweza tu kuanza then kisheria watapata full report na underlying evidence na watahoji watu wote wanaowataka. Kimbembe ni kwamba hawawezi kupata grand jury materials bila kuanza mchakato huo. Mpira upo kwa Dems, wanatakiwa kuamua cha kufanya na mwisho wa siku hawawezi kumuondoa Trump.