Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,409
- 31,393
Dr Kitila Mkumbo anakula matapishi yake
ACT kuvuruga juhudi za katiba ya Wananchi
CCM yapumua, ujio wa ACTkupunguza nguvu za upinzani
Wanajamvi,
Siku za karibuni chama kipya cha ACT(Alliance for Change and Transparency) kimepata usajili wa kudumu. ACT inaungana na mlolongo wa vyama vya upinzani vingine vikiwa vya briefcase
Katika mfululizo wa mabandiko yajayo, tutaangalia chimbuko, mikakati na athari za ACT katika siasa za nchi yetu. Tutakuwa na sehemu V ili kueleza kwa undani hayo tuliyoyasema.
Sehemu I
ACT kinaundwa na kundi la wanachama wa Chadema waliofukuzwa kutokana na kile kilichojulikana kama Waraka wa siri. Fuatilia uzi huu. https://www.jamiiforums.com/great-t...pecial-mgogoro-kambi-ya-upinzani-chadema.html
ACT inaundwa na watu wasiojulikana kisiasa, hakuna siri tena, ACT ina mikono ya wanachama wa CDM waliofukuzwa. Ushahidi wa hilo unapatikana kwa kauli ya Dr Kitila Mkumbo akijitambulisha kama mwanachama wake.
Yaliyojiri A
Mtakumbuka Kitila alianza harakati kwa makala gazetini akitaka uwepo wa chama mbadala cha kisiasa nje ya CCM na Chadema. Makala zililenga kuundaa umma hasa wanachama wa Chadema kupokea ujio wa ACT. Kuandika makala za matukio mbali mbali ni sehemu ya uandishi wa Kitila, kwa hili tunasema ni makusudi na wala si makala za kuhabarisha kama ilivyoonekana.
Yaliyojiri B
Wiki iliyopita ACT kimepata usajili wa kudumu. Wiki moja baadaye Kitila akasikika katika vyombo vya habari akijitambulisha rasmi kama mwanachama, na kwenda mbali kwa kusema anamshawishi Zitto Kabwe ajiunge na agombee uenyekiti.
Yaliyojiri C
Katika bunge la katiba mh Zitto alizungumzia suala la muungano.
Huko nyuma aliwahi kuzungumzia serikali 3 katika makala ambayo kumbu kumbu zetu inayo.
Kinyume na msimamo wa awali Zitto alisimama kati na kati bila kuweka msimamo wake wa wazi kuhusu suala hilo.
Yaliyojiri D
Ukawa walitoka bungeni na Zitto akiwa mmoja wapo. Katika mikutano yao kule Zanzibar mh Zitto hakuhudhuria na wala hajasikika akizungumza popote pale.
Yaliyojiri F
Baada ya usajili wa kudumu ACT kupitia mwenyekiti wake wameeleza uwepo wa jopo la wataalamu watakaoandaa katiba ya ACT. Kwa maana hiyo uongozi uliopo ni wa mpito na huenda kukakawa na uchaguzi wa mpito pia
Huu ni mtiririko kwa ufupi kuhusu chanzo na ujio wa ACT chama kinachopigiwa upatu wa kuendeshwa kitaalamu.
Hebu tuangalie sehemu ya pili tukipitia hoja za hapo juu na kuzifafanua,
Inaendelea..........