Nimemsoma vizuri lakini kwa mwenye kutaka kuelewa akiwa nje ya Box la Uchama atagundua kuwa hizi ni njama nyinginezo kwa jicho la kujenga chuki dhidi ya watu hawa. Kwa vyovyote itakavyokuwa Kitila na Zitto wamefukuzwa na chama tena kwa sababu za Kichama. Kwa nini mnafikiri Zitto na Kitila wapo hapo kusambaratisha Upinzani waklati wao wamejiunga na Upande huo badala ya kuingia CCM moja kwa moja. Milango ilikuwa waiz tena toka vyama vyote wakikaribishwa na hadi kubwa kubwa lakini wamekataa katu na kuunda chama chao wenyewe.
Kwa siasa za Bongo, Zitto angeweza kujiunga CCM na akaendelea kupeta kisiasa. Angeweza kujiunga NCCR na huko hata Uenyekiti angepewa kwa jinsi navyowafahamu jamaa hao kutaka umaarufu. Kitila angeweza kujiunga CCM na kawa na nafasi bora zaidi ndani ya chuo na nje ya chuo kwani hatuwafahamu CCM.. Lakini hawa watu wamepitia mangapi? Zitto keshajitoa mhanga kwa jina la Upinzani, Kitila kisha punguzwa hadi makali yake chuo Kikuu kwa sababu ya msimamo wake kisiasa na kwa kuitetea Chadema lakini leo hii hawa ndio wabaya wa Chadema. Hao wengine wamepitia machungu gani, hao wanaopiga vuvuzela hata siku mojka hawajawahi kupanda jukwaani akapigwa mawe na kuzomewa.
Pamoja na makosa waloyafanya hadi wakafukuzwa. Swala la wao kujiunga na ACT au CCM liwe swala walolitegemea Chadema Na hivyo wagange yaliyopo. Hivi kweli mlitegemea Zitto baada ya kufukuzwa angerudi Kigoma kuvua migebuka! au mlitegemea nini. Na kwa nini haiwezekani mtu yeyote anayejiunga na chama kingine nje ya Cjhadema ni pandikizi la CCM lakini sio hao waliomo Chadema wanaojaribu kwa kila Hila kuhakikisha Chadema inapoteza mwelekeo!
zumbemkuu, Mkuu niliipenda sana Chadema lakini kwa mwendo huu na kutokana na yale nayofahamu juu ya baadhi ya watu walojiunga Chadema kwa kutafuta ajira na wengne kutumiwa kisiasa, nadiriki kusema waswahili walosema KIKULACHO KII NGUONI MWAKO hawakuwa mbali na ukweli. Hawa watu tunaowapokea kwa sababu ya darasa au kauli zao za ULIMI pasipo kujua dhamira zao kujiunga na Chadema ndio hawa watakao kivuruga chama zaidi kwa sababu utawasikia matamshi yao pindi wanapobanwa na hoja zile akili nyingi huondosha maarifa kabisa wakaonekana sura zao halisi.
Kuendeleza haya na kuwafuatilia kina Kitila na Zitto ni dalili za wazi kabisa kwamba inatuuma kila tunapoona wanafanikiwa. Maana binafsi yangu siamini kwamba CCM wameishiwa mbinu hadi wawatumie Zitto na Kitila ambao tayari wameisha athirika kisiasa. Nia mna malengo ya wengi ni kuwaona watu hawa wamekwama kisiasa hata bkama wana malengo mazuri kwa Taifa letu. Na wanapotukosoa tunakataa kuyaona makosa kwa ubishi ule ule ulopelekea kuwafukuza chama japo tuliwahitaji Kitaifa!